Pendekezo: Majina ya viongozi yaondolewe miradi ya umma

Viongozi wa Tanzania waliopo na waliopita wamepachika au wamepachikiwa majina yao kwenye mali na miradi ya nchi, hili jambo halina maana wala tija yoyote ile.

Kwa mfano, si sawa kwa stendi ya mabasi ya kimataifa ya Mbezi Luis, uwanja wa soka wa Taifa, viwanja vya ndege, madaraja, vivuko, shule, hospitali na mali nyingine za Taifa kupewa majina ya viongozi, wawe hai au wamekufa. Hii ni kwa sababu mali za umma zimegharamiwa na kodi za wananchi, hivyo si haki kuweka jina la kiongozi, eti kwa vile tu vitu hivyo vilijengwa wakati mhusika akiwa madarakani, wala hata hakutumia hela za mfukoni mwake. Huku ni kukengeuka, halafu ni nani anayependekeza majina hayo na kwa mchakato upi?

Kusimamia ujenzi wa kitu chochote katika nchi haimaanishi kwamba mhusika anayo hati miliki ya jina lake kupachikwa kwenye huo mradi. Hii ni kwa vile pesa zilizotumika kujenga miradi ya nchi si zake binafsi, ni hela za umma. Majina yanayopaswa kuitwa miradi hiyo yawe majina ya maeneo ulipo mradi huo, mfano uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, daraja la Busisi, barabara ya Mwendokasi, mradi wa umeme Kinyerezi, nk.

Lakini mali za umma kama stendi ya Mbezi Luis kuiita jina la mtu mmoja ni sawa na ubaguzi uliojaa ubinafsi. Napendekeza stendi ya Mbezi iitwe "Stendi ya Mabasi ya Mikoa ya Mbezi Luis". Jambo hili linaweza kuondoa nuksi, laana, na mikosi itokanayo na kutumia jina la mtu mmoja tu tena ambaye hajawahi kuwa mkazi wa eneo hilo na wala hajawahi hata kupanda mabasi yenyewe. Uwanja wa Taifa wa soka urudishiwe jina lake la awali na jina la Nyerere liondolewe kwenye uwanja wa ndege, urudi kuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam.

Kama tunataka kuwaenzi marehemu wetu au hata viongozi waliopo, basi ni rahisi sana. Majina yao yawekwe kwenye ofisi za vyama vyao, kwa mfano, badala ya kuita ofisi ya chama Kisiwandui, basi iitwe "Ofisi ya Magufuli Kisiwandui".

Naomba kuwasilisha.
"Miradi ya umma" ndiyo ipi?
 
Vp kama mradi wa umma ungepewa jina la mumeo Mbowe.?
 
Kuna watu, si wachache wenye imani za dini hawaendi uwanjani kwakuwa viwanja vimepewa majina ya watu na wanaona ni ibada ya mizimu/wafu.
Kwanini unaita stebdi ya Magufuli, kwanini siyo stendi kuu Mbezi yaani hata kama mtu yupo Kamachumu Bukoba anajua hiyo stebdi ipo Mbezi.
Sasa ukimwambia mtu shukia magufuli anakuuliza ipo wapi?
Zamani tulikuwa na Kisutu Bus Stand na Mnazi mmoja na zilifahamika, kwanini haya matukuzo ?
Hakika
 
Bila kupoteza muda....ni sawa baadhi ya miradi iwaenzi walio ianzisha na kusimamia.

Ila sioni logic ya kila kitu kua na jina linalojirudia rudia. Reference Kwa awamu zote sio iliyopita tu.

Wanaoelewa wameelewa!
 
Viongozi wa Tanzania waliopo na waliopita wamepachika au wamepachikiwa majina yao kwenye mali na miradi ya nchi, hili jambo halina maana wala tija yoyote ile.

Kwa mfano, si sawa kwa stendi ya mabasi ya kimataifa ya Mbezi Luis, uwanja wa soka wa Taifa, viwanja vya ndege, madaraja, vivuko, shule, hospitali na mali nyingine za Taifa kupewa majina ya viongozi, wawe hai au wamekufa. Hii ni kwa sababu mali za umma zimegharamiwa na kodi za wananchi, hivyo si haki kuweka jina la kiongozi, eti kwa vile tu vitu hivyo vilijengwa wakati mhusika akiwa madarakani, wala hata hakutumia hela za mfukoni mwake. Huku ni kukengeuka, halafu ni nani anayependekeza majina hayo na kwa mchakato upi?

Kusimamia ujenzi wa kitu chochote katika nchi haimaanishi kwamba mhusika anayo hati miliki ya jina lake kupachikwa kwenye huo mradi. Hii ni kwa vile pesa zilizotumika kujenga miradi ya nchi si zake binafsi, ni hela za umma. Majina yanayopaswa kuitwa miradi hiyo yawe majina ya maeneo ulipo mradi huo, mfano uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, daraja la Busisi, barabara ya Mwendokasi, mradi wa umeme Kinyerezi, nk.

Lakini mali za umma kama stendi ya Mbezi Luis kuiita jina la mtu mmoja ni sawa na ubaguzi uliojaa ubinafsi. Napendekeza stendi ya Mbezi iitwe "Stendi ya Mabasi ya Mikoa ya Mbezi Luis". Jambo hili linaweza kuondoa nuksi, laana, na mikosi itokanayo na kutumia jina la mtu mmoja tu tena ambaye hajawahi kuwa mkazi wa eneo hilo na wala hajawahi hata kupanda mabasi yenyewe. Uwanja wa Taifa wa soka urudishiwe jina lake la awali na jina la Nyerere liondolewe kwenye uwanja wa ndege, urudi kuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam.

Kama tunataka kuwaenzi marehemu wetu au hata viongozi waliopo, basi ni rahisi sana. Majina yao yawekwe kwenye ofisi za vyama vyao, kwa mfano, badala ya kuita ofisi ya chama Kisiwandui, basi iitwe "Ofisi ya Magufuli Kisiwandui".

Naomba kuwasilisha.
"A rose by any other name would smell as sweet". William Shakespeare, Romeo and Juliet, Act II, Scene II.

Jina ni label tu. Ukiuita moto maji haina maana utaweza kuunywa moto ukate kiu yako.

Kwa nini tunajikita sana kwenye label ya kitu badala ya kujikita kwenye actual character ya kitu?

Kama kiongozi ndiye ana nguvu ya kujenga na kubomoa, kupanga na kupangua, hiyo rasilimali itakuwa ya huyo kiongozi tu, hata kama ukiibadilisha jina.

Jikite kwenye kupunguza nguvu za viongozi, si kwenye kubadilisha majina.

Itakusaidia nini ikiwa hatutauita uwanja jina la Samia, wakati Samia anachukua hela zote zinazozalishwa na uwanja huo na hakuna mtu wa kumfanya kitu?
 
Tunakwepa laana
 
Viongozi wa Tanzania waliopo na waliopita wamepachika au wamepachikiwa majina yao kwenye mali na miradi ya nchi, hili jambo halina maana wala tija yoyote ile.

Kwa mfano, si sawa kwa stendi ya mabasi ya kimataifa ya Mbezi Luis, uwanja wa soka wa Taifa, viwanja vya ndege, madaraja, vivuko, shule, hospitali na mali nyingine za Taifa kupewa majina ya viongozi, wawe hai au wamekufa. Hii ni kwa sababu mali za umma zimegharamiwa na kodi za wananchi, hivyo si haki kuweka jina la kiongozi, eti kwa vile tu vitu hivyo vilijengwa wakati mhusika akiwa madarakani, wala hata hakutumia hela za mfukoni mwake. Huku ni kukengeuka, halafu ni nani anayependekeza majina hayo na kwa mchakato upi?

Kusimamia ujenzi wa kitu chochote katika nchi haimaanishi kwamba mhusika anayo hati miliki ya jina lake kupachikwa kwenye huo mradi. Hii ni kwa vile pesa zilizotumika kujenga miradi ya nchi si zake binafsi, ni hela za umma. Majina yanayopaswa kuitwa miradi hiyo yawe majina ya maeneo ulipo mradi huo, mfano uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, daraja la Busisi, barabara ya Mwendokasi, mradi wa umeme Kinyerezi, nk.

Lakini mali za umma kama stendi ya Mbezi Luis kuiita jina la mtu mmoja ni sawa na ubaguzi uliojaa ubinafsi. Napendekeza stendi ya Mbezi iitwe "Stendi ya Mabasi ya Mikoa ya Mbezi Luis". Jambo hili linaweza kuondoa nuksi, laana, na mikosi itokanayo na kutumia jina la mtu mmoja tu tena ambaye hajawahi kuwa mkazi wa eneo hilo na wala hajawahi hata kupanda mabasi yenyewe. Uwanja wa Taifa wa soka urudishiwe jina lake la awali na jina la Nyerere liondolewe kwenye uwanja wa ndege, urudi kuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam.

Kama tunataka kuwaenzi marehemu wetu au hata viongozi waliopo, basi ni rahisi sana. Majina yao yawekwe kwenye ofisi za vyama vyao, kwa mfano, badala ya kuita ofisi ya chama Kisiwandui, basi iitwe "Ofisi ya Magufuli Kisiwandui".

Naomba kuwasilisha.
Okay
 
1. John Fitzgerald Kennedy (JFK) International Airport - USA
2. General Charles De Gaulle Airport - France
3. Hastings Kamuzu Banda Boulevard - Malawi
4.
Sijui niendelee?
 
Back
Top Bottom