Pengine Unamsikia tu Shetani Juu juu. Humfahamu Vizuri na Unasema ni Adui Yako

Mkuu andiko lako ni ziri mno mno na nimependa maana umeandika mengi yaliyo na uhalisia
Mungu na akasema tumuumbe mtu kwa mfano wetu. Hii n kumaanisha sisi tunauwezo wa Kiingu,yan tunaumba kwa kinywa. Na shetani analifahamu hilo ila anatuchanganya na kutufanya tujiumbie mabaya . Mfano tunaitana mbwa.paka na majina mengne mabaya ambayo yanaenda kutukaa.

Shetani anatushika na kutuzui tusimtolee Mungu sadaka iliyo safi na nzuri ndo maana leo hii mtumishi wa Mungu akisiamma na kutoa somo kuhusu kutoa sadaka vita vinainuka.

Tunaomba pasipo kuambatanisha maombi yetu na sadaka,hatushukuru baada ya kujibiwa sasa hizi ndizo mbinu shetani anatumi ili kutudidimiza, na shetani atatafuta mawakala wake na kuwajengea hali ya kuelezea sadaka namna inawafaidisha watu wa Mungu na watu wataamin. Hii inajenga gap kati ya wanadamu na Mungu. Sadaka shetan mwenyewe anaiogopa kutokana na nguvu yake kwahyo sadaka anaipinga kuliko kawaida

Kitu nilochojifunza kihusu sadaka. Kwa shetani watu wanafanikiwa sana maana sadaka zao ni kubwa sana mfano mtu anamtoa kafara mzazi wake ili awe tajiri. Mtu anaua gar nzima ili awe tajiri. Kwa shetani hakuna sadaka ndogo na ndo maana mtu akienda kwa mganga sadaka yake ndogo utasikia kuku. Sasa kwa Mungu ni wangap wanatoa hata hiyo kuku? Shetan anashika sana fahamu zetu hata biblia hatuisomi na kuona nguvu ya sadaka ilivyoandikwa katika maandiko matakatifu.

Shetani amekuja kwaajili ya kuchinja na kutuangamiza na hana jema kwetu.

Barikiwa sana kwa andiko hili.
Yesu kristu akupe afya njema nyenye kila aina ya mafanikio na baraka
Nextime usichoke kuleta andiko zuri kama hili
Hapo kwenye sadaka hata mm nimekupinga!! sio Kila unapoomba lazima uwe sadaka!! Muhimu ni maombi yako yaambatane na neno(ahadi) lililoandikwa kwenye Biblia! Mfano unatamani mafanikio , unasema Bwana uliahidi kuwa " utaenda mbele yangu na kusawszisha Mahali palikopaluza Isaya 45:2-
 
Maana yeye Mungu amejifunga kwenye neno lake(ahadi)) maana Yeye sio mwanadamu hata aseme uongo!!
 
Mungu ndio Shetani mwenyewe kwa maana Mungu alianza umba ulimwengu na mema na mabaya kabla ya kuumbwa Shetani Mungu alishaumba mema na mabaya kwa vyovyote hata Shetani asingekuwepo duniani basi ujue maovu yangekuwepo tu kwa maana Mungu alishaumba maovu kwa maneno rahisi Mungu ndio Shetani na yeye anawachora tu na kuwacheka
 
Sasa kwanini huyu mungu alitususia li shetani lenye uwezo kiasi hicho lije kutuvuruga

Yaani litutese duniani halafu lisababishe tuende na moto wa milele

Kweli huyu Mungu anatupenda?
 
Unajua wakristo au hata waislamu tunadhani kumtetea saana Mungu ndio kupendwa saana na Mungu kumbe Mungu anataka tutumie Common sense zetu kuntukuza yeye na si kujiona tunamjua saana.
Hawajiulizi kama viongozi wa dini zetu tunao waamini wanatenda mambo ya ajabu madhabahuni mahali tunapoamini ni patakatifu kwann upuuzie uwezo wa shetani kama anauwezo wa kuvuruga madhabahu??
Mi simuamini kiongozi yyte wa dini,kwanza Hana Cha kunisaidia!
Pili ,Mungu wetu Jesus,Jehova,Elohim ,Bwana wa majeshi ...hatetewi,ila anajitetea ....

Ila kuhusu kumwabudu,kumtukuza , kumtumikia yeye ni sahihi ndo anachotaka
 
Hao ni vyombo tuu vinatyowa wakati wowote
 
Pengine unamsikia tu shetani juu juu, humfahamu vizuri na unasema ni adui yako.

Unawezaje kupambana na adui usiyeijua nguvu yake?

Anafafanua kwa ufupi Mwl . Makungu m.s
0743781910

Kamwe Usimfananishe shetani na majini , mapepo , mizimu wachawi n.k. Ambao una uwezo wa kufanya nao vita kirahisi tu hata kwa kuweka mfupa wa nguruwe mlangoni na harufu ya bangi ndani ya chumba..

