Paul Makonda: Ukitaka kujua kwanini Tanzania ni maskini pitia mkataba wa Yanga wanaosaini Leo

Paul Makonda: Ukitaka kujua kwanini Tanzania ni maskini pitia mkataba wa Yanga wanaosaini Leo

Je mkataba wa ile timu inayouzwa umekaaje?
 
Haw
Alianza Zito, akaja tundu lisu, sasa makonda. Huo mkataba una nini?? Tunaomba uwekwe wazi kwanza kabla ya kupitishwa


====================
Makonda atoa ya moyoni kuhusu Yanga, aihusisha Yanga na umasikini kwa watanzania

Kitendo cha klabu ya Yanga kumruhusu mwnyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji kuikodi klabu hiyo kwa miaka 10 kinaonekana kuendelea kuwagusa watu wengi na mmoja wapo amekuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye pamoja na kuguswa na kitendo hicho pia ameamua kuandika katika mitandao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Makonda aliandika “Unataka kujuwa kwa nini Tanzania ni masikini pamoja na UTAJIRI MKUBWA WA MALIASILI tulizonazo? Soma Mkataba wa Yanga wanaosaini LEO”

Baada ya kuweka picha hiyo wadau mbalimbali wa soka nchini wamekuwawakiweka maoni yao katika picha hiyo, wengine wakimtaka asizungumze mambo ya Yanga, wengine wakimtaka afanye kazi za serikali na aache kujihusisha na soka na mashabiki wa wapinzani wa Yanga wakiwasema watani wao wa jadi kwa kukubali timu yao kukodishwa kwa mtu mmoja na akiwaachia majengo.

Awali Makonda aliweka picha ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga na kusema kuwa alikuwa na maswali 87 kwa kiongozi huyo wa Yanga lakini baada ya kutizama mahojiano aliyofanyiwa na kituo cha Clouds Tv aligundua kwamba kiongozi huyo bado hajaelewa ni kitu gani kinaendelea klabuni.
Hawa jamaa wamebanwa kodi kwenye biashara zao sasa kwa kuwa kwenye vilabu hivo masuala ya kodi ni kama sifuri hivo wanafanya kila wawezavo kujikita huko. Naomba serikali itupie jicho huko kama ilivofanya kwenye taasisi za kidini. Kama kweli wanapesa na ni wapenzi wa soka waanzishe vilabu vyao kama Azam FC.
 
Huyu dogo ana matatizo! Mi staki hata kusikia maneno yake! Ni kama boss wake! Anachokiwaza anakiongea bila kutafakari.

Eti aondoe ombaomba Dar
Eli walimu wasilipe nauli

eti .... yaani mambo ya ajabu ajabu
Mkuu, kwa hili kila Mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi hii hawezi acha upuuzi huu utamalaki.
 
Mkodisho fc, hili jina punde litafukiwa jf kwa nyotanyota likiandikwa
 
Mikia tu hiyo, wa matopeni hao, cc tunawaza mambo ambayo hawatayaelewa ila watayaelewa baadae sana... Tumekodisha tayari...
 
Makonda alichosema ni kweli , lakini nadhani kabla ya kuhoji huu mkatanba basi angeanza kuhoji mikataba iliyoingiza na inaendelea kuingiza taifa hasara kubwa
 
Hoja Yangu ya kuwa Siasa zitauza football inamshiko na maneno haya ya Makonda

SIMBA NA YANGA Tuachane kabisa na Matajiri hawa wenye mrengo wa CCM Au hata wa Vyama vingine vya Siasa... wote ni wapenzi na washabiki wa kutupwa wa CCM ..Tuachane kabisa kuuza timu au kukodisha hizi timu ambazo zinaunganisha Watanzania wote bila ya kujali tofauti za Kisiasa au Dini Kuna Hatari zake.
Nitakupeni Mfano wa wazi.
Kabla Ya Uchaguzi wa Kwanza wa Vyama vingi Kule Zanzibar Football ilipanda Juu sana. Timu za Zamani kama
Malindi
Miembeni
Vikokotoni
Kikwajuni
KMKM
Jamhuri

na zile Mpya kama
Small Simba
Black Fighters
Annur
Shangani nk


zilikua katika hali ya kiwango cha Juu na kuweza kutoa wachezaji wengi wazuri kwenye timu Ya Taifa Stars...
Malindi mwaka 1994 ilikua chini ya Mohammed Raza Na Naushad, Mwana CCM kINDAKI NDAKI...iliweza kusajili wchezaji wazuri na makocha wa nje. Ilifanikiwa Kuingia Fainali ya FA la Africa...
Baadhi ya Timu Hizi zimewahi kuchukua Ubigwa wa Tanzania Wakati ule Ligi ni Moja
Small Simba nayo ilikuwa chini ya Raza mdogo
nazo Timu za Shangani , Annur zilipata Ufadhili wa Matajiri wa CCM...Zote zilikuja Juu.
Ukaja Uchaguzi 1995 Na majimbo haya ambayo timu hizo zipo kwa bahati nzuri yaka chukuliwa na CUF.... Hawa wafadhili wakapata pressure na hatimae wakkaacha kufadhili hizi timu...Hatua Hii haikutarajiwa kabisa na hizi timu waliwaachia hawa wafadhili kila kitu ...hizi Timu zikafa kabisa na kushuka Daraja.. Hili likaleta athari kubwa ya Football Zanzibar. ..Kila Mtu atakubali kuwa hali ya Football zanzibar iko chini sana , imeanguka kweli kweli...Sasa hivi hakuna Small Simba wala Malindi wala Miembeni....Sasa hivi Mpira Zanzibar Unachezwa hivo hivo na Timu za Majeshi. Kuna
Mafunzo
Kmkm
JKU
Na Timu ya CCM Valantia au Green Guards....nao hawachezi mpira ..wanajitoa majasho tu kusukuma siku.

