Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Pengo sio kiongozi mkuu wa kabisa katoliki,he us a mere askofu
Kardinali sio askofu wa kawaida.

Ujue kwanza ni askofu wa Raisi wa nchi. Magufuli askofu wake ni pengo, pili kardinali ana Siri za kanisa katoliki za dunia nzima na za Vatican ambazo askofu mwingine wa kawaida Hana sababu ni mjumbe wa vikao vizito vya Vatican ambavyo husimamia Mambo Ya kanisa. Pengo ni mtu wa Karibu na Papa. Magufuli akitaka kitu cha kumwambia Papa anaongea na pengo ambaye ni mtu wa karibu na Papa akamwambie hawezi kuongea na Niwemugizi ambaye mwisho wake ngara
 
Pamoja na uhuru uliokuwa na wa kutoa mawazo, BAK, maneno uliyotumia kujadili mada kuhusu Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini, Mhadhama Kardinali Pengo, ni ya kitoto. Kama wewe ni mtu mzima ni mtu mzima hovyo.

Siyo tu umemdharirisha kama yeye, bali hata nafasi katika jamii, Kanisa Katoliki na waumini wake wote.

Sikubali kwamba kauli ya Askofu mtajwa na Kardinali Pengo inawakilisha mawazo ya Watanzania mlio wengi. Ni kauli inayowakilisha wanasiasa wenye uchu wa madaraka.

Niliwahi kuandika humu jamvini, kwamba wanaotaka Katiba mpya si wananchi ila wanasiasa tena uchwara. Katika Katiba JMT, nikikuuliza ni Ibara ipi inamnyima raia kufanya shughuli zake za kimaendeleo, au haki na uhuru wake? Utabaki kuropoka tu.

JITAMBUE KWANZA NDIO UWEZE KUMJIBU MTU KAMA MHADHAMA KARDINALI PENGO.

Kama hukufunzwa na wazazi wako, utafunzwa na dunia. Hata maandiko matakatifu yanatutaka kutii mamlaka, na kuheshimu wazazi, tupate maisha mema na bora duniani.
Haya ni mawazo yako. kwa upande wangu Pengo amejidhalilisha sana kupinga uwepo wa katiba mpya. na huwezi kusema suala la katiba si la wananchi wakati hao hao wananchi ndio waliotoa maoni ya namna wanavyotaka nchi yao itawaliwe. Katiba na maendeleo huwezi kuvitenganisha
 
Sasa Pengo mbona anapiga Dana Dana si aseme sasa msimamo wa kanisa ni upi. Manake enzi za JK walikuwa hawakawi kuja ni misimamo.

Ubaguzi wao hautawaacha salama.
 
Kardinali sio askofu wa kawaida. Ujue kwanza ni askofu wa Raisi wa nchi. Magufuli askofu wake ni pengo
.pili kardinali ana Siri za kanisa katoliki za dunia nzima na za Vatican ambazo askofu mwingine wa kawaida Hana sababu ni mjumbe wa vikao vizito vya Vatican ambavyo husimamia Mambo Ya kanisa. Pengo ni mtu wa Karibu na Papa. Magufuli akitaka kitu cha kumwambia Papa anaongea na pengo ambaye ni mtu wa karibu na Papa akamwambie hawezi kuongea na Niwemugizi ambaye mwisho wake ngara
Kulikuwa na watu wako karibu na Yesu lakini wapuuzi tu itakuwa kuwa karibu na binadamu kama Papa? Yuda alikuwa mweka hazina wa Yesu lakini msaliti tu tumbo mbele, unashangaa pengo kuweka tumbo (ubinafsi) mbele!!? Aliongoza matamko na nyaraka za kanisa wakati wa JK na hakukuwa na matukio ya ukatili kama ya huyu Mkatoliki mwenzake, lakini Leo kimya, hakuna anachokemea, wakionana "Tumsifu Yesu Kristo". Mnamsifu Yesu Kristo gani na damu za watu mikononi!??? Yesu hadhihakiwi, asubiri maswali kuhusu wajibu wake siku ya haki.
 
Mm tokea aingie kwenye 18 za gwajima cjawahi kumwelewa tena huyu mzee ila mungu aendelee kumbariki naona ipo siku atajua kua hakua sahihi pia
 
esitena tetena,

Huyu sasa yeye akisema ndiyo msimamo wa kanisa katoliki?

Naye kasema ya kwake tu kama alivyosema yule mwingine. Wanaodai katiba mpya hawasemi yote yaliyopendekezwa ni maovu isipokuwa wanataka maovu yaliyowekwa yaondolewe na mazuri yaliyoacha yawekwe pia. Huyu naye asubiri mshahara vatican tu.

