Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Huu ni ushauri ambao naupeleka kwa Ndugu Paulina Gekul, ambaye ametumbuliwa kwa ukatili dhidi ya Ubinadamu, kwamba Nchini Tanzania unaweza ukafutwa uanachama na chama chako au ukajifuta mwenyewe lakini bado ukaenda mahakamani kuupigania ubunge wako.
Halima Mdee na Wasaliti wenzie hadi leo wako bungeni pamoja na kutimuliwa kisheria na Mkutano Mkuu wa Chadema, Mwingine ni Mamluki Mwambe wa Ndanda, huyu alijiondoa mwenyewe Chadema baada ya kununuliwa na Humphrey Polepole, akajivua ubunge na kurudi kwao kulima korosho, akarudisha mpaka chumba cha Gesti aliyopanga Dodoma, lakini akaitwa na Spika wa wakati ule Job Ndugai arejee bungeni bila Chama na akarejea na kumalizia ubunge wake.
Kwahiyo tunatarajia Gekul naye apite njia hiyo hiyo.
Angalizo: Siungi mkono Unyama wake kama vile nisivyounga mkono unyama wa Makonda, bali nataka wana JF muone wenyewe jinsi Katiba ya Tanzania inavyosiginwa