PC Emanuel Keralyo Waitara, mmoja wa askari aliyeuawa na Hamza

Unasomeka vyema mkuu labda mtu ajitoe ufahamu tu
 
Huyo Askari (pichani) nimemtambua, mara kibao tu alikuwa akilinda pale ABSA [formerly Barclays] Bank pale Slipway Hotel.

Very humble man, sikujua jina lake.

Pole Kwa familia yake, it’s so tragic…. RIP.
 
Kwenye mikutano ya wapinzani tu ndio utawaona wakijitutumua 😁
 
Nilikuwa najiuliza kwanini police walipoteza chanzo cha taarifa kizembe.

Kumbe kuna tuhuma kubwa ilikuwa inafichwa. Hili tukio ni sawa na lile la wale wafanyabishara wa madini waliouwawa pale Sinza tukatangaziwa kuwa ni majambazi na yule afande aliyekuwa amamkaimu afande Tiba.
 
JembeKillo, Mkuu jana wametoka kumpiga dereva wangu wa daladala hapo banana bila sababu, eti wana haraka kwanini anasabisha foleni, walivyojibiwa kuna ajali, kuna gari zimepigana pasi, ndo wanashangaa wakati wameshamuumiza mkono hadi umevimba balaa na kidonda juu. Wanatumia nguvu nyingi, akili kidogo
 
Kuna ulazima wa kubadilisha mitaala ya jeshi la polisi ili liendane na wakati wa sasa.

Hili la sasa, halina tofauti kubwa na lile la Mkoloni tulilo lisoma kwenye vitabu vya Historia. Limejaa vitendo vingi vya uonevu, dhuluma, kubambikia kesi raia wema, kupenda sana rushwa, kutumiwa na dola (ccm) kunyima watu haki zao za msingi, nk.
 
Unadhani bila katiba mpya CCM ikitoka kwa bahati mbaya watakua raia wema wakati 98 ya silaha zote halali na haramu wanamiliki wao na hawajazoea kudhulumiwa wala kubambikwa kesi za ugaidi au kuporwa ushindi. Unakumbuka kuna OcD alipigwa mtama na mgombea wa CCM ili apishe kura ziibiwe. CCM hawajazora kudhulumiwa na vyombo vya mabavu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…