Pendekezo: Itungwe sheria ya upimaji wa DNA kwa mtoto. Sheria iwe lazima pindi tu mtoto anapozaliwa

Mama na dada zako ni DNA machine tosha wakimwangalia tu mtoto wako akizaliwa.

Nimeiona hata kwenye maafa ya watoto kudumbukia majini,wakina jamaa wa jeshi la wokozi(fire)wakitafuta wakishindwa,uwa wanauliza kama shangazi mtu aje hata kama yupo mbali.
 
USA asilimia 40+ ya DNA zina wakataa wababa. Jimbo la Florida baba kabla ya kusaini cheti cha mtoto,lazima huyo mtoto awe amepimwa DNA, mafeminist wa US hii sheria hawaitaki kuisikia.

Bongo huku unakuta demu mmoja anawanaume lukuki, wakumlipia kodi, wakumnulia matolea mapya ya simu na bundle, wakumlipia hela ya vikoba, wakumlipia mchezo wake wa majina matatu, wakumlipia mikopo yake, wakumvalisha nk na wote anawapa papuchi.Halafu mimba anangalia mwenye hela sana ndiye anayempa mtoto.
Dah!!
Hali inatisha ndugu yangu......yaani hali ni mbaya sana......
 
Habari wakuuu..,....

Hali ilipofikia sio kuzuri.......palipofikia tena sio kwa kuoneana aibu.......watu wanalia kwa kutoa milio wengine wanalia kwa vibration na wengine wagugumia ndani ndani......

Siku hizi kitanda kinazaa haramu kwa kuwa wanandoa wameamua kuwa wana haramu......

Kwa hali ilipofikia sio tena kufumbiana macho tuambiane ukweli wa mambo.........

Hii ni dhuruma kubwa inafanyika lakini watu wanaiona ni kawaida.......

Hili pendekezo Tu......

NB;
Mzee wa miaka 62 ajitoa uhai baada ya kugundua wanae watano aliowalea sio wa kwake......imetokea huko Kenya....

Hakuna mfumo duniani utakaozingatia maslahi ya Mwanaume, hata sheria za ndoa za Taifa Kinara wa Democrasia, USA zina sheria kandamizi kwa Mwanaume
 
Ni ile Hali ya kuogopa kuukabili Ukweli, kitu ambacho sisi waafrika kipo ndani ya damu yetu na kutuzunguka ktk Kila sekta ya maisha, Ukweli humuweka mtu huru daima.
Unaukimbia ukweli ambao baadae unakuja kukuua na presha......
 
Hii wanawake ni chungu mno kwao. Ikipitishwa ndoa hazitadumu nyingi mno.

Kuna jamaa mtoto wa baba mdogo mke kazalishwa na ka msela tu na anamsomesha shule za ghalama sana daah Yani siku akijua ataua mtu
Nasi ishatuwia ngumu kumwambia asee
Hivi tunapata wapi ujasiri wa kusema "akija kujua". Kama ameamua kufanya hivyo akiwa anajua kabisa mtoto siyo wa kwake wewe inakusumbua nini? Hapa wanaume tumefeli maana tunatoa maelezo jumuishi tukisahau kwamba kuna akina baba waliooa wanawake wenye mtoto tayari. Sasa ulitaka baba wa hivyo wawatimue hao watoto? Sawa inaumiza kama ni mtoto wa katikati huko ndiye anazaliwa kwa baba mwingine lakini huyu uliyemkuta tayari kazaliwa wala huna uhalali wa kulalamika mkeo maana ulikuwa unajua kabisa. Hivyo ni uamuzi wako uendelee kukaa naye au umtimue, na ukimtimua utakuwa baba la hovyo sana!
 
Nadhani msingi wa mada ni kumbambikizia mimba huku muhusika akiamini kuwa yeye ni biological father hali ya kuwa sio...... waswahili wanasema hiyari yashinda utumwa.....kulea mtoto wa kambo sio jambo baya ikiwa ni utashi wa mtu mwenyewe kwa namna anavyoona inafaa lakini kumwambia kuwa ni mwanaye huku ukijua si mwanaye huo sio uungwana na ni utapeli

Inawezekana kusibadilike kwenye maisha ya kawaida juu ya malezi ya mtoto lakini kwa kiasi kikubwa umeujeruhi moyo wa Baba mlezi.....na hata mtoto.....na haya mambo huwa hayaelezeki mpaka yakukute lakini katika maisha ya kiungwana si vyema kumlaghai mtu aliyeamua kujitoa kwako.....
 
Kabisa, tumepigwa haswa! Yani kupona kwa Mwanaume ni uungwana wa mwanamke!
Kupona kwako kwenye hili ni kwenda na mwanamke kwa machale machale Sana......ingawa si vyema lakini nyakati hizi ushetani umekuwa mwingi kuliko ubinadamu....hivyo basi kuzama kwenye penzi na kuziacha fahamu zako mbali na wewe ni Sawa kujitengenezea jahanam yako na iko siku utajua kulia kilio kikuu na hakutakuwa na wa kukubembeleza......

Siku zote za maisha yako mwanaume mwenzangu BEBA FAHAMU ZAKO.....USILEWESHWE NA MANENO MATAMU KWENYE SAUTI NZURI KAMA KASUKU........NI MTEGO HUO.....
 
Ni vyema sana sana kukaa kimachale, kwa sisi tuliotendwa vibaya na ndoa, mioyo yetu ipo na status ya “auto pilot” yani hata usipodhamiria, inamwangalia mwanamke kwa Machame!
 
Ndio hivyo kaka......dunia na walimwengu ndio wamezifikisha nyoyo zetu hapa ambapo hatukutaka tufike.....
 
Nadhani msingi wa mada ni kumbambikizia mimba huku muhusika akiamini kuwa yeye ni biological father hali ya kuwa sio...... waswahili wanasema hiyari yashinda utumwa.....kulea mtoto wa kambo sio jambo baya ikiwa ni utashi wa mtu mwenyewe kwa namna anavyoona inafaa lakini kumwambia kuwa ni mwanaye huku ukijua si mwanaye huo sio uungwana na ni utapeli

Inawezekana kusibadilike kwenye maisha ya kawaida juu ya malezi ya mtoto lakini kwa kiasi kikubwa umeujeruhi moyo wa Baba mlezi.....na hata mtoto.....na haya mambo huwa hayaelezeki mpaka yakukute lakini katika maisha ya kiungwana si vyema kumlaghai mtu aliyeamua kujitoa kwako.....
Kikubwa nafikri tusifanye generalization kwamba wanaume wote wanabambikiwa, wengine wamekubali kuishi na huyo mtoto kwa mapenzi makubwa tu waliyonayo kwa mama. Hii inatokea kama umemkuta my wife mke wangu yuko na mtoto! Wala haina sababu ya kumbagua maana ulijua kabisa tangu mwanzo kwamba huyo siyo wa kwako. Mama mdogo alijichanganya kwangu eti nagharamika kusomesha mtoto ambaye siyo wa kwangu akasahau na yeye kama alienda kwenye ndoa akiwa na mtoto wa mwanaume mwingine, nikamlipua ikabidi awe mdogo kama Piriton. Sijui alidhani tulivyokuwa wadogo tulikuwa hatujui.
 
Nadhani hujaelewa mada........

Msingi wa mada ni kubambikiwa........

Kuna watu wanaoa mwanamke mwenye mimba huku akijua kuwa mimba si yake.....na kuna watu wanaoa mwanamke ana mtoto mchanga huku akijua mtoto si wake.....Sisi tunachotaka mtu afanye jambo kwa utashi wake na sio kumtapeli........ mwanaume Kwa hiyari yake anaweza kulea hata watoto kumi......

Hata wewe huyo unayemlea ni hiyari yako hujabambikiwa
 
Back
Top Bottom