Paulo wa Tarso jasusi la kiroma lililopewa misheni ya kubadili mwelekeo wa Ukristo na kuwa upagani

Ndiyo, Paulo alilitesa kanisa (Mdo 8:1-3), lakini mabadiliko yake ya ghafla yalishuhudiwa na wengine. Kwa mfano Anania alithibitisha maono ya Paulo (Mdo 9:10-17), na baadaye kanisa lilimkubali baada ya kushuhudia matunda ya huduma yake (Mdo 9:26-30)

Ni sawa, ni ushuhuda binafsi (Mdo 9:3-7), lakini ulithibitishwa na mabadiliko ya maisha yake, huduma yake, na ufunuo aliopewa – Gal. 1:11-12.

Mitume waliendeleza huduma ya Yesu kwa Wayahudi (Mathayo 10:5-6), lakini Paulo alipewa wito wa kipekee kwa mataifa (Mdo 9:15; Warumi 11:13). Yesu ana mamlaka ya kumchagua anayemtaka kwa kusudi maalum.

Paulo hakupinga Torati; alifundisha kuwa wokovu haupatikani kwa matendo ya torati bali kwa neema kwa njia ya imani (Gal. 2:16). Yesu mwenyewe alisema hakuja kuiondoa torati bali kuitimiliza (Mathayo 5:17), na Paulo alieleza utimilifu huo ni kwa njia ya Kristo (Warumi 10:4).

Mafundisho ya Paulo yaliendana kabisa na yale ya mitume. Ndio sababu walipokutana Yerusalemu, waliungana naye na walimpa mkono wa ushirika (Gal. 2:1-9). Hakuandika kwa kubuni bali kwa ufunuo wa Roho Mtakatifu (1 Wakor. 2:10-13).

Kitabu cha Warumi 13:1-7 kinawalenga Wakristo waliokuwa chini ya utawala wa Rumi. Paulo aliwahimiza kutii mamlaka ili kuepuka mateso yasiyo ya lazima, sio kwa kuhalalisha udhalimu. Isitoshe, Biblia ina mifano mingi inayoonyesha jinsi Mungu anavyoweza kutumia hata tawala dhalimu kwa kusudi lake (Dan. 4:17).

Mafundisho ya Paulo kuhusu kutafuta mambo ya rohoni ndio msingi wa Ukristo (Wakol. 3:1-2). Yesu mwenyewe alisema: “Ufalme wangu si wa dunia hii” (Yoh. 18:36). Paulo hakusema watu wasifanye kazi au kutafuta maendeleo ya kimwili bali alihimiza kutanguliza uzima wa milele.

Pumzika na Mungu akusaidie usiwe jasusi lililopewa misheni ya kufundisha mafundisho ya mashetani.
"Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani.."(1 Tim 4:1-5)

cc: K11 Covax
Ubarikiwe
 
4. Paulo alienda kinyume na Mafundisho ya Yesu hasa yanayohusu Torati ya Musa.
Paulo ndiye mhusika pekee aliyeipotosha Biblia na kuipa mrengo wa kipagani.
Mafundisho ya sabato
Kumfanya Yesu Mungu
Kuruhusu kula chakula chochote n.k.
Wasabato, waislamu na washika torati wote lazima mchukie mafundisho ya paulo sababu yananyang'anya kujiona mnastahili kuliko wengine.

Kuhusu chakula hata Yesu alipuuza na kusema Chochote kinachoingia tumboni kisha chooni hakiwezi kukufanya najisi, tofauti kabisa na Torati inayosema baadhi vyakula vikiingia kwenye tumbo la mtu vinamfanya kuwa najisi. (Marko 7:19)

Kuhusu Sabato baada ya wayahudi kumsonga sana, Yesu aliaamua kuwaambia Yeye ndiye BWANA wa vyote na ni BWANA wa Sabato pia, Hivyo anaweza kufanya chochote siku inayoitwa ya sabato kwa sababu yeye ndiyo MKUU/LORD wa vyote ikiwemo sabato. (Marko 2:28)
Ndiyo maana yeye na baba yake hawajawahi kupumzika. (Yohana 5:17)

Kuhusu Uungu wa Yesu mwanzilishi ni Yesu mwenyewe kwa kujiita yeye ni Mwana wa Mungu, kwa kuwa ni mwana wa Mungu basi inampa sifa ya Yeye kuwa Mungu. Uungu ni Asili ambayo inarisishwa, hata wewe kama umekuwa mwana wa Mungu basi tukikuita Mungu hatukosei.
 
