Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
BAADA ya kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizofanyika Agosti 4,2025 nimejipa jukumu la kuzungumza na baadhi ya wagombea ambao wapo tayari.Mmoja wa wagombea niliyezungumza naye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kutoka Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya.
Mwakajumba ni mmoja wa wateule Wanne waliopigiwa kura na wajumbe wa chama hicho Wilayani Kyela. Pigia mstari neno Wajumbe.
SHUKRANI.
Anaanza kwa kusema kuwa kwanza kabisa anamshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ushupavu wake wa uongozi na kuongoza vikao vyote na yeye pia kuwa mmoja wa wateule wa Jimbo la Kyela.
Anasema shukrani hizo ni pamoja na kujionea miradi mingi ya Maendeleo kujengwa katika Wilaya ya Kyela ikiwemo shule ya wasichana ya mkoa wa Mbeya.
Na kwamba miradi ni mingi na Rais Samia anastahili kuwa mgombea wa awamu hii kazi na utu tunasonga mbele.
Pili anawashukuru wananchi wa Jimbo la Kyela bila kujali itikadi zao za vyama vya siasa kwa kujitokeza kwenye mikutano ya kampeni ya wagombea.
Tatu anawashukuru wajumbe wote waliompigia kura za heshima na hata ambao hawakumpigia kura.
GUMU ALILOKUTANA NALO
Ndugu Paul Mwakajumba anasema siku ya kuamkia kwenda kupiga kura alizushiwa kifo jambo ambalo lilizua taharuki kubwa na kupelekea baadhi ya wananchi kwenda Hospitali ili kuhakikisha.
Anasema jambo hilo hawezi kulisahau.
Alipoulizwa kuwa anahisi kwanini lilitokea jambo hilo anatoa jawabu kwamba ni kutokana na yeye muda mwingi kushinda nyumbani tofauti na wagombea wenzake hivyo akazushiwa.
Kuhusu maono yake anasema alichukua fomu ili awe daraja la wananchi wa Kyela kwasababu amebaini kuwepo kuwa viongozi wengi wapo mbali na wananchi.
"Kuna gape kubwa sana kati ya watawala na wananchi" amesema Mwakajumba.
Anasema changamoto zinazowakabili wana Kyela ni nyingi licha ya baadhi kutatuliwa lakini kwa uchache anataja mawasiliano ya Simu kuwa taabu, umeme na Maji...
*********
Vikao vya chama bado kuteua wagombea au wapeperusha bendera ya chama hicho lakini waswahili wanasema Moyo usio na shukrani haupaswi kuwa sehemu ya mwili wa binadamu na kwa kutambua hilo, ndugu Paul Mwakajuma anamshukuru Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na wananchi wa Kyela huku akisema kuwa baadhi ya changamoto hata asipokuwa Mbunge atazibeba kama mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kutoka katika Wilaya ya Kyela.
Hii ni sauti kutoka Nyikani.