Hivyo Tusifanye Makosa hatua hizi zinaweza kuja angusha kabisa Mpira wa Tanzania. Siasa zetu bado sio zile zilizokomaa sana..
Tujifunze na Kusoma Ilikuwaje Simba..Ikagombana na Hatimae Ikagawanyika na Kuundwa RED STARS
Na ilikuwaje Yanga Ikavurugika na kugawanyika na Kuzaliwa PAN AFRICAN......
Pia someni Historia ya Cosmopolitan. Cosmo Ilikua Timu moja Kongwe zaidi na ilokuwa na ushawishi zaidi ya Simba na Yanga Miaka Ya nyuma. Ilikua na Uhusiano Maalum na Timu Kongwe ya Vikokotoni Zanzibar..Hizi Timu zote zilikua zikiongozwa na Ndugu wawili wa Kizanzibari Mansour Magram alikua Cosmo na Said Magram alikua Kocha wa Vikokotoni. Wakati huo huo Mzanzibari mwengine Abdalla Khalifa Salim ( Kinara) ndie alikua Rais wa Cosmo
Cosmo iliporomoka....Karume hakua anaipenda Vikokotoni Akaziwezesha Simba na Yanga....Cosmo Ikabaki kwenye vitabu vya historia.
Pia tusome Kisa na uhusiano wa Mwalimu na Tabu Mangara ..mara baada ya Ile Mechi Maarufu ya Yanga na Simba Kule Nyamagana Mwanza
Moja ya sababu ya migongano hiii ilikua ni Siasa......


HISTORIA NI MWALIMU MZURI
 
  • Thanks
Reactions: DBA
Binafsi jibu ni rahisi sana kwa Watz. kuwa masikini japokuwa na rasilimali zote ni kwasababu ya CCM kushindwa kuwaondolea Watz. yale maswahiba ya Ujinga,Umasiki,Maradhi,Ufisadi n.k. na hatimaye kuendelea kuyalea na kuyalinda vema.
 
Siku zote nikiona adui yangu anapinga kile ninachotaka kukifanya uwa naendelea nacho,toka lini mikia wakaionea huruma Yanga hadi povu liwatoke!
 
huyo makondakta afanye siasa na kutuachia mpira wetu.yeye zitto na wanasiasa wote.wangekuwa wanafahamu sana mpira wangekuwa viongozi katika medani ya mpira na sio siasa.ndio maana soka letu haliendelei kwasababu ya siasa zinazoisumbua tz tangu enzi hizo.miaka zaidi ya 80 timu zimeendeshwa kwa mfumo ule ule na hatujaona kipya.wazungu wanasema insanity is doing the same thing over and over while expecting to get different results.sasa sahivi tunataka revolution especially mental revolution kwanza ili mpira wetu uendeshwe kitajiri zaidi.mpira pesa bana na sio siasa.tena waache kujifanya wao ndo thinkers wakubwa eti tuwasikilize kila wasemalo. time for change is now.both simba na yanga waachieni timu wenye pesa mpira usonge mbele.wanachama wenyewe hata ada hawalipi sasa kuna maana gani ya timu kuendeshwa na wanachama
 
Mkuu, kwa hili kila Mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi hii hawezi acha upuuzi huu utamalaki.
Unajua hakuna mtu anayetaka upuuzi kutokea! Ila inapendeza kama mtu akiongea jambo akatoa ufafanuzi unaoeleweka, sio kuongea vitu alafu vikabaki hewani hewani!
 
Unajua hakuna mtu anayetaka upuuzi kutokea! Ila inapendeza kama mtu akiongea jambo akatoa ufafanuzi unaoeleweka, sio kuongea vitu alafu vikabaki hewani hewani!
Mkuu, huyu Makonda na Ummi ni wanaharakati lakini pana wakati wanazungumza mambo ya hakika.
 
Safi sana, kifo au anguko la yanga furaha kwetu! Acha WASAINI tu.
 
Mambo ya klabu awaachie wana yanga wenyewe, kwanini yeye kama yeye Haoni kwa nini nchi ni masikini wakati kila siku wanasaini mikataba ya hovyo hovyo huku wakikataa bunge kuonyeshwa laivu, why?
 
Back
Top Bottom