Unapotaka kufanya vita na adui ili umshinde kwanza elewa uwezo wake na mifumo yake inavyofanya kazi..

Umewahi kujiuliza kwann majini na mapepo yalikuwa yakimuona Yesu yanahangaika,yanapiga kelele, yanagalagala, yananywea na kukimbia lkn shetani alikaa na Yesu wakapiga story, wakajadili vifungu vya biblia na kubishana kwa hoja kwa siku 40 nyikani? ( Soma Vitabu vya injili).

Umewahi kujiuliza iliwezekanaje shetani aliyepigwa pmj na jeshi lake kule mbinguni akafukuzwa akatupwa duniani, lkn wana wa Mungu (wako wengi siyo Yesu tu-ntakufafanulia ktk andiko lijalo) walipokuwa wanakwenda kujihudhurisha mbele za Mungu mara kadhaa siku tofauti tofauti shetani pia alikuwa anajumuika pamoja nao katkat yao mbele za Mungu na wale wana wa Mungu wala hawakumfukuza na Mungu alipomuona wakajadiliana naye juu ya mustakabari wa wanadamu duniani. (Soma kitabu cha Ayubu) .

Na unajua mwisho wa siku Mungu alimwambia nini shetani juu ya Ayubu? Alimruhusu shetani amfanyie mambo / mapigo yote anayotaka lkn kasoro jambo moja tu "asiitoe roho yake".
Hii maana yake nini? Mungu akikaa pembeni , Shetani ana uwezo wa kutoa roho ya mtu.
Kwahiyo wale ambao hata wakiona watu wamekufa kinyama kwenye ajali wanakimbilia kusema " kazi ya Mungu haina makosa . Ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu" , Jiepusheni kumsingizia Mungu Kila kitu . Kazi nyingine ni kazi za shetani zina makosa...

Shetani ni adui yako mkubwa unayepambana naye kwahiyo unatakiwa kumfahamu vizuri.

Shetani Kabla hajaasi mbinguni na kuwa shetani Alikuwa ni malaika mkuu anayeitwa jina zuri lenye utukufu Lucifer ( Nyota ya asubuhi) .

Alikuwa na uwezo mkubwa Sana wa ajabu kuzidi malaika wengine wote aliopewa na Mungu mwenyewe mpk akajiona Kama yupo sawa na Mungu . Na ndiyo maana robo tatu ya malaika ilimuamini na ikaamua kuungana naye kupigana na Mungu. Wakiamini Lucifer atashinda .

Wanadamu wanaimba mpk sauti ya 4 . Lkn unaambiwa Lucifer Alikuwa anaimba sauti mpk sauti ya 12 peke yake..

Akinyanyua mabawa yake akiyashusha zinalia sauti za vinanda tupu.

Alikuwa ndiyo kiumbe wa karibu Sana na Mungu kuliko malaika wengine . Maana yake Ni kuwa alimuelewa na kuielewa mipango mingi ya Mungu.

Aikuwa ni Kama waziri mkuu ktk serikali ya mbinguni . Kwahiyo Alikuwa na mamlaka makubwa ktk kuiendesha ile serikali ..
Na tafsiri nyingine Ni kuwa alielewa Siri nyingi za serikali ya mbinguni..

Mungu ni roho , shetani ni roho na malaika ni roho ( hawana umbo maalumu lkn wana uwezo wa kujiweka na kujigeuza ktk umbo lolote ..
Na mwanadamu wa kwanza kabisa kuumbwa aliumbwa ktk umbo la mwanadamu lkn lenye roho ya uungu (nusu Mungu) ndani yake.. Ndiyo maana Alikuwa na uwezo wa kakaa nao na kuzungumza nao wanyama na miti na wakaelewana..

Najua hujanielewa vizuri hapo . Ngoja nikupe hii.
Mungu aliumba vitu vyote kwa kutamka neno tu na kwa kutumia umoja , yaani " na liwepo anga ,likawa". Lakini ilipofika muda wa kumuumba mwanadamu Mungu hakutumia neno tu na aliongea kwa nafsi ya wingi.

Yaani " na tumfanye mtu kwa mfano wetu " .
Unajua Alikuwa anawaambia wakina Nani ?
Na huo mfano ni wa sura au jinsia pekee?
Na unajua kwann shetani alichukia kuumbwa mwanadamu?

- kwanza uelewe mwanadamu aliumbwa ile siku ya 6 ya uumbaji baada ya Mungu kuwa kaumba vitu vyote vya msingi kabakiza vichache. Ilikuwa Siku 1 kabla ya kupumzika . Na shetani alichukia kuumbwa mwanadamu . Hii maana yake ni kuwa wakati mwanadamu anaumbwa tayari mbinguni kulikuwa na viumbe tyr vimeshaumbwa ( malaika) na shetani (Lucifer) ndiyo alikuwa malaika mkuu . Soma Mwanzo sura ya 2 ..

