Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Hamjamuelewa Pengo. Kasisitiza kuwa kuna utaratibu wa kanisa kuhusu kutoa matamko ya kisiasa. Sasa wapinga kila kitu wanakuja na mipash yao. Kwani pengo kasosea wapi? kwani Pengo kasema hataki katiba mpya?
Maelezo yooote bado hujamuelewa tu.
 
Hufuati kauli ya Askofu? Basi wewe si Mkatoliki. Kama unatawaliwa na ushawishi wako unatawaliwa na ushawishi wa shetani. Endelea na hoja yako kama katiba inavyokuruhusu lakini futa kusingizio cha ukatoliki.

Kama wewe unafuatafuata tu uamuzi wako. Kwangu siyo hivyo - lazima nichuje baba - a 'methodical doubt' approach!
 
Tafuta ufafanuzi wa neno hili la kilatin ROMANA LOCUTA KAUTAFILITA.

Kisha ww ni mmoja unayepinga na kutoka nje waliowengi hubaki ndani bado hujajitafakari.

Soma vizuri construction ya sentensi zangu na uelewe na ndiyo unijibu. Kwa kukusaidia nimesema "sifuati tu" (I don't just follow) kama mbuzi, ninafuata kama yananigusa kiimani, kimaadili na kijamii. Huu ndio msimamo wangu. Kiongozi yoyote anayesema mambo yanayogusa (katika mambo hayo) najifunza kwake. Kiongozi anayesema mambo yanakwaza (maana hata hawa wapo) sifuati.

Hii ndiyo ilikuwa maana yangu ya msingi na sikutaka ieleweke kwamba ukiwa Mkatoliki basi wewe unafuata tu bila kutumia akili (maana ndilo lengo la mtoa hoja kutaka kuwaaminisha wasomaji kuwa Wakatoliki 'wanafuata tu' kinachosemwa na viongozi wao kitu ambacho si kweli). So, don't drag me out of the context.
 
Nimekuelewa vizuri, ateast hata wengine walio nje ya mfumo catholic tunaweza elewa, niko na swali lingine, mfano ukiangalia katika archibishops or bishops wengi, majina yao mengi yanaanza na Rev francis,or Rev Musa, lakini ikifika kwa cardinal wanaanza na His eminence makanga etc, pengine haiwezi ikawa ni unification figure within the Catholic Church and society?.

Kanisa Katoliki lina mbwembwe nyingi sana mojawapo ni hiyo. Makardinali ili kujitofautisha na maaskofu wengine walipangwa waitwe hivyo, sio wao tu askofu wa kawaida husalimiwa kwa His Lordship.....Askofu Mkuu ni His Grace....... Kardinali His Eminence na Papa His Holiness na ole wako hukosee hizo salamu! Hata Majina ya Papa ile wanasema John Paulo wa Pili ile "wa pili" hata uwe unatoka kabila gani lazima uiandike kirumi na sio vinginevyo. Angalia hata vikofia vyao vinatofautiana rangi kwa seniority. Hapa Tanzania hawa Maaskofu wetu wanavaa makanzu meupe ni ruhusa maalumu tu kwa sbb ya joto waone wakienda vatican lazima makanzu meusi....mnakumbuka mke wa Trump hakujifunika kichwa chake Saudia lakini alijifunika mbele ya papa!!!!!!

Watanzania wanadanganywa sana kwa sababu ya uvivu wa kujisomea......hivi wanavyosema ni kauli yake binafsi sio kweli.....kauli ya askofu popote pale ni msimamo wa kanisa kwa wale anaowaongoza.....kwa maana nyingine askofu ndio jimbo na jimbo ndio askofu....! Papa aliposema yeye ni nani hata hawahukumu mashoga..... usidhani ni kauli eti yake binafsi..... ni msimamo rasmi huo wa kanisa! Ambao tumeishi nao hawa jamaa wana mbwembwe sana kwa mfano akikupigia simu hajitambulishi kwa jina lake...... atasema jimbo linaongea!!!!!!
 
Pengo ni kati ya viongozi wa RC wanaonifanya niutafakari sana Ukatoliki wangu
 
Asiyejitambua huyu! Kauli ile ni msimamo wa Watanzania tulio wengi. Unazidi kupoteza mvuto kwenye jamii ya Watanzania kwa kutokemea maovu ya dikteta uchwara.

Watanzania mlio wengi ni nani nani??? Mbona mimi na ninao wafahamu hicho sio kipaumbele chetu??
 
Asiyejitambua huyu! Kauli ile ni msimamo wa Watanzania tulio wengi. Unazidi kupoteza mvuto kwenye jamii ya Watanzania kwa kutokemea maovu ya dikteta uchwara.
Sasa kama ni watanzania mlio wengi unadhani automatic ndio utakuwa msimamo wa Kanisa Katoliki? Hebu soma vizuri msomi anavyokueleza kuwa Kanisa Katoliki lina taratibu zake sasa yeye kasema kama yeye binafsi. Who are you kulazimisha ndio msimamow a Kanisa Katoliki?
 
Kardinali sio askofu wa kawaida. Ujue kwanza ni askofu wa Raisi wa nchi. Magufuli askofu wake ni pengo
.pili kardinali ana Siri za kanisa katoliki za dunia nzima na za Vatican ambazo askofu mwingine wa kawaida Hana sababu ni mjumbe wa vikao vizito vya Vatican ambavyo husimamia Mambo Ya kanisa. Pengo ni mtu wa Karibu na Papa. Magufuli akitaka kitu cha kumwambia Papa anaongea na pengo ambaye ni mtu wa karibu na Papa akamwambie hawezi kuongea na Niwemugizi ambaye mwisho wake ngara

Mhu! Hapa kuna kuchanganya mambo! Hujaelewa vizuri mfumo wa uongozi kwenye Kanisa Katoliki.
Kwa cheo cha pengo ukuu wa wilaya,mkoa hata huo urais c chochote kwa kardinal hata uraia wa kardinal ni mataifa yote duniani mfano anaweza kuwa raia wa Tanzania lkn akawa mwakilishi wa papa popote duniani au kuwa kardinal wa Marekani wakati ni ktanzania hata tu askofu wa wa kawaida hawezi linganishwa na wilaya au mkoa.

Mhu! Unajua ukadirnali siyo cheo cha madaraka? Cheo cha madaraka ni uaskofu.
 
Sizani kama kuna nilichokosea hapo,lkn unajua yakuwa askofu pia ni padri?na ili uende hatua ya uaskofu radhma upitie upadri lkn ili ufike kwenye ukardinal radhma ufike kwenye uaskofu je kardinal ni nini?jina au?plz nieleweshe mkuu
 
Nani anamjua Nimewemugizi bhana? Pengo ndo kiongozi mkuu wa kanisa katoliki Tanzania, ndio maana wakatoliki kote Tanzania humuombea Pengo katika sala zao baada ya pope, huyu jamaa ndo anatoa report ya maaskofu wote Tanzania kwa pope juu ya mienendo yao na ku propose nani amrithi hapo baadae ,kwa hiyo pengo ni mkubwa wao.

Kaldinari Pengo angesaidia sana kama yeye angeweka maoni yake binafsi ya kanisa analoongoza ili kuweka utofauti kati yake na yake maoni mengine.
 
HV huyu anafikiria kweli?

Aliuoataje uaskofu?

Hauoni kama tukiwa serious na katiba mpya hata huyo mtoto hawezi kukosa dawa au kufa njaa?

Huyu askofu Pengo huyu ndo maana gwajima alimuuliza umekula maharagwe ya wapi. Leo nimeelewa
 
Kwa mujibu wa taratibu za kanisa katoliki,askofu pengo sio msemaji wa kanisa,Msemaji ni Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania,

Rais wa Baraza la Maaskofu ndio Bosi wa Maaskofu wote nchini na hata askofu pengo anakuwa yuko chini yake, pia kama askofu pengo hakiutumwa na Rais wa Baraza la Maaskofu,na yeye pia hana mamlaka ya kulisemea kanisa katoliki na alichosema ni maoni yake


Ukadinali wake ni kwa ajili ya kupiga kura kumchagua Papa tu,ila yeye akiwa Tanzania kicheo ni Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam,anataka watu waone kwamba Ukadinali ndio Ukubwa wa kanisa,Mkubwa wa kanisa ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,na ni askofu wa Iringa Askofu Ngalalekumtwa na anayefatia kwa Cheo ni huyo Niwemugizi, Pengo yuko chini yake Rais wa Baraza

"first among equals" Pengo hamzidi Askofu yeyote kwa cheo,ni sawa na rafiki yangu sheikh mkuu wa mkoa wa Dar ajione mkubwa kuliko mashehe wa mikoa mingine
Hujui nini maana ya cheo, hawazidiani cheo cha uaskofu,lakini cheo cha mfuatano wa kikangazi ya kanisa kwa kufuata hairakia ya kanisa Pengo ni mkubwa kuliko askofu mwingine wa nchi na taifa la kikanisa.
 
HATA HAYO ALIYOSEMA PENGO NI MANENO YAKE BINAFSI, Maneno ya Kanisa katoriki hutolewa na Mwenyekiti wa baraza za maasikofu Tanzania ambaye ni Askofu Severini Niwemugizi.
 
HV huyu anafikiria kweli?
Aliuoataje uaskofu?
Hauoni kama tukiwa serious na katiba mpya hata huyo mtoto hawezi kukosa dawa au kufa njaa?
Huyu askofu Pengo huyu ndo maana gwajima alimuuliza umekula maharagwe ya wapi
Leo nimeelewa
Kwa hiyo kazi Ya askofu ni kutafuta katiba mpya? Uwiii mbavu zangu mie
 
Hovyo sana huyu jamaa. Mbona yeye ana kimbilia kujibu as if ndiye msemaji wa Kanisa? Kila nikilifikiria kanisa kwa hivi sasa na huyu jamaa, huwa naomba mapenzi ya Mungu yatimizwe juu yake
We Jamaa!!unaomba mapenzi ya MUNGU YATIMUZWE JUU YAKE?hahahaha
 
Pengo yuko sahihi maana Kuna hawa wanasiasa uchwara huwa wanaenda kuwatumia viongozi wa dini kama njia.
Naona vijana wa Bavicha mnatokwa na povu baada ya Pengo kuwapiga za uso.
 
esitena tetena,

Wakuu, nionavo mie tatizo si akisemacho Pengo ila ni wale waliomuhoji kutaka afafanue kauli ya Askofu Niwemugizi. Ladba walitumwa ila ingekuwa jambo la busara kupata ufafanuzi wake yeye mwenyewe Askofu Niwemugizi.
 
Pengo yuko sahihi maana Kuna hawa wanasiasa uchwara huwa wanaenda kuwatumia viongozi wa dini kama njia.
Naona vijana wa Bavicha mnatokwa na povu baada ya Pengo kuwapiga za uso.
Hata yeye anatumika mkuu. Anajifanya ndo Kanisa Katoliki la Tanzania.
 
Back
Top Bottom