Pre GE2025 Paul Makonda: Ukimchukia Rais Samia unamkosea Mungu

Pre GE2025 Paul Makonda: Ukimchukia Rais Samia unamkosea Mungu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Upuuzi mtupu. Ama kweli mtu ukikosa akili, unakosa hata aibu.

Kama kuna mtu alitoa machozi, yumkini alimkumbuka Ben Sanane, na kustaajabu kuona muuaji anatamba majukwani bila ya kuwepo wa kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.

Mungu wetu, tunaomba laana itembee daima na mtu huyu na kizazi chake chote kwa uovu alioutenda na hadaa anazoendelea kuzifanya. Atembelee viongozi wote wa dini, apande mikokoteni na hata punda, lakini milele asipate amani moyoni mwake.

RIP Ben Sanane, RIP Azory Gwanda, na amani na mafanikio yaambatane na Tundu Lusu. Na zaidi ya yote, tunaomba utukufu wa Mungu uzidi kudhihirika dhidi ya mtu huyu na wale wote wenye kuambatana naye.
Acha kuchafua watu kwa kuandaki vitu usivyo na ushahidi navyo.
 
Picha ya watoa machozi iko wapi wewe malaya wa akili?

Huyo zero brain mwenyewe wakati wa maporomoko ya udongo Hanang hakwenda alikua SA huko.
Mheshimiwa Makonda ni akili kubwa na mtu mwenye maono makubwa sana
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa Paul Makonda Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa hapo jana huko babati Mkoani Manyara ametoa hotuba ya mwaka,hotuba iliyoteka na kugusa hisia za watu,hotuba iliyowafanya watu washindwe kujizuia machozi na hivyo kujikuta wakibubujikwa na kutiririka machozi kutoka katika macho yao,hotuba iliyoacha historia na kuwatia moyo wana babati.

Ni baada ya kusema kuwa Ukimchukia Rais Samia unakuwa Unamkosea Mungu Mwenyewe,kwa kuwa Rais Samia alijipangia kuishi maisha ya kawaida kabisa na wala hakuwahi kupanga wala kuwaza kuwa makamu wa Rais wala Rais wa Tanzania.lakini Mungu na mipango yake alipanga iwe hivyo kwa kumuinua na kumpa umakamu wa Rais na baadaye Urais.

Mheshimiwa Makonda aliendelea kusema kuwa hata yeye hapo alipo kwa sasa ni mipango ya Mungu Mwenyewe aliye juu na wala siyo mipango yake,maana alikuwa tayari yupo nje ya msitari. Aliendelea kuzungumza huku wananchi wakitekwa na hotuba hiyo iliyojaa hisia kali sana na mguso wa aina yake kwa kusema kuwa hata wao wasikate tamaa na wajipe moyo na wala wasiumie wanapodharauliwa na mtu.

Kwa hakika Mheshimiwa Makonda ni mtu ambae ukisikiliza hotuba zake lazima uguswe sana ndani ya moyo wako, ni mtu anayezungumza toka ndani kabisa ya moyo wake, ni mtu anayeongea na kuzungumza kwa kugusa hisia za watu,anaongea uhalisia wa maisha, anazungumza kile kinachogusa yale yaliyopo kwa watu na wananchi.ndio maana watu wanafurika na kumiminika sana kwenye mikutano yake.

Ni mtu ambae ukimsikiliza unapata matumaini na nguvu kubwa sana ya kusonga mbele kimapambano,anatia moyo na faraja sana.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

IMG_3869.jpg

IMG_6223.jpg
 
Alijisajili kuwa chawa wa Tulia, naona hakifanikiwa kama alivyotarajia.
Mimi ni msema kweli ninayemuunga mtu yeyote anayefanya vyema katika kutimiza majukumu yake. Ninaendelea na Nitaendelea kumuunga mkono pia Mheshimiwa dkt Tulia Acksoni Mwansasu
 
"Mimi ni Mungu mwenye wivu"

Ukuu wa Mungu hauchangamanishwi na yeyote. Huyu ounguani anaitafuta laana ya Mungu. Anachokitafuta atakipata. Mungu huwa hachelewi, wala hakawii, hutenda kwa wakati wake.
Tangia lini umekuwa msemaji wa Mungu juu ya hukumu.
 
Mungu na wahalifu wapi na wapi? Naona amepata jukwaaa la kujisafisha hivyo anamtaja Mungu akidhani tutamuona ni mcha Mungu. Damu za alizozimwaga atalipia hapa hapa duniani.
Damu za nani? Acha kuropoka ujinga usio na ushahidi nao. ukiambiwa ulete ushahidi utaleta?
 
Back
Top Bottom