"Na tumfanye mtu kwa mfano wetu"..

-Mungu anasema "na tumfanye mtu kwa mfano wetu". Siyo sura pekee yake au jinsia bali ni mtu mwenye nusu uungu na uwezo ndani yake Kama walivyo wao kule mbinguni. Ndiyo maana shetani alichukia maana Mungu alihamishia mapenzi kwa mwanadamu kuliko kwa malaika.

Nimegusia jinsia hapo juu. Biblia haijawahi kusema Kama Mungu ana jinsia . Lkn biblia inaweka wazi kuwa wana wa Mungu wana jinsia .. Tukianzia na Yesu . Na wale wana wa Mungu walioshuka duniani nyakati za Nuhu na wakavutiwa na binti za wanadamu na wakawaoa wakazaa nao ,wakazaliwa watu wenye uwezo wa ajabu ,hodari na majitu (Giants) wanefili.. (soma Mwanzo 6:1> )... Japokuwa ktk jambo hili la kitheolojia kuna nadharia 2 zinapingana na Kila mmoja ameachwa aamini nadharia anayoitaka yeye.. Wapo wanaoamini wana wa Mungu walioshuka na kuzaa na wanadamu zama hizo walikuwa ni malaika toka mbinguni.. Na wapo wanaoamini wana wa Mungu hao walikuwa ni watoto wa uzao wa Sethi wacha Mungu wa Kipindi kile .. Biblia haijafafanua kwa uwazi tofauti ya wana wa Mungu waliotajwa ktk Ayubu na hawa waliotajwa nyakati za Nuhu.
Swali la kujiuliza na kujiongeza Ni kuwa " kwann baada ya wana wa Mungu hawa kuzaa na wanadamu walizaliwa binadamu wenye sifa na uwezo mkubwa tofauti na binadamu wa kawaida"?

Shetani anaijua vizuri biblia kuliko unavyoijua wewe . Ndiyo maana Alikuwa anabishana na Yesu kwa vifungu. Na anaitumia Kila siku ili apate njia za kukupoteza wewe kwa kutumia hiyo hiyo biblia.
Kwahiyo kama unadhani unaweza kumtisha shetani kwa kuishika biblia au rozali au msalaba bila kuwepo na roho ya Mungu pembeni yako unajidanganya.

- Huwa tunayatoa mapepo na majini ndani ya mtu na wakati mwingine yanajitaja Hadi majina ( makata,subiani,maimuna,n.k) . Lkn Ulishawahi kusikia tumemtoa shetani ndani ya mwili wa mtu na akajitaja na jina kuwa mm ni Lucifer?

Sisi watu wa Tanga na Zanzibar kuna wakati Huwa tunakutana na majini tunayaona live . Lkn nani aliishawahi kukutana na Lucifer?

- Mungu anamwambia Musa " hakuna mwanadamu atakayeniona akaishi" .
Pengine hii ni sababu ya pili iliyomfanya Musa afe mapema .. baada ya Musa kung'ang'ania Sana kutaka kumuona Mungu sura yake , Mungu alimziba Musa macho na alipopita akamuachia Musa akamuona kisogo na mgongo..

Shetani naye huiga Kila kitu kinachoendeshwa ktk ufalme wa Mungu . Kwahiyo huwezi kumuona Lucifer wewe na imani yako ndogo hiyo.

Shetani na malaika zake pamoja na kumuasi Mungu ,walipigwa kule mbinguni lakini hawakuuliwa. Zingatia neno " hawakuuliwa" . Wakatupwa duniani .
Tena Biblia inasema " Ole ole kwa wanadamu maana yule mshitaki wenu ametupwa kwenu " .. Na ukumbuke ana hasira za kupigwa.
- Mwanadamu alipomuasi Mungu Kipindi cha Nuhu akafutwa na gharika . Kipindi cha sodoma akafutwa na moto .. Lkn shetani hakuuliwa alitupwa kwetu .

Huyo ndiyo adui unayeshindana naye wewe.. Umjue jinsi alivyo . Sijui km unanielewa..

Shetani alipotupwa duniani hakuna sehemu Biblia inasema kuwa aliondolewa au kunyang'anywa zile nguvu zake na uwezo wake mkubwa aliokuwa nao mbinguni kuliko malaika wote .. Uwezo uliomfanya yeye ajione ni Kama Mungu .
Sasa fikiria huyo ndiyo kiumbe unashindana naye wewe ..

Ndugu yangu bila uwepo wa roho ya Mungu ndani yako na pembeni yako , utamchukia shetani tu lkn hutaweza hata kuligusa tu pindo la vazi lake . Tena siyo wewe utakayeshughulika naye ,ni Mungu mwenyewe.

Shetani anapenda ukuu, utukufu , na kuabudiwa km Mungu anavyoabudiwa.

Shetani Anapenda usafi , harufu nzuri za pafyumu, marashi ,udi , uvumba, manemane na marhamu . Kama vile tu Mungu anavyopenda . ( Soma torati ya Musa). Ndiyo maana majini yananukia kupita kiasi..

Anapenda damu na nyama kupita kiasi kuliko sadaka yoyote ile . Kama vile tu Mungu alivyokuwa anapenda Kabla ya kifo cha Yesu . ( Soma Agano la kale uone jinsi Mungu alivyokuwa anapenda damu na harufu nzuri ya nyama ya kuchoma km sadaka ) . Mungu aliacha ila shetani ameendeleza . Unajua kwann ? Damu huwa inaongeza nguvu na uwezo kwa viumbe vilivyo ktk ulimwengu wa roho. Kawaulize wachawi wanapotaka kuboost nguvu zao wanafanya nn..

Hakuna kiumbe kinachomfikia shetani kwa uzuri wa sura anapokuwa ktk umbile la kimwili.. unawakumbuka wale malaika walioenda kwa lutu kule sodoma na gomora jinsi walivyokuwa wanawavutia wale wajinga wa sodoma wenye ushetani ? Basi Lucifer kabla hajawa shetani ndiyo alikuwaga kiongozi wao kule mbinguni na hakuna malaika Aliyekuwa anamzidi kwa lolote.
Huwa tunafanya makosa Sana kumchora shetani na sura ya kutisha kiasi kwamba watoto wanakariri hivyo na inakuwa rahisi kuanguka ktk dhambi ya uzinzi maana wanakutana na sura nzuri nzuri tu bila kujua kuwa hao ndiyo vibaraka wa Shetani wapo kazini ..

Shetani anao uwezo wa kufanya miujiza ya kumponya mtu ( soma ufunuo atagundua mengi) ..
Ndiyo maana leo hii yapo baadhi ya makanisa yanayotilia mashaka ktk miujiza wanayofanya.
Kama unalijua neno la Mungu unawagundua kirahisi.

Shetani anao uwezo wa kumtoa mtu mapepo /majini. Pitia habari za beerizebuli ktk injili utagundua hilo..
kwahiyo usidanganywe na miujiza ya mtu , mpime huyo mtu kwanza.

Shetani anao uwezo wa kumpa mtu mafanikio . Na hilo linajionesha wazi kabisa ktk mahojiano yake na Yesu kule nyikani..
Kwahiyo usitamani mafanikio ya mtu bila kujua kayatoa wapi?

Shetani anao uwezo mkubwa wa ubunifu wa kisayansi na kiteknolojia. Na wanadamu wengi tunaingia kwny mitego ya shetani anayetumia akili nyingi kwa ujanja sana..
Ndani humo humo ya teknolojia nzuri tu kunakuwa na kajambo kadogo tu ka kishetani ndani yake.. Anachotaka ni kuona watu wanafanya kinyume na maagizo ya Mungu anavyotaka. Na kwa kuwa watu wengi hawasomi maandiko basi hawajui iwapasavyo kuenenda na wanapotea..

Tawala nyingi, mamlaka na falme za duniani zipo chini ya/ zinaendeshwa na shetani Lucifer. Rejea maagizo ya shetani kwa Yesu kule nyikani. Shetani huzishikilia tawala za dunia ili maamuzi yanayopitishwa na tawala hizo yawe ni ya kumkufuru Mungu na kumtukuza yeye. Ndiyo maana leo Kuna mambo km ya haki za ndoa za jinsia moja . Soma vizuri habari za mnyama ktk kitabu cha Ufunuo utaelewa.

Huyo ndiyo shetani Lucifer tunayedhani tunapambana naye direct kumbe tunapambana na vibaraka wake tu ..

ANGALIZO MUHIMU
Andiko hili halijaandikwa ili kumsifia shetani ,bali kuelezea ukweli halisi wa Shetani ( Lucifer) ili kukufanya ndugu mpendwa kujua nguvu ya adui unayepambana naye .
Ukiijua nguvu na uwezo na mbinu zake utajua jinsi ya kumkwepa/ kupambana naye..
Na usipambane na shetani bali mkwepe au muite Mungu apambane naye kwaajili yako.. Wewe Huna uwezo wa kupambana na Lucifer peke yako..

Makungu m.s
0743781910
Shetani ni jini aliyekuwa kwenye kundi la malaika.

Hakuna malaika aliyewahi kumuasi Mungu.
 
..........Mungu ni roho , shetani ni roho na malaika ni roho.....

