Acheni bangi aisee! PCB ni ngumu mno aisee ni ngumu mno narudia! Pure maths haiwez ingia kwa biology hata kidogo.
Daaaaaaaah nilitaka nipite bila kutia neno lkn hii comment yako imefanya nitamani kushare kitu maana dharau zimeanza.
Tanzania pmj na duniani kote Mathematics ndiyo somo gumu kuliko somo lolote lile (Nasemea mtazamo kiujumla si mtazamo wangu binafsi) haijalishi ni level gani Advance au Ordinary Level.
Hapa tutaenda na takwimu ukifatilia Matokeo ya Ordinary Level F za Mathematics ni nyingi kuliko somo lolote na hata Ufaulu wake Kwa wastani unachezea 17% kushuka chini hapa ni Ukilinganisha na Biology utajua lip ni somo gumu.
Ukienda Advance Level Bado Advance Mathematics ni ngumu kuliko somo lolote lile ukiangalia Ufaulu wake kiujumla bado wastani wake ni mule mule 17% kushuka chini tofauti na Biology na somo jingine.
Swali la kizushi kwako km Unasema Biology ni ngumu kwanini Level zote Mathematics inaoneka kuwa na F nyingi kuliko Biology Jibu Baki nalo tu
Utofauti unakuja wa BIOLOGY na ADVANCE MATHEMATICS upande wa Advance Level unaletwa na Wasomaji wenyewe na Namna uchaguzi wa Combination unavyopatikana.
a) Wengi wao(sio wote) wanaosoma BIOLOGY advance ni wale waliotokana na kupata Ufaulu wa Biology Kwa Mgongo wa Practical (O level Practical zote Uwaga zina Marks 50) na Kwa bahati nzuri Mostly Practical Questions zinakuwa ni rahisi kujulikana kutokana na uandaaji wa Specimens zake. Ss unakuta mtu ana C & B ambavyo ni 44 mpk 74 ambapo 80% ya Ufaulu huo umechangiwa na Practical. Kwa hiyo 35 mpk 40 ya Marks zake za Biology ni Practical Factor Kwa hesabu za Shule ya Msingi (44 - 35, 74 - 40) utapata 9 mpk 34 imetokana na Theory.
Kwa Akil ya kawaida tu unategemea mtu huyu aliepata 9 akapate A ya BIOLOGY Advance ambapo kuna Theory Papers 2 ni kitu ambacho hakuna.
b) Wengi ya watu wanaosoma Advance Mathematics A Level wanajua na kupenda Hesabu na ni miongoni mwa watu wachache waliopatikana kwenye 17% ya Ufaulu wa Somo ilo. Hivyo bhasi C & B za Mathematics O level Uwaga zinakuwa zenyewe Bila kuwa na mchango wa factor yoyote km Ilivyokuwa Kwa Biology ndy maana inaonekana ni Rahisi kupata A ya Mathematics Advance kuliko Biology Kwa sababu wanaosoma Wengi wao wanaijua.
Mathematics ina wenyewe na Wenyewe ndy wanaosoma Advance Mathematics. Ni rahisi kusema Mpira ni rahisi kucheza Kwa kumtazama Neymar Jr, Mesut Ozil , Christian Ronaldo & Messi wakicheza huo Mpira lkn sio Kwa kumtazama Jobe, au Mkwala. Ni Sawa na kusema Maths ni nyepes Kwa kuwaona wachache waliopenda na kufaulu Hesabu wakisoma na kusahau O level kuna 83%+ waliopata F ya somo ilo.
USHAURI:
Uwaga sipendi Mwanafunzi achague Combination baada ya matokeo kutoka Combs Uwaga inapangwa ukiwa form 1 au darasa la 7 then Mwanafunzi uanze kusoma Kwa kufata Chagua lako. Na Mtu aliesoma Sayansi O level akiwa na C flat kwenye Combs yake km hawezi kujitoa Uwaga simshauri kusoma Comb hzo Advance. Kingine Combination za Sayansa A Level Uwaga hayasomwi Kwa Timetable ukifanya hivyo ni rahisi kufeli.