Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Maadam sasa tumeamua kufanya mabadiliko basi ni vema Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ikaletewa watu wapya ili kuondoa manung'uniko.
Mutungi ametumika mara kadhaa kupandikiza migogoro kwenye vyama vya siasa kwa kuyalinda makundi ya wahalifu , huku akisimamia kugawa ruzuku halali ya Cuf kwa rafiki yake Lipumba kwa kutumia akaunti binafsi ya raia , kuna uvumi kwamba Mutungi alipewa 10% ( hajawahi kukanusha ), sasa mtu kama huyu ama Msaidizi wake Sisty Nyahyoza, ambaye hajawahi kuficha mapenzi yake kwa ccm hawafai kuendelea kukalia ofisi hii nyeti ya Umma.
Iko wazi kwamba vyama vya siasa kwa kipindi cha miaka 6 chini ya Utawala wa Magufuli vilipigwa marufuku kufanya shughuli zote za kisiasa kinyume kabisa cha Katiba ya nchi na kinyume cha Sheria za vyama vya siasa , lakini Mutungi akiwa mlezi wa vyama hivyo na huku akijua kwamba sheria za nchi zinavunjwa hakuwahi kukemea , aliamua kuufyata na kunyamaza , kiongozi kama huyu muoga anasubiri nini kwenye ofisi hii?