Pendekezo: Kiswahili kitumike kama lugha ya kufundishia ngazi zote za elimu, ili tukomboke kifikra

Pendekezo: Kiswahili kitumike kama lugha ya kufundishia ngazi zote za elimu, ili tukomboke kifikra

Ushora Ndago,
..Nakubaliana na wewe kwamba Kiswahili pia kinatakiwa kupewa msukumo.

..Sasa hivi kumeibuka kundi kubwa la vijana waliohitimu masomo lakini hawazungumzi Kiswahili fasaha.

..Vilevile wako wanaozungumza Kiswahili fasaha lakini uwezo wao wa kujenga hoja na kuwasiliana ni mdogo ukilinganisha na kiwango cha elimu walichohitimu.

..Kwa ujumla tunatakiwa tuboreshe ufundishaji wa KISWAHILI na KIINGEREZA na iwe " must " kwa wahitimu wetu kuzungumza lugha hizo kwa UFASAHA.
 
Naiunga mkono hi hoja! Kwa yale maneno ya kitaalamu ya vitu au vyombo viandikwe kwa jina hilo hilo kwa matamshi yetu. Siyo dhambi. Hi dhana ya wataalamu wetu wa Kiswahili kukaa chini na kutafuta neno la kiswahili mfano computer iitwe kompyuta lakini nsikilizie majina yanayotengezwa mapya ni vurugu tupu. MASSHELE,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila shaka mnataka kujifungia ndani ya box. Mawazo kama haya kutolea na watu ambao hawajawahi kutoka nje tz. Sisi tunaoishi nchi za watu tunapata sana tabu na Kiinglishi chetu cha kuunga unga. I wish tungekuwa tunatumia Kiinglishi in our daily communication from home to the business.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani tatizo kubwa hapa ni kudhani kuwa ili mtu ajifunze lugha ni lazima lugha hiyo itumike kama lugha ya kufundishia. Advocates wa Kiswahili wanachosema ni kuwa tutumie Kisw kama lugha ya kufundishia lakini pia Kiibgereza kifundishwe vizuri kama lugha kwa wanafunzi wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mb
Unawafundishia kiswahili alafu baada hapo utawatumiaje wakati huna teknolojia

Sent using Jamii Forums mobile app
mbona wewe huna akili kabisa kwani technolojia haiwezi fundishwa kwa kiswahili jinga kweli wachina wanajua kiingereza? mbona wameenda mwezini

hakuna utumwa mbaya kama wa fikra afadhali wa kipato
 
Nanye Go, Mawazo mawili:
1. Kiingereza kime-dominate
2. Kuna watu hawajui Kiswahili kwa ufasaha.

My take
1.Suala la msingi la kujiuliza Kiingereza kimedominate positively au negatively. Tutasemaje Kiingereza kimedominate wakati wanafunzi na hata walimu ni victims wa lugha hii katika mchakato wa kufundisha na kujifunza?
2. Kwamba kuna watu hawajui Kiswahili kwa ufasaha - tulinganishe idadi hiyo na wale tusiojua Kiingereza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani tatizo kubwa hapa ni kudhani kuwa ili mtu ajifunze lugha ni lazima lugha hiyo itumike kama lugha ya kufundishia. Advocates wa Kiswahili wanachosema ni kuwa tutumie Kisw kama lugha ya kufundishia lakini pia Kiibgereza kifundishwe vizuri kama lugha kwa wanafunzi wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app

..hizi hoja zinatokana na " frustrations " za baadhi ya viongozi ambao wana changamoto ya kuwasiliana kwa Kiingereza.

..Ukiangalia kwa umakini utagundua kuwa wahitimu wetu na idadi kubwa ya waTz hawazungumzi Kiswahili fasaha.

..Kwa hiyo hata hicho Kiswahili kinachopigiwa upatu nacho kina changamoto kubwa na nyingi.

..Kwa ujumla tunatakiwa kuboresha ufundishaji wa KISWAHILI na KIINGEREZA. wahitimu wetu wanatakiwa wazungumze lugha hizo mbili kwa ufasaha.
 
kwani ukiwa hujui lugha ambayo si asili yako ni dhambi? ujue kiingereza kushinda kiswahi ili iweje kama naweza broken english tatizo iko wapi? wewe mtumwa wala huelewi usemalo
 
Bila shaka mnataka kujifungia ndani ya box. Mawazo kama haya kutolea na watu ambao hawajawahi kutoka nje tz. Sisi tunaoishi nchi za watu tunapata sana tabu na Kiinglishi chetu cha kuunga unga. I wish tungekuwa tunatumia Kiinglishi in our daily communication from home to the business.

Sent using Jamii Forums mobile app
Haita kaa itokee hata siku moja asilani abadani watanzania milioni 55 wote waje kuishi huko uliko wewe na wenzio wachache mnaopata tabu kuongea kiingereza ! Idadi kubwa tutabaki Tanzania tukiwasiliana kwa lugha yetu tamu ya kiswahili ! 😎
 
kwani ukiwa hujui lugha ambayo si asili yako ni dhambi? ujue kiingereza kushinda kiswahi ili iweje kama naweza broken english tatizo iko wapi? wewe mtumwa wala huelewi usemalo

..kujua lugha mbalimbali siyo utumwa.

..kwa mfano, baba yangu anazungumza lugha ya kabila letu na lugha za makabila ya jirani. Je, yeye ni mtumwa?