Ndugu yangu mtoa mada umesema ukweli. Wewe hapo ulipo ni muislamu ila hujijui tu. Hebu soma Quran utaona ilivyosema watu wamebadili maneno ya Mwenyezi Mungu katika Taurati na Injili na wakaweka wanayoyataka wao na kuondoa wasiyoyataka.

In fact ile injili ya kweli na Taurati ya kweli haipingani na Quran. ila iliyobadilishwa ndio inapingana. Injili ya kweli inasema Yesu ni Mtume wa Mungu ila Paulo akabadilisha na kusema Yesu ndio Mungu..

Endelea kusoma ndugu yangu ipo siku Mwenyezi Mungu atakufikisha kwenye ukweli ambao ni uislamu.
 
Hivi inawezekanaje eti Mungu akawa na mwana? au inawezekanaje kukawa na Mungu watatu? Hivi vitu hata akili ya kawaida ya binadamu haikubali.

Yani Yesu awe Mungu kisha auawe msalabani hiyo inawezekanaje?

Na huyu Paulo kwa ujanja aliokuwa nao akawaambia Wakristo wasiulize maswali bali waamini tu; kwa sababu mtu yeyote mwenye akili timamu lazima atauliza tu. Ni mambo yasiyoingia akilini kabisa.
 
Hamjambo!

Kwa upande wangu, Paulo aka Sauli ninamchukulia kama mwandishi mashuhuri aliyepewa nafasi na Dola la Rumi Kwa Siri Ili kubadili uelekeo wa Ukristo na kuufanya uwe upagan.

Paulo/Saul: kiasili ni Myahudi
Raia; Warumi
Elimu: Farisayo, elimu ya juu ya Dini ya kiyahudi.

Paulo hakuwahi kuonana na Yesu popote kipindi Yesu yupo Hai.

Utume wa Paulo ni mission Kwa sababu zifuatazo;

1. Paulo alikuwa adui wa Wakristo wa mwanzoni.
Lakini akapiga U-turn Kwa kile alichosema ametokewa na mtu aliyejitambulisha Kwa Jina la Yesu.

2. Paulo hakuwahi kumwona Yesu popote kipindi Yesu akiwa Duniani.
Hata hoja yake ya kutokewa na Yesu kimiujiza akiwa anaenda Dameski Haina uthibitisho. Ni ushuhuda binafsi. Ni sawa na hawa manabii wakileo wanaosema wametokewa na Yesu.
Hata waliokuwa na Sauli/Paulo hawakumwona Wala kuisikia Sauti ya Yesu ila Paulo anadai alitokewa na kusikia sauti.

3. Hakuna mantiki ya Yesu kumchagua Paulo wakati walikuwepo wanafunzi kumi na Moja waliobakia aliowafundisha Kwa miaka miitatu...
Ndio maana hata wanafunzi wa Yesu walimchukulia Paulo kama Mamluki wa Waroma. Hasahasa Petro.

4. Paulo alienda kinyume na Mafundisho ya Yesu hasa yanayohusu Torati ya Musa.
Paulo ndiye mhusika pekee aliyeipotosha Biblia na kuipa mrengo wa kipagani.
Mafundisho ya sabato
Kumfanya Yesu Mungu
Kuruhusu kula chakula chochote n.k.

5. Wakati huo Injili ilikuwa haijaandikwa. Paulo hajakutana na Yesu kipindi Yesu akiwa Duniani. Paulo anakinzana na wanafunzi wa Yesu. Kwa vyovyote vile mazingira ya Paulo kuwa na mafundisho Halisi ya Yesu uwezekano ni mdogo sana.

6. Paulo ndiye aliyesema Mamlaka zote zinatoka Kwa Mungu. Na watu waheshimu mamlaka. Fundisho ambalo sio kweli. Alikuwa akitetea Dola la rumi Kwani yeye alikuwa raia wa Roma ingawaje alikuwa myahudi.
Sio Kila Mamlaka inatoka Kwa Mungu.
Zipo mamlaka dhalimu, zakishetani, katili na zakinyama ambazo hazitoki Kwa Mungu.

