Peniela (Story ya kijasusi)

Peniela (Story ya kijasusi)

Roho nyeusi mtakuwanazo ninyi msiojua subra ni nini.? LEGE pia ni mtu wa majukumu, yanini tumkimbize au kumshurtisha afanye haraka kanakwamba tunamlipa humu?
Sasa hapa unapata burudani gani kusoma vijipande vya story kisa haraka zako?

We mbwiga mbona unajipendekeza hivyo,

Kwani aliyesema story inakuja leo ni sisi au ni Lege? Wewe ndiye unayetaka story ije hapa saa tano kwa kipi ulichonacho..!!

Lege akisema hii story inakuja kesho, keshokutwa, mtondogoo tutamsikiliza, siyo wewe pangu pakavu, kama watu wamevumilia wiki mbili watashindwaje masaa.!!!!! Lege akisema story inakuja saa tano tunasambaratika hapa lakini siyo kwa kupitia kinywa chako pangu pakavu wewe..

Angalia usije kumfunulia skirt kisa Story.. Unajipendekeza vibaya sana.

BACK TANGANYIKA
 
SEHENM YA 2


“ Shhh..!!My love I’m not here to fight.Please calm
down and tell me whats wrong with you and why you are so
angry at me today.Sijawahi kukuona ukiwa katika hali hiyo
hata siku moja.Lakini kabla ya yote tafadhali naomba nikupe
kile ambacho umekuwa unakihitaji sana.” Akasema Peniela
na kumkumbatia Dr Joshua na kuanza kumwagia mabusu
mfululizo.Dr Joshua akakosa cha kusema kwani hasira
zikampotea ghafla na kujikuta akipandwa na mdadi na
kumkumbatia Peniela.Peniela anamfahamu Dr Joshua na
anayafahamu maeneo ambayo yanampa uchizi mzee huyu
hivyo akayatumia vyema kumpagawisha na kumfanya atoe
miguno.
“ You called me devil,I’m going to show you I’m a real
devil” akawaza Peniela na kumsukumia Dr Joshua kitandani
akaanza kumchojoa nguo moja moja na kuendela na utundu
wake huku Dr Joshua akilalama kama mtoto na kuongea
maneno ambayo hayakuwa yakisikika vizuri,yote hii
ilisababishwa na raha alizozipata.Peniela alipohakikisha Dr
Joshua amepagawa vya kutosha akajiweka tayari kwa ajili ya
mtanange.
Mtanange wa dakika thelathini ulimuacha Dr Joshua
akivuja jasho kama mkimbiaji wa mbio ndefu.
“ This woman is real amazing.Kila ninapokutana naye
ananifanyia vitu ambavyo sijawahi fanyiwa na kuzidi
kunipagawisha.Sijui ni uchawi gani anaoutumia kunivuruga
akili yangu namna hii.Mambo aliyonifanyia leo yamenifanya
hata hasira zangu zote nilizokuwa nazo juu yake zipotee.I
think I still love this woman so much.Pamoja na yote ambayo
jaji Elibariki alinieleza kuhusu Peniela but I still love her and I
don’t know what I’m going to do because I cant let her
go..Mara ya kwanza alinisaliti kwa kuanzisha mahusiano na
Edson na kwa namna alivyoniudhi nilitamani afungwe kifungo
kirefu gerezani ili apotee kabisa lakini ikashindikana na
nilipokuja kuonana naye tena hasira zangu zote juu yake
zikapotea na nikajikuta nikimpenda zadi na zaidi.Safari hii
tena baada ya kupata taarifa za anachokifanya dhidi yangu
nilimchukia na nikamuweka katika orodha ya watu ninaotaka
kuwashughulikia lakini baada ya kuonana naye hasira zote
zimepotea na kwa mara nyingine ninajikuta nikizidi
kumpenda Peniela.Mapenzi niliyonayo kwa Peniela ni
makubwa mno na sijui kwa nini ameshindwa kulitambua
hilo.Ni kiasi gani anacholipwa na hao watu wanaomtumia?
Ninaamini hakuna kiasi anachoweza kulipwa kinachoweza
kulingana na upendo wangu kwake” akawaza Dr Joshua na
kugeuka akamtazama Peniela
“ Muda si mrefu nitamaliza kipindi changu cha
uongozi na kwenda kuishi nje ya nchi.Nitaishi maisha ya
kifahari mno kwa nini basi nisiende kuanza maisha yangu
mapya na mrembo huyu ambaye ametokea kunipagawisha
kuliko wanawake wote hapa duniani? Siwezi kumfanya
chochote Peniela hata kama ni kweli amekuwa anatumika na
watu kutaka kunihujumu kwa sababu bado ninampenda
sana.Ni mwanamke pekee ambaye ananifanya nijione nina
miaka ishirini kila ninapokuwa naye.Lazima nifanye kila
ninavyoweza mpaka niondoke naye.Utajiri wote nitakaokuwa
nao hautakuwa na maana kama sintakuwa na Peniela..”
“ Dr Joshua ..!!” akaita Peniela kwa sauti laini na
kumuondoa Dr Joshua mawazoni.
“ Unasemaje Peniela? Akauliza Dr Joshua
“ Earlier you called me evil witch ,what was the
meaning to call me that? Am I a witch to you now? Akauliza
Peniela Dr Joshua hakumjibu kitu akamkazia macho
“ Sikutegemea kabisa kama siku moja Dr Joshua
ungeweza kunitamkia maneno kama yale.Kitu gani kibaya
nilichokufanyia mpenzi wangu kiasi cha kuniita majina yale
mabaya? Tafadhali nieleze Dr Joshua kama kuna chochote
nilichokukosea”
Dr Joshua akainuka na kukaa kitandani
“ Peniela you you know how much I love you,right?
Akauliza Dr Joshua
“ Yes I know?” akajibu Peniela
“ Toka tumekuwa na mahusiano nimekuwa tayari
kukufanyia jambo lolote ili kukuonyesha ni kwa namna gani
ulivyo muhimu kwangu.Hukuwahi kuniambia chochote
nikasema hapana lakini pamoja na kukupenda kote kwa nini
unanifanyia hivi? Akauliza Dr Joshua
“ Nimekufanyia nini Dr Joshua? Peniela naye akauliza
“ Usitake kuniudhi Peniela.How much do they pay
you? Tell me please how much?? Akasema Dr Joshua kwa
ukali
“ Nani hao? Mbona sikuelewi Dr Joshua ?? akauliza
Peniela
“ Team SC41.How much do they pay you?
Peniela akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Team SC41 ni nini? Akauliza
“ Tuokoe muda Peniela.Ninafahamu kila kitu kuhusu
wewe.Ninafahamu kwa nini uko na mimi na kitu gani
unakihitaji toka kwangu.Nimeskitika sana Peniela baada ya
kufahamu jambo unalonifanyia na ndiyo maana ninataka
kufahamu unalipwa kiasi gani na hao waliokutuma kwangu?
“ Dr Joshua nashindwa kukuelewa unazungumzia kitu
gani kwani hiyo team sijui nini sifahamu ni kitu gani na
wanahusika na nini? Umetoa wapi taarifa hizo?
“ Peniela najua machoni unakataa lakini moyoni
umestuka sana na unajiuliza nimefahamu vipi.Just tell me
how much they pay you and I can pay you back a hundred
times.”
“ Dr Joshua I don’t understand what you are talking
about” akasema Peniela.Dr Joshua akamtazama Peniela kwa
sekunde kadhaa na kusema
“ Kwa nini unanifanyia hivi Peniela? kwa nini unataka
kunifanyia ukatili huu wakati mambo ninayoyafanya ni kwa
ajili yetu sote? Ninataka nitakapomaliza kipindi changu cha
uongozi mimi na wewe tuishi maisha kama ya mfalme lakini
kwa nini hutaki kulielewa hilo na kutaka kuvuruga mipango
yangu? Nilikupa nafasi ya kuchagua sehemu yoyote duniani
unayotaka kwenda kuishi ili tukaishi nitakapomaliza kipindi
changu cha uongozi lakini yote haya umeyaweka pembeni
..Why Peniela??
“ Dr Joshua I real don’t understand you.Mambo
unayonieleza ni mambo mageni kabisa kwangu na siyaelewi.”
 
