Paulina ukifukuzwa uanachama CCM kimbilia Mahakamani ukazuie ubunge wako kama wale akina Mdee

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Screenshot_2023-11-26-21-24-03-1.png

Huu ni ushauri ambao naupeleka kwa Ndugu Paulina Gekul, ambaye ametumbuliwa kwa ukatili dhidi ya Ubinadamu, kwamba Nchini Tanzania unaweza ukafutwa uanachama na chama chako au ukajifuta mwenyewe lakini bado ukaenda mahakamani kuupigania ubunge wako.

Halima Mdee na Wasaliti wenzie hadi leo wako bungeni pamoja na kutimuliwa kisheria na Mkutano Mkuu wa Chadema, Mwingine ni Mamluki Mwambe wa Ndanda, huyu alijiondoa mwenyewe Chadema baada ya kununuliwa na Humphrey Polepole, akajivua ubunge na kurudi kwao kulima korosho, akarudisha mpaka chumba cha Gesti aliyopanga Dodoma, lakini akaitwa na Spika wa wakati ule Job Ndugai arejee bungeni bila Chama na akarejea na kumalizia ubunge wake.

Kwahiyo tunatarajia Gekul naye apite njia hiyo hiyo.

Angalizo: Siungi mkono Unyama wake kama vile nisivyounga mkono unyama wa Makonda, bali nataka wana JF muone wenyewe jinsi Katiba ya Tanzania inavyosiginwa

Screenshot_2023-09-13-15-16-13-1.png
 
Umeona mbali. Hii kesi itawafanya watu wajiulize mengi sana na waone madhaifu ya sheria zetu,viongozi na mamlaka zenye wajibu wa kusimamia sheria. Wakikurupuka wanafungua maboksi ya wateule wengi tu. Ni mwendo wa comparison mpaka mwakani.Kwanini kwa yule ilikuwa hivi kwa huyu iwe hivi? Wajipange.
 
View attachment 2826112

View attachment 2826111
Karma is the bitch. CCM sasa hivi itabidi wanywe dawa waliyojitengenezea🤣🤣🤣🤣
 
Kina Mdee walifanya uhalifu kama huu wa Gekul? Wewe Erythrocyte ungeandika huu uzi kama mwanao angeingiziwa chupa huko nyuma? Sio kila kitu siasa mkuu... suala la kina Mdee ni la kisiasa na hili la Gekul ni jinai na hata viongozi wako wa CHADEMA wamelaani hiki kitendo alichofanya. Nchi nzima iko against Gekul. Ni wewe na wapuuzi wachache mnaotaka kuingiza siasa hapa.
 
Hana huo ubavu . Hiyo hoteli yake itapigwa mnada kisa madeni ya kodi
 
Kina Mdee walifanya uhalifu kama huu wa Gekul? Wewe Erythrocyte ungeandika huu uzi kama mwanao angeingiziwa chupa huko nyuma? Sio kila kitu siasa mkuu... suala la kina Mdee ni la kisiasa na hili la Gekul ni jinai na hata viongozi wako wa CHADEMA wamelaani hiki kitendo alichofanya. Nchi nzima iko against Gekul. Ni wewe na wapuuzi wachache mnaotaka kuingiza siasa hapa.
Kwani hukumu imetolewa na kuthibitisha jinai aliyofanya?
 
Umeona mbali. Hii kesi itawafanya watu wajiulize mengi sana na waone madhaifu ya sheria zetu,viongozi na mamlaka zenye wajibu wa kusimamia sheria. Wakikurupuka wanafungua maboksi ya wateule wengi tu. Ni mwendo wa comparison mpaka mwakani.Kwanini kwa yule ilikuwa hivi kwa huyu iwe hivi? Wajipange.
Hapo ndipo iliposimamia hoja yangu , asante kwa kunielewa , akienda mahakamani hawawezi kumuondoa , njia pekee ni kumuua tu
 
Kina Mdee walifanya uhalifu kama huu wa Gekul? Wewe Erythrocyte ungeandika huu uzi kama mwanao angeingiziwa chupa huko nyuma? Sio kila kitu siasa mkuu... suala la kina Mdee ni la kisiasa na hili la Gekul ni jinai na hata viongozi wako wa CHADEMA wamelaani hiki kitendo alichofanya. Nchi nzima iko against Gekul. Ni wewe na wapuuzi wachache mnaotaka kuingiza siasa hapa.
Unafahamu kuna watu wameuliwa kwenye hilo sakata la akina Mdee ? kuua watu na kuingizwa chupa lipi kubwa ? Makonda ameua ( kwa mujibu wa USA ) lakini kateuliwa , hili jambo halikushangazi ?
 
Hapo ndipo iliposimamia hoja yangu , asante kwa kunielewa , akienda mahakamani hawawezi kumuondoa , njia pekee ni kumuua tu
Ukitazama hili jambo kwa jicho la tatu kwa kuangalia pongezi alizopewa Mh. Rais ni kwamba watanzania hawafurahishwi na watu wanyanyasaji kuwa madarakani au na vyeo fulani. Pauline hayuko mwenyewe,je kwa hatua hii itambidi kuwachukulia hatua na wengine wanaolalamikiwa? Tricky!
 
Hana ubavu huo na Kwa sababu ni zao la chadema tunamfukuza arudi chadema
Chadema tunamkaribisha kwa mikono miwili. Ni kijana wetu, tumemlea na kumkomaza wenyewe kisiasa; alirubuniwa tu ndiyo maana akaondoka. Atakuwa mwana mpotevu anayerudi nyumbani. Wakiendelea kumfuatilia tunaiambia dunia kuwa ni mhanga wa kisiasa.
 
Back
Top Bottom