Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Yote hayo anayasema Pengo leo ni kwa sababu anayetawala sasa ni Mkatoliki ambaye inadaiwa kwa makusudi anaipa Favor ya juu taasisi ya Ukatoliki hapa Tanzania.

Kama mtawala angekuwa ni Muislamu (kama kipindi kile cha Kikwete) Askofu Pengo ungemwona yuko busy kila Jumapili kuikosoa serikali na kudai uwepo wa katiba mpya yenye kutoa haki kwa Watanzania.
 
Kwa mujibu wa taratibu za kanisa Katoliki, askofu Pengo sio msemaji wa kanisa,Msemaji ni Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania,

Rais wa Baraza la Maaskofu ndio Bosi wa Maaskofu wote nchini na hata askofu pengo anakuwa yuko chini yake, pia kama askofu pengo hakiutumwa na Rais wa Baraza la Maaskofu,na yeye pia hana mamlaka ya kulisemea kanisa katoliki na alichosema ni maoni yake.


Ukadinali wake ni kwa ajili ya kupiga kura kumchagua Papa tu,ila yeye akiwa Tanzania kicheo ni Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam,anataka watu waone kwamba Ukadinali ndio Ukubwa wa kanisa,Mkubwa wa kanisa ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,na ni askofu wa mwanza,pengo yuko chini yake Rais wa Baraza

"first among equals" Pengo hamzidi Askofu yeyote kwa cheo,ni sawa na rafiki yangu sheikh mkuu wa mkoa wa Dar ajione mkubwa kuliko mashehe wa mikoa mingine
Kiongozi wa Kanisa katoliki Tanzania !
 
Mwamini ninayejitabua sipangiwi. Katiba mpya ni lazima.
 
Na yeye sio msemaji wa sisi waumini.
 
Nimesikitishwa sana na kauli ya Kardinali Pengo juu ya Katiba Mpya. Nilitegemea Kardinali Pengo angeungana na Watanzania kutaka Katiba Mpya badala yake anasema eti IJE BAADAE.
Walianza wapinzani, wakaja media, wakaja.........
Bado kidogo dini nayo itaanza kuisoma namba na akili zao ndo zitakaa mguu pande mguu sawa.
 
Pengo anaposema Kipaumbele chake ni kuona wananchi wanapata huduma kwanza na sio katiba mpya, inaashiria Akili yake imeanza kuzeeka vibaya.

Mimi nilitaka kumuuliza tu, kwanini Kanisa katoliki miaka yoyote limekuwa likitenga bajeti kubwa sana kwa ajili ya kuhubiri injili, kuwatunza vizuri Mapadri na Masista, kujenga makanisa makubwa na mazuri kuliko kutenga bajeti kubwa kwa ajili ya kuwanunulia chakula wahanga wote wanaokufa kwa njaa duniani?

Kipaumbele chao ni nini?
 
Nimesikitishwa sana na kauli ya Kardinali Pengo juu ya Katiba Mpya.Nilitegemea Kardinali Pengo angeungana na Watanzania kutaka Katiba Mpya badala yake anasema eti IJE BAADAE.
Uingereza haijawahi kuwa na katiba na haina mpango wa kuwa na katiba lakini ni nchi iliyoendelea. Katiba sio kipaumbele cha maendeleo.
 
Wataalam wa mambo ya Akili huwa wanasema ukiwa na umri mkubwa unavyozidi kukua kiumri ndiyo uwezo wa kufikiri hupungua.
 
Mhashamu Askofu Kardinali Pengo amesema kuwa kauli iliyotolewa na askofu Niwemugizi kuwa katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi sio msimamo wa kanisa kwa sababu kanisa lina taratibu zake za kuishauri serikali au kuzungumzia masuala ya jamii.
pia amesema kwake yeye katiba ni kitu kije baadaye si cha haraka.
chanzo: gazeti la Mwananchi via facebook.
Mtu asiejulikana
 
Mhashamu Askofu Kardinali Pengo amesema kuwa kauli iliyotolewa na askofu Niwemugizi kuwa katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi sio msimamo wa kanisa kwa sababu kanisa lina taratibu zake za kuishauri serikali au kuzungumzia masuala ya jamii.
pia amesema kwake yeye katiba ni kitu kije baadaye si cha haraka.
chanzo: gazeti la Mwananchi via facebook.

Hii ni aibu kubwa kwa Kanisa Katoliki...kuwa na kiongozi wa dini wa aina hii.
Mbona amekuwa mnafiki kiasi hiki?
 
Back
Top Bottom