Pendekezo: Kitengo cha Upelelezi kitolewe Polisi

Pendekezo: Kitengo cha Upelelezi kitolewe Polisi

Tanzania Bureau of Investigation(TBI) ipo miaka mingi sana, ukienda ghorofa ya Saba wizara ya mambo ya ndani Dar utawakuta hapo wamejaaa na kazi wanapiga sanaaa.
Wa polisi ni ma CID, na wao wanafanya kazi nzuri sana.
Kuwepo na idara ya kusajili "Private bureaus of investigation"
Kama zile Private security co.
 
Nchi ya wasanii hii ccm na serikali yake wanafaidika na mifumo mfu isiyo na tija kwa dunia ya sasa.

Wanajua sana Ila wanafanya makusudi kwa kudumisha utawala wa kiimla,jeshi la polisi,mahakama,katiba tume huru vinakasoro nyingi tu,hata tiss IPO kisiasa tu haipo kiuchumi .

Kwa kweli si idara ya upelelezi tu inayotakiwa kufumuliwa ila yanatakiwa mageuzi makubwa sana kiuchumi,kisiasa,kiusalama na kijamii na hapo ndio maendeleo ya kweli yatapatikana na si usanii unaoendelea sasa.
 
Unapotaka kuanzisha kitu ili hali kitu hicho unacho lazima ufanye monitoring and evaluation ujue kwamba kwa mwaka Kuna kesi ngapi? Zimekamilika ngapi? Zimeenda mahakamani ngapi? Zimekosewa ngapi? Zimeshindwa ngapi? Zimeshinda ngapi? Na Aina gani ya makosa yamefanikiwa zaidi? Na Aina gani ya makosa hayajafanikiwa Zaid?

Baada ya kujua hayo ndio utajua upungufu au uimara wa sehemu husika na kujua ufanye Jambo gani ili kuboresha sehemu husika

Na kuboresha hakuihtaji kubadili mfumo weka vifaa Bora,lipa maslah stahk kwa wapelelezi,wafanyekaz kitaalamu na sio shinikizo,na weka muda sahihi pindi offense inapotokea tu ndani ya siku kadhaaa teyar kila kitu kishakamilika.

Na tatizo jingne sio polisi tu hata mahakama wanaharibu kesi kwa mapungufu madogo ya polisi na kesi nying huwa hvyo
 
Kitendo cha Polisi na waendesha mashtaka wa serikali kuendelea kupeleka watuhumiwa mahakamani bila ya kuwa na ushahidi wa kutosha dhidi ya tuhuma zao ni kuidharau mahakama?

Kwanini wapeleke watu mahakamani kisha waseme kuwa upelelezi haujakamilika?
 
Ukweli mtupu kwa asilimia 100

Inakuwaje mathalani kwa kesi ya kutakatisha pesa na uhujumu uchumi ya Kabendera, hivi sasa ni miezi sifa, kila ifikapo mahakamani Polisi wanadai kuwa upelelezi haujakamilika!

Inaonekana kuwa ni "staili" mpya iliyobuniwa na Polisi, kuwabambikia wananchi kesi zisizo na dhamana, huku wakiendelea kumsotesha mahabusu mtuhumiwa wakidai kuwa ushahidi haujakamilika

Mahakama inapaswa izitupilie mbali kesi hizo za "kubambika" wanazoleta hao Polisi kwa nia ya kuwakomoa watuhumiwa, huku wakijua fika kuwa hawatashinda kesi hizo hapo mahakamani
 
Ukweli mtupu kwa asilimia 100

Inakuwaje mathalani kwa kesi ya kutakatisha pesa na uhujumu uchumi ya Kabendera, hivi sasa ni miezi sifa, kila ifikapo mahakamani Polisi wanadai kuwa upelelezi haujakamika!

Mahakama inapaswa izitupilie mbali kesi hizo za "kubambika" wanazoleta hao Polisi kwa nia ya kuwakomoa watuhumiwa, huku wakijua fika kuwa mashitaka hayo hayana dhamana
Sheria haisemi hivyo bali imeweka utaratibu wa kushughulikia jinai mkuu
 
Mahakama nayo imekubali kuendeshwa na siasa. Hawafuati mongozo tena
Kitendo cha Polisi na waendesha mashtaka wa serikali kuendelea kupeleka watuhumiwa mahakamani bila ya kuwa na ushahidi wa kutosha dhidi ya tuhuma zao ni kuidharau mahakama? Kwani nini wapeleke watu mahakamani kisha waseme kuwa ushahidi haujakamilika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom