Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Kwa mtu mwenye akili timamu kabisa hawezi kudhani kuwa katiba ni kipaumbele cha kwanza kwa Watanzania.
Kipaumbele cha kwanza kabisa kwa Watanzania ni maendeleo, yaani uwepo wa huduma bora za jamii nk.

Tunachokihitaji kikubwa kabisa sisi Watanzania ni pamoja na commitment, uadilifu na uzalendo wa viongozi na wananchi wake.

KATIBA inaweza kuwa ni nzuri kabisa lakini watu wake wakawa ni maskini wakutupwa nk.

Kwa hiyo mimi naunga mkono kauli ya Askofu Pengo.
 
Mimi ni mkatoliki kabisa. Pengo kwakwel binafsi nilimtoa thamani kitambo sana.
Huyu Mzee enzi za utawala wa Muislam kikwete alikuwa busy kwa mkatoliki Slaa. Leo karudi kwa Sinzonje mkatoliki mwenzake.

Mbinguni hatutaingia kupitia pengo kama mpaka mafuta wa bwana bali tutaingia kupitia matendo mema. Hata suala la Lissu kanisa Katoliki walitoa statement baada ya kelele nyingi za watu ukizingatia Lissu ni mkatoliki.
Duuh kanisa Kwasasa siyo la wenye haki.
 
Uingereza haijawahi kuwa na katiba na haina mpango wa kuwa na katiba lakini ni nchi iliyoendelea.Katiba sio kipaumbele cha maendeleo
Kutokuwa na katiba ni tofauti na kuwa na katiba mbovu. Na siyo kwamba hawana katiba. Kwani katiba ni kitu gani zaidi ya muongozo? Unataka kuniambia hawana muongozo?

Hivi kwanini mung’ang’anie katiba ile ile mkoloni aliyokuwa anaitumia kutunyanyasa nayo? Kwasababu mmegeuka wakoloni weusi?
 
Kwa maoni yangu ninaona kabla ya kulaumu/kubeza n.k ni vizuri tukachua muda wa kutosha kusoma kwa makini na kuelewa: 1. Kilichosemwa na Mwadhama Kardinali Pengo, 2. Kilichosemwa na Mhashamu Askofu Niwemugizi, 3. Hairakia ya kanisa Katoliki Tanzania. Tofauti na hapo kuna hatari ya: 1. Kueleza visivyo yaliotamkwa/dhamiriwa na wasemaji wenyewe, 2. Kutoa matamshi mabaya kwa hawa viongozi. Mfano kuna mmoja hapo juu amesema Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania ni askofu wa Mwanza! Jamani tusome, tuulize kutoka vyanzo husika.
 
Askofu asiyejua matatizo ya nchi ni mnafiki. Kumbe ndio maana alikuwa anatoa baraka kwa akina Bashite.
 
Uingereza haijawahi kuwa na katiba na haina mpango wa kuwa na katiba lakini ni nchi iliyoendelea.Katiba sio kipaumbele cha maendeleo
Hakika.Maana niliuliza hapa mtu akivunja katiba nini kinafuata?Hakuna aliyejibu.Kama iliyopo tu inavunjwa na ni kawaida wala anayevunja hashtuki,hata ikiwekwa katiba gani haitasaidia kitu.
 
Kwa mujibu wa taratibu za kanisa katoliki,askofu pengo sio msemaji wa kanisa,Msemaji ni Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania,

Rais wa Baraza la Maaskofu ndio Bosi wa Maaskofu wote nchini na hata askofu pengo anakuwa yuko chini yake, pia kama askofu pengo hakiutumwa na Rais wa Baraza la Maaskofu,na yeye pia hana mamlaka ya kulisemea kanisa katoliki na alichosema ni maoni yake


Ukadinali wake ni kwa ajili ya kupiga kura kumchagua Papa tu,ila yeye akiwa Tanzania kicheo ni Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam,anataka watu waone kwamba Ukadinali ndio Ukubwa wa kanisa,Mkubwa wa kanisa ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,na ni askofu wa mwanza,pengo yuko chini yake Rais wa Baraza

"first among equals" Pengo hamzidi Askofu yeyote kwa cheo,ni sawa na rafiki yangu sheikh mkuu wa mkoa wa Dar ajione mkubwa kuliko mashehe wa mikoa mingine
Uko sahihi kabisa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kila askofu ni bosi Wa jimbo lake na kamwe hawaingiliani na hawezi Fanya ibada mkoa /jimbo lolote bila ruhusa ya aliyepo
 
Hamjamuelewa Pengo. Kasisitiza kuwa kuna utaratibu wa kanisa kuhusu kutoa matamko ya kisiasa. Sasa wapinga kila kitu wanakuja na mipash yao. Kwani pengo kasosea wapi? kwani Pengo kasema hataki katiba mpya?

Na ajue yeye sio msemaji wa Katoliki
 
Pengo amekuwa mnafiki sana, mimi ni Mkatoliki ila simpendi hata kidogo.
 
Naungana na askofu Gwajima kuhoji "MAHARAGE ALIYOKULA" huyo nafasi ya jino lililongolewa ni kutoka wapi. Mwenye jibu pleaseeee.
 
Kwani kauli ya pengo ndo ya wakatoliki? Aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Mimi ni mkatoriki lakini kauli ya kiongozi wangu imenikera
 
Hamjamuelewa Pengo. Kasisitiza kuwa kuna utaratibu wa kanisa kuhusu kutoa matamko ya kisiasa. Sasa wapinga kila kitu wanakuja na mipash yao. Kwani pengo kasosea wapi? kwani Pengo kasema hataki katiba mpya?
Soma vizuri na uelewe....

hatuitaji uwe mtetezi wa huyu mzee aliyekumbatia watesi wa watu wa mungu....

huyu tunamjua amefunga ndoa na farao na yupo kwa manufaa ya farao tokea enzi za katiba mpya ya warioba na alikubali kujitenga na maaskofu wengine wote japo anajiaminisha kuwa yeye ndio kubwa la maaskofu wote tanzania.

#maharageyawapialiyokulahuyumzee#
 
Pengo ni askofu mkuu wa jimbo la DSM. Sio msemaji wa kanisa katoliki. Kama vile maoni ya Askofu Niwemugizi nae ni vivyo hivyo.
 
Pengo yuko sahihi hata uingereza kipaumbele chao sio katiba na hawajawahi kuwa na katiba na hawatarijii kuwa na katiba. kipaumbele ni kero halisia za raia wake kutatuliwa. Askofu pengo yuko sahihi asilimia 100
Uingereza wanayo katiba sema haijaandikwa acha kudanganya watu hapa
 
Hiyo unwritten constitution koko yako iweke basi. Katiba isiyoandikwa ilipitishwa lini weka mwaka ilipopitishwa na bunge la uingereza na kupigiwa kura na wananchi. Weka hapa huo ushahidi
UK wana values na customs ambazo kwazo ndio muongozo labda tuanze kujadili aina za katiba otherwise funga domo lako usidanganye hapa
 
Back
Top Bottom