Lakini atambue kwamba kanisa katoliki siyo pengo. Lna watu na hao watu binafsi ndio wenye maamuzi juu ya maisha yao, vinginevyo aweke kipengele kwenye litugia kinachowaamrisha wafuasi kuwa watii kwake na ccm.
 
kwa hiyo yeye hataki sisi tupate katiba mpya
 
Mh. Pengo upo sahihi kabisa. Kipaumbele cha Watanzania ni maisha bora, siyo katiba.
Nayasema haya kwa sababu naamini mtu hawezi kula katiba, hawezi kuvaa katiba, hawezi kutibiwa na katiba.
Ebu tujiulize, katika familia zetu kuna katiba?
Bila shaka hakuna, na mambo yote katika familia zetu yanatekelezwa vizuri na kwa ufanisi mzuri tu pamoja na kutokuwa na katiba ya familia.
kama kipaumbele cha watanzania siyo katiba yale maoni wananchi waliyokuwa wanatoa walikuwa wanataka nini? kweli nimeamini bado watanzania wengi ni wajinga sana
 
Kadinali Pengo alisema yeye binafsi kipaumbele chake ni kuona huduma za jamii kama zile elimu na afya zinaendelea kuboreshwa kwa kasi kama ambavyo Serikali ilivyoanza kufanya

Huyu Pengo anashindwa kuelewa kwamba hizo huduma za jamii pia zingeboreka zaidi kama tungepata katiba bora zaidi. Tunatakiwa tuwe na katiba mpya ambayo itapunguza mamlaka ya rais na kugusa maeneo yote muhimu ya maslahi ya wananchi. Kwa mfano, kwa sasa rais anakurupuka na kujenga kiwanja cha ndege Chato au ananunua Bombadier bila kulishirikisha Bunge ambalo ndio chombo rasmi cha uwakilishi wa wananchi. Katiba mpya inatakiwa iweke wazi nini cha kumfanya rais endapo anafanya makosa kama haya...

Ubinafsi wa kujenga viwanja vya ndege nyumbani na sifa za kununua ndege ambazo hazina maslahi kwa wananchi wa chini, zitaokoa pesa nyingi na pesa hizo zitatumika kuhudumia wananchi wanyonge ambao Pengo anadai anataka wahudumiwe. Kwa ufupi tu nimejaribu kumpa uhusiano na umuhimu wa huduma za jamii na katiba bora. Katiba hii ya sasa (1977) imempa rais madaraka makubwa mno na ipo kimnya maeneo mengi. Hivyo basi, kama anapatikana rais asiye na busara, anajigeuza mtukufu na mkuu wa yote!
 
Tusizungushe akili za watu bure, Wakatoliki tumekuwa na ubinafsi sana hasa endapo mgombea anatokea katika dhehebu letu la RC, nakumbuka sana namna maaskofu walivyo kimya hata kwa ukiukaji wa katiba na namna demokrasia inavyokandamizwa. Wakati wa Jakaya ilikuwa daily matamko kutoka kwa maaskofu. Mhashama huyu anatakiwa aelewe kuwa hata upande mwingine unaweza toa raisi mwenye busara zaidi.
ahsante.umeamua kuwa muwazi
 
Kipaumbele cha kwanza cha waumini ni katiba mpya mengine yatakuja yenyewe tu.
 
Ni mtu mwenye akili finyu tu ambaye anaweza kusema katiba mpya si kipaumbele cha nchi. Huwezi kuwa na Serikali bora ambayo inajua fika itaiba kura ili kung'ang'ania madarakani hivyo hata IVURUNDE vipi haina hofu tena kwa wapiga kura maana wanajua watashinda tu. Kutoongwa mkono na 51% ya Watanzania katika kupata katiba mpya haina maana katiba hiyo haina umuhimu. Tatizi ni hao watakaoikataa hiyo katiba mpya kiwango chao cha elimu ni kipi?

Hata vyama vingi wengi hawakuvitaka kama si Baba wa Taifa leo hii baada ya miaka 56 bado tungekuwa na chama kimoja. Imagine madudu chungu nzima ya hawa wahuni na mafisadi ambayo yamewekwa hadharani na vyama vya upinzani tangu tulipoanza rasmi mfumo huo 1992. Fungua akili yako uone mbali zaidi.


Hivi haya ulosema hayana uhusiano wa moja kwa moja na katiba?,hivi hizo Huduma mnazosema ni akina nani zinawahusu?,katiba inalinda utu wa MTU,inasimamia taratibu sahihi za kustawisha utu na maisha ya MTU,sasa ni MTU wa aina gani ambae hata akipewa Huduma bora lkn anafinyangwa utu wake atae furahia Huduma hizo,
Wakuu mimi nimesema hapo awali katiba mpya nzuri ni jambo la lazima. Hapa tunachopishana ni ktk kuweka kipaumbele kulingana na hali iliopo.

Pili ningependa kuwakumbusha uwepo wa katiba safi/nzuri haituhakikishii kwamba viongozi wataitii au kuyatekeleza matakwa yake ipasavyo. Kwani mara ngapi hapa tunaona katiba haifuatwi? Mara ngapi tunaona sheria zinavunjwa? Mara ngapi tunaona viongozi hasa wa kiafrika wanabadili katiba nzuri kuweka kipengele kibaya kinachowapa fursa ya kutenda mabaya yao? Katiba ni sheria mama, tumeona madudu ya EPA, ESCROW, kashifa ya RADAR, RICHMOND, na zile vurugu za operesheni tokomeza zilizosababisha watu kutendewa uhalifu kinyume na katiba lakini pamoja na kwamba katiba yetu inayo vipengele vya kuzuia hayo bado haikuweza kuzuia.

