Pendekezo: Kitengo cha Upelelezi kitolewe Polisi

Pendekezo: Kitengo cha Upelelezi kitolewe Polisi

Kwamba unaweza kumpeleka mtu mahakamani bila ya kuwa na ushahidi wa kutosha?
Sheria haiwezi kusema hivyo. Kumbuka kama hakuna kesi ya kupelekwa mahakamani hata hizo mahakama hazitakuwa na umuhimu wa kuwepo, hata mahakimu/Majaji hawataajiriwa mkuu. Sheria zote zinasisitiza kupeleka watuhumiwa mahakamani ndiyo maana zinasema ndani ya masaa 24.
 
Tukikaa nao ili tukamilishe ushahidi mnalazimisha tuwapeleke mahakamani,.dawa.ni moja tu ML
Kitendo cha Polisi na waendesha mashtaka wa serikali kuendelea kupeleka watuhumiwa mahakamani bila ya kuwa na ushahidi wa kutosha dhidi ya tuhuma zao ni kuidharau mahakama? Kwani nini wapeleke watu mahakamani kisha waseme kuwa ushahidi haujakamilika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukikaa nao ili tukamilishe ushahidi mnalazimisha tuwapeleke mahakamani,.dawa.ni moja tu ML
Yote mawili ni kosa kisheria na kama mahakama ingekuwa imara isingeendelea na hizo kesi zinazopelekwa mahakamani bila ya kuwa na ushahidi toshelevu au watuhumiwa walikamatwa na kushikiliwa na Polisi kinyume na sheria.
 
Sheria haisemi hivyo bali imeweka utaratibu wa kushughulikia jinai mkuu
Sheria yako wewe kada wa Lumumba ndiyo haisemi hivyo

Hivi inakuwaje mahakama iendelee ku-entertain kesi hizo, huku ikijulikana wazi kuwa Polisi wamembambikia mtu huyo hiyo kesi kwa lengo tu la kumkomoa?
 
Sheria zote zinasisitiza kupeleka watuhumiwa mahakamani ndiyo maana zinasema ndani ya masaa 24.
Pia kuna sheria ya kukamata mtu, huwezi kukamata mtu kama huna ushahidi wa kutosha na hizo saa 24 zimewekwa kuifanya Polisi isikamate watu hovyo.

Maana yake ukimkamata mtu ni LAZIMA uwe na ushahidi umpeleke mahakamani ama kama huna umwachie ndani ya hizo saa 24. Sawa wakili msomi?
 
Sheria yako wewe kada wa Lumumba ndiyo haisemi hivyo

Hivi inakuwaje mahakama iendelee ku-entertain kesi hizo, huku ikijulikana wazi kuwa Polisi wamembambikia mtu huyo hoyo kesi kwa lengo tu la kumkomoa?
Mkuu Mahakama itajuaje kama Polisi wamembambikia kesi mtu bila kuisikiliza hiyo kesi? Pia sheria inaruhusu kuishitaki Serikali kama umeonewa na Polisi kwa kubambikiwa kesi. Acha siasa mkuu.
 
Mkuu Mahakama itajuaje kama Polisi wamembambikia kesi mtu bila kuisikiliza hiyo kesi? Pia sheria inaruhusu kuishitaki Serikali kama umeonewa na Polisi kwa kubambikiwa kesi. Acha siasa mkuu.
Unaongea mambo yanayopingana na sheria. Ili mtu aseme kabambikiwa kesi si lazima kwanza kesi ianze kusikilizwa, sasa haisikilizwi kwa kuwa polisi wanasema "Ushahidi haujakamilika". Mtu atasemaje kuwa amebambikiwa kesi kama kesi yenyewe haisikilizwi kwa kuwa ushahidi haujakamilika?

Jambo jingine huwezi kuishtaki serikali kabla kesi haijaisha. Sasa kama kesi haisikilizwi itakwisha lini ili serikali ishitakiwe kwa kubambika kesi raia wake?
 
Pia kuna sheria ya kukamata mtu, huwezi kukamata mtu kama huna ushahidi wa kutosha na hizo saa 24 zimewekwa kuifanya Polisi isikamate watu hovyo.

Maana yake ukimkamata mtu ni LAZIMA uwe na ushahidi umpeleke mahakamani ama kama huna umwachie ndani ya hizo saa 24. Sawa wakili msomi?
Hahaha Wakili msomi unanisikitisha sana unaposema eti mtuhumiwa anakamatwa tu ukiwa na ushahidi wa kutosha! Ingekuwa hivyo then kusingekuwa na haja ya upelelezi baada ya mtuhumiwa kukamatwa. Sijawahi ona ama kusikia hata huko mataifa makubwa yaliyoendelea kama mtuhumiwa hukamatwa tu na kufikishwa mahakamani na kesi ikaanza kusikilizwa hasa kwenye kesi hizi za Money Laundering na Cyber Crime.
 
Unaongea mambo yanayopingana na sheria. Ili mtu aseme kabambikiwa kesi si lazima kwanza kesi ianze kusikilizwa, sasa haisikilizwi kwa kuwa polisi wanasema "Ushahidi haujakamilika". Mtu atasemaje kuwa amebambikiwa kesi kama kesi yenyewe haisikilizwi kwa kuwa ushahidi haujakamilika?

Jambo jingine huwezi kuishtaki serikali kabla kesi haijaisha. Sasa kama kesi haisikilizwi itakwisha lini ili serikali ishitakiwe kwa kubambika kesi raia wake?
Hali ndiyo hiyo sasa na sheria ndiyo hizo! Unashauri nini sasa Wakili Msomi.
 
Sijawahi ona ama kusikia hata huko mataifa makubwa yaliyoendelea kama mtuhumiwa hukamatwa tu na kufikishwa mahakamani na kesi ikaanza kusikilizwa hasa kwenye kesi hizi za Money Laundering na Cyber Crime.
Kwanza ni kwa nini kesi hizo za utakatishaji fedha na makosa ya kimtandao zisiwe na dhamana?

Kesi ili iwe mahakamani ni lazima kuwe na ushahidi na kuendelea kumshikilia mtu kwa kisingizio kwamba ushahidi haujakamilika ni kinyume cha sheria.
 
Back
Top Bottom