PAYE kwa Wafanyakazi imepunguzwa kutoka 9% hadi 8%. Kodi kwenye marupurupu imeondolewa; hatua hii itaongeza mshahara!

Marupurupu hayakua na kodi miaka mingi tu.

Marupurupu kama hela ya nyumba, chakula, nauli, safari nk hayakua na kodi.

Hiyo ya 8% ni ya watu wa kima cha chini cha laki 270,000.

Tunataka kodi ipungue kwa ambao mishahara wa digiti 7.

Kikubwa zaidi kodi ya ongezeko la thamani ipungue kutoka 18% hadi 15%.

Pili kodi ya kuagiza magari ipungue, watanzania tunaendesha mikweche ya miaka 20, 17 iliyopita. Tunataka kodi ipungue tusukume gari kali za miaka ya karibuni.

Kodi za gari Tanzania ni za ajabu Dunia. Nashukuru yule kamishna wa kodi za nje mlimtimua pale TRA, alikua anamshauri Magufuli ujinga. Mpumbavu sana. Alikua anajipangia kuongeza CIF ya magari ambayo alikua anajua anapoitoa mwenyewe. Nashukuru Magufuli alimshtukia baadae akamuondoa pale.

Haiwezekani watanzania tunaendesha magari ambayo huko kwa wenzetu yamepigwa marufuku. Gari ya miaka 20?

Punguza kodi za gari punguza ajali, punguza uchafuzi wa mazingira, okoa maisha.
 
CCM hawa ambao hawakujipanga wataweza vipi kufanya mambo kama haya?
 
Kodi nyingine msubiri Dr Mwigullu Nchemba bungeni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…