Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Hivi Moses Kulola amefufuka?

No. Nilichomaanisha ni kwamba wote hawa wawili katika umri wa kufanana (wa uzee) waliegemea sana ccm. Kumbuka coments za Moses Kulola kuhusu Kikwete na ccm wakati ule; linganisha na hizi za Pengo sasa. Same shit.
 
Moses Kulola anasemaje chifu? Sijamsikia!

Reference yangu ni coments za marehemu Kulola kwa Kikwete na ccm in his old age during those days of Kikwete reign. Kuna mfanano wa kutosha na coments za Pengo katika uzee wake huu.
 
Siku hizi hata ukimuuliza muumini Wa kawaida Wa kanisa katoliki hamjui huyu pengo.
Unazungumzia kanisa Katoliki tulijualo au la kwako hilo ambalo waumini hawamjui Mwadhama Kardinali Pengo?
 
Natumaini na maoni aliyotoa Mwadhama ni yake si ya Kanisa Katoliki
Kwanza hakufuata utaratibu wa ndani wa kusuluhisha tofauti za ndani.Kawahi mbele kumwanika mwenzie vibaya kwa kiasi cha kutosha.Na kam siye msemaji ni wazi kuwa Gwajima ana mashiko kuwa huyu jamaa kalishwa nini?Mbona anakwenda kinyume na wenzie?Kaamua kuwa Lipumba wa katholic.
 
Nadhani wampuuze kama kipindi kile cha katiba pendekezwa
Ugonjwa haupuuzwi. Alipuuzwa kipindi gwajima alisema anashangaza,sasa wenzie nao wanshangaa.Yupo kinyume nao.Na kwa nini asema yeye km yeye sie msemaji?Huyu mzee anaweza kuwa muasi sasa hivi.
 
Kardinali Pengo,amesema jambo ambalo ni sahihi kwamba alichosema Askofu Niwemugizi sio msimamo wa Kanisa Katoliki bali ni wa Askofu Niwemugizi.Sasa alichokosea ni kipi?Au mlitaka aseme huo ndio msimamo wa Kanisa wakati si kweli?
 
Pengo amwombe Roho Mtakatifu ili daima asimame kwenye mafundisho ya Kanisa. Anajitahidi kuyashinda mapenzi yake binafsi. Najua yeye ni mkatoliki kiongozi, anayezijua siri za imani, matokeo ya watu mbalimbali akiwemo Mama Bikira Maria na miujiza yake kwa wateule wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Kati ya siri alizoambiwa Sr Lucia ni kwamba kuanzia mwaka 2000 shetani atafanya kazi kubwa kwa kupitia viongozi wa Kanisa. Viongozi wengi watatumika na shetani, wengi wa waumini watapotea kwa kuwasikiliza viongozi wanaotumika na shetani, maana watadhani kauli zao ni takatifu kumbe ni kazi ya shetani.

Kuna taarifa za uhakika kabisa 100% kuwa kuna watu wawili tu ambao Mkuu wetu anawasilikiliza. Hao hata kama wakimwambia kuwa tunataka uje mara moja, atakwenda. Lakini amekataa kupokea ushauri wa mamilioni ya Watanzania. Wanaosikilizwa mmoja ni Pengo na wa pili ni Ben.

Kule Rome kuna Papa ambaye alijishikamanisha sana na watawala wa Dunia, hata akamkalisha kwenye kiti cha Upapa mfalme wa Ufaransa. Wakakubaliana kuyahamisha makao makuu ya kanisa toka Rome kwenda Paris. Walihamisha kila kitu lakini walipotaka kuchukua mifupa ya Petro na Paulo, kengele zilianza kugonga pekee yake. Waliporudisha zikatulia. Hicho ndicho kilichozuia Kanisa kutohamishwa makao yake makuu mpaka leo.

Pengo ajiangalie sana. Asije akakubali kutumika na watawala kwa faida zao kwa gharama ya imani yake na waumini wanaomwamini. Ayaishi mafundisho ya Papa Francis, 'Kanisa siku zote lijiepushe na kutetea watawala na matajiri. Wakati wote lisimame na watu wa kawaida, maskini na wanyonge maana hao hawana wa kuwatetea'
 
Uingereza haijawahi kuwa na katiba na haina mpango wa kuwa na katiba lakini ni nchi iliyoendelea.Katiba sio kipaumbele cha maendeleo
Usikariri! Nani aliyekudanganya kuwa UK haina katiba? UK does not have a codified constitution. Hiyo haina maana kuwa haina katiba. Katiba yao imeundwa na Acts of Parliament, Court Judgments na Conventions.
 
Kardinali Pengo,amesema jambo ambalo ni sahihi kwamba alichosema Askofu Niwemugizi sio msimamo wa Kanisa Katoliki bali ni wa Askofu Niwemugizi.Sasa alichokosea ni kipi?Au mlitaka aseme huo ndio msimamo wa Kanisa wakati si kweli?
Kwani ni wapi Askofu Niwemugizi alisema huo ni msimamo wa kanisa?

