Paul Makonda usifanye siasa zako kama wapinzani wanavyotaka!

Nsanzagee

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2023
Posts
2,209
Reaction score
4,769
Kuna wakati ujinga wa wapinzani, hujianika peupe kiasi cha nyeti za kuku mbele za upepo wa kisulisuli. Nijuacho ni hiki!

Anguko lolote la CCM, ni sherehe kwa wapinzani, iweje sasa wachukizwe na namna ya matamko ya Mwenezi wa CCM ndugu Paul Makonda?

Mpinzani unataka Paul Makonda afanye siasa zitakazo ifanya CCM iendelee kupendwa? Au ni mtego wenu mbele za CCM kupitia Makonda?

Tangu lini mpinzani aihurumie CCM isianguke?
 
Makonda shikilia hapo hapo usiachie kabisa, yaani hapo ndiyo penyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…