Mwanahabari Huru
Askofu Pengo unafiki sio sehemu yetu wakatoliki, sikutaka kuandika chochote kuhusiana na wewe, mimi nimebatizwa katika RC nimekuwa muumini mkubwa, nimesoma shule ya Upadri St Mary's Seminary, ninaijua Rc.
Nimesikitishwa sana na kauli zako za kipuuzi, zilizo jaa unafiki, tumekusikia sana ukijipambanua kuwa wewe si muumini wa mabadiliko, tuambie upande wako ni UPI.
Askofu wangu Pengo umemjibu Askofu Niwemugizi alie jitokeza hadhalani na kusema watanzania wanataka katiba mpya, umefufuka ulikotoka na kumshambulia Askofu kuwa katiba au maneno ya Askofu sio msimamo wa RC lakini hakusema kuwa ni msimamo wa RC. Lakini unajua Askofu Niwemugizi si msemaji wa Rc, maana yake alisema kama Mawazo yake kikatiba, na wewe unamjua msemaji wa RC ulitaka kutafuta uhalali wa kujibu mashambulizi la watawala, of target.
Naona umetoka kwa kasi sana kujibu shambulizi hill!,! Lakini hutoki hadhalani kuonya matukio ya kuuwawa kwa watanzania na kutupwa kwenye maji wakiwa wamefungwa mikono Nyuma, wanaopigwa Risasi kama kina tundu Lissu, kuonya viongozi wanao toa maneno ya kibaguzi na kikabila, huwezi kuonya kufokea au kushauri, kazi yako imekuwa ni kujibu mashambulizi kwa wanao ikosoa serikali,
Au unavyeti feki? Unamiliki Mali zisizo halali? Kiongozi wa kiroho unashindwa kujua nini wajibu wako? Sio mala ya kwanza kupingwa na maaskofu wenzio akiwepo Gwajima na kupelekana mahakamani ambapo Askofu Gwajima alikushinda kesi.
Viongozi wa dini simamieni haki na sio unafiki kujipendekeza kama mnataka ubunge, au teuzi za kina mama Lwakatale sawa, Hata mkitaka usemaji wa Ccm nafasi za kina polepole.
Swali la Kizushi: WATU WASIOJULIKANA WANATOKEA RWANDA PREY FOR TUNDU LISSU