Mafundisho hayohayo ya kikafiri hutumika na Dola nyingi dhalimu kutawala watu kishenzi na kimabavu.

Paulo angekuwa sio Jasusi la kiroma Wala asingesema hayo. Angesema, mamlaka zinazofuata haki zinatoka Kwa Mungu huku zile zinazofanya udhalimu zikitoka Kwa yule muovu.

7.;Paulo ndiye Mhusika pekee aliyeandika Falsafa za kuwafanya wasililizaji na wasomaji wa maandiko yake kuacha kupigania mambo ya mwili na kukazana na mambo ya roho..
Lengo lake ni kuwafanya watu waache kujikita na mambo ya ulimwengu Ili Dola la rumi lizidi kustawi na kutawala bila shida.

Acha nipumzike
Chanzo cha habari zako kiko wapi vinginevyo wewe ni mpagani unayevuta watu waishi kipagani
 
Tumia akili zako za kuzaliwa kujibu hoja hapo nikama unasapoti hoja aliopo mezani kwamba Paulo ndo alianzisha Dini ya Ukuristo huja pangua hoja Hata moja unaleta irrelevant quotation kumbe wewe sio msomi ni mtu wa C&P.
Nachojua a religion so called Christianity ilianzishwa na emperor Constantine. Kulingana na Biblia, Paulo alikuwa mmisionari katika misheni za kuanzisha makanisa
 
Hamjambo!

Kwa upande wangu, Paulo aka Sauli ninamchukulia kama mwandishi mashuhuri aliyepewa nafasi na Dola la Rumi Kwa Siri Ili kubadili uelekeo wa Ukristo na kuufanya uwe upagan.

Paulo/Saul: kiasili ni Myahudi
Raia; Warumi
Elimu: Farisayo, elimu ya juu ya Dini ya kiyahudi.

Paulo hakuwahi kuonana na Yesu popote kipindi Yesu yupo Hai.

Utume wa Paulo ni mission Kwa sababu zifuatazo;

1. Paulo alikuwa adui wa Wakristo wa mwanzoni.
Lakini akapiga U-turn Kwa kile alichosema ametokewa na mtu aliyejitambulisha Kwa Jina la Yesu.

2. Paulo hakuwahi kumwona Yesu popote kipindi Yesu akiwa Duniani.
Hata hoja yake ya kutokewa na Yesu kimiujiza akiwa anaenda Dameski Haina uthibitisho. Ni ushuhuda binafsi. Ni sawa na hawa manabii wakileo wanaosema wametokewa na Yesu.
Hata waliokuwa na Sauli/Paulo hawakumwona Wala kuisikia Sauti ya Yesu ila Paulo anadai alitokewa na kusikia sauti.

3. Hakuna mantiki ya Yesu kumchagua Paulo wakati walikuwepo wanafunzi kumi na Moja waliobakia aliowafundisha Kwa miaka miitatu...
Ndio maana hata wanafunzi wa Yesu walimchukulia Paulo kama Mamluki wa Waroma. Hasahasa Petro.

4. Paulo alienda kinyume na Mafundisho ya Yesu hasa yanayohusu Torati ya Musa.
Paulo ndiye mhusika pekee aliyeipotosha Biblia na kuipa mrengo wa kipagani.
Mafundisho ya sabato
Kumfanya Yesu Mungu
Kuruhusu kula chakula chochote n.k.

5. Wakati huo Injili ilikuwa haijaandikwa. Paulo hajakutana na Yesu kipindi Yesu akiwa Duniani. Paulo anakinzana na wanafunzi wa Yesu. Kwa vyovyote vile mazingira ya Paulo kuwa na mafundisho Halisi ya Yesu uwezekano ni mdogo sana.

6. Paulo ndiye aliyesema Mamlaka zote zinatoka Kwa Mungu. Na watu waheshimu mamlaka. Fundisho ambalo sio kweli. Alikuwa akitetea Dola la rumi Kwani yeye alikuwa raia wa Roma ingawaje alikuwa myahudi.
Sio Kila Mamlaka inatoka Kwa Mungu.
Zipo mamlaka dhalimu, zakishetani, katili na zakinyama ambazo hazitoki Kwa Mungu.

Mafundisho hayohayo ya kikafiri hutumika na Dola nyingi dhalimu kutawala watu kishenzi na kimabavu.

