Pendekezo: Watumishi wa umma tukatwe mishahara walau asilimia 2 pesa ikasaidie Serikali kupambana na Corona

Pendekezo: Watumishi wa umma tukatwe mishahara walau asilimia 2 pesa ikasaidie Serikali kupambana na Corona

Eberhard

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2010
Posts
1,153
Reaction score
809
Kwanza niseme wazo kuwa mimi ni muumini wa ahadi za MwanaTANU. Ambapo msisitizo ni uzalendo kwa nchi.

Nikiwa Mtumishi wa umma huku nikiiona changamoto ya kupambana na covid-19 napendekeza serikali itukate watumishi wa umma wote walau asilimia mbili za mishahara yetu na pesa iende kusaidia mapambano dhidi ya corona. Katika hilo naomba tutangulize uzalendo. Nchi ni yetu na matatizo ni yetu.

Hata hivyo natoa wito kwa watanzania wenzangu wote tukumbuke kuomba risiti tutakaponunua bidhaa madukani jambo ambalo litasaidia kuimalisha uchumi wetu.
 
Duu
 

Attachments

  • IMG_20200406_171608.jpg
    IMG_20200406_171608.jpg
    62.6 KB · Views: 1
Serikali haina njaa, tena uiombe radhi! Tunayo akiba ya kututosha kuendesha nchi bila kufanya kazi kwa miezi sita
 
Mleta mada unahamu ya kutukanwa.
5 yrs with no salary increment halafu wewe unasema tukatwe 2%.
Unajua kama JK angeendelea kuwa mtawala mpaka sasa ningekuwa ninalipwa SH.ngapi?
Hajui kuwa kuna mfumuko wa bei tayari ? Leo kilo ya sukari imepanda toka 2,600/= hadi 3,000/=. Hilo ongezeko ni zaidi ya 2% anayoipendekeza.
 
Mimi sio mtumishi wa umma ila ninahakika Kama JK angeendelea kutawala au magufuli asingewapindulia meza watumishi wa umma kila mtumishi kwasasa angekwa na angalau ongezeko la laki mbili kwenye mshahara wake na wale wa bodi ya mikopo wasingekatwa kionezi ingekuwa sahihi kufanya hili pendekezo lako lakini magu alishasema anataka watu waishi kama masheitwani na ndicho kinachotokea Sasa hivyo sio sahihi kuwakata Tena hiyo 2%
 
Back
Top Bottom