HAPANA
: HAPA UMEPOTOSHA KWA KIWANGO CHA AJABU SANA.
KILICHO ROHO NI MUNGU PEKE YAKE, MALAIKA SIYO ROHO NA HIVYO SHETANI SIYO ROHO KWA SABABU NI MALAIKA.
SIKU SHETANI ATAKAPOKUJA KUCHOMWA MOTO, POSSIBLY UTAMUONA KWA MACHO YAKO SIKU HIYO

MUNGU ANAO UWEZO WA KUWEPO KILA MAHALI KWA SABABU YEYE NI ROHO, SHETANI HANA HUO UWEZO WA KUWEPO KILA MAHALI KWA SABABU YEYE KAMA MALAIKA, IS AN INDIVIDUAL PERSONALITY NA HIVYO ANAPOKUWEPO SEHEMU MOJA, HAWEZI KUWEPOE SEHEMU NYINGINE TENA

KWA MFANO, KIPINDI MALAIKA GABRIEL ANATUMWA NA MUNGU KWENDA KWA MARIAMU KUMWAMBIA KUWA ATAMZAA MTOTO YESU, KWA MUDA WOTE USE AMBAO MALAIKA GABRIEL ALIKUWA YUPO PAMOJA NA MARIAM WANAONGEA, KWA MUDA HUO MALAIKA GABRIEL HAKUWEPO SEHEMU NYINGINE YOYOTE ILE ISIPOKUWA TU MAHALI PALE ALIPOKUWEPO PAMOJA NA MARIAM

HOWEVER SHETANI ANAO UWEZO ULE WA KU-MANIFEST AS IF YUPO KILA MAHALI KWA KUTUMIA MALAIKA ZAKE WAOVU ALIONAO NA AMBAO WAMETAPAKAA KILA MAHALI

KWA HIYO NI MUNGU PEKEE AMBAYE YUPO KILA MAHALI NA SI SHETANI WALA KIUMBE KINGINE CHOCHOTE KILE

TAFADHALI SANA NAOMBA UZINGATIE HILI NA UKAE MAKINI SANA NALO

Sweya Makungu
 
You're so protective about God the case which is very good!

Lakini ukweli ni huu:

Shetani pia ni Roho!

Sikiliza:Ebu kasome pale palipoandikwa...HAPO MWANZO ALIKUWEPO NENO... endelea mpk mwisho!

Sasa ukiongea habari ya Mungu na Shetani ujue unaongea na POSITIVE VERSUS NEGATIVE ENERGIES.

Constructive THOUGHTS produce some GODISH PRODUCTS.

DESTRUCTIVE THOUGHTS produce some delvish products.

Ondoa physicality unapoongea haya mambo-utapata ufahamu uliobora zaidi!
 
Pengine unamsikia tu shetani juu juu, humfahamu vizuri na unasema ni adui yako.

Unawezaje kupambana na adui usiyeijua nguvu yake?

Anafafanua kwa ufupi Mwl . Makungu m.s
0743781910

Kamwe Usimfananishe shetani na majini , mapepo , mizimu wachawi n.k. Ambao una uwezo wa kufanya nao vita kirahisi tu hata kwa kuweka mfupa wa nguruwe mlangoni na harufu ya bangi ndani ya chumba..

Unapotaka kufanya vita na adui ili umshinde kwanza elewa uwezo wake na mifumo yake inavyofanya kazi..

Umewahi kujiuliza kwann majini na mapepo yalikuwa yakimuona Yesu yanahangaika,yanapiga kelele, yanagalagala, yananywea na kukimbia lkn shetani alikaa na Yesu wakapiga story, wakajadili vifungu vya biblia na kubishana kwa hoja kwa siku 40 nyikani? ( Soma Vitabu vya injili).

Umewahi kujiuliza iliwezekanaje shetani aliyepigwa pmj na jeshi lake kule mbinguni akafukuzwa akatupwa duniani, lkn wana wa Mungu (wako wengi siyo Yesu tu-ntakufafanulia ktk andiko lijalo) walipokuwa wanakwenda kujihudhurisha mbele za Mungu mara kadhaa siku tofauti tofauti shetani pia alikuwa anajumuika pamoja nao katkat yao mbele za Mungu na wale wana wa Mungu wala hawakumfukuza na Mungu alipomuona wakajadiliana naye juu ya mustakabari wa wanadamu duniani. (Soma kitabu cha Ayubu) .

Na unajua mwisho wa siku Mungu alimwambia nini shetani juu ya Ayubu? Alimruhusu shetani amfanyie mambo / mapigo yote anayotaka lkn kasoro jambo moja tu "asiitoe roho yake".
Hii maana yake nini? Mungu akikaa pembeni , Shetani ana uwezo wa kutoa roho ya mtu.
Kwahiyo wale ambao hata wakiona watu wamekufa kinyama kwenye ajali wanakimbilia kusema " kazi ya Mungu haina makosa . Ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu" , Jiepusheni kumsingizia Mungu Kila kitu . Kazi nyingine ni kazi za shetani zina makosa...

Shetani ni adui yako mkubwa unayepambana naye kwahiyo unatakiwa kumfahamu vizuri.

Shetani Kabla hajaasi mbinguni na kuwa shetani Alikuwa ni malaika mkuu anayeitwa jina zuri lenye utukufu Lucifer ( Nyota ya asubuhi) .

Alikuwa na uwezo mkubwa Sana wa ajabu kuzidi malaika wengine wote aliopewa na Mungu mwenyewe mpk akajiona Kama yupo sawa na Mungu . Na ndiyo maana robo tatu ya malaika ilimuamini na ikaamua kuungana naye kupigana na Mungu. Wakiamini Lucifer atashinda .

Wanadamu wanaimba mpk sauti ya 4 . Lkn unaambiwa Lucifer Alikuwa anaimba sauti mpk sauti ya 12 peke yake..

Akinyanyua mabawa yake akiyashusha zinalia sauti za vinanda tupu.

Alikuwa ndiyo kiumbe wa karibu Sana na Mungu kuliko malaika wengine . Maana yake Ni kuwa alimuelewa na kuielewa mipango mingi ya Mungu.

Aikuwa ni Kama waziri mkuu ktk serikali ya mbinguni . Kwahiyo Alikuwa na mamlaka makubwa ktk kuiendesha ile serikali ..
Na tafsiri nyingine Ni kuwa alielewa Siri nyingi za serikali ya mbinguni..

Mungu ni roho , shetani ni roho na malaika ni roho ( hawana umbo maalumu lkn wana uwezo wa kujiweka na kujigeuza ktk umbo lolote ..
Na mwanadamu wa kwanza kabisa kuumbwa aliumbwa ktk umbo la mwanadamu lkn lenye roho ya uungu (nusu Mungu) ndani yake.. Ndiyo maana Alikuwa na uwezo wa kakaa nao na kuzungumza nao wanyama na miti na wakaelewana..

Najua hujanielewa vizuri hapo . Ngoja nikupe hii.
Mungu aliumba vitu vyote kwa kutamka neno tu na kwa kutumia umoja , yaani " na liwepo anga ,likawa". Lakini ilipofika muda wa kumuumba mwanadamu Mungu hakutumia neno tu na aliongea kwa nafsi ya wingi.

Yaani " na tumfanye mtu kwa mfano wetu " .
Unajua Alikuwa anawaambia wakina Nani ?
Na huo mfano ni wa sura au jinsia pekee?
Na unajua kwann shetani alichukia kuumbwa mwanadamu?

- kwanza uelewe mwanadamu aliumbwa ile siku ya 6 ya uumbaji baada ya Mungu kuwa kaumba vitu vyote vya msingi kabakiza vichache. Ilikuwa Siku 1 kabla ya kupumzika . Na shetani alichukia kuumbwa mwanadamu . Hii maana yake ni kuwa wakati mwanadamu anaumbwa tayari mbinguni kulikuwa na viumbe tyr vimeshaumbwa ( malaika) na shetani (Lucifer) ndiyo alikuwa malaika mkuu . Soma Mwanzo sura ya 2 ..

"Na tumfanye mtu kwa mfano wetu"..

-Mungu anasema "na tumfanye mtu kwa mfano wetu". Siyo sura pekee yake au jinsia bali ni mtu mwenye nusu uungu na uwezo ndani yake Kama walivyo wao kule mbinguni. Ndiyo maana shetani alichukia maana Mungu alihamishia mapenzi kwa mwanadamu kuliko kwa malaika.

Nimegusia jinsia hapo juu. Biblia haijawahi kusema Kama Mungu ana jinsia . Lkn biblia inaweka wazi kuwa wana wa Mungu wana jinsia .. Tukianzia na Yesu . Na wale wana wa Mungu walioshuka duniani nyakati za Nuhu na wakavutiwa na binti za wanadamu na wakawaoa wakazaa nao ,wakazaliwa watu wenye uwezo wa ajabu ,hodari na majitu (Giants) wanefili.. (soma Mwanzo 6:1> )... Japokuwa ktk jambo hili la kitheolojia kuna nadharia 2 zinapingana na Kila mmoja ameachwa aamini nadharia anayoitaka yeye.. Wapo wanaoamini wana wa Mungu walioshuka na kuzaa na wanadamu zama hizo walikuwa ni malaika toka mbinguni.. Na wapo wanaoamini wana wa Mungu hao walikuwa ni watoto wa uzao wa Sethi wacha Mungu wa Kipindi kile .. Biblia haijafafanua kwa uwazi tofauti ya wana wa Mungu waliotajwa ktk Ayubu na hawa waliotajwa nyakati za Nuhu.
Swali la kujiuliza na kujiongeza Ni kuwa " kwann baada ya wana wa Mungu hawa kuzaa na wanadamu walizaliwa binadamu wenye sifa na uwezo mkubwa tofauti na binadamu wa kawaida"?