Katiba ya Marekani ina maneno machache au mistari michache lakini wale jamaa jamii nzima wana utashi wa kutii katiba na sheria wanaishi vizuri. Huku hakuna utashi wa kutii katiba na uadilifu kwa jamii kwa asilimia kubwa. Huku hata ulete katiba ya Marekani hali itazidi kuwa mbaya. Ona mfano Kenya wapata katiba nzuri mpya na imewezesha kutengua matokeo ya ushindi wa uchaguzi mkuu lakini ulimsikia Kenyatta? Alisema subiri washinde tena kisha wataanza kushughulikia mahakama. Huu ndio mfano wa hayo niliyoeleza hapo awali kuhusu viongozi wetu wa kiafrika.
 
Mkuu BAK tumepata vyama vingi lakini mbona havijaondoa ufisadi? Mbona kipindi hiki cha vyama vingi ndio tumepata matukio mengi ya ubadhirifu (ufisadi) na rushwa nyingi na kubwa sana kuliko kipindi cha chama kimoja? Jibu ni kwamba tatizo letu sio sheria, au katiba au kelele za vyama vya upinzani bali utashi, utayari wa viongozi wetu na jamii nzima kuwa waadilifu. Tatizo hilo huchangiwa zaidi na jamii ambayo asilimia kubwa hawana elimu ya kutosha. Na ndio maana UKAWA(Lowassa) walisisitiza elimu, na CCM(Magufuli) wamesisitiza elimu kama hii ELIMU BURE ya sasa. Elimu ndio italeta uelewa na utashi wa kubadili hii hali.
 
Hawa ndio viongozi wanaosababisha waumini wayumbeyumbe na kuishia kukimbia kanisa. Kwahiyo yeye anasema kama nani hapo? Shame!
 
Mwanahabari Huru

Askofu Pengo unafiki sio sehemu yetu wakatoliki, sikutaka kuandika chochote kuhusiana na wewe, mimi nimebatizwa katika RC nimekuwa muumini mkubwa, nimesoma shule ya Upadri St Mary's Seminary, ninaijua Rc.

Nimesikitishwa sana na kauli zako za kipuuzi, zilizo jaa unafiki, tumekusikia sana ukijipambanua kuwa wewe si muumini wa mabadiliko, tuambie upande wako ni UPI.

Askofu wangu Pengo umemjibu Askofu Niwemugizi alie jitokeza hadhalani na kusema watanzania wanataka katiba mpya, umefufuka ulikotoka na kumshambulia Askofu kuwa katiba au maneno ya Askofu sio msimamo wa RC lakini hakusema kuwa ni msimamo wa RC. Lakini unajua Askofu Niwemugizi si msemaji wa Rc, maana yake alisema kama Mawazo yake kikatiba, na wewe unamjua msemaji wa RC ulitaka kutafuta uhalali wa kujibu mashambulizi la watawala, of target.

Naona umetoka kwa kasi sana kujibu shambulizi hill!,! Lakini hutoki hadhalani kuonya matukio ya kuuwawa kwa watanzania na kutupwa kwenye maji wakiwa wamefungwa mikono Nyuma, wanaopigwa Risasi kama kina tundu Lissu, kuonya viongozi wanao toa maneno ya kibaguzi na kikabila, huwezi kuonya kufokea au kushauri, kazi yako imekuwa ni kujibu mashambulizi kwa wanao ikosoa serikali,

Au unavyeti feki? Unamiliki Mali zisizo halali? Kiongozi wa kiroho unashindwa kujua nini wajibu wako? Sio mala ya kwanza kupingwa na maaskofu wenzio akiwepo Gwajima na kupelekana mahakamani ambapo Askofu Gwajima alikushinda kesi.

Viongozi wa dini simamieni haki na sio unafiki kujipendekeza kama mnataka ubunge, au teuzi za kina mama Lwakatale sawa, Hata mkitaka usemaji wa Ccm nafasi za kina polepole.

Swali la Kizushi: WATU WASIOJULIKANA WANATOKEA RWANDA TUMUOMBE TUNDU LISSU
 
Unamuongelea Gwajima?

Namuongelea Pengo, yule unaemjua kwa unafiki. Msema hovyo anayefikiri anatusemea wakatoliki wakati hana cheo hicho. Gwajima anafahamu zake sio kama huyu mgonjwa .

Angekuwa na fahamu zake asingengea utumbo wa kumpinga huyu mzalendo anayetetea katiba mpya. Kama sio uchizi ni nini kumpinga huku akijua ni maoni yake binafsi, au pengo alimpinga kama nani? Nani alimwambia aliwasemea wakatoliki? PENGO SIO MSEMAJI WA TAASISI YOYOTE LICHA YA KUWA ASKOFU WA DSM. UPUUZI NA MAUDHI
 
Back
Top Bottom