Kardinali sio askofu wa kawaida.Pengo sio kiongozi mkuu wa kabisa katoliki,he us a mere askofu
Wakatoliki kondoo wa gwajima huyu kaingiaWasiokula nyama ijumaa kuu ni upumbavu wao
Wakristo tunaongozwa na biblia na siyo maagizo ya watu wajinga kama kina Pengo.
Haya ni mawazo yako. kwa upande wangu Pengo amejidhalilisha sana kupinga uwepo wa katiba mpya. na huwezi kusema suala la katiba si la wananchi wakati hao hao wananchi ndio waliotoa maoni ya namna wanavyotaka nchi yao itawaliwe. Katiba na maendeleo huwezi kuvitenganishaPamoja na uhuru uliokuwa na wa kutoa mawazo, BAK, maneno uliyotumia kujadili mada kuhusu Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini, Mhadhama Kardinali Pengo, ni ya kitoto. Kama wewe ni mtu mzima ni mtu mzima hovyo.
Siyo tu umemdharirisha kama yeye, bali hata nafasi katika jamii, Kanisa Katoliki na waumini wake wote.
Sikubali kwamba kauli ya Askofu mtajwa na Kardinali Pengo inawakilisha mawazo ya Watanzania mlio wengi. Ni kauli inayowakilisha wanasiasa wenye uchu wa madaraka.
Niliwahi kuandika humu jamvini, kwamba wanaotaka Katiba mpya si wananchi ila wanasiasa tena uchwara. Katika Katiba JMT, nikikuuliza ni Ibara ipi inamnyima raia kufanya shughuli zake za kimaendeleo, au haki na uhuru wake? Utabaki kuropoka tu.
JITAMBUE KWANZA NDIO UWEZE KUMJIBU MTU KAMA MHADHAMA KARDINALI PENGO.
Kama hukufunzwa na wazazi wako, utafunzwa na dunia. Hata maandiko matakatifu yanatutaka kutii mamlaka, na kuheshimu wazazi, tupate maisha mema na bora duniani.
Na wewe uwe makini unapoandika hoja zako.Jibu hoja zangu pasipo kusimjibia BAK.
Hakuna neno lolote nimeandika kuwa Pengo ni malaika.
Uwe tu makini unapojibu hoja.
Kulikuwa na watu wako karibu na Yesu lakini wapuuzi tu itakuwa kuwa karibu na binadamu kama Papa? Yuda alikuwa mweka hazina wa Yesu lakini msaliti tu tumbo mbele, unashangaa pengo kuweka tumbo (ubinafsi) mbele!!? Aliongoza matamko na nyaraka za kanisa wakati wa JK na hakukuwa na matukio ya ukatili kama ya huyu Mkatoliki mwenzake, lakini Leo kimya, hakuna anachokemea, wakionana "Tumsifu Yesu Kristo". Mnamsifu Yesu Kristo gani na damu za watu mikononi!??? Yesu hadhihakiwi, asubiri maswali kuhusu wajibu wake siku ya haki.Kardinali sio askofu wa kawaida. Ujue kwanza ni askofu wa Raisi wa nchi. Magufuli askofu wake ni pengo
.pili kardinali ana Siri za kanisa katoliki za dunia nzima na za Vatican ambazo askofu mwingine wa kawaida Hana sababu ni mjumbe wa vikao vizito vya Vatican ambavyo husimamia Mambo Ya kanisa. Pengo ni mtu wa Karibu na Papa. Magufuli akitaka kitu cha kumwambia Papa anaongea na pengo ambaye ni mtu wa karibu na Papa akamwambie hawezi kuongea na Niwemugizi ambaye mwisho wake ngara
kama kipaumbele cha watanzania siyo katiba yale maoni wananchi waliyokuwa wanatoa walikuwa wanataka nini? kweli nimeamini bado watanzania wengi ni wajinga sanaMh. Pengo upo sahihi kabisa. Kipaumbele cha Watanzania ni maisha bora, siyo katiba.
Nayasema haya kwa sababu naamini mtu hawezi kula katiba, hawezi kuvaa katiba, hawezi kutibiwa na katiba.
Ebu tujiulize, katika familia zetu kuna katiba?
Bila shaka hakuna, na mambo yote katika familia zetu yanatekelezwa vizuri na kwa ufanisi mzuri tu pamoja na kutokuwa na katiba ya familia.
Kadinali Pengo alisema yeye binafsi kipaumbele chake ni kuona huduma za jamii kama zile elimu na afya zinaendelea kuboreshwa kwa kasi kama ambavyo Serikali ilivyoanza kufanya
ahsante.umeamua kuwa muwaziTusizungushe akili za watu bure, Wakatoliki tumekuwa na ubinafsi sana hasa endapo mgombea anatokea katika dhehebu letu la RC, nakumbuka sana namna maaskofu walivyo kimya hata kwa ukiukaji wa katiba na namna demokrasia inavyokandamizwa. Wakati wa Jakaya ilikuwa daily matamko kutoka kwa maaskofu. Mhashama huyu anatakiwa aelewe kuwa hata upande mwingine unaweza toa raisi mwenye busara zaidi.
Ni mtu mwenye akili finyu tu ambaye anaweza kusema katiba mpya si kipaumbele cha nchi. Huwezi kuwa na Serikali bora ambayo inajua fika itaiba kura ili kung'ang'ania madarakani hivyo hata IVURUNDE vipi haina hofu tena kwa wapiga kura maana wanajua watashinda tu. Kutoongwa mkono na 51% ya Watanzania katika kupata katiba mpya haina maana katiba hiyo haina umuhimu. Tatizi ni hao watakaoikataa hiyo katiba mpya kiwango chao cha elimu ni kipi?
Hata vyama vingi wengi hawakuvitaka kama si Baba wa Taifa leo hii baada ya miaka 56 bado tungekuwa na chama kimoja. Imagine madudu chungu nzima ya hawa wahuni na mafisadi ambayo yamewekwa hadharani na vyama vya upinzani tangu tulipoanza rasmi mfumo huo 1992. Fungua akili yako uone mbali zaidi.
Wakuu mimi nimesema hapo awali katiba mpya nzuri ni jambo la lazima. Hapa tunachopishana ni ktk kuweka kipaumbele kulingana na hali iliopo.Hivi haya ulosema hayana uhusiano wa moja kwa moja na katiba?,hivi hizo Huduma mnazosema ni akina nani zinawahusu?,katiba inalinda utu wa MTU,inasimamia taratibu sahihi za kustawisha utu na maisha ya MTU,sasa ni MTU wa aina gani ambae hata akipewa Huduma bora lkn anafinyangwa utu wake atae furahia Huduma hizo,
Unamuongelea Gwajima?