Shetani anaijua vizuri biblia kuliko unavyoijua wewe . Ndiyo maana Alikuwa anabishana na Yesu kwa vifungu. Na anaitumia Kila siku ili apate njia za kukupoteza wewe kwa kutumia hiyo hiyo biblia.
Kwahiyo kama unadhani unaweza kumtisha shetani kwa kuishika biblia au rozali au msalaba bila kuwepo na roho ya Mungu pembeni yako unajidanganya.

- Huwa tunayatoa mapepo na majini ndani ya mtu na wakati mwingine yanajitaja Hadi majina ( makata,subiani,maimuna,n.k) . Lkn Ulishawahi kusikia tumemtoa shetani ndani ya mwili wa mtu na akajitaja na jina kuwa mm ni Lucifer?

Sisi watu wa Tanga na Zanzibar kuna wakati Huwa tunakutana na majini tunayaona live . Lkn nani aliishawahi kukutana na Lucifer?

- Mungu anamwambia Musa " hakuna mwanadamu atakayeniona akaishi" .
Pengine hii ni sababu ya pili iliyomfanya Musa afe mapema .. baada ya Musa kung'ang'ania Sana kutaka kumuona Mungu sura yake , Mungu alimziba Musa macho na alipopita akamuachia Musa akamuona kisogo na mgongo..

Shetani naye huiga Kila kitu kinachoendeshwa ktk ufalme wa Mungu . Kwahiyo huwezi kumuona Lucifer wewe na imani yako ndogo hiyo.

Shetani na malaika zake pamoja na kumuasi Mungu ,walipigwa kule mbinguni lakini hawakuuliwa. Zingatia neno " hawakuuliwa" . Wakatupwa duniani .
Tena Biblia inasema " Ole ole kwa wanadamu maana yule mshitaki wenu ametupwa kwenu " .. Na ukumbuke ana hasira za kupigwa.
- Mwanadamu alipomuasi Mungu Kipindi cha Nuhu akafutwa na gharika . Kipindi cha sodoma akafutwa na moto .. Lkn shetani hakuuliwa alitupwa kwetu .

Huyo ndiyo adui unayeshindana naye wewe.. Umjue jinsi alivyo . Sijui km unanielewa..

Shetani alipotupwa duniani hakuna sehemu Biblia inasema kuwa aliondolewa au kunyang'anywa zile nguvu zake na uwezo wake mkubwa aliokuwa nao mbinguni kuliko malaika wote .. Uwezo uliomfanya yeye ajione ni Kama Mungu .
Sasa fikiria huyo ndiyo kiumbe unashindana naye wewe ..

Ndugu yangu bila uwepo wa roho ya Mungu ndani yako na pembeni yako , utamchukia shetani tu lkn hutaweza hata kuligusa tu pindo la vazi lake . Tena siyo wewe utakayeshughulika naye ,ni Mungu mwenyewe.

Shetani anapenda ukuu, utukufu , na kuabudiwa km Mungu anavyoabudiwa.

Shetani Anapenda usafi , harufu nzuri za pafyumu, marashi ,udi , uvumba, manemane na marhamu . Kama vile tu Mungu anavyopenda . ( Soma torati ya Musa). Ndiyo maana majini yananukia kupita kiasi..

Anapenda damu na nyama kupita kiasi kuliko sadaka yoyote ile . Kama vile tu Mungu alivyokuwa anapenda Kabla ya kifo cha Yesu . ( Soma Agano la kale uone jinsi Mungu alivyokuwa anapenda damu na harufu nzuri ya nyama ya kuchoma km sadaka ) . Mungu aliacha ila shetani ameendeleza . Unajua kwann ? Damu huwa inaongeza nguvu na uwezo kwa viumbe vilivyo ktk ulimwengu wa roho. Kawaulize wachawi wanapotaka kuboost nguvu zao wanafanya nn..

Hakuna kiumbe kinachomfikia shetani kwa uzuri wa sura anapokuwa ktk umbile la kimwili.. unawakumbuka wale malaika walioenda kwa lutu kule sodoma na gomora jinsi walivyokuwa wanawavutia wale wajinga wa sodoma wenye ushetani ? Basi Lucifer kabla hajawa shetani ndiyo alikuwaga kiongozi wao kule mbinguni na hakuna malaika Aliyekuwa anamzidi kwa lolote.
Huwa tunafanya makosa Sana kumchora shetani na sura ya kutisha kiasi kwamba watoto wanakariri hivyo na inakuwa rahisi kuanguka ktk dhambi ya uzinzi maana wanakutana na sura nzuri nzuri tu bila kujua kuwa hao ndiyo vibaraka wa Shetani wapo kazini ..

Shetani anao uwezo wa kufanya miujiza ya kumponya mtu ( soma ufunuo atagundua mengi) ..
Ndiyo maana leo hii yapo baadhi ya makanisa yanayotilia mashaka ktk miujiza wanayofanya.
Kama unalijua neno la Mungu unawagundua kirahisi.