Kwanza uelewe Pengo hana mamlaka ya kiuaskofu nje ya jimbo lake la Dar es salaam.

Pili uelewe Pengo siyo Kiranja wa Maaskofu wenzake.

Tatu uelewe maaskofu wote wa majimbo Tanzania wana hadhi sawa hili wengi hamlijuhi, hakuna mkuu wa Maaskofu.
 
Wakuu natanguliza salamu .

Maelekezo makuu ya Mungu kwa wanadamu ni kuishi katika kweli iliyojaa haki tupu , kutenda mema na kukataa maovu , hivyo tunategemea kiongozi yeyote wa dini ya kweli aishi na atende kama Mungu alivyoelekeza .

Kardinali Pengo anatenda kinyume na Maagizo haya ya Mungu , ni wazi ameamua kujipambanua kuukumbatia unafiki , Amejipachika usemaji wa Kanisa kinyume cha utaratibu .

Ni vema sasa Kwa kulinda heshima yake lililojiwekea miaka mingi , kanisa Katoliki linapaswa KUMTIMUA kardinali Pengo ili akaendeleze harakati zake za kupinga katiba mpya ndani ya chama chake cha ccm .

Naomba kuwasilisha .
Tatizo lenu mnapenda kuyasikia yanayopendeza masikio yenu tu.
Pengo hang'oki kwa mkutano kama simba wanavyotimua kiongozi wao,au KKKT,tulieni tu dawa iwaingie,mlijaribu kutukana masheikh sasa mmeingia kwa viongozi wenu,hiyo dola atakupeni nani kila sehemu mmetukana ndio maana Lowassa aliwaambia acheni uanaharakati hamuwezi kuchukua dola kwa kutukana watu.
 
Hamjamuelewa Pengo. Kasisitiza kuwa kuna utaratibu wa kanisa kuhusu kutoa matamko ya kisiasa. Sasa wapinga kila kitu wanakuja na mipash yao. Kwani pengo kasosea wapi? kwani Pengo kasema hataki katiba mpya?
Khaa unashida wewe askofu Ningemugizi hakusema hili ni tamko la kanisa katoliki iweje ajekumpiga as if yeye ndiyo analisemea kanisa hapo huoni?
 
Nani anamjua Nimewemugizi bhana? Pengo ndo kiongozi mkuu wa kanisa katoliki Tanzania, ndio maana wakatoliki kote Tanzania humuombea Pengo katika sala zao baada ya pope, huyu jamaa ndo anatoa report ya maaskofu wote Tanzania kwa pope juu ya mienendo yao na ku propose nani amrithi hapo baadae ,kwa hiyo pengo ni mkubwa wao.
 
Kwa hiyo anayoyasema Pengo ni maoni yake au ndiyo msimamo wa kanisa.
Kwa nini hakuwapa nafasi viongozi wa Baraza la maasikofu wakalitolea ufafanuzi?.
 
Usiwe mjinga wa kiasi hicho Seminary ya St Mary's inamilikiwa na Pengo ipo Visiga, Kibaha.
Acha ujinga wewe hiyo ni visiga seminary na siyo saint Mary wewe vipi. Kwanza we mkatoliki gani mbabaishaji hivyo?
 
Msimamo wa kanisa hutolewa mara baada ya Baraza la maaskofu kuketi,so wote hao kila mmoja ametoa maano yake binafsi.
Na kwa inshu ya ukubwa sijaelewa unamaanisha nini kwani kwa mujibu wa kanisa daraja ni la upadri tu hivyo vingine ni vyeo tu vinavyowekwa ili kuwepo kwa usimamizi na kardinali ndio msemaji wa mwisho wa kanisa ktk inchi husika so acha kupotosha watu.
Umesema usichokijua, rudi kaulize tena. Msemaji wa Kanisa katoliki Tz,ni Rais wa Tec ambaye kwa sasa ni askofu wa Jimbo Katoliki Iringa,Mhasham Baba Askofu Ngalalekumtwa. Wewe ndo Unapotosha
 
Kiukweli huyu jamaa nilitokea kumchukia Sana, ni Kati ya viongozi WA kanisa wanaosababisha nisiende kanisani siku hizi, nikiamini ni wapiga dili tu.
Nenda kanisani kwajili ya imani yako kwa Mungu wako,cyo kwasababu ya huyu Mtu
 
Acha ujinga wewe hiyo ni visiga seminary na siyo saint Mary wewe vipi. Kwanza we mkatoliki gani mbabaishaji hivyo?

Visiga ni eneo! Shule hiyo inaitwa St.Mary's Seminary. Mimi nilisoma St Peters Junior Seminary, Morogoro chini ya uongozi wa Fr.Octavian Linuma, padre wa Jimbo la Mahenge. Enzi za Mwadhama Laurian Kardinali Rugambwa. Wakati huo visiga yako hata uwanja haujanunuliwa!
 
Back
Top Bottom