Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawa jamaa wamebanwa kodi kwenye biashara zao sasa kwa kuwa kwenye vilabu hivo masuala ya kodi ni kama sifuri hivo wanafanya kila wawezavo kujikita huko. Naomba serikali itupie jicho huko kama ilivofanya kwenye taasisi za kidini. Kama kweli wanapesa na ni wapenzi wa soka waanzishe vilabu vyao kama Azam FC.Alianza Zito, akaja tundu lisu, sasa makonda. Huo mkataba una nini?? Tunaomba uwekwe wazi kwanza kabla ya kupitishwa
====================
Makonda atoa ya moyoni kuhusu Yanga, aihusisha Yanga na umasikini kwa watanzania
Kitendo cha klabu ya Yanga kumruhusu mwnyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji kuikodi klabu hiyo kwa miaka 10 kinaonekana kuendelea kuwagusa watu wengi na mmoja wapo amekuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye pamoja na kuguswa na kitendo hicho pia ameamua kuandika katika mitandao.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Makonda aliandika “Unataka kujuwa kwa nini Tanzania ni masikini pamoja na UTAJIRI MKUBWA WA MALIASILI tulizonazo? Soma Mkataba wa Yanga wanaosaini LEO”
Baada ya kuweka picha hiyo wadau mbalimbali wa soka nchini wamekuwawakiweka maoni yao katika picha hiyo, wengine wakimtaka asizungumze mambo ya Yanga, wengine wakimtaka afanye kazi za serikali na aache kujihusisha na soka na mashabiki wa wapinzani wa Yanga wakiwasema watani wao wa jadi kwa kukubali timu yao kukodishwa kwa mtu mmoja na akiwaachia majengo.
Awali Makonda aliweka picha ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga na kusema kuwa alikuwa na maswali 87 kwa kiongozi huyo wa Yanga lakini baada ya kutizama mahojiano aliyofanyiwa na kituo cha Clouds Tv aligundua kwamba kiongozi huyo bado hajaelewa ni kitu gani kinaendelea klabuni.
Mkuu, kwa hili kila Mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi hii hawezi acha upuuzi huu utamalaki.Huyu dogo ana matatizo! Mi staki hata kusikia maneno yake! Ni kama boss wake! Anachokiwaza anakiongea bila kutafakari.
Eti aondoe ombaomba Dar
Eli walimu wasilipe nauli
eti .... yaani mambo ya ajabu ajabu
Who cares about 'what one posts here in JF'!Mpira wa miguu hauna democrasia... Democrasia ipo kwenye siasa tuu
Unajua hakuna mtu anayetaka upuuzi kutokea! Ila inapendeza kama mtu akiongea jambo akatoa ufafanuzi unaoeleweka, sio kuongea vitu alafu vikabaki hewani hewani!Mkuu, kwa hili kila Mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi hii hawezi acha upuuzi huu utamalaki.
Mkuu, huyu Makonda na Ummi ni wanaharakati lakini pana wakati wanazungumza mambo ya hakika.Unajua hakuna mtu anayetaka upuuzi kutokea! Ila inapendeza kama mtu akiongea jambo akatoa ufafanuzi unaoeleweka, sio kuongea vitu alafu vikabaki hewani hewani!