24hrs ilinifanya kuwa mtumwa ndani ya wiki nzima sikuangalia hata taarifa ya habari. Hadi leo haipiti wiki bila kuiangalia japo kidogo
Duuuh umenikumbusha 24hrs nilitesekaa sana nilizikusanya zotee 1-8 sikuwa nsweza fanya chochote. Juzi mjinga mmoja kaniibia external drive yangu siba tena aisee.
 
mzigo nipo nao hapa ngoja nianze kufanya mchakato ila mzigo wa sasa utanisumbua sana kuutupia aisee.tatizo na nyie mnamchecheto sana ngoja niweke hivyo hivyo
Mkuu kwanini unasema kuwa utakupa shida....je kuna kitu tunaweza kusaidia kurahisisha😵😵😵
 
SEHEM YA 3

“ Peniela ninakupenda sana ndiyo maana
nnakwambia haya ili ufahamu nina lengo zuri na wewe.Mimi
ni rais wa nchi na ninafahamu kila mtu aliye karibu
yangu.Ninafahamu kila kinachoendelea.Uko hapa na mimi
muda huu kwa sababu nimetaka iwe hivyo kutokana na
upendo mkubwa nilionao kwako vinginevyo muda huu
usingekuwapo katika ulimwengu huu”
Peniela akamtazama Dr Joshua huku machozi
yakimchuruzika akasema
“ Dr Joshua ninaomba unieleze ni nani aliyekuambia
maneno hayo? Ni nani huyo asiyetutakia mema katika
mapenzi yetu na anataka kukutenganisha? Do you believe
them than me??
“ Peniela mimi ni raisi na ninazungukwa na watu
ambao wamekula kiapo cha kunilinda hata kama ikiwabidi
kuyatoa maisha yao kwa ajili yangu hivyo ninawaamini kwa
kila watakachioniambia”
Peniela akamtazama na kutikisa kichwa
“ Siamini maneno hayo kama yanatoka kwako.Lini Dr
Joshua utaniamini?
“ How can I trust you Peniela? You are a professional
liar.A cheater !!” akasema Dr Joshua kwa ukali.Peniela
akamnasa kibao
“ Iwe ni mara ya kwanza na ya mwisho kunitamkia
maneno hayo machafu.Kama ningekuwa nina nia mbaya
ningekwisha kufanyia kitu kibaya muda mrefu .You killed
Edson na kesi ikaniangukia mimi.NiIiifahamu wewe ndiye
uliyemuua Edson lakini sikufumbua mdomo wangu kusema
chochote.Nimeteseka gerezani mwaka mzima lakini sikuwahi
kuufungua mdomo wangu na kutamka neno lolote la
kukuhusisha wewe na kifo cha Edson.Iweje leo hii unitamkie
maneno hayo machafu? Akauliza Peniela huku akilia
“ Do you have any proof? Una ushahidi kwamba
ninahusika katika kifo cha Edson? Akauliza Dr Joshua
“ Na wewe una ushahidi wa hayo unayonituhumu
kuyafanya? Akauliza Peniela
“Ndiyo nina ushahidi .Usitake niyaanike mambo yako
Peniela.Ninafahamu kila kitu unachokifanya.Ninaifuatilia kila
hatu unayopiga kwa hiyo ninakufahamu zaidi ya
unavyojifahamu.Nafahamu umetumwa kwangu na Team
SC41,ninafahamu unashirikiana na mtu anayeitwa Mathew
ambaye aliwahi kufanya kazi katika idara ya usalama w a taifa
.Nafahamu umetembea na Dr Kigomba na ulimtumia ili
kufanikisha mipango yenu.Ulimpa saa ya mkononi
mliyoiwekea kifaa maalum cha kuweza kutambua kila mahala
alipo .Kama haitoshi mliunganisha simu yake na mtandao
wenu na mkayasikia mawasiliano yake yote.Peniela
ninazifahamu mbinu zako zote chafu..” akasema Dr Joshua
.Peniela akamtazama na kusema
“ Dr Joshua kitu gani unakitafuta toka kwangu? Kwa
nini umeukubali uongo huu bila ya kufanya kwanza
uchunguzi? Watu unaosema eti ninashirikiana nao ni mara
yangu ya kwanza kuwasikia leo hii.I don’t know them.Halafu
unasema eti nilikuwa na mahusiano na Dr Kigomba? Mimi
Peniela naweza kumuonyesha utupu wangu mtu kama Yule?
Sikutegemea kabisa mtu kama wewe unaweza kuwa
mwepesi kusikia na kuamini maneno ya watu wasiokutakia
mema” akasema Peniela
“ Peniela mambo haya nimeyapata toka kwa mtu
ninayemuamini na ambaye mlikuwa mnashirikiana naye
katika mipango yenu bila ya ninyi kufahamu kuwa alikuwa ni
m tiifu kwangu.Hamkuwa mkijua kama jaji Elibariki ni mtu
wangu.Hahahahaaa…” akasema Dr Joshua na kutoa kicheko
cha dharau
“ Jaji Elibariki ???..Peniela akashangaa
“Ndiyo.Mbona umestuka ? Humjui?
“ Jaji Elibariki Yule aliyehukumu kesi yangu na
kuniachia huru ndiye aliyekuletea habari hizi? Akauliza
Peniela na kutoa kicheko kidogo
“ Nilijua tu kitu kama hiki lazima kitatokea.You are so
fool Dr Joshua.Jaji Elibarikiamekuingiza katika mtego na
wewe kwa kutokuwa na umakini umeingia katika mtego
wake..” akasema Peniela na kutoa kicheko kidogo.Dr Joshua
hakusema kitu akabaki anamtazama
“ Ni hivi naomba unisikilize vizuri Dr Joshua” akasema
Peniela
“ Nilikuwa najiuliza sana ni nani ambaye anaweza
kunitungia uongo mkubwa kama huu? Nilijua tu lazima mtu
ambaye amenitungia uongo mkubwa kama huu atakuwa na
lengo baya na mimi la kuniharibia maisha yangu kwa kutaka
unichukie na uniache kumbe ni jaji Elibariki !!!!..akasema
Peniela na kutulia kidogo halafu akaendelea
“ Nilimfahamu Elibariki alipoanza kusikiliza shauri
langu .Mahakama haikunikuta na hatia na nikaachiwa
huru.Baada ya kuachiwa huru jaji Elibariki akanifuata na
kuanza kunitongoza akidai kwamba yeye ndiye aliyeniweka
