Pendekezo: Itungwe sheria ya upimaji wa DNA kwa mtoto. Sheria iwe lazima pindi tu mtoto anapozaliwa

Wao waliamini kitanda hakizai haramu, kwaiyo tuwaache kwanza
Hakika ndugu yangu......iliaminika hivyo kwa kuwa wema ulimalaki kwenye jamii na usaliti ulikuwa jambo la aibu na fedheha sio tu kwa mwanamke bali kwenye familia yake nzima..... tofauti na nyakati hizi usaliti na umalaya vimekuwa sifa mpaka mtu muaminifu na mtiifu anazusha mishangao kwenye jamii......

Kitanda hakizai haramu ilikuwa kwa wanandoa kabla hawajawa wana haramu......
 
Mbali na hayo pia heshima ya wake kwa waume zao ilikuwepo ya kiwango kikubwa japo kabambikiwa mzigo was mtu. Ila sahv unabambikiwa mtoto na bado mwanamke anakuoneshea dharau na kiburi
 
Najaribu kuwaza yani wataalamu wetu duniani wameshindwa kutengeneza kipimo portable....kama cha HIV ambapo mtu anaweza kupima kwa risk yake mwenyewe..
Kiwe portable ili upime mwenyewe, ukipata frustration unyonge mtoto na mama πŸ˜‚

Hakiwezi kuwa portable hiki kina matokeo yanayogusa maisha ya watu moja kwa moja.

Kwa usalama wa watu hiki kipatikane kwenye taasisi za afya tu πŸ™πŸ».
 
Hapa ni kuomba Serikali ishushe bei ya hiki kipimo, mtoto akizaliwa me ntapima hata kama sheria haijapitishwa.

Nikigundua si wangu namtaarifu mama mzazi ajue anafanyaje kuhusu mwanae.

Mambo yaende hivyo siwezi pambania maisha kwa nguvu af mwisho wa siku nijikute nazeeka na kwenye ndoa sina mtoto hata mmoja, it’s so sad 😞.
 
Duuuu,. Yani hapo kunauwezekano wa kuongeza tena watoto wengine. Wanaume kazi tunayo ila ukishaona mwanamke ni mzinifu piga chini,. Hakuna ndoa na wazinifu. Ukijifanya unahuruma ndo hivyo
 
Ndugu yangu haya mambo yanatisha Sana.....huwa yanafurahisha tu ukiwa una hadithia lakini yakukute......

Mungu atuepushie mbali
 
Mnayataka? Mtajinyonga
We ukiona huwezi kuyavumilia usipime DNA yahitaji ujasiri.

Ila vifo vya wanawake vitazidi sipati picha vile umehangaikia kuhonga dem since courtship hadi ndoa then mimba unalea af ujue kid si wako hahah πŸ˜€

Yataka moyo ila kweli humuweka mtu huru, wanawake wamezidi kutuonea sasa hii ndy ushindi kwa wanaume we Acha turuke nayo tu.
 
Hili likifungwa litakuwa goli la ushindi
 
Kumbuka kupima DNA ni hela na SI watu wote wanauwezo huo na si watu wote hujifungulia hospitalini
 
Kiwe portable ili upime mwenyewe, ukipata frustration unyonge mtoto na mama πŸ˜‚

Hakiwezi kuwa portable hiki kina matokeo yanayogusa maisha ya watu moja kwa moja.

Kwa usalama wa watu hiki kipatikane kwenye taasisi za afya tu πŸ™πŸ».
Sasa mkuu kama HIV test tunajipima....na zinatoa majibu hasi na chanya why isiyo hyo.

Lengo ni kuweka maisha ya amani....mtu akiua nae auawe,kabla ya kupima hcho kimachine kiwe kinatoa ushauri
 
Sasa mkuu kama HIV test tunajipima....na zinatoa majibu hasi na chanya why isiyo hyo.

Lengo ni kuweka maisha ya amani....mtu akiua nae auawe,kabla ya kupima hcho kimachine kiwe kinatoa ushauri
Kitoe na ushauri tena πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ujinga mtupu mtu kama humwamini.mia kwa mia ulimchukua wa nini ?
Eti mpime kila wakati mtoto akizaliwa ujinga mtupu
Hauhitaji kumuamini au kutomuamini mtu, kinachohitajika ni uhakika.
Kumuoa mtu haina maana unamuamini kwa asilimia 100, unaoa sababu ya vigezo, siyo imani swala la imani wa kumuamini ni Mungu siyo binaadam hata Adam alimuamini Eva akasahau ya Mungu wake.
 
Sasa mkuu kama HIV test tunajipima....na zinatoa majibu hasi na chanya why isiyo hyo.

Lengo ni kuweka maisha ya amani....mtu akiua nae auawe,kabla ya kupima hcho kimachine kiwe kinatoa ushauri
Mkuu sio jambo JEPESI.....unaweza ukajipima nyumbani na majibu ukayakimbia.....kipimo unakirushia t shirt unakifunika unaenda kukitupa kwenye ndoo ya taka......
 
Unaona sawa mkeo kuzaa Nje ya ndoa? (Azae na mwanaume mwingine)?

Kama ni sawa basi ni kwako. Na jamaa atakuja kujua tu hakuna Siri hapa chini ya jua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…