Paulo wa Tarso jasusi la kiroma lililopewa misheni ya kubadili mwelekeo wa Ukristo na kuwa upagani

Paulo wa Tarso jasusi la kiroma lililopewa misheni ya kubadili mwelekeo wa Ukristo na kuwa upagani

Mkuu katika hili tuko pamoja kabisa.

Ni ukweli kwamba mafundisho ya Paulo yanatofautiana sana na yale ya Yesu kama yalivyorekodiwa katika Injili. Yesu alisisitiza sheria, toba, na kumtii Mungu mmoja (Mathayo 5:17–19), lakini Paulo alihubiri kuwa sheria haifai tena (Warumi 6:14, Wagalatia 3:13).

Pia, Paulo hakumjua Yesu kwa maisha, bali anadai kumuona kwenye maono (Matendo 9), jambo linaloacha mashaka. Aidha, mafundisho yake yalienea sana kwa sababu aliungwa mkono na utawala wa Kirumi aliotumia barua zake kueneza Ukristo wa mtazamo mpya kwa mataifa.

Hii ndiyo sababu baadhi ya wachambuzi wanaona Paulo kama muasisi wa "Ukristo wa Kipagani", tofauti na Ukristo wa Yesu wa Kiyahudi.

Upo sahihi Kabisa.
Paulo Mimi namchukulia kama Mwandishi wa teolojia ambaye nikisoma habari zake sizipi uzito mkubwa. Na wala sizihesabu kama amri au sheria kutoka kwa Mungu.

Ila naweza kuzitumia kifalsafa, kujua akili za watu wa wakati huo, kujua msimamo na mtazamo wa mwandishi, n.k.
 
Hamjambo!

Kwa upande wangu, Paulo aka Sauli ninamchukulia kama mwandishi mashuhuri aliyepewa nafasi na Dola la Rumi Kwa Siri Ili kubadili uelekeo wa Ukristo na kuufanya uwe upagan.

Paulo/Saul: kiasili ni Myahudi
Raia; Warumi
Elimu: Farisayo, elimu ya juu ya Dini ya kiyahudi.

Paulo hakuwahi kuonana na Yesu popote kipindi Yesu yupo Hai.

Utume wa Paulo ni mission Kwa sababu zifuatazo;

1. Paulo alikuwa adui wa Wakristo wa mwanzoni.
Lakini akapiga U-turn Kwa kile alichosema ametokewa na mtu aliyejitambulisha Kwa Jina la Yesu.

2. Paulo hakuwahi kumwona Yesu popote kipindi Yesu akiwa Duniani.
Hata hoja yake ya kutokewa na Yesu kimiujiza akiwa anaenda Dameski Haina uthibitisho. Ni ushuhuda binafsi. Ni sawa na hawa manabii wakileo wanaosema wametokewa na Yesu.
Hata waliokuwa na Sauli/Paulo hawakumwona Wala kuisikia Sauti ya Yesu ila Paulo anadai alitokewa na kusikia sauti.

3. Hakuna mantiki ya Yesu kumchagua Paulo wakati walikuwepo wanafunzi kumi na Moja waliobakia aliowafundisha Kwa miaka miitatu...
Ndio maana hata wanafunzi wa Yesu walimchukulia Paulo kama Mamluki wa Waroma. Hasahasa Petro.

4. Paulo alienda kinyume na Mafundisho ya Yesu hasa yanayohusu Torati ya Musa.
Paulo ndiye mhusika pekee aliyeipotosha Biblia na kuipa mrengo wa kipagani.
Mafundisho ya sabato
Kumfanya Yesu Mungu
Kuruhusu kula chakula chochote n.k.

5. Wakati huo Injili ilikuwa haijaandikwa. Paulo hajakutana na Yesu kipindi Yesu akiwa Duniani. Paulo anakinzana na wanafunzi wa Yesu. Kwa vyovyote vile mazingira ya Paulo kuwa na mafundisho Halisi ya Yesu uwezekano ni mdogo sana.

6. Paulo ndiye aliyesema Mamlaka zote zinatoka Kwa Mungu. Na watu waheshimu mamlaka. Fundisho ambalo sio kweli. Alikuwa akitetea Dola la rumi Kwani yeye alikuwa raia wa Roma ingawaje alikuwa myahudi.
Sio Kila Mamlaka inatoka Kwa Mungu.
Zipo mamlaka dhalimu, zakishetani, katili na zakinyama ambazo hazitoki Kwa Mungu.

Mafundisho hayohayo ya kikafiri hutumika na Dola nyingi dhalimu kutawala watu kishenzi na kimabavu.

Paulo angekuwa sio Jasusi la kiroma Wala asingesema hayo. Angesema, mamlaka zinazofuata haki zinatoka Kwa Mungu huku zile zinazofanya udhalimu zikitoka Kwa yule muovu.

7.;Paulo ndiye Mhusika pekee aliyeandika Falsafa za kuwafanya wasililizaji na wasomaji wa maandiko yake kuacha kupigania mambo ya mwili na kukazana na mambo ya roho..
Lengo lake ni kuwafanya watu waache kujikita na mambo ya ulimwengu Ili Dola la rumi lizidi kustawi na kutawala bila shida.

Acha nipumzike
Je Ellen G. White alikuwa jasusi wa Dola ya Marekani kugeuza ukristo kuwa Upagani !?
 
Wasabato wengi wanamchukia Mtume Paulo kwasababu maandiko yake mengi yanaipinga sabato/hayatoi umuhimu wa kutunza sabato wala sheria za vyakula 😂😂😂

Sio Wasabato.
Usabato umeanza juzijuzi hauna hata Karne 3.

Paulo anapingwa mpaka na Wanafunzi wa Yesu

Paulo anapingwa mpaka na Wayahudi wa zamani na waleo hii.

Wasabato kumpinga Paulo hakuna athari yoyote kama ambavyo alivyo na anavyopingwa na wayahudi wenyewe.

Ukisikia wayahudi wanaukataa Ukristo, ujue ni ukristo wenye mafundisho ya Paulo.

Paulo anapingwa na Torati ya Musa
 
Ukiwa jasusi hayo ni Mambo ya Kawaida.

Bila ya Paulo pasingekuwa na wakristo wanaoabudu Jumapili.
Bila Paulo wakristo wasingekula Nguruwe na vyakula vingine vilivyokatazwa na Torati.
Bila Paulo kusingekuwa na kunena kwa lugha kihovyohovyo.

Yote hayo ni mambo ya Paulo

Ukimtoa Paulo hakuna Ukristo unaouona hivi leo
Hadi Paulo anakufa hayo yote hayakuwepo kwenye ukristo KWA ushahidi wa kihistoria.
MENGI ni matokeo ya kutoelewa maandiko ya Paulo maana Hata Petro anasema kumuelewa Paulo inahitaji utulivu.

Mkuu Mfano Glossolalia ( kunena KWA Lugha zisizoeleweka) kukisoma matendo 2 tu utagundua na vitu nje ya BIBLIA.
 
Alikuwa mwanafunzi wa mkufunzi Mashuhuri myahudi wa aina Yake Gamaliel kutoka Tarsus modern day Istanbul.

Paulo alikuwa na majigambo kabla ya YESU MUNGU kumtokea akielekea kuwaua wakristo eti yeye myahudi kazaliwa tarsus ametahiriwa.

Ila mwamba kuna kauli Yake naipendaga sana.

IF JESUS IS WITH US WHO THE HELL CAN BE AGAINST US, WHO?

Maamaee Paulo!

adriz

Paulo ni Jasusi ambalo liliwaasi wayahudi.
 
Ndiyo, Paulo alilitesa kanisa (Mdo 8:1-3), lakini mabadiliko yake ya ghafla yalishuhudiwa na wengine. Kwa mfano Anania alithibitisha maono ya Paulo (Mdo 9:10-17), na baadaye kanisa lilimkubali baada ya kushuhudia matunda ya huduma yake (Mdo 9:26-30)

Ni sawa, ni ushuhuda binafsi (Mdo 9:3-7), lakini ulithibitishwa na mabadiliko ya maisha yake, huduma yake, na ufunuo aliopewa – Gal. 1:11-12.

Mitume waliendeleza huduma ya Yesu kwa Wayahudi (Mathayo 10:5-6), lakini Paulo alipewa wito wa kipekee kwa mataifa (Mdo 9:15; Warumi 11:13). Yesu ana mamlaka ya kumchagua anayemtaka kwa kusudi maalum.

Paulo hakupinga Torati; alifundisha kuwa wokovu haupatikani kwa matendo ya torati bali kwa neema kwa njia ya imani (Gal. 2:16). Yesu mwenyewe alisema hakuja kuiondoa torati bali kuitimiliza (Mathayo 5:17), na Paulo alieleza utimilifu huo ni kwa njia ya Kristo (Warumi 10:4).

Mafundisho ya Paulo yaliendana kabisa na yale ya mitume. Ndio sababu walipokutana Yerusalemu, waliungana naye na walimpa mkono wa ushirika (Gal. 2:1-9). Hakuandika kwa kubuni bali kwa ufunuo wa Roho Mtakatifu (1 Wakor. 2:10-13).

Kitabu cha Warumi 13:1-7 kinawalenga Wakristo waliokuwa chini ya utawala wa Rumi. Paulo aliwahimiza kutii mamlaka ili kuepuka mateso yasiyo ya lazima, sio kwa kuhalalisha udhalimu. Isitoshe, Biblia ina mifano mingi inayoonyesha jinsi Mungu anavyoweza kutumia hata tawala dhalimu kwa kusudi lake (Dan. 4:17).

Mafundisho ya Paulo kuhusu kutafuta mambo ya rohoni ndio msingi wa Ukristo (Wakol. 3:1-2). Yesu mwenyewe alisema: “Ufalme wangu si wa dunia hii” (Yoh. 18:36). Paulo hakusema watu wasifanye kazi au kutafuta maendeleo ya kimwili bali alihimiza kutanguliza uzima wa milele.

Pumzika na Mungu akusaidie usiwe jasusi lililopewa misheni ya kufundisha mafundisho ya mashetani.
"Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani.."(1 Tim 4:1-5)

cc: K11 Covax
Ahsante Sana na
Mungu akubariki. Sijui kama amekuelewa lakini.
 
Nakupa shule mtumishi.
Paul ni mfano wa mtu aliyekuwa gizani bila amani akapata Nuru na kutumia nguvu zake zote ili kujaribu kuusahisha Uovu wake.
Paul ni kielelezo cha kwamba yeyeto yule hata awe dhambi kiasi gani anaweza geuka akaiona Nuru halisi.

Hata Leo wapo watumishi wengi sana historia zao za nyuma zilikuwa chafu na aibu Leo ni watumishi wakubwa sana hapa nchini,wapo waliokuwa mashoga,wauaji, makahaba, waganga, wachawi, majambazi wakubwa wameua watu wengi sana kwa bunduki na kwa uchawi pia.
Leo hii ni watumishi wa kweli kabisa na wana nguvu za Mungu ndani mwao wakitumika kama daraja la kuwatoa watu kwenye giza na kuwaleta kwenye NURU.
 
Hadi Paulo anakufa hayo yote hayakuwepo kwenye ukristo KWA ushahidi wa kihistoria.
MENGI ni matokeo ya kutoelewa maandiko ya Paulo maana Hata Petro anasema kumuelewa Paulo inahitaji utulivu.

Mkuu Mfano Glossolalia ( kunena KWA Lugha zisizoeleweka) kukisoma matendo 2 tu utagundua na vitu nje ya BIBLIA.

Unajua Biblia tangu mwanzo mpaka Malaki inaeleweka kabisa.
Shida inaanzia kwa Injili ambapo ukisoma kwa kina, kuanzia kifalsafa, kihistoria, kifasihi, kijasusi unagundua kabisa kuna Jambo halipo sawa.

Paulo,maandishi yake yapo kikafiri, mpango wake ulikuwa ku- neutralise uyahudi kwa kupunguza ukali na uzito wa Sheria za Musa(ambaye inadaiwa alipewa na Mungu).

Paulo ni aina ya watu kama kina Masanja Mkandamizaji.

Alikuwa anataka kufanya utandawazi katika Dini. Kufanya watu wa Dunia waabudu kama wapo katika kijiji kimoja lakini kwa namna ya tamaduni zao.

Mfano, kama unaenda Kwa wala Panya, Paulo angesema Kula Panya sio Kosa, na mtu asiwahukumu ninyi kwa Kula Panya. Ilhali Torati inasema vinginevyo.
Huo ndio Ukafiri na upagani wenyewe.

Kueneza Injili sio kuirahisisha na kuziathiri amri za Mungu. Kwa kisingizio unaeneza Dini.

Paulo anaeleweka sema ukitaka umtetee ndio utajifanya haeleweki.
Lakini yupo Wazi!
Paulo ni Mixed Culture
 
Nakupa shule mtumishi.
Paul ni mfano wa mtu aliyekuwa gizani bila amani akapata Nuru na kutumia nguvu zake zote ili kujaribu kuusahisha Uovu wake.
Paul ni kielelezo cha kwamba yeyeto yule hata awe dhambi kiasi gani anaweza geuka akaiona Nuru halisi.
Paulo hajawahi kuwa gizani.
Paulo ni Farisayo, mtu anayeijua Dini kuliko unavyofikiria, kuliko mimi na wewe na wachungaji wa kileo.
Kusema alikuwa gizani unakosea pakubwa Sana.

Hata Leo wapo watumishi wengi sana historia zao za nyuma zilikuwa chafu na aibu Leo ni watumishi wakubwa sana hapa nchini,wapo waliokuwa mashoga,wauaji, makahaba, waganga, wachawi, majambazi wakubwa wameua watu wengi sana kwa bunduki na kwa uchawi pia.
Leo hii ni watumishi wa kweli kabisa na wana nguvu za Mungu ndani mwao wakitumika kama daraja la kuwatoa watu kwenye giza na kuwaleta kwenye NURU.

Humjui Paulo na KAZI zake?

Nafikiri hujui kwa nini alikuwa anaua wakristo.
 
KAZI ya kujadili kwa hoja au kiimani?
Kiimani unaweza kuamini chochote
Kihoja lazima mantiki iwepo

Neno hujadiliwa kwa neno...

Sasa nimekuwekea namna ambavyo Nabii Isaya amabye aliishi miongo mingi kabla ya uwepo wa Paulo, yeye Isaya alimuita Yesu kama Mungu pamoja na wanadamu...

Sasa nimeshangazwa tu na quote yako kwamba unabii wa Isaya haukumuhusu Yesu...
 
Paul yupo sahihi ni kweli kabisa mamlaka zote duniani utoka kwa Mungu lakini Mungu aingilii utashi wa mwanadamu, mtawala anapomuacha Mungu na kuamua kumfuata shetani Mungu anamfutia kibali cha kuongoza ndio hao wanaoshindwa kwenye uchaguzi,wanaouwawa madarakani nk hawa huwa Mungu amewaondolea ulinzi wake kwao.
Mfano mtawala anauwa watu wasio na hata manati, kwa sababu ya tumbo lake kisa wapo kinyume nae, mtawala kama huyu tayari alishafutiwa kibali ndo maana ya menemene teke na pelesi yaani utawala wako umepimwa hautoshi.
Unapewa madaraka uwaongoze watu na sio uwaue,huna mamlaka ya kutoa uhai wa mwanadamu Hilo jukumu ni la mmoja tu aliyeuweka huo uhai ndani mwake ndie mwenye mamlaka.
Ukiua mtu MUNGU anakufutia kibali machoni pake na machoni pa wanadamu.
 
Hakuna utata Mkuu.
Wanaoleta utata ni wale wanaoziamini.
Utata unakuwa kwa asiye amini au Neno Imani linawapiga chenga.Kwa sisi wakatoliki kuna tunasema "Fumbo la Imani twalitangaza duniani kote" sasa ukianza kuweka questions hiyo sio imani ni mtihani wa kawaida tu.
 
Paulo hajawahi kuwa gizani.
Paulo ni Farisayo, mtu anayeijua Dini kuliko unavyofikiria, kuliko mimi na wewe na wachungaji wa kileo.
Kusema alikuwa gizani unakosea pakubwa Sana.



Humjui Paulo na KAZI zake?

Nafikiri hujui kwa nini alikuwa anaua wakristo.
Paul hakuwa mwanafunzi wa Yesu kabla ndo maana ya gizani hizi ni lugha za kiroho.
Kuwa na elimu ya dini hakukuondolei giza, angekuwa kwenye Nuru asingeuwa watu.
 
Back
Top Bottom