#3..
Mantiki ya Yesu kumchagua Paulo badala ya wanafunzi 12
Yesu alikuja kuokoa waliopotea ,
Paulo alikuwa amepotea ,elimu ya dini aliyoipata na bidii yake katika dini yake yake akiamini anafanya kama Mungu anavyotaka kumbe ,alikuwa chukuzo mbele za Mungu.
Kwa nini Yesu akamchagua Paulo badala ya wengine ..Yesu aonavyo ni tofauti na wanadamu,akili zake hazichunguziki,wema wake ,fadhili zake,rehema zake,upendo wake hauna mipaka...
Hata leo Yesu anawatoa watu katika uuaji,ujambazi,uchawi,ukahaba,uganga wa kienyeji,ulevi.. na wanarudi kumtumikia Yesu,hata watu wa dini nyingine wanabadilika na kuwa watumishi wa Yesu hata ambao mwanzo walikuwa wanamtukana Yesu leo wameokolowe na wanatumika kumuhubiri Yesu...(MANTIKI MANTIKI ni akili zetu sisi wanadamu..ila kwa Yesu yote yanawezekana hata ambayo kwa akili zetu tunafikiri haitakiwi iwe hivyo au isingewezekana).
#4..& 5
Baada ya paulo kujazwa roho mtakatifu ubatizo wa roho..ile Roho ya Mungu ndani ya Paulo ikamfundisha paulo ,pamoja na mafundisho aliyoyapata kuhusu Yesu..akajazwa na nguvu...
Akagundua elimu ya dini aliyokuwa nayo awali ilikuwa ni POTOFU akafahamu.Akaanza kumuhubiri Yesu kwa bidii kubwa bila woga na kwa viwango vikubwa na kwa ufahamu mkubwa kuliko hata wanafunzi wa Yesu.
Mafundisho ya Paulo hayapingani na mafundisho ya Yesu.
Yesu ni Mungu katika utatu mtakatifu Baba Mwana Roho mtakatifu,sabato ni kweli ni amri ya Mungu na Yesu aliitolea ufafanuzi sabato hasa mafarisayo wanafiki waliokaa katika kiti cha Musa waliokuwa na torati lakini matendo yao na mioyo yao ilikuwa mbali na Mungu,wenye usafi wa mavazi na miili na mambo ya mwili ila uchafubwa roho na matendo na walimtega Yesu mara nyingi kuhusu sabato ila wapate kumshitaki na Yesu aliwaumbua. unafiki wao.
#6
Paulo kusema mamlaka zinatoka kwa Mungu,ni kweli mamlaka zinatoka kwa Mungu,Mungu alifanya kila kitu dunia na ulimwengu wote na vyote viujazavyo ulimwengu ..
na Mungu aliumba kila kitu kwa kusudi lake hata wabaya kwa siku ya ubaya.
Vyote ni kazi ya mikono yake..hata Nebuchadnezzer mfalme babeli ,Pilato,na hata SHETANI na hawa wote kuna baadhi walimjaribu Yesu ,Yesu akawajibu haya mamlaka uliyonayo yanatoka kwa baba,ufalme wako unaweza ukagawanywa kwa waamedi na wajemi..MENE MENE TEKELI NA PERESI...Mungu huweza pia kuwanyanganya watu ufalme na kuwapa wengine.
UTII ni mafundisho ya Yesu ,Yesu alikuwa mtii hata mauti..
Tofauti ya Utii wa Yesu na ni kwamba Yesu alikuwa na uwezo wa kuita jeshi la malaika mbinguni na kushinda vita ila alijishusha ..na alikuwa na uwezo hata wa kuvanishi au kukimbia au kujiponya asisikie maumivu..mfano petro alikatwa sikio akaliunga hapo hapo ..immortality au achomwe mkuki udunde au misumari na mijeledi asiumie..lakini alitii
Hata alipoulizwa ni HALALI KULIPA KODI KWA KAISARI..akajibu ya kaisari apewe kaisari..utii kwa serikali kulipa kodi n.k YESU anatifundisha utii
Lakini si kutii maovu..mfano ,Yesu alikemea maovu,(UTII HAIMAANISHI KUTII MAOVU)YESU ALIKEMEA Na kupinga MAOVU.
#7 pigania mambo ya rohoni
ni kweli mwili na roho mara nyingi vinapingana
Tamaa mbaya za mwili na mawazo mabaya ya mwili hupelekea mauti,na ili tuweze kusulubisha tamaa zetu mbaya za mwilini na mawazo yake mabaya tunahitaji...kulinda sana moyo Roho zetu ndipo zitokapo chemichemi za uzima,
ili tusifanye yale tusiyoyataka na kuacha kufanya yale tunayoyataka,mana mwili ni dhaifu japo roho i radhi.
Paulo aliishi kama vile YESU angekuja mapema sana kama kesho tu au anytime soonest anakuja kunyakua kanisa kwa maana ya watu wake watakatifu wake walioko duniani mapema sana kesho tu au mapema mno..
na mambo ya mwilini hayangekusaidia mtu kwenda mbinguni kunyakuliwa kuingia mbinguni.akaona kama ni ubatili mtupu kama mavi akahesabu fahari na tamaa za mwili kama hasara.
Na yeye siyo wa kwanza kuhesabu au kuona fahari na anasa za dunia kama ni ubatili..hata mfalme suleiman/king solomon pamoja na ufahari wake wate ila mwishoni alisema vyote ni ubatili mtupu,..hata ukipata vitu vyote unavyovitamani hapa duniani havitakata kiu ya tamaa mbaya kiu ya uzinzi,self esteem mali na kadhalika...desire self esteem KIU za tamaa za mwili hazitosheki..Maji ya uzima ambayo ukiyanywa hutaona tena kiu ni YESU akiingia ndani yako.
SO VILE alivyoishi Paulo kama vile any time soonest muda wowote anakuja Yesu
Na ndivyo inatakiwa tuishi hata sasa haya mambo ya mwilini tunayoyapigania 24/7 yasitutenge mbali na Mungu ,yasitufarakanishe na Mungu na wanadamu wenzetu.
Itafaa nini mtu akiupata ulimwengu wote na fahari zake halafu akaishia kutupwa jehanamu ya moto wa milele.
Yesu mwenyewe mara nyingi sana amefundisha tusisumbukie mambo ya mwilini,kesho,na tusiweke hazina yetu duniani..Kesho siyo yetu.siri ya kesho yetu au next minute yako anayojua kesho yako ni Mungu ,binadamu hana uwezo wa kuongeza urefu wa maisha yake hata kwa siku moja tu ,kwa kujishughulisha au kwa kufight .