Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Huyu bwana ukimfuatilia vizuri, ni wazi amekuwa ni zaidi ya wakili kwani anakuwa pia ni kama mwanaharakati wa kupigania haki za binadamu hasa katika mataifa yanayoongozwa na watawala katili/madikteta wa kiafrika.
Ukifuatilia katika akaunti yake ya twitter,utaona jinsi anavyojitoa kulaani ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa dhidi ya raia katika mataifa mbalimbali ya kiafrika zikiwemo Tanzania, Uganda, Cameroon kama sikosei pamoja na nchi nyingine.
Uthibitisho wa taasisi yake kujitoa kupigania haki na utu wa watu ni maneno katika tweet yake hii ya tarehe 14/11/2020 ambapo aliandiki hivi:
"Our firm can guarantee nothing but try everything to help those who were disenfranchised so violently by the impostor"
Na hiki ndio anaonekana kukifanya sasa hata huko Uganda ambako nako kuna mambo ya hovyo hovyo yanayoendelea kuhusiana na uchaguzi.
Sitaki kuamini kuwa watu katika mataifa haya ya kiafrika wanaonyanyaswa na kuteswa na watawala, wana hela za kutosha kumlipa zaidi ya yeye na kampuni yake ya uwakili kujitolea tu kusaidia au kutoa huduma hiyo ya kisheria kwa kutoza gharama kidogo tu za kuchangia huduma hiyo na sio kupata faida.
Wapo mawakili wengi, lakini naona huyu na taasisi yake wanajitoa sana hivyo anastahili kupewa nishani kutambua mchango wake.