huru.Aliendelea kunisonga sana na siku moja usiku alikuja
kwangu akiwa ametapakaa damu akaniomba nimuhifadhi
kwa madai kwamba kuna watu wanamtafuta na wanataka
kumuua.Nilimuonea huruma nikamruhusu alale pale kwangu
na kesho yake asubuhi wakati nikioga alinivamia
bafuni.Unajua alinifanya nini?? Akauliza Peniela kwa
hasira.Dr Joshua hakujibu kitu akabaki anamtazama
“ He raped me !!!!..akasema huku machozi
yakimtoka.Maneno yale yalimfanya Dr Joshua astuke kidogo
na kumtazama Peniela kwa hasira
“ Nilikasirika sana na nikamuweka wazi kwamba
lazima nikueleze kuhusu jambo lile akanitolea vitisho vingi
kwamba nikithubutu kukueleza chochote ataniua.Alipoona
nimeshikilia msimamo wangu wa kuja kukueleza akaondoka
na baadae akarudi akiwa ameongozana na mke wa rais
mstaadfu Rosemary Mkozumi .Kwanza aliniomba msamaha
halafu akaniambia kwamba amemleta Rosemary mkozumi
kwangu kuna jambo wanataka kuzungumza nami.Rosemary
Mkozumi akaniambia kwamba kuna jambo wanataka
kunishirikisha ambalo endapo litafanikiwa nitapata fedha
nyingi sana.Nilitaka kufahamu ni jambo gani hilo na
wakanieleza kwamba kuna kifaa Fulani unacho ambacho
natakiwa kufanya jitihada nikipate na nkifanikiwa basi
nitakuwa bilionea.Waliniahidi kunipa shilingi bilioni kumi
endapo ningefanikiwa.Nilitaka wanifafanulie ni kitu gani
hicho lakini hawakuwa tayari na kwa kuwa tayari jaji Elibariki
alikwisha nifanyia kitendo kibaya cha udhalilishaji mkubwa
sikuwa tayari kushirikiana nao kwa lolote.Baada ya jitihada
zao zote za kunishawishi kushidnikana wakanitolea vitisho na
kunipa muda wa kutafakari na kufanya maamuzi na
wakanionya kwamba nisithubutu kufungua mdomo wangu
na pindi nikikifanya hivyo wataniua.Pamoja na kitisho cha
kuniua lakini sikukubaliana nao na kama utakumbuka
nilikupigia simu na nikakwambia kwamba ninataka kuonana
nawe lengo lilikuwa ni kukueleza kuhusu jambo hili lakini
hatukuweza kuonana kutokana na msiba wa Flaviana.Juzi
usiku nilivamiwa na watu ambao nina hakika walitumwa kuja
kuniua kwa bahati nzuri nilifanikiwa kutoroka na nyumba
yangu ikachomwa moto.Nilijihifadhi kwa rafiki yangu na leo
hii nimeamua nije katika hii nyumba uliyonipa niishi.Kwa hiyo
Dr Joshua mambo aliyokwambia jaji libariki hayana ukweli
hata kidogo.Amewahi kuja kwako na kukupa uongo huu
mkubwa kwani alijua lazima ningekuja kukuona na kukueleza
mambo haya.He lied to you na wewe ukawa mwepesi
kuamini.Dr Joshua mimi sina mpango wowote mbaya nawe
ila nisikilize vizuri ,jaji Elibariki na Rosemary Mkozumi kuna
jambo baya wanalipanga dhidi yako,kuna kitu wanakitafuta
toka kwako.Sikulazimishi uniamini huo ni uamuzi wako.Mimi
nimekwisha kueleza ukweli wangu na utapima nani mkweli
kati yangu mimi au Elibariki” akasema Peniela
Mathew na Anitha waliokuwa garini wakifuatilia
mazungumzo yote kati ya Peniela na Dr Joshua kupitia kifaa
cha mawasiliano alichokivaa Peniela sikioni,wakatazamana
na Mathew akatabasamu
Peniela is real a professional liar.Sikutegemea kama
angeweza kutunga uongo ule mkubwa kwa haraka” akasema
Mathew Anitha hakujibu kitu naye akatabasamu
******
Maneno aliyoambiwa na Peniela yalimfanya Dr
Joshua abaki kima akitafakari.
“ Kwa hiyo Dr Joshua “ akasema Peniela na
kumfanya Dr Joshua ainue kichwa
“ Ni juu yako kuchagua na kuamini yupi mkweli kati
yangu na jaji Elibariki”
Dr Joshua akavuta pumzi ndefu na kusema
“ I don’t know anymore the meaning of these two
words,believe and trust.I don’t know who to believe or who
to trust.”
Peniel akamtazama kwa makini na kusema kwa sauti
ndogo ya kimahaba
“You don’t believe even the woman you love the
most as you always say? You don’t believe me? That’s too
bad.”
Akamtazama tena Dr Joshua na kusema
“Kila siku umekuwa unaniambia kwamba unanipenda
na uko t ayari kwa lolote kwa ajili yangu sasa ni wakati wako
wa kulithibitisha hilo kwa vitendo.Nitaumia mno endapo
utashindwa kuniamini na kuchagua kumuamini mtu ambaye
: ana lengo la kukuangamiza.One more thing,if y u choose not
to trust me today then there is no any meaning for us to
contnue with our relationship.We have to put an end to us
!!!!..akasema Peniela kwa ukali kidogo
“ Peniela my love,si kwamba sitaki kukuamini lakini
….” Dr Joshua akasita
“ Lakini nini Dr Joshua? Unashindwa kweli kuniamini
mimi? Nasikitika sana kwa hilo.Sasa nimegundua yale
maneno yote uliyokuwa unaniambia kila siku kamba
unanipenda hayakuwa ya kweli.Lengo lako lilikuwa ni
kutimiza tu haja zako za mwili na si kweli kwamba ulikuwa na
nia ya dhati ya kufanya jambo lolote kwa ajili yang….”
“ Peniela stop !!” akasema Dr Joshua
“ Kwanza naomba samahani sana kwa maneno yale
niliyoyatamka mwanzo.NIsamehe sana Peniela.Nilitamka
maneno yale kutokana na hasira nilizokuwa nazo juu yako
kwa sababu ya maneno niliyolishwa na jaji Elibariki na mimi
nikayaamini.Maneno uliyonieleza ni mazito na ninakuahidi
nitayafanyia kazi kwa haraka na hawa wote wanaojifanya ni
watu wangu wa karibu kumbe ni chui wanaoiwinda damu
yangu watakiona cha moto” akasema Dr Joshua halafu
akamtazama Peniela kwa sekunde kadhaa akamsogeza
karibu yake akambusu
“ Peniela nakupenda sana malaika wangu zaidi ya n
inavyoweza kukueleza.Sikumbuki ni mara ngapi
nimekutamkia neno hili kwamba ninakupenda lakini usiku wa
leo nataka nikukumbushe kwamba ninakupenda kuliko
chochote hapa duniani.Japokuwa kuna nyakati h uwa
: unaniudhi mfano ulipoanzisha mahusiano na Yule kijana
Edson nilichukia sana lakini kila pale ninapokuwa na hasira
juu yako ninapokuona tu hasira zote hupotea na hutabasamu
tena.Nakuomba Peniela usiwe na shaka yoyote juu ya
upendo wangu kwako na kwa ajili yako niko tayari kwa lolote
“ akasema Dr Joshua na kumbusu tena Peniela
“ Peniela muda wangu wa uongozi unakaribia
kumalizika .Utafanyika uchaguzi na atapatikana rais mpya na
mimi nitaenda kupumzika.Ninao u tajiri mkubwa sana ambao
utanifanya niishi maisha mazuri ya kifahari baada ya kustaafu
hadi siku ninaingia kaburini .Hivi karibui ninatarajia kupata
ukaazi wa kudumu nchini Marekani kwa hiyo baada tu ya
kustaafu nitakwenda kuishi huko.Sintokwenda huko
mwenyewe bali nitaongozana nawe malaika wangu
unayejenga tabasamu usoni pangu kila niionapo sura
yako.Peniela una nafasi ya pekee kabisa katika moyo wangu
kwa hiyo kokote niendako nitaambatana nawe.Nataka tuishi
maisha yenye furaha ,tuzunguke dunia nzima tukistarehe na
kuyafurahia maisha.” Akasema Dr Joshua na kumbusu
Peniela
“ Peniela sitaki kukupoteza wala kuruhusu jambo
lolote baya likutokee.Kwa Elibariki na mshirika wake
Rosemary Mkozumi ntajua n ini cha kuwafanya .Kwa hiyo
basi kuanzia sasa hadi hapo nitakaporidhika kwamba hakuna
shaka ya usalama wako utakaa humu ndani na hutatoka hadi
hapo nitakapokuruhusu kutoka.”
“ No !Dr Joshua yu cant do that to me !!.akasema
Peniela
“ Yes you will.Thats an order!!! Akasema Dr Joshua
kwa sauti ya ukali
“ Peniela I’m doing this for you,for us,kwa hiyo
naomba usikasirike wala usinione mimi mkatili .Maisha yako
yana thamani kubwa kwangu na jambo hili ni la muda tu na
nitakapohakikisha hali ya usalama imeboreka basi utakuwa
huru .Utapata kila unachohitaji na ulinzi nitauimarisha zaidi
hapa.Nitakuelekeza Kareem ahakikishe kunakuwa na ulinzi
wa kutosha hapa.Kila jioni nitakuwa nakuja hapa na tunapata
wasaa wa kuwa pamoja.Peniela this is our moment to be
happy.Give me a chance to show you how much I love
you.Mwanamke kama wewe unapaswa kuishi zaidi ya
malkia” akasema Dr Joshua .Peniela akaachia tabasamu
kubwa akambusu Dr Joshua na kusema
“ Dr Joshua nafahamu unanipenda na una nia nzuri
na mimi hasa kwa wakati huu ambao usalama wangu uko
shakani lakini siwezi kukubali kufungiwa humu ndani.Nahitaji
kuwa huru mpenzi wangu”
“ Usijali Peniela.This is just for few days.Nataka
ukitoka hapa japokuwa si rasmi lakini uishi kama mke wa rais
kwa hiyo naomba unipe siku chache tu niweze kuyafanya
mambo makubwa ambayo nataka kukufanyia.Sawa malaika
wangu? Akasema Dr Johsua.Peniela akatabasamu na kwa
sauti laini akasema
“ Dr Joshua you’re the king here.Nitatekeleza yote
unayoyasema but I have one request na endapo
utanitekelezea hilo nitaamini kwamba kweli unanienda and
I’ll go with you anywhere you wat us to go”
“ Peniela,neno lako ni amri kwangu.Tafadhali nieleze
chochote nitakutekelezea bila kusita” akasema Dr Joshua
kwa kujiamini
Peniela akainamisha kichwa na alipoinua kumtazama
Dr Joshua macho yake yalijaa machozi.Dr Joshua akastuka
“ Whats wrong my queen? Akauliza Dr Joshua
“ Dr Joshua nimedhalilishwa sana na jaji Elibariki .He
raped me.He raped the woman you real love.I want him for
what he did.Can you help me make him pay?
Dr Joshua akamkumbatia Peniela na kusema
“ My dear Peniela,siwezi kukueleza ni namna gani
nimeumizwa na taarifa hizo za kitendo kiovu alichokifanya
Elibariki.Edson nilimuondoa kwa sababu moja tu ya kuwa na
mahusiano na mwanamke wangu ninayempenda kuliko
wote.Peniela you are mine and mine alone kwa hiyo yeyote
atakayekuumiza wewe atakuwa ameniumiza mimi
pia.Nakuahidi Peniela, Elibariki will pay very dearly !!!!...
akasema Dr Joshua huku akiuma meno kwa hasira.
“ Ahsante sana my love.Sasa naamini maneno yako
kwamba unanipenda,Unajua sikuwahi kufikiri hata siku moja
kama ninaweza kudhalilishwa kiasi kile.Inaniumiza sana na
sijui nitafanya nini ili niweze kuliondoa jambo hili katika akili
yangu”
“ Peniela I’m right here.Nitakufuta machozi na
kukusahaulisha jambo hili.Narudia tena kukuahidi jaji Elibariki
lazima atalipa uovu wake..!”
Peniela akaanza tena utundu wake na Dr Joshua
akazidi kupagawa
 
We mbwiga mbona unajipendekeza hivyo,

Kwani aliyesema story inakuja leo ni sisi au ni Lege? Wewe ndiye unayetaka story ije hapa saa tano kwa kipi ulichonacho..!!

Lege akisema hii story inakuja kesho, keshokutwa, mtondogoo tutamsikiliza, siyo wewe pangu pakavu, kama watu wamevumilia wiki mbili watashindwaje masaa.!!!!! Lege akisema story inakuja saa tano tunasambaratika hapa lakini siyo kwa kupitia kinywa chako pangu pakavu wewe..

Angalia usije kumfunulia skirt kisa Story.. Unajipendekeza vibaya sana.

BACK TANGANYIKA
Sawa mkuu, nashukuru sana kwa kila herufi ya tusi uliyoiandika humu dhidi yangu. Labda nahisi mi ndio sijui. All the best "thia kat an"
 
SEHEM YA 4

“ Dah ! hatimaye nimefanikiwa kumteka akili huyu
mzee.Elibariki alifanya kosa kubwa sana
kutusaliti.Nitahakikisha anakosa kila kitu.Dr Joshua hana tena
kauli yoyote kwangu na lazima mipango yetu yote iende
kama tunavyotaka.Kwa kuwa amenitaka nisitoke nje ya
nyumba hii ngoja nimkubalie matakwa yake lakini natakiwa
kutafuta namna ili niweze kulichukua kasha langu na
kuwapelekea akina Mathew.Kitu kizuri ni kwamba anasema
Kareem ndiye atakayekuwa hapa nyumbani akihakikisha
ninakuwa salama.Kareem hana kauli kwangu atafanya kila
nitakachomuamuru kufanya.” Akawaza Peniela huku
akiendelea kumfanyia Dr Joshua utundu,ambaye alikuwa
anaguna kimahaba kwa mambo aliyofanywa na muda si
muda wakaingia katika mzunguko wa pili.Peniela akashika
usukani alimpeleka vilivyo Dr Joshua na kumfanya alalame
kama mtoto mdogo.Hadi mzunguko wa pili unamalizika Dr
Joshua alikuwa hoi amechoka kupita maelezo.
“ I swear Peniela sintamuacha hata itokee nini.Huyu
binti ananipa raha ambayo siwezi kupewa na mtu
yeote.Nitafanya kila linalowezekana hadi niw…..” Dr Joshua
akashindwa kuendelea kuwaza akapitiwa na usingzi.
“ Dr Joshua!!.Dr Joshua .!!” akaita Peniela lakini
tayari D Joshua alikuwa katika usingizi mzito.
“ Kwisha habari yake” akawaza Peniela na kuinuka
akaelekea chooni akakigonga kile kifaa cha kuwasiliana
alichokiweka sikioni.
“ Hallow Mathew,can you hear me?!!! Akauliza
Peniela.
“ Ndiyo Peniela.Tumesikia kila kilichoendelea hapo
ndani.Good job” akasema Mathew
“ Ahsante.Kama mlivyosikia huyu mzee hataki nitoke
humu ndani . What are we going to do? Tunatakiw akuonana
na Deus Mkozumi,right?
“ Usijali kuhusu hilo tutatafuta namna nyingine ya
kufanya kuweza kuonana na Deus Mkozumi ila kwa sasa
wewe endelea kukaa humo humo ndani kama
anavyotaka.Endelea kumfanya akuamini tena na wakati
ukiwa hapo ndani jaribu kutafuta chochote kinachoweza
kutusaidia katika mpango wetu wa kukipata kirusi Aby”
“ Sawa Mathew,nitafanya nhivyo ila kesho
nitamtuma Kareem alete ule mzigo hapo nyumbani.
Mathew,tutawasiliana kesho.Good night”akasema Peniela
na kurejea chumbani ambako Dr Joshua alikuwa amelala
fofofo.
“ Nini kinafuata baada ya hapa? Akauliza Anitha
wakiwa ndani ya gari baada ya Peniel kumaliza kuongea na
Mathew
“ Tunarudi nyumbani kwani Peniela hawezi kutoka
mle ndani leo,kwa hiyo hatuna haja ya kuendelea kukaa
hapa”
“ Are you sure she’ll be ok? Ninawasi wasi kidogo
kwani mchezo anaoucheza ni wa hatari sana.Anacheza na
akili ya Dr Joshua,unadhani nini kitatokea endapo dr Joshua
atagundua kuwa Peniela anamdanganya? Akauliza Anitha
“ Hilo haliwezi kutokea kabla hatujakamilisha
mpango wetu.Peniela ni mjanja mno.Akili yake inafanya kazi
haraka sana na anaweza kufanya jambo lolote muda
wowote.Amenishangaza sana kwa namna alivyoweza
kubadili upepo kati ya Dr Joshua na jaji Elibariki.Ameweza
kuuvaa vyema uhusika na mtu yeyote angeweza kumuamini
alichokisema” akasema Mathew kisha wakaondoka kurejea
nyumbani.
*******
Watu hawakuwa wengi nyumbani kwa rais usiku huu
uliko msiba wa Flaviana.Wengi wa waliobaki ni ndugu na
watu wa karibu na familia ya rais.Anna akamuulizia Jaji
Elibariki akaambiwa kwamba ameondoka ameelekea
nyumbani kwake kupumzika
“ Nitamfuata huko huko nyumbani kwake” akawaza
na bila kupoteza wakati akaelekea katika gari lake na
kuondoka kumfuata jaji Elibariki nyumbani kwake
“ Leo lazima nifahamu ni kitu gani kinachoendelea
kati ya baba na jaji Elibariki.Kama alivyonieleza Mathew
lazima kuna kitu kinachoendelea kati yao.I must find out”
akawaza na kuanza kuyakumbuka maneno aliyoambiwa na
Mathew
“ Kila nikiyakumbuka maneno ya Mathew kuhusu
baba,mwili wote unanisisimka.Ni mambo mazito mno.Hatua
aliyofikia baba si hatua ya ubinadamu.Amefikia hatua ya
ukatili uliopitiliza.Amebariki mke wake na mwanae wauawe
kwa sababu ya pesa???..!! Atapata raha gani kama atazipata
hizo pesa lakini hana mtu wa kutumia naye? Ni ujinga
: mtupu” akawaza Anna akiwa katika mwendo mkali akielekea
nyumbani kwa jaji Elibariki
“ Kwa kila nitakavyoweza lazima nimsaidie Mathew
kuhakikisha baba na genge lake wote wanafikishwa katika
vyombo vya sheria ili na kupata dhabu stahiki.Siwezi katu
kulifumbia macho suala hili kwa vile muhusika mkuu ni baba
yangu.Nitapambana bega kwa bega na Mathew mpaka
tuhakikishe tunashinda” akawaza Anna na sura ya Mathew
ikamjia kichwani
“ Mathew ni mtu shujaa ambaye anastahili sifa za
kipekee kabsa.Ameweza kufukunyua na kugundua mambo
mazito kama haya .Lazima nimuunge mkono.Nadhani nikiwa
karibu naye nitafahamu mambo mengi zaidi.Anaonekana ni
mtu anayefahamu mambo mengi sana mabaya
yanayofanywa na watu mbali mbali wa hapa nchini.Natakwa
kutafuta namna ya kumfanya aniamini.Halafu kuna kitu
Kareem aliniambia ,eti Mathew na Anitha ni mtu na mpenzi
wake.Kuna ukweli wowote katika hili? Nitamuuliza Mathew
nikionana naye” akawaza
“ Lakini kwa nini nifuatilie mambo binafsi ya Mathew
na Anitha? Kama ni wapenzi mimi inanihusu nini? Kazi yangu
mimi ni kumsaidia na kuhakikisha tunawafikisha mbele ya
sheria baba na mtandao wake.Lakini mhhh!!Mathew
amenivutia sana.He’s real a gentleman.Anajiamini na kwa
namna nilivyomsoma kwa haraka ni mwanaume ambaye
hana tamaa na wanawake kama hawa wanaume wengine ..”
Anna aliwaza mambo mengi sana akiwa njiani
kuelekea nyumbani kwa jaji Elibariki.Alifika katika makazi ya
jaji Elibariki ,akasimamishwa na askari wawili wenye silaha
..kulikuwa na ulinzi mkali eneo lile.Anna akawasalimu askari
wale na kujitambulisha kwao.Mmoja wa askari wale akaenda
kumfahamisha jaji Elibariki kuhusu ujio wa Anna.Jaji Elbariki
akatoa ruhusa Anna aruhusiwe kuingia ndani.Anna akashuka
garini na kulakiwa na jaji Elibariki akamkaribisha sebuleni.
“ I’m sorry Anna,sina kinywaji kingine chochote
kikubwa humu ndani zaidi ya hii whysky ninayokunywa”
akasema jaji Elibariki ambaye macho yake yalikuwa
mekundu kwani toka aliporejea amekuwa akinywa pombe
kali
“ Usijali Elibariki hata kama kungekuwa na vinywaji
nisingekunywa.Look,Im here for one reason only.I want to
know whats going on between you and my father? Akauliza
Anna.Elibariki akamtazama kwa sekunde kadhaa na kusema
“ Anna imekuwa vizuri umekuja .Kuna mambo
kadhaa ambayo nataka tuongee na itakuwa vyema kama
tutautumia usiku hu wa leo kuongea kila kile kinachotuhusu
lakini kabla sijasema chochote naomba kwanza nitumie
nafasi hii kukupa pole sana kwa kifo cha dada
yako.Nimeumizwa mno kwa kifo cha mke wangu” akasema
Elibariki na kuinamisha kichwa.
“ Elibariki I think you know me,huwa si mtu wa
kutaka hadithi nyingi.Nahitaji uende moja kwa moja kujibu
swali langu nililokuuliza,whats going on between you and my
father? Jeshi la polisi walitangaza msako mkali dhidi yako kwa
kusababisha kifo cha Flaviana.Nikiwa Afrika ya kusini
nilikupigia simu na ukanihakikishia kwamba hauhusiki kabisa
na hicho kinachodaiwa na jeshi la polisi halafu nikakuuliza
kama baba anahusika katika matukio ya vifo vya mama na
dada ukakubali kwamba ni kweli baba ndiye muhusika mkuu
wa vifo hivyo na kwamba hata wewe umejificha kuepuka
kuuawa kwa vile tayari unayafahamu madhambi ya
baba.Ghafla bila kutegemea umeibuka toka mafichoni na
unaonekana ukiwa umeongozana na baba mtu ambaye ulidai
anataka kukuua.Na kama haitoshi,jeshi la polisi lililokuwa
linakusaka kwa udi na uvumba wanadiriki kujitokeza mbele
ya watanzania na kukusafisha kwamba ulikuwa umetekwa na
majambazi na kwa hiyo tuhuma ulizokuwa ukitafutwa kwazo
hauhusiki nazo.Nataka uniondolee hizi picha picha kichwani
kwangu na unieleze ukweli wa nini kinaendelea kati yako na
baba? Nataka unieleze ukweli wote.You know I do trust you
with all my heart so tell me nothing but the truth.Nataka ukiri
tena ile kauli yako uliyonieleza kwamba baba anahusika na
vifo vya mama na dada.If you real love my sister you are
going to tell me the truth”
Jaji Elibariki akanywa whysky halafu akainamisha
kichwa na alionekana kuzama katika mawazo mengi.Baada ya
ya kufikiri kwa muda akasema
“ Ok I’m going to tell you the truth”
Jaji Elibariki akainamisha tena kichwa alionekana
kuwa katika majonzi mazito…
“ Anna kwanza kabisa nataka nikiri tena kwamba yale
maneno niliyokwambia ukiwa afrika kusini kuhusiana na
baba yako ni ya kweli kabisa.Yeye ndiye muhusika mkuu wa
vifo vya mama na dada yako.” Akanyamaza akainamisha
kichwa kidogo halafu akainua kichwa na kumuelea Anna kila
kitu kilichotokea toka mama yake alipofariki .Maneno
aliyoyasema jaji Elibariki ni sawa na yale yale kama Anna
aliyoambiwa na Mathew.
“Kwa hiyo Anna hivyo ndivyo ilivyokuwa” Mathew
akaendelea
“ Baada ya Dr Joshua na kundi lake kugundua
kwamba tayari nimefahamu wanahusika katika kifo cha Dr
Flora wakasuka mpangowaniue.Nilinusurika katika shambulio
lililoratibiwa na mtandao wa Dr Joshua.Nawashukuru sana
Mathew na wenzake kwa jitihada zao hadi leo niko hai”
akainama akawaza kidogo kisha akaendelea kumsimulia
Anna kila kitu bila kumficha.UKimya ukatanda pale
alipomaliza.Anna alimtazama Elibariki kwa jicho la chuki
“Kwa hiyo Anna baada ya matukio haya yote
nikajikuta maisha yangu yakibadilika ghafla” akaendelea jaji
Elibariki
“ Sikuwa na muelekeo na nilipoteza kila kitu katika
maisha yangu.Niliishi bila kuifahamu kesho yangu.Kwa ufupi
nilikuwa nimekwama na sikuwa na namna nyingine ya
kujikwamua ili maisha yangu yasonge mbele kwani nilikuwa
sawa na mtu asiye na uhai na ndipo nilipoamua kufanya
jambo ambalo kila ninapolifikiria nahisi kama moyo wangu
unakatwa katwa na kisu kikali” akasema jaji Elibariki na
kuinama akashika mahali ulipo moyo wake
“ Moyo unaniuma sana kwa jambo nililolifanya”
akasema jaji Elibariki
“ Ulifanya nini” akauliza Anna
“ Baada ya kuona nimekwama na maisha yangu
yamekwama nililazimika kutafuta namna ya kujikwamua na
njia pekee ya kurejesha tena maisha yangu ni kwa
kujisalimisha kwa Dr Joshua.Niliwasaliti wenzangu na kwa
kumtumia Rosemary Mkozumi ambaye nilimfungua toka
mahala pa siri alipokuwa amefichwa na Mathew,nilifanikiwa
kuonana na Dr Joshua ,nikaongea naye na ili anisamehe
nikalazimika kumueleza kila mpango mimi na wenzangu
tuliokuwa tumeupanga dhidhi yake.Dr Joshua alifurahi kwa
niliyomuleleza akanisameheh tukaufungua ukurasa mpya.I’m
free now”
Anna akamtazama kwa hasira na kusema
“ Hukupaswa hata kumuoa dada yangu mtu kama
wewe.Kwa nini ukafanya jambo kama hilo la kijinga Elibariki?
Baada ya kufahamu yote ambayo baba ameyafanya na hadi
kuhusika katika kusababisha kifo cha mkeo kwa nini badala
ya kumfikisha mbele za sheria ukawageuka wenzako na
kuungana na muuaji? Wewe na yeye nyote mko sawa..You
are both monsters!!! Akasema Anna
“ Yes I’m a monster!! Akasema kwa ukali jaji Elibariki.
“ I had no choice.Nilifanya kile ambacho mtu yeyote
kama angekuwa mahala pangu angekifanya.Hupaswi
kunilaumu mimi kwani ni Flaviana ndiye aliyeniingiza katika
vita dhdi ya rais na baada ya kufariki sikuona sababu ya
kuendeleza vita ile ambayo hata ningefanya nini
nisingeshinda,nikaamua kujisalimisha”
“Is that all you wanted ?only to be free” akauliza
Anna
Nilichokuwa nakihitaji sana nI kuwa huru ili
niendelee na maish a yangu ya kawaida lakini baada ya
kumueleza Dr Joshua mambo yale makubwa yaliyopangwa
dhidi yake amefanya maamuzi .Anataka niwe rais ajaYe wa
Tanzania baada ya yeye kumaliza muda wake wa uongozi”
akasema jaji Elibariki huku akitabasamu kidogo
“ What??!! Anna akapatwa na mshangao mkubwa
“ Tell me it’s a lie!! Akasema
“ Its true Anna.I’m going to be the next president”
Anna aliyekuwa amekunja sura akalazimika kutoa kicheko
kidogo.
“ Ama kweli dunia inaelekea ukingoni.You ?? Next
president?? That cant be” akasema Anna
“ Anna utake usitake nitakuwa rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania baada ya baba yako kumaliza muda
wake hiyo ni ahadi aliyonipa.Kwani siwezi kuongoza nchi?
Akauliza Elibariki
“ Kama umeshindwa kuvumilia na ukawasaliti
wenzako itakuwa nchi? Si utaiuza nchi na watu wake wewe??
Hebu acheni hayo masihara “
“ Si masihara Anna.Hili ni jambo la kweli na ndivyo
itakavyokuwa”
“ Hivyo ndivyo baba alivyokudanganya?
“ Hajanidanganya .He’s going to make me the next
president .Right now I’m the only one he trust the most”
“ Elibariki kitu gani kimekuingia kichwani na
kukubadilisha kiasi hiki? I know me and you we never seen
eye to eye but down deep I know you are a good guy,what
turns you to a monster?
“ I’m serving a monster so I have to be a monster
too!! Akasema jaji Elibariki kwa sauti ya juu akionekana
kukerwa na maneno yale ya Anna
“ Sikiliza Anna.Hakuna ubishi kwamba nitakuwa rais
ajaye wa Tanzania kwa hiyo badala ya kunikashifu na
kunivunja moyo unapaswa kuniunga mkono kwani mimi na
wewe tuna maisha marefu huko mbeleni”
“ What do you mean ?? akauliza Anna akimtazama
Elibariki kwa hasira
“ Sikiliza.Kwa sasa sisi sote tumewapoteza wapenzi
wetu.Umempoteza Edson na mimi nimempoteza Flaviana
hivyo basi kwa kuwa ninaelekea kushika wadhifa mkubwa na
wa juu katika uongozi nahitaji kuwa na mwenza na kwa vile
kwa sasa uko mwenyewe basi si vibaya kama tukianzisha
mahusiano na baada ya mimi kushika urais you are going to
be the first lady” ak asema Elibariki .Ana akamtazama kwa
hasira na kusema
“ You are sick Elibariki and you need treatment.Hivi
unathubutuje kutamka maneno kama hayo? Unafahamu
kabisa kwamba ninakuchukua sana sana na kwa hili
ulilolifanya limenifanya nikuchukie hata zaidi kwa hiyo
naomba usirudie tena kunitusi kwa kunitamkia maneno hayo
” akafoka Anna
“ Hata mimi si kwamba ninakupenda Anna bali huo
ni ushauri toka kwa baba yako na ndivyo anavyotaka
 
SEHEM YA 5

iwe.Anataka familia yake iendelee kushika nafasi za juu za
uongozi na mimi siwezi kuipinga kauli yake”
“ You are both devils !!! I’m out of here but I’ll come
back again .Our conversation is not over yet!!
Akasema Anna na kutoka kwa hasira hadi katika gari
lake akaondoka
“ Dah ! kweli haya ni maajabu ya Musa.Haya mambo
yanayotokea ni kama vile filamu lakini ni ya kweli kabisa.Is
my father a real human? Akajiuliza Anna akiwa garini
“ mambo anayoyafanya baba yananipa wasi wasi na
wakati mgumu kumuelewa ni kiumbe mwenye damu ya
namna gani.Kwa kumtazama anaonekana ni mtu mwema
lakini kwa ndani ana moyo wa kishetani.Yaani kwa tamaa ya
pesa anadiriki bila huruma kuutoa uhai wa mwanamke
aliyenileta duniani ambaye nilimpenda kuliko wote .I’ll never
forgive him for that.Kwa kusababisha vifo vya mama na dada
amechukua kila kitu cha thamani katika maisha yangu na
lazima nihakikishe hafanikiwi katika mipango yake yoyote”
akaendelea kuwaza Anna
“ Halafu kituko kingine bila hata ya aibu eti anataka
kumfanya Elibariki awe rais wa Tanzania baada ya yeye
kumaliza muda wake.Hiki ni kichekesho kabisa.Kwa kuwa
Elibariki naye ameamua kushirikiana na baba naye pia lazima
nihakikishe anaozea gerezani.Hakuna atakayesalimika”
Anna alifika nyumbani kwao na kukuta tayari watu
wamekwisha lala .Ni watu wachache tu waliokuwa wamekaa
kivikundi wakiongea hili na lile huku wakiendele a na
vinywaji.Alimtafuta baba yake lakini aliambiwa kwamba
alitoka muda mrefu .Kwa kuwa alikuwa tayari na uchovu
mwingi moja kwa moja akaelekea chumbani kwake
kupumzika.Kabla ya kulala akamtumia baba yake ujumbe
katika simu akamtaka waonane asubuhi kuna jambo la
maana sana anataka waongee.
*******
Mathew na Anitha waliwasili katika makazi yao na
moja kwa moja Mathew akaenda sebuleni akajitupa sofani
.Alionekana kuwa na mawazo mengi.Anitha akamtazama kwa
sekunde kadhaa na kusema
“ Unaonekana hutaki kabisa kupumzika siku ya leo.Its
been a long day Mathew let us take some rest”
“ Sina hakika kama jicho langu litafumba leo”
“ Kwa nini Mathew” Kitu gani kinakunyima usingizi?
Akauliza Anitha
“ Nitawezaje kupata usngzi wakati sina hakika na
usalama wa Peniela? Ni vipi kama Dr Joshua atagundua
wamba Peniela anamdanganya? Suala hili linaniumiza mno
kichwa changu.I will never forgive myself if anything bad
happens to Peniela” akasema Mathew.Anitha akatumia
sekunde kadhaa kumtazama Mathew halafu akasema
“ Mathew kuna kitu nataka kukuuliza and please be
honest with me.”
“ Uliza Anitha”
“ Ni kuhusu wewe na Peniela.Nikiwatazama ninyi
wawili kuna vitu Fulani naviona kwenu vinavyonifanya
nijiulize maswali mengi.Is there anything going on between
you two?
Mathew akatabasamu kidogo na kusema
“ Hakuna chochote kinachoendelea kati yetu.”
“ Kama hakuna kinachoendelea kwa nini kila
linapokuja suala la Peniela kutumia mbinu yake ya kuutumia
mwili waake kufankisha jambo Fulani umekuwa unapinga
sana? Unaonekana kuumia moyoni.Do you love her?
“ Anitha its like this .Peniela ni mtu ambaye
tunamtegemea mno katika operesheni hii kwa hiyo lazima
niwe makini sana kuhusu usalama wake.Tukimpoteza yeye
tumepoteza kila kitu.Kuhusu kutembea na watu mbali mbali
ili kupata taarifa za muhimu na kufanikisha baadhi ya mambo
ni kweli imetusaidia sana lakini toka ndani ya moyo wangu
sifurahii kabisa hali hii.Peniela hastahili maisha kama haya ya
kuutumia mwili wake kama chambo.Ni jambo la hatari sana
kwake.Ndoto yangu kubwa toka nilipoyafahamu maisha yake
ni kumsaidia aanze maisha yake yenye staha na
amani.Nataka nimtoe na kumsahaulisha kabisa maisha yake
ya sasa.Kujibu swali lako kama ninampenda Peniela au la,ni
kwamba ninampenda Peniela kama ndugu yangu,kama
mdogo wangu,kama binadamu wengine na si
vinginevyo.Natumai umeridhika Anitha”
“ Ndiyo Mathew na samahani sana kwa mawazo
niliyokuwa nayo juu yenu.Pamoja na hayo narudia tena
kukuomba kama una hata chembe moja ya mawazo kuhusu
kuwa na mahusiano na Peniela naomba ufute kabisa wazo
hilo.Peniela is not good for you”
“ Ahsante kwa ushauri wako Anitha” akasema
Mathew halafu ukimya ukapita
“ Mathew !! akaita Anitha
“ Kwa sasa wakati tuko peke yetu kuna jambo nataka
kulifahamu”
“ jambo gani hilo Anitha?
“ Kabla hajaaga dunia ,John Mwaulaya alitaka
kuonana nawe na mpaka leo hii hakuna anayefahamu wewe
na John mliongea kitu gani.Mathew umekuwa ni mtu wangu
wa karibu kupita wote katika hii dunia na hata siku moja
hujawahi kunificha jambo lolote.I think I deserve to know
what you and John Mwaulaya talked”
Mathew akafikiri kidogo na kusema
“ Ok nitaueleza uweli” akasema na kunyamza tena
halafu akaendelea
“ Kwanza haikuwa rahisi kukubali wito ule wa John
Mwaulaya kutokana na historia yangu naye kuwa si
nzuri.Nafsini mwangu nilichokuwa nakiwaza ni kisasi
tu.Baada ya kutafakari nikaamua kwenda kumuona.Nilipofika
nilikuwa na hasira na akalitambua hilo akaniomba nisiwe na
hasira kwani anayotaka kunieleza ni ya muhimu sana
kwangu” Mathew akatulia baada ya sekunde kadhaa
akaendelea
“ Kwanza alianza kwa kuniomba samahani kwa kile
kilichotokea wakati ule na kusababisha mimi na yeye kuwa
maadui.John alikuwa katika maumivu na alikuwa anapumua
kwa shida.Nilimuonea huruma nikamtaka anieleze
alichoniitia pale.Aliniambia kwamba kuna mambo mawili
,kwanza ni kuhusu Peniela.Alisema kwamba yeye atakufa na
hataweza kuitimiza ndoto yake ya kubadili maisha ya Peniela
kwa kumtoa Team SC41 ili aweze kuishi maisha ya kawaida
.Alikiri kwamba alikosea sana kumuingiza Peniela Team SC41
na kuziharibu ndoto zake nyingi za maisha.kwa hiyo
alinikabidhi mimi jukumu la kwaza kuhakikisha ninamsaidia
Peniela atoke Team SC41 na pili kuhakikisha Team SC41
inatoweka katika ardhi ya Tanzania.Kuhusu Peniela
aliniambai kwamba kuna mamo ya siri yanayomuhusu
ambayo ameyaweka katika kisanduku alichompatia
akihifadhi.Alisisitiza kwamba katika kisanduku hicho kuna
mambo muhimu na ya msingi ambayo hatakiwi mtu
mwingine kuyafahamu zaidi ya Peniela na mimi.Alirudia
kunisisitiza kwamba nimlinde Peniela zaidi ya mboni yangu ya
jic ho kwani ni binadamu mwenye thamani kubwa .NIlimtaka
anifafanulie ana maanisha nini kwa kauli hiyo akasema
kwamba kila kitu alichokisema kimo ndani ya sanduku
alilompa Peniela.Alinielekeza kwa Askofu Edmund Dawson
kwamba ni mtu muhimu na msaada mkubwa kwetu.Alinipa
maelekezo namna ya kufika kwa askofu Edmund ambaye
ndiye aliyetusaidia hadi hapa tulipofika” akatulia kidogo kisha
akaendelea
“ John Mwaulaya alinieleza jambo lingine
linalonihusu mimi” akasema Mathew
“ Jambo gani hilo? Akauliza Anitha.Mathew
akainamisha kichwa
“ tell me Mathew.Ni jambo gani hilo alilokwambia
John?
“ John…John..” Mathew akababaika
“ Niambie Mathew.John alikueleza nini? akasisitiza
Anitha ,akaingiwa na hofu akamsogelea Mathew karibu zaidi
“ Mathew kuna tatizo gani? John alikueleza nini?
“ Its about my family”
“ Alikueleza nini kuhusu familia yako?
“ Familia yangu bado iko hai.My wife and children
are all still alive”
“ Whats ?? Anitha akashangaa
“ No ! that’s not true.Ulitueleza kwamba familia yako
yote iliteketea kwa moto”
“ Hata mimi nilijua hivyo lakini kumbe haikuwa
hivyo.”
“ What real happened?haya mbona kama
mazingaombwe? Waliotekete katika nyumba yako kama si
familia yako ni akina nani basi?
“ John alisema kwamba lengo lao lilikuwa si
kuiteketeza familia yangu kwani hawakuwa na kosa ila
walitaka kunichanganya akili kwa kunifanya niamini familia
yangu iliteketea kwa moto ili wanikamate kirahisi.Alisema
kwamba watu waliokutwa wameteketea mle ndani yan
nyumba ni maiti walizozitoa katika chuo kikuu cha
utabibu.Kwa hiyo Anitha familia yangu iko salama kabisa”
“ Jesus Christ !! Anitha akapatwa na mshangao
mkubwa
“ So where are they now?
“ Wanaishi Marekani .Alinipa anuