Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Alilolisema Askofu NiweMugizi lina mashiko,vilevile lile alilolisema Kadinali Pengo nalo linamashiko.

Tatizo ni ubinafsi au kutafuta njia ya mkato kufikia kile tunachokitarajia.

Askofu wanaomuunga mkono wanachotaka ni katiba mpya kwa mawazo na fikra zao ndio mwarobaini wa maendeleo,udhibiti wa Mali za umma na uteuzi wa maofisa wa ngazi mbalimbali.

Maamuzi ya mambo muhimu yafanywe kwa utashi wa sheria sio utashi wa viongozi walioko madarakani. Askofu kaeleza msimamo wake kama Mtanzania, japo ni vigumu kumtofautisha mawazo yake na wadhifa wake.

Kadinali Pengo naye kilio chake ni Katiba mpya ila anaomba suala hili liende taratibu na kwa mpangilio huku juhudi zikiendelea kufanywa na serikali katika kuhakikisha Huduma za afya na elimu vinaboreshwa.

Waamini Katoliki ni watiifu kwa viongozi wao ndo maana baada ya kauli ya Askofu Severin NiweMugizi sintofahamu imejitokeza je? Huu ndo msimamo wa kanisa?

Kadinali kwa nafasi yake kama Askofu mkuu wa jumbo kuu la Dar es salaam anawajibika kuwaeleza kondoo wake aliokabidhiwa kuwachunga.

Hivyo na Maaskofu wengine katika himaya zao nao wakiona sintofahamu kwa kondoo wao itawabidi kutoa ufafanuzi.

Kisha kanisa kwa utaratibu wake litakutana na kutoa msimamo wake wa kichungaji na kuitaka serikali nini ifanye kwa wananchi wake.
 
Mkuu raisi wa baraza la maaskofu ni wa Iringa, Ngalalekumtwa alichukua kutoka kwa huyo wa Mwanza Dr. Ruweichi na msaidizi ni Niwemugizi wa jimbo la Rulenge kama sijakosea!
Ndivyo ilivyo mkuu. Huyu pengo anataka kutuaminisha kwamba maneno yake ndo msimamo wa kanisa. Anataka kuwa kama makonda anajifanya yeye ndo mkuu wa wakuu wote wa mikoa
 
Unakumbuka alichokifanya baba Kardinal Pengo wakati wa mvutano wa mahakama ya Kadhi?
 
Hamjamuelewa Pengo. Kasisitiza kuwa kuna utaratibu wa kanisa kuhusu kutoa matamko ya kisiasa. Sasa wapinga kila kitu wanakuja na mipash yao. Kwani pengo kasosea wapi? kwani Pengo kasema hataki katiba mpya?
We nae umekutupuka tu msome pengo mpaka mwisho ndo ujue mawazo yake juu ya katiba anataka nini.
 
Nae si alipewa mgao wa Escrow? Ndo maana haoni umhimu wa katiba
 
Pengo ni mtu wa heshima na anajua mipaka yake ya madaraka. Usilazimisha aingie kwenye siasa kama unavyotaka wewe.
Angejua mipika yake ya madaraka asingekuwa anasemea kanisa. Maana yeye siyo msemaji wa kanisa. Msemaji ni Mkutwa
 
Hata yy aliyoyasema si msimamo wa baraza la maaskofu ninavyofaham Mhasham Baba Askofu Niwemugizi ni makamu wa rais wa baraza la Maaskofu Tanzania lbd kama kuna mabadiliko yalifanyika lkn pia kardnal kwa sasa c mwenye afya njema kwa muda mrefu lkn pia na uzee hatuwezi jua hiyo ni kazi ya MUNGU szan kama yuko sawa sana ki fikra tumwachie roho mtakatifu ambaye ndiye mlinzi wetu,lkn pia c vibaya kwa pengo kumtetea rafiki yake huyu sizonje, niwemugizi ni mtu wa kusema kweli.
Asiyejitambua huyu! Kauli ile ni msimamo wa Watanzania tulio wengi. Unazidi kupoteza mvuto kwenye jamii ya Watanzania kwa kutokemea maovu ya dikteta uchwara.
 
Hilo ni Pengo kweli aisee si ndio huyu alisema waacheni wana nchi wachague kula ya ndio au hapana wala wasishauliwe juu ya Katiba alaf sahivi anasema nini tena!!!! Hili pengo linatumika na serikali.
 
kubali kuelimishwa na wanaojua protocol ya kanisa katoliki. Tunaojua 2nakucheka tu, kwa Ww kuona Cardinal ni mkuu wa Maaskofu ktk nchi husika. Umeelimishwa lakini bado unajitia uchizi.
 
Mkuu, Pengo ni askofu mkuu jimbo kuu katoliki la Daresalaam lkn pia ni kardinal Tanzania.
 
Pengo anatumika vibaya sana aachane na uaskofu ateuliwe hata ukuu wa wilaya...
 
Naona kama Kardinali alikuwa out of context kabisa!
Askofu Pengo amekuwa misquoted. Yeye kasema Askofu Niwemugizi ni Mtanzania ana haki ya kutoa maoni yake, lakini ili kutowakwaza waamini ni vyema asisitize kuwa ni msimamo binafsi. Hii ni kwa vile Mkristu ukiona Askofu wako akisema yuko tayari kufa "kutetea katiba ya Warioba" au yuko tayari "kuitwa mchochezi" kutaka katiba mpya, huyo haongei Kimungu.

Halafu kasema yeye Pengo hana uelewa wa economics au kilimo cha kisasa, kwa hiyo si sawa kujipiga kifua akitoa maneno makali halafu adai ni maoni binafsi. Ila kasema iwapo Askofu Niwemugizi angesema "Mungu ni mmoja", hapo angeeleweka kwa vile ana utaalamu nalo.

Hii ni safari ya pili Askofu Pengo kuokoa jahazi: wakati wa mchakato wa katiba, huyu huyu Niwemugizi aliitaka serkali ichapishe kaiva vitsbu milioni 27 kuwatosha wapiga kura wote (ni nyingi kuliko Biblia), akasema Watanzania waisome katiba tarajiwa, waielewe, halafu waikatae (vitabu milioni 27 tule hasara!!), na kwenye uchaguzi waikatae CCM.

Ndipo Kard. Pengo akawataka Watanzania waisome katiba, waielewe, halafu waamue wenyewe.

Askofu Niwemugizi wa Dayosisi ya Ngara anajulikana katika Kanisa kuwa ni mtu wa CHADEMA. Kabila lake ni Mhutu.
 

Siyo kweli! Mimi ni Mkatoliki na sifuati kauli tu kwa vile imesemwa na papa, askofu, padre, katekista au kiongozi wa jumuiya ndogondogo mpaka iwe na ushawishi kwangu kwamba haipingani na neno la Mungu na ina mchango chanya kwa imani ya Kanisa na imani yangu na pia ustawi wangu na wa familia yangu. Nje ya criteria hii, papa, askofu, padre, katekista au kiongozi wa jumuiya ndogondogo anajisumbua maana sitafuata neno lake.

Hivyo, siyo kweli kwamba "Wakatoliki ni watiifu kwa viongozi wao". Labda ungesema "baadhi ya Wakatoliki ni watiifu kwa viongozi wao" (maana hata wakiambiwa mambo yasiyo ya msingi wanatii). Kwangu siyo hivyo - hata mahubiri ya padre nayachuja kama hayakidhi kiwango hata sisikilizi, natoka nje ili amalize au nakacha kabisa. Ninafuata imani yangu kwa uhuru na si kwa kumwogopa kiongozi wa kiroho maana hivi ndivyo nilivyoelelewa.
 
kubali kuelimishwa na wanaojua protocol ya kanisa katoliki. Tunaojua 2nakucheka tu, kwa Ww kuona Cardinal ni mkuu wa Maaskofu ktk nchi husika. Umeelimishwa lakin bado unajitia uchiz.

Siyo kweli. Lengo Siyo msemaji wa Kabisa Mkatoliki,Msemaji ni Rais wa Baraza la Maaskofu. Kila Jimbo Lin askofu wake ambaye anareport kwa balozi wa Vatican ndiyo sababu Pengo hana uwezo wa kumsimamisha Padre au Askofu wa Jimbo lolote labda jimboni kwake tu.
 

Askofu Niwemugizi alieleweka vizuri sana, labda Kardinali Pengo ndiye hakumwelewa.
 
Anafafana na huyu wa tz mana mda wake umeisha amekomaa na kudai akizindua parokia 100 bas atastaafu amefika 120 amebadili eti mpk afe akiwa askofu sasa anatetea mwenzie mi sishangai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…