..au alipojifunza Kiswahili ambayo siyo lugha yake ya asili, unaweza kumuita mtumwa?

..hoja yangu ni kwamba kama tunafundisha miaka 7 kwa kutumia Kiswahili basi wahitimu lazima wazungumze lugha hiyo kwa ufasaha.

..Na kama sekondari mpaka chuo kikuu ni Kiingereza basi waliohitimu ktk ngazi hizo lazima wazungumze Kiingereza fasaha.
 
JokaKuu,
na mimi sikumaanisha kujua lugha fulani ni dhambi nilichokata ni kuwashambulia watanzania ambao hawajui kiingereza vizuri hilo ndo shida yangu na wewe na wengine wenye mawazo kama yako. mnataka kuwaaminisha watanzania kuwa kama hajui kiingereza basi si lolote katika uwanja wasomi
 
Chakulinga,
Kijijini nilikotoka mimi walimu shule za msingi wanabidi kuongea lugha ya wenyeji ili kuweza kuwasiliana na wanafunzi,akija mwalimu asiyefahamu hiyo lugha anapata changamoto sana kufundisha watoto, na huko ukiwauliza itumike lugha gani kufundishia watatamani ile lugha wanalifahamu.

Sijui lini tutaanza kuelewana,mfumo upo tuutumie huo na lugha iliyopo na inayotumika sasa.
 
Hivi hujui kuwa kuna wanafunzi wa Kisw wanapata PhD na wamesoma vitabu vya Kiingereza? Hata Wajerumani, Wajapani na Wachina wanasoma vitabu vya Kiingereza na lugha nyingine lakini wanatumia lugha zao kama lugha za kufundishia.

Sent using Jamii Forums mobile app

Tatizo ni hapo hiyo lugha ya kiingereza umeijuaje kama huisomi? Naona mnajichanganya. Wenzetu wana printing house za kuchapicha vitabu na kuna vitabu wanatafsiri kwa lugha zao wanaingia mkataba na watuzi na publishers.

Sasa wewe unaongelea kusoma kwa kiingereza wakati huohuo hufundishwi sasa hiyo elimu itakuwa ngumu kwa kiasi gani?. China sasa hivi watu wengi sana inabidi waanze tena kujifunza kiingereza na matajiri inabidi wapeleke watoto wao nje ukienda Canada na US wanafunzi wanaoongoza kwa idadi ni wachina.

Sisemi kwamba tusijifunze lugha yetu lakini nachosema ni makosa makubwa kuacha kiingereza. Kuna mambo mengi sana inabidi yafanyike ili tuondoe kiingereza na itakuwa ngumu kwa elimu ya juu kusoma Tanzania maana materials mengi ya kusoma ni ya lugha nyingine
 
Kiswahili sio lugha ya sayansi wala ugunduzi. Ni lugha ya kawaida ya mawasiliano.

Watu wengi wanadhani kiswahili kikiwa lugha ya kufundishia itakuwa rahisi. Wanakosea sana sana.

Hebu jiulize, kwanini watoto waoongea kiswahili muda wote bado wanafeli somo la kiswahili?

Pili, jiulize, kwa wale waliosoma masomo ya sayansi, ni neno gani la kisayansi unalolijua kwa kiswahili?

Ukichunguza masomo ya Hesabu, physics, biology, chemistry nk 98% ya maneno yanayotumika hayana kiswahili chake kilicho tayari kwa matumizi. Hii ina maana wataalam wataanza kutafuta maneno mbadala na hapo ndipo kiswahili kinarudi kuwa kigumu kuliko hicho kiingereza ambacho 70% unacho tayari.

Angalia ugumu wa maneno mapya yaliyoingizwa kama tafsiri? ya kiingereza kuja kiswahili kwa baadhi ya maneno. Password..nywila..[emoji3] its a joke.

Nashindwa kupata picha ya hesabu zitakuwaje kwa maneno kama
..integrate
..differentiate
..tabulate
..calculate
..manipulate
..differential equation
Hyperbolic equation
Formula
Formulate
nk.

Wao wakitaka kuwe na sylubus ya kiingereza na ya kiswahili na ziwepo shule na vyuo watu wachague ndipo watu watajua makosa yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wyatt Mathewson,
Ukiangalia hao waliyosoma wengi wao pamoja na elimu zao ambapo walisoma kwa kutumia kiingereza lakini bado hawawezi kukiongea hicho kiingereza,kwahiyo mkuu huna haja ya kukataa kuwa kuna watoto hushindwa na masomo ya secondary kwa kikwazo cha lugha ya kiingereza na wengine wanasoma kiujanja ujanja tu ila lugha ya kufundishiwa inawapiga chenga.
 
n

na mimi sikumaanisha kujua lugha fulani ni dhambi nilichokata ni kuwashambulia watanzania ambao hawajui kiingereza vizuri hilo ndo shida yangu na wewe na wengine wenye mawazo kama yako. mnataka kuwaaminisha watanzania kuwa kama hajui kiingereza basi si lolote katika uwanja wasomi

..kuna mambo hayako sawa tunatakiwa kuyarekebisha.

..zamani kulikuwa na tatizo la waTz kutokuwa fasaha ktk kiingereza.

..leo tatizo limeongezeka na kuhamia mpaka kwenye Kiswahili.

..tatizo lingine ni mfumo wetu wa elimu unazalisha wahitimu ambao hawakidhi mahitaji ya soko la ajira, wako kinadharia zaidi.
 
Back
Top Bottom