SoC01 Pendekezo: Serikali iweke Tozo kwa Wamachinga kukabiliana na changamoto kwenye Majiji na Miji

SoC01 Pendekezo: Serikali iweke Tozo kwa Wamachinga kukabiliana na changamoto kwenye Majiji na Miji

Stories of Change - 2021 Competition

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,236
Reaction score
15,677
Kwa miaka mingi serikali imekuwa ikipambana na tatizo la wajasiriamali wadogo wadogo (maarufu kama wamachinga) ambao wametapakaa kwenye miji mikubwa ya nchi hii. Ukiangalia kwa jiji kama Dar es salaam, imekuwa sasa ni kawaida kuona mabanda ya wamachinga karibu kila kona unayokatiza.

Ni kweli kwamba utapanyo wa wamachinga kwenye miji na majiji umeharibu kabisa taswira na muonekano wa kupendeza wa miji yetu. Mabanda ya kila aina utayakuta mpaka katikati ya jiji, mengine yakifuka moshi wakati wa mchana. Hakuna barabara utayokatiza jijini, usikutane na utapanyo wa mabanda pembezoni mwa barabara.

Kingine kibaya ni kwamba, biashara za wamachinga mbali na kwamba karibu zote hazipo ‘formally registered’ pia biashara hizo hazipo katika mfumo wowote wa kuchangia mapato serikalini, kama zifanyavyo biashara nyingine, mbali na kile kitambulisho cha umachinga ambacho utekelezaji wake ni kama umefeli.

Kulingana na hoja hii, ndipo nimeona fursa kwamba, kutengenezwe utaratibu ambao utawafanya hawa wamachinga nao wawe sehemu ya kuchangia maendeleo ambayo yatafidia ule uharibifu ambao unafanywa na biashara zao ambazo zimezagaa bila utaratibu.

Uhalali wa hii tozo ni upi?
Uhalali wa kulipa hii tozo unatokana na kigezo kwamba, wamachinga wengi, mbali na kufanya biashara ndogo ndogo, ila utafiti wangu umeniambia kwamba, wamekuwa wakitengeneza kiasi kizuri sana cha pesa, ambacho mimi naamini haitakuwa vibaya kwa wao kuanza kuchangia maendeleo. Kipindi cha wiki tatu kilichopita, nilijaribu kuwahoji baadhi ya wamachinga, na kwa kweli sikuamini, maana kuna wengine kipato chao cha mwezi ni Zaidi ya Milioni moja kwa biashara hizo hizo wanazofanya humo mabarabarani.

Faida ya hii tozo itakuwa ni ipi?
  1. Utaongeza wigo wa makusanyo ya kodi na idadi ya wanaotakiwa kulipa kodi; ukiangalia nchi yetu tuna tatizo kubwa kwenye mambo ya kodi. Idadi ya watu wanaolipa kodi ‘tax base’ bado ni ndogo sana, na hii imepelekea serikali kuwanyonya hawa wanaolipa kodi kwa kuwapa makadirio makubwa ya kodi. Lakini kitendo cha hawa wajasiriamali kuanza kulipa kodi, maana yake ni kwamba taratibu taratibu nchi itaanza kuongeza wigo wa walipa kodi ambao ndio chachu ya kukusanya kodi nyingi.
  2. Pesa itayotokana na hii tozo kwa wamachinga itasaidia sana kuboresha miundombuni kwenye mitaa ya miji na majiji, kama; zahanati, shule, shughuli za usafi, na hata ulinzi.
  3. Kutengeneza ajira; kupitia kuboresha miundombini kwenye mitaa ya majiji na miji, hii itasaidia pia kutengeneza ajira kwa watanzania wenye uhitaji, kama ambavyo tutaona hapa chini.

Namna itavochangia maendeleo kwenye miji na majiji?
Ntatoa mfano wangu kwa halmashauri ya jiji la Ilala pekee, na kuonyesha namna kitu hichi nnachokisema kitafanikiwa. Kwenye halmashauri ya Ilala kwa makadirio ya haraka haraka, kuna idadi ya wajasiriamali Zaidi ya 10,000.

Mapendekezo yangu ni kwamba, halmashauri ya jiji la Ilala ilete tozo ya siku ya Tsh. 1,000 ambayo itatozwa kwa kila mjasiriamali.

