ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,030
- 61,298
nimekuwa nikiona jinsi mataifa mbalimbali yanavyohifadhi historia zao kwa kuanzisha siku maalumu za kumbukumbu. Kwa mfano Timor-Leste huadhimisha kila mwaka tarehe 12 Novemba kuwakumbuka waliopoteza maisha katika tukio la Santa Cruz ambapo siku hio mamia ya wanafunzi waliokuwa wakiandamana walikutana na mauaji ya kimbari toka kwa wanajeshi wa kiindonesia koloni lake siku ambayo pia imekuwa sehemu muhimu ya historia ya taifa lao.
Ningependa kupendekeza Tanzania pia iwe na Siku ya Kumbukumbu ya october 29, kwa lengo la kuwakumbuka wahanga wa tukio hilo na kutoa nafasi kwa taifa kutafakari, kujifunza na kuhimiza amani ili matukio ya aina hiyo yasijirudie.
Kuwa na siku ya kumbukumbu si kwa ajili ya kufufua maumivu au chuki, bali ni kuhifadhi historia, kuwapa heshima waliopoteza maisha na kufundisha vizazi vijavyo umuhimu wa amani, haki na umoja.