Pendekezo: Majina ya viongozi yaondolewe miradi ya umma

1. John Fitzgerald Kennedy (JFK) International Airport - USA
2. General Charles De Gaulle Airport - France
3. Hastings Kamuzu Banda Boulevard - Malawi
4.
Sijui niendelee?
Msiige , hawa wa Tanzania hawafai
 
1. John Fitzgerald Kennedy (JFK) International Airport - USA
2. General Charles De Gaulle Airport - France
3. Hastings Kamuzu Banda Boulevard - Malawi
4.
Sijui niendelee?
Hao ni watu waliozifanyia nchi zao mambo makubwa, sasa John Kijazi au Mfugale wamefanya nini kikubwa katika taifa hili
 
Uwanja wa ndege wa kimataifa Dar es Salaam haukutoa hela ya ujenzi, hela ametoa mama Samia mwenyekiti wa CCM hivyo hauwezi kumchagulia majina. Wewe tafuta hela zako uweke majina unayoyataka, hakuna atakaye kuuliza.
 
Ubungo, Mbezi na Kimara inawezekana ni majina ya watu, lakini hakuna mtu mwenye hakimiliki wa majina hayo hivyo wenyewe ni wakusadikika.
 
Mamluki njooni mnitukane na huku
 
Umewapandisha hasira, sasa stesheni hazitakuwa za miji husika stesheni na treni zitaitwa majina ya yao viongozi wa CCM.
 
Hakika ni kujikweza kwa hali ya juu mali za umma kuitwa kwa majina ya watu. Kama kiongozi kasimamia mradi ilikuwa ni jukumu lake na alilipwa kwa kazi hiyo. Huu ni ugonjwa wa cancer kwa wanasiasa wanaopenda kujikweza kwa sababu wataalamu hawana kasumba hiyo.
 
Ni utamaduni tu na sizan km kuna ubaya
Ziwa victoria ni jina la mtu
Mtaa wa livingston ni jina la mtu
Bibi titi ni jina la mtu
Forodhani jina la mjukuu wa mfalme

Shida watanzania tumechanganyikiwa na huu ugumu wa maisha na mdororo wa uchumi ad unasababisha tunashindwa kuwaza mambo makubwa tunawaza mawazo ya kitoto sasa jina la raisi au kiongozi likitumika km utambulisho lina madhara gan au linapunguza nini ktk huo mradi na ata sku akitoka itabakia km kumbukumbu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…