Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Ukifuatilia kwa umakini na ukatafakari kwa undani na ukatizama kile anachokifanya Mheshimiwa Makonda Mwamba Mwenyewe katika majukumu yake anayokuwa amepewa na kuaminiwa na mamlaka za juu. Unakuja kugundua katika ulimwengu wa kiroho kuwa huyu Mwamba ni mpakwa mafuta wa Mungu Mwenyewe aliye hai na alie Alfa na Omega.
Unakuja kuona kuwa ameinuliwa na kupakwa mafuta na kupewa kibali na Mungu Mwenyewe ili atende matendo ya kuwasaidia watu, kuwafuta watu machozi,kuwapa faraja, matumaini, kuwashika mkono,kuwatua mizigo ya kero na shida na kuwainua watu kutoka chini kupitia mkono na kinywa cha Makonda. Ikumbukwe ya kuwa Mungu hutenda miujiza kupitia watu waliopo hapa hapa Duniani.na ndio maana imeandikwa katika kitabu cha WAEBRANIA sura ya 13 mstari wa pili kuwa msisahau kuwafadhili wageni maana kwa njia hiyo wengine wamekaribisha malaika pasipo kujuwa.
Leo tunashuhudia namna ambavyo kupitia Mwamba Makonda namna wajane ,masikini ,yatima,wazee na watu mbalimbali wakipata haki zao walizodhulumiwa na baadhi ya watu wenye pesa zao kwa uonevu tu. Tunaona namna ambavyo watu wakifurika na kumkimbilia Mwamba kutaka kusaidiwa shida na kero zao.tunaona namna watu wanavyo tafuta upenyo walau wa kumshika hata vazi lake tu ili wapate kuonwa na kusaidiwa shida zao zinazowabubujisha machozi na kuwakosesha raha na amani kila siku.
Mnafikiri ni kwanini Mheshimiwa amekuwa kimbilio na tumaini la watu sana kila anaposimama Kama kiongozi? Kwanini iwe Makonda tu ndugu zangu? Kwanini anaaminika sana na watu huyu mtu? Kwanini anapendwa na kukubalika kiasi hiki utafikiri malaika aliyeshushwa na Mungu kuwaokoa watu wake? Kwanini yeye tu anavuma na kuteka hisia za watu? Kwanini atafutwe na masikini waliodhulumiwa haki zao? Kwanini watu wabubujike machozi mbele yake utafikiri mwanamke aliyefiwa na mumewe au mama aliyepoteza mtoto?
Jibu ni kwa kuwa Mheshimiwa Makonda anazungumza lugha za watu,anajibu kero za watu,anagusa maisha ya watu,ni kiongozi mnyenyekevu na anayefikika na watu wa aina zote bila ubaguzi. Hii ni kwa kuwa ni kiongozi ambaye ukiwa na shida ni lazima akusaidie mpaka jibu lipatikane na siyo kuishia njiani.ndio maana tumeona kwa mkono wake akisaidia watu wengi sana wenye shida na mahitaji ya hali na mali.Tofauti na viongozi wengine ambao hujifanya Miungu watu,watu special sana ,watu wa matawi ya juu,watu ambao kuwapata na ukasikilizwa kwa umakini shida yako ni sawa na kuokota dhahabu au almasi njiani.
Lakini kwa Makonda Mwamba kwake utumishi ni dhamana ya kuwatumikia watu, kuwasikiliza watu na kuwapa majibu.kwake Mwamba uongozi ni kuwamulikia watu taa wawapo gizani na kuwaongoza njia.ndio maana anakimbiliwa sana.ndio maana mtu anaona ni bora aende kwanza kwa Makonda kuliko kwenda mahakamani,ndio maana mtu anaona ni bora asafiri umbali mrefu kwa miguu huku akitokwa jasho mwili mzima kama analima ili tu akaufikie uso wa Mheshimiwa Mwamba Mwenyewe Makonda.
Kaka yangu Mwamba Mwenyewe Makonda neno langu kwako ni moja tu .Bwana Mungu asema Uwe hodari na moyo wa ushujaa na hata kuacha katika kazi yako hiyo ya kitume ya kuwatumikia watanzania wanyonge wanaohitaji msaada na kufutwa machozi. Mungu alimwambia YOSHUA kuwa hatamuacha kama ambavyo hakumuacha Musa na kwamba atakuwa naye siku zote za maisha yake. Na ndio maana kupitia YOSHUA aliwavusha wana wa islael. Mungu ataendelea kuwa na wewe Mheshimiwa na wala hatakuacha hata kidogo.kazi unayoifanya ni sawa na kuwa unamkopesha Mungu ambaye atakulipa malipo makubwa sana wewe na uzao wako wote kuanzia wajukuu,vitukuu,vilembwe mpaka vilembwekezi.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.
Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.