PAYE kwa Wafanyakazi imepunguzwa kutoka 9% hadi 8%. Kodi kwenye marupurupu imeondolewa; hatua hii itaongeza mshahara!

Serikali imepunguza kodi ya PAYE kutoka 9% na sasa itakuwa 8%

Punguzo hili litasababisha mshahara kuongezeka kadhalika kodi kwenye marupurupu imeondolewa.

Kazi Iendelee!
Hapo kwenye marupurupu ndo inamaanisha allowances?

Na hii ni kwa watumishi wa serikali tu au kwa wote? Maana PAYE inakula kwenye kila kitu ya mfanyakazi wa taasisi binafsi
 
Serikali imepunguza kodi ya PAYE kutoka 9% na sasa itakuwa 8%

Punguzo hili litasababisha mshahara kuongezeka kadhalika kodi kwenye marupurupu imeondolewa.

Kazi Iendelee!
Kumbuka hii kitu inaitwa PAYE ( Pay As You Earn )

Hilo punguzo la kodi kama hupati kima cha chini cha mshahara halikuhusu, utaendelea kukatwa 18% na kuendelea.

Ila nimpongeze Rais anaonekana no mkweki na nia ipo.

Maana nadhani kuna wengine deni la bodi limeisha leo baada ya RF ya 6% kuondolewa.

Wafanyakazi masikini kupunguziwa 1% kwenye PAYE.

Madaraja, na Ajira ( Kama itakuwa kweli )

Kwa kuanzia tu, siyo mbaya sana.
 
Kwani hapo aliposema Mimi na nyinyi tutakatwa 8 badala ya 9 anamaanisha mshahara wa raisi ulikuwa unakatwa 9?
 
Bwashee tupeni ajira basi na sisi tusionazo tu enjoy hizo punguzo na nyongeza.
 
Assad alishasema 60% ya watumishi wa umma ni incompetent!

Utakuta MATAGA halijui hesabu hiyo 1% limeona ni punguzo kumbe ni kituko...

MATAGA nawapeni homework tafuteni 1% ya 100k ndio mtajua...
 
Serikali imepunguza kodi ya PAYE kutoka 9% na sasa itakuwa 8%

Punguzo hili litasababisha mshahara kuongezeka kadhalika kodi kwenye marupurupu imeondolewa.

Kazi Iendelee!
Mama kaanza vizuri kwa kuonyesha kuwa anajali masurufu ya mfanyakazi. Punguzo hili la PAYE litawagusa wafanyakazi wote, yaani wa umma na hata wale wa sekta binafsi. Ingawaje punguzo hili la 1% bado ni kiasi kiduchu kuweza kumpa ahueni na unafuu zaidi mfanyakazi aliyenyimwa nyongeza yake kwa miaka mitano mfululizo.

Ahadi ni deni, Mama kaahidi kuongeza, tofauti na mwendazake ambaye alikuwa wala hana nia wala ndoto ya kuongeza. Tuzidi kuomba ya kuwa Mama asipite katika njia za Rai's aliyemtangulia.
 
Unafanya kazi wapi?
Mbona sisi tunakatwa ,isipokuwa tu hela pango,maji na mawasiliano.
 
Hivi nani Ana uhakika na rate ya mapato inayotumika sass hivi, mi kwangu nikifanya calculation napata 18%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…