Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Sheikh mkuu wa Dar#kadinali pengo
--Mbona huyu hajatolea jibu rushwa ya Kilaini kama ilikuwa ni ya kilaini kama kilaini ama ya kanisa?
 
Yaani huyu Mzee kwa kweli anachekesha sana,alikuwa anampinga Kikwete kila jambo lakn sasa hivi eti anakanusha hata ukweli ulio wazi jamani hatari sana.
Alikuwa anampinga JK kwa kuwa hakuwa upande wake sasa hv huyu aliyekuwepo ni wa kwake atafanya kila liwezekanalo kumlinda.
 
Mhashamu Askofu Kardinali Pengo amesema kuwa kauli iliyotolewa na askofu Niwemugizi kuwa katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi sio msimamo wa kanisa kwa sababu kanisa lina taratibu zake za kuishauri serikali au kuzungumzia masuala ya jamii.

Pia amesema kwake yeye katiba ni kitu kije baadaye si cha haraka.

chanzo: gazeti la Mwananchi via facebook.
Huyu naye si yupo Escrow? duuuuuh hapa anatafuta huruma ya dikteta uchwara au mie simuelewi vile
 
Kwenye ile kongamano alialikwa yeye kama yeye au alikuwa anawakilisha kanisa
 
Hapa ndio maana humpenda Gwajima. Hatafuni maneno
 
A person from the same system will never reject the boss.
 
Pengo ni mtu wa heshima na anajua mipaka yake ya madaraka. Usilazimisha aingie kwenye siasa kama unavyotaka wewe.
Busara yake ya dini, kuzingatia amani na upendo ingemtuma kwenda kujadiliana mwenzake aidha amshauri aje athibitishe yeye mwenyewe kuwa hayo yalikuwa mawazo yake mwenyewe. Kuchukua uamuzi wa kumpinga hadharani si ukomavu kidini, si busara wala haionyeshi kuheshimiana wala kupendana kama dini inavyowataka wawe mfano mzuri kwa waumini wao
Kwahiyo kwa hilo amekuwa mwanasiasa zaidi badala ya kiongozi wa dini.
 
Wakati wa Jakaya Kanisa lilishiriki kuishinikiza Serikal kuleta Katiba Mpya japo hapakuwa na Huduma bora, Leo Wanatumia kigezo cha Huduma bora kukataa Katiba Mpya, kweli Mchezaji kwao hutuzwa,
Hongera Rais John Joseph kwa kuungwa Mkono na Kanisa kwa kila jambo
 
Huyu mzee anazeeka vibaya maana yeye syo msemaji wa maaskofu wala kikanisa syo kwamba yeye no bosi wa maaskofu wenzake
Vijana wa upinzani hata leo Mungu akirudi akasem anaikubali ccm mtampiga mawe
 
esitena tetena,

Kuna kitu nashangaa hapa. Haikuwa na haja kumjibu askofu au kufafanua,maana askofu aliyetamka hayo alisema kabisa kwa uwazi kabisa kuwa anayoongea si msimamo wa kanisa ni msimamo wake binafsi.
Napata mashaka kidogo km viongozi wa dini tena wasomi hawajui umuhimu wa katiba bora kiasi wanaona siyo kiaumbele,maisha yetu ya kila siku yamefungwa na yanaathiriwa moja kwa moja na katiba,
 
Soma vizuri na uelewe....

hatuitaji uwe mtetezi wa huyu mzee aliyekumbatia watesi wa watu wa mungu....

huyu tunamjua amefunga ndoa na farao na yupo kwa manufaa ya farao tokea enzi za katiba mpya ya warioba na alikubali kujitenga na maaskofu wengine wote japo anajiaminisha kuwa yeye ndio kubwa la maaskofu wote tanzania.

#maharageyawapialiyokulahuyumzee#
Naogopa kusema wewe ndio hujanielewa!
 
Asiyejitambua huyu! Kauli ile ni msimamo wa Watanzania tulio wengi. Unazidi kupoteza mvuto kwenye jamii ya Watanzania kwa kutokemea maovu ya dikteta uchwara.

Nyie msiopoteza mvuto muuonyeshe kwa kuijenga nchi yenu lakini si kuibomoa. Kuwa domokaya majukwaani na Ustashi wa kusimamia yale unayoropoka ni vitu viwili tofauti.

Kutokana na uchovu wenu mmewapoteza kisiasa baadhi ya waliokuwa bright kwenye upinzani.

Huwa najiuliza, endapo Magufuli angeachana na ajenda za maadili, hivi CHADEMA wangeweza kuibeba tena agenda yao ya maadili tangu Lowassa na "ma-grand EPA" wengi kumfuata CHADEMA?
 
Back
Top Bottom