Paulo angekuwa sio Jasusi la kiroma Wala asingesema hayo. Angesema, mamlaka zinazofuata haki zinatoka Kwa Mungu huku zile zinazofanya udhalimu zikitoka Kwa yule muovu.

7.;Paulo ndiye Mhusika pekee aliyeandika Falsafa za kuwafanya wasililizaji na wasomaji wa maandiko yake kuacha kupigania mambo ya mwili na kukazana na mambo ya roho..
Lengo lake ni kuwafanya watu waache kujikita na mambo ya ulimwengu Ili Dola la rumi lizidi kustawi na kutawala bila shida.

Acha nipumzike
Maandiko bila rejea huishia kuwa ni dalili hafifu na uvivu wa kusoma kwa mwandishi husika
 
4. Paulo alienda kinyume na Mafundisho ya Yesu hasa yanayohusu Torati ya Musa.
Paulo ndiye mhusika pekee aliyeipotosha Biblia na kuipa mrengo wa kipagani.
Mafundisho ya sabato
Kumfanya Yesu Mungu
Kuruhusu kula chakula chochote n

Mkuu mbona kwenye maandiko ya manabii wa kale kama Isaya, anataja juu ya mtu atayekuja kama Mungu na ataishi na wanadamu na jina lake ni Emanuel, iweje tena useme mafundisho ya Paulo ndiyo yameandikwa kwa nia ya kumfanya Yesu kuwa Mungu?
 
Maandiko bila rejea huishia kuwa ni dalili hafifu na uvivu wa kusoma kwa mwandishi husika
Mkuu rejea gani unazitafuta hizo ni historical facts kila mwana historia wa theology anajua hilo kwamba Paulo ndo muanzilishi wa ukuristo sio Yesu.
 
Tafuta rejea za hizo fact. Hakuna fact isiyo na rejea. Unless umeamua kujifurahisha ila sio kutoa elimu.
 
Mkuu katika hili tuko pamoja kabisa.

Ni ukweli kwamba mafundisho ya Paulo yanatofautiana sana na yale ya Yesu kama yalivyorekodiwa katika Injili. Yesu alisisitiza sheria, toba, na kumtii Mungu mmoja (Mathayo 5:17–19), lakini Paulo alihubiri kuwa sheria haifai tena (Warumi 6:14, Wagalatia 3:13).

Pia, Paulo hakumjua Yesu kwa maisha, bali anadai kumuona kwenye maono (Matendo 9), jambo linaloacha mashaka. Aidha, mafundisho yake yalienea sana kwa sababu aliungwa mkono na utawala wa Kirumi aliotumia barua zake kueneza Ukristo wa mtazamo mpya kwa mataifa.

Hii ndiyo sababu baadhi ya wachambuzi wanaona Paulo kama muasisi wa "Ukristo wa Kipagani", tofauti na Ukristo wa Yesu wa Kiyahudi.
Soma 1 wakorintho 9:21-24 hayo maswali mnayojiuliza waliuliza hata wayahudi na warumi lakini Paulo mwenyewe alishayajibu
 
Mkuu katika hili tuko pamoja kabisa.

Ni ukweli kwamba mafundisho ya Paulo yanatofautiana sana na yale ya Yesu kama yalivyorekodiwa katika Injili. Yesu alisisitiza sheria, toba, na kumtii Mungu mmoja (Mathayo 5:17–19), lakini Paulo alihubiri kuwa sheria haifai tena (Warumi 6:14, Wagalatia 3:13).

Pia, Paulo hakumjua Yesu kwa maisha, bali anadai kumuona kwenye maono (Matendo 9), jambo linaloacha mashaka. Aidha, mafundisho yake yalienea sana kwa sababu aliungwa mkono na utawala wa Kirumi aliotumia barua zake kueneza Ukristo wa mtazamo mpya kwa mataifa.

Hii ndiyo sababu baadhi ya wachambuzi wanaona Paulo kama muasisi wa "Ukristo wa Kipagani", tofauti na Ukristo wa Yesu wa Kiyahudi.
Yesu alikuwa Mkristo wa Kiyahudi?
Unakataa kuamini ufunuo wa Yesu Kwa Paulo ambao ulikuwa na mashahidi (Kwa sababu alipofuka na kuzimia) Unauamini wa yule aliyepewa pangoni bila kuwa na third party.
Anyway ngoja tupate darsa!
 