Shetani anao uwezo wa kumtoa mtu mapepo /majini. Pitia habari za beerizebuli ktk injili utagundua hilo..
kwahiyo usidanganywe na miujiza ya mtu , mpime huyo mtu kwanza.

Shetani anao uwezo wa kumpa mtu mafanikio . Na hilo linajionesha wazi kabisa ktk mahojiano yake na Yesu kule nyikani..
Kwahiyo usitamani mafanikio ya mtu bila kujua kayatoa wapi?

Shetani anao uwezo mkubwa wa ubunifu wa kisayansi na kiteknolojia. Na wanadamu wengi tunaingia kwny mitego ya shetani anayetumia akili nyingi kwa ujanja sana..
Ndani humo humo ya teknolojia nzuri tu kunakuwa na kajambo kadogo tu ka kishetani ndani yake.. Anachotaka ni kuona watu wanafanya kinyume na maagizo ya Mungu anavyotaka. Na kwa kuwa watu wengi hawasomi maandiko basi hawajui iwapasavyo kuenenda na wanapotea..

Tawala nyingi, mamlaka na falme za duniani zipo chini ya/ zinaendeshwa na shetani Lucifer. Rejea maagizo ya shetani kwa Yesu kule nyikani. Shetani huzishikilia tawala za dunia ili maamuzi yanayopitishwa na tawala hizo yawe ni ya kumkufuru Mungu na kumtukuza yeye. Ndiyo maana leo Kuna mambo km ya haki za ndoa za jinsia moja . Soma vizuri habari za mnyama ktk kitabu cha Ufunuo utaelewa.

Huyo ndiyo shetani Lucifer tunayedhani tunapambana naye direct kumbe tunapambana na vibaraka wake tu ..

ANGALIZO MUHIMU
Andiko hili halijaandikwa ili kumsifia shetani ,bali kuelezea ukweli halisi wa Shetani ( Lucifer) ili kukufanya ndugu mpendwa kujua nguvu ya adui unayepambana naye .
Ukiijua nguvu na uwezo na mbinu zake utajua jinsi ya kumkwepa/ kupambana naye..
Na usipambane na shetani bali mkwepe au muite Mungu apambane naye kwaajili yako.. Wewe Huna uwezo wa kupambana na Lucifer peke yako..

Makungu m.s
0743781910
Mkuu samahani, na utani sahihisha kma nitakuwa nmekosea.

Kama malaika ni roho(nafsi), IMEANDIKWA: Kila nafsi itaonja umauti. Kwangu naamini malaika watatolewa roho na watakufa pia[emoji3581]

Kama mwanadamu ana roho(nafsi), IMEANDIKWA: Kila nafsi itaonja umauti. Kwangu naamini wanadamu wote watatolewa roho na watakufa pia[emoji3581]

Kama shetani ni roho(nafsi), IMEANDIKWA: Kila nafsi itaonja umauti. Kwangu naamini mashetani/ shetani watatolewa roho na watakufa pia[emoji3581]

Sasa pia uliandika MUNGU, nae ni roho (nafsi)[emoji777]

Hapo ipo vipi ?? wakati huo kwenye Quran and bibble imeandikwa kila nafsi itaonja umauti. Vipi kuhusu hili?? Kiufupi naomba ungemuelzea vizuri MUNGU kwa utukufu wake na ukubwa wake kwa unyenyekevu wa hali ya juu plz.

Ukiniambia MUNGU ni ROHO, kama inani changanya hivi. Kwa maana imeandikwa kila nafsi/roho itaonja umauti.

Kama nakosea naomba nikoselewe ili nielimike[emoji3578]
 
Umefanya uchambuzi mzuri
 
You're so protective about God the case which is very good!

Lakini ukweli ni huu:

Shetani pia ni Roho!

Sikiliza:Ebu kasome pale palipoandikwa...HAPO MWANZO ALIKUWEPO NENO... endelea mpk mwisho!

Sasa ukiongea habari ya Mungu na Shetani ujue unaongea na POSITIVE VERSUS NEGATIVE ENERGIES.

Constructive THOUGHTS produce some GODISH PRODUCTS.

DESTRUCTIVE THOUGHTS produce some delvish products.

Ondoa physicality unapoongea haya mambo-utapata ufahamu uliobora zaidi!
Shetani ana physical body kama ya kwako. Hicho kitu kinamwondolea sifa ya kuwa ni Roho; Roho ni Mungu
Mbali na hilo, Mungu kuwa ni Roho ni kitu ambacho kinampa sifa ya pekee ya yeye kuwepo kila mahali (omnipresent). Shetani hana sifa ya kuwa omnipresent kwa sababu yeye si Roho. Ana mwili ambao unapokuwa upo Manzese, Kariakoo anakuwa hayupo isipokuwa malaika zake
 
Back
Top Bottom