Makusanyo ya tozo kwa mwaka

Idadi ya wajasiriamaliTozo kwa sikuMapato ya tozo kwa sikuMapato ya tozo kwa mweziMapato ya tozo kwa mwaka
10000​
1,00010,000,000300,000,0003,600,000,000


Kwa hiyo, kwa kuleta tozo hii kwa wamachinga, halmashauri ya Ilala itakuwa na wastani wa kiasi cha Zaidi ya Tsh. 3.6 Billioni kila mwaka ambacho kinaweza kuelekezwa kwenye shughuli za maendeleo kwenye mitaa.

Namna Bilioni tatu na nusu kwa mwaka inaweza kuleta maendeleo mitaani.

Sehemu ya matumiziBajeti kwa mweziKinachoweza kufanyikaMafanikio
Chakula kwa shule za msingi za halmashauri
100,000,000​
Magunia 2000 ya maindi kila mwezi kwa shule za msingi kwa ajili ya chakulaWatoto watapata uhakika wa kula au kunywa uji mashuleni
Kuwekeza kwenye majengo ya zahanati
100,000,000​
Kwa milioni 100 inawezekana kabisa kila mwezi kukajengwa jengo la zahanati kwa kila mtaaBaada ya mwaka mmoja kutakuwa na majengo zaidi ya kumi ya zahanati
Ulinzi shirikishi wa mitaa korofi
50,000,000​
Kwa bajeti ya milioni 50 kila mwezi, inaweza kulipa posho ya mwezi kwa walinzi 700 ambao watalinda usiku kama ulinzi shirikishi (Posho ya Tsh 70,000 kwa kila mlinzi)Hii itatengeneza ajira 700 kwa wasio na kazi
Usafi wa mitaa michafu
50,000,000​
Kwa bajeti ya milioni 50 kila mwezi itatosha pia kuwalipa wafanya usafi karibu 500 ambao watakuwa wanajukumu la kufanya usafi na kufanya mitaa iwe safi.Hii itatengeneza ajira 500 kwa wasio na kazi
Jumla
300,000,000


Hitimisho

Kwa kuwa huu ni mfano, ila ambacho nataka kukionesha ni kwamba, kwa sababu serikali ni kwamba imeshindwa kabisa kuondoa shughuli za wamachinga, basi inaweza kuja na sera mbadala ambazo zinaweza kuleta matokeo chanya kwa jamii, tofauti na hali ilivo kwa sasa ambapo, wamachinga wametapakaa kila mahala, na hawatoi mchango wowote kwa serikali mbali na kuonekana kuchafua taswira ya jiji na miji.

Hivo basi, sera hii ya tozo kwa wamachinga, itajaribu ku correct negative externality kwa ku create positive value kutoka kwenye unaoonekana ni uchafuzi wa shughuli za wamachinga kwenye viunga vya miji na majiji hapa Tanzania.

Karibuni tujadili kwa mapana hoja hii

N.Mushi
 
Upvote 2
Hivi Kodi hizi zote zilizoongezwa bado hazitoshi tu??.
Nimeangalia kwenye angle kwamba iwe ni kama njia ya ku regulate impact ambayo inasababishwa na wamachinga kwa sababu serikali ni kwamba mpaka sasa haina sera yoyote ya kueleweka kuhusu kudhibiti wamachinga.
 
Hivi Kodi hizi zote zilizoongezwa bado hazitoshi tu??.
Machinga analipa kodi ngapi?

nashauri wapewe EFD kabisaa
Na mauzo yao yafuatiliwe walipe kodi
Vinginevyo watoke barabarani

kigezo cha vizimba mijini kiwe uwe na mashine na ulipe kodi
Tena iwe daily mana wanaweza kuhama any time
 
Machinga analipa kodi ngapi?

nashauri wapewe EFD kabisaa
Na mauzo yao yafuatiliwe walipe kodi
Vinginevyo watoke barabarani

kigezo cha vizimba mijini kiwe uwe na mashine na ulipe kodi
Tena iwe daily mana wanaweza kuhama any time
We Jamaa una hasira na machinga, waliwahi kukuzibia riziki Nini??.
 
Back
Top Bottom