6. Paulo ndiye aliyesema Mamlaka zote zinatoka Kwa Mungu. Na watu waheshimu mamlaka. Fundisho ambalo sio kweli. Alikuwa akitetea Dola la rumi Kwani yeye alikuwa raia wa Roma ingawaje alikuwa myahudi.
Sio Kila Mamlaka inatoka Kwa Mungu.
Zipo mamlaka dhalimu, zakishetani, katili na zakinyama ambazo hazitoki Kwa Mungu.

Mafundisho hayohayo ya kikafiri hutumika na Dola nyingi dhalimu kutawala watu kishenzi na kimabavu.

Paulo angekuwa sio Jasusi la kiroma Wala asingesema hayo. Angesema, mamlaka zinazofuata haki zinatoka Kwa Mungu huku zile zinazofanya udhalimu zikitoka Kwa yule muovu.
Hata Yesu alisema ya Kaisari mpe Kaisari. Naye alikuwa raia wa Roma? Ndugu Mtibeli nakushauri piga chini Biblia yote ili uwe huru.
 
Wasabato, waislamu na washika torati wote lazima mchukie mafundisho ya paulo sababu yananyang'anya kujiona mnastahili kuliko wengine.

Kuhusu chakula hata Yesu alipuuza na kusema Chochote kinachoingia tumboni kisha chooni hakiwezi kukufanya najisi, tofauti kabisa na Torati inayosema baadhi vyakula vikiingia kwenye tumbo la mtu vinamfanya kuwa najisi. (Marko 7:19)

Kuhusu Sabato baada ya wayahudi kumsonga sana, Yesu aliaamua kuwaambia Yeye ndiye BWANA wa vyote na ni BWANA wa Sabato pia, Hivyo anaweza kufanya chochote siku inayoitwa ya sabato kwa sababu yeye ndiyo MKUU/LORD wa vyote ikiwemo sabato. (Marko 2:28)
Ndiyo maana yeye na baba yake hawajawahi kupumzika. (Yohana 5:17)

Kuhusu Uungu wa Yesu mwanzilishi ni Yesu mwenyewe kwa kujiita yeye ni Mwana wa Mungu, kwa kuwa ni mwana wa Mungu basi inampa sifa ya Yeye kuwa Mungu. Uungu ni Asili ambayo inarisishwa, hata wewe kama umekuwa mwana wa Mungu basi tukikuita Mungu hatukosei.
Hapo ndipo watu wanajitoa ufahamu nakushindwa kuielewa. Mungu ni Roho safi, Yesu hakuwahi kuchafua Roho yake hivyo moja kwa moja anakuwa anashare Uungu mmoja na Baba kwa Roho mtakatifu. Hivyo Yesu kuwa Mungu Wala sio jambo la kushangaza kwa sababu hicho ni cheo TU Cha utukufu.
"Ili wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako, hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kuamini ya kwamba ndiwe uliyenituma. Nami utukufu ule uliyonipa nimewapa wao, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja; mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wakamilifu katika umoja; ili ulimwengu upate kujua ya kwamba ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi."
(Yohana 17:21-23 - SUV)
 
Paulo ni MTUME SAHIHI.
ANASEMA ALIYAPATA MAFUNUO KWA KUKUTANA NA YESU. NA KUKAA JANGWANI MIAKA MITATU SAUDIA ARABIA AKIWA ANAFUNDISHWA HUKO KIMYAKIMYA KWA MUJIBU WA MAANDIKO YAKO.

POINT ZAKO ZITAKUWA SAHIHI KAMA YESU HAKUFIFUKA. SIO DEAD BEING.
 
Tumia akili zako za kuzaliwa kujibu hoja hapo nikama unasapoti hoja aliopo mezani kwamba Paulo ndo alianzisha Dini ya Ukuristo huja pangua hoja Hata moja unaleta irrelevant quotation kumbe wewe sio msomi ni mtu wa C&P.
Unadhani usomi ndio unsolve kila kitu? Yako mambo hutaweza kuyajua kwa kuwa ni lazima uamini.Imani sio football, mieleka au formula One ni mambo ya rohoni.Imekuwapo tokea enzi na enzi japo tunatofautiana katika imani hizo.Hata walioanzisha elimu za philosopihia bado hawakupata majibu.
 
Back
Top Bottom