Hayo ni maoni yako na una haki kikatiba! Hata hivyo kwa mwenendo wa serikali ya sasa na mahala Tanzania ilipofikia kimtanziko, hakika ukimtoa rais Mwinyi wa Zanzibar hakuna kiongozi yeyote ndani ya CCM anayefaa kuongoza taifa hili baada ya JPM! Kuna mgawanyiko mkubwa sana wa kisiasa, taifa halina umoja tena tulokuwa nao! Chuki na ubaguzi wa kisiasa, visasi na vinyongo vimetamalaki mno ndai ya taifa letu! Hivyo kiogozi ajaye akitokea ccm ni lazima ataedeleza alipoishia wa awali.
In fact tunahitaji mtu wa mtazamo wa tofauti kabisa na rais wa sasa ili aweze kuliunganisha taifa na kurudisha umoja wetu wa hiari na sio umoja wa kulazmishwa na vyombo vya dola.
Katika hili nafikiri rais kutoka upinzani anafaa zaidi, wapinzani ni sawa na wachezaji walio nje ya uwanja , hivyo wana nafasi kubwa ya kuyaona mapungufu ya serikali kwa miaka yote na katika mambo kadhaa ya msingi na kama tutakosa kichwa makini kutoka upinzani basi ni bora tumchukuwe rais Mwinyi kule Zenji tumkabidhi hii nchi anaweza kutuvusha!
Ifahamike kwamba pamoja na kufanya vizuri ndani ya hizi siku zake za mwanzo wa urais wake kule Zenji, lakini bado Mwinyi ataathiriwa kwa namna flani na uongozi wa bara ulioko Ikulu, Hivyo akipewa nchi na kuwa na mamlaka kamili yasiyoathiriwa na dhoruba toka upande wowote anaweza kufanya mengi makubwa.