Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Viongozi wa Tanzania waliopo na waliopita wamepachika au wamepachikiwa majina yao kwenye mali na miradi ya nchi, hili jambo halina maana wala tija yoyote ile.
Kwa mfano, si sawa kwa stendi ya mabasi ya kimataifa ya Mbezi Luis, uwanja wa soka wa Taifa, viwanja vya ndege, madaraja, vivuko, shule, hospitali na mali nyingine za Taifa kupewa majina ya viongozi, wawe hai au wamekufa. Hii ni kwa sababu mali za umma zimegharamiwa na kodi za wananchi, hivyo si haki kuweka jina la kiongozi, eti kwa vile tu vitu hivyo vilijengwa wakati mhusika akiwa madarakani, wala hata hakutumia hela za mfukoni mwake. Huku ni kukengeuka, halafu ni nani anayependekeza majina hayo na kwa mchakato upi?
Kusimamia ujenzi wa kitu chochote katika nchi haimaanishi kwamba mhusika anayo hati miliki ya jina lake kupachikwa kwenye huo mradi. Hii ni kwa vile pesa zilizotumika kujenga miradi ya nchi si zake binafsi, ni hela za umma. Majina yanayopaswa kuitwa miradi hiyo yawe majina ya maeneo ulipo mradi huo, mfano uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, daraja la Busisi, barabara ya Mwendokasi, mradi wa umeme Kinyerezi, nk.
Lakini mali za umma kama stendi ya Mbezi Luis kuiita jina la mtu mmoja ni sawa na ubaguzi uliojaa ubinafsi. Napendekeza stendi ya Mbezi iitwe "Stendi ya Mabasi ya Mikoa ya Mbezi Luis". Jambo hili linaweza kuondoa nuksi, laana, na mikosi itokanayo na kutumia jina la mtu mmoja tu tena ambaye hajawahi kuwa mkazi wa eneo hilo na wala hajawahi hata kupanda mabasi yenyewe. Uwanja wa Taifa wa soka urudishiwe jina lake la awali na jina la Nyerere liondolewe kwenye uwanja wa ndege, urudi kuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam.
Kama tunataka kuwaenzi marehemu wetu au hata viongozi waliopo, basi ni rahisi sana. Majina yao yawekwe kwenye ofisi za vyama vyao, kwa mfano, badala ya kuita ofisi ya chama Kisiwandui, basi iitwe "Ofisi ya Magufuli Kisiwandui".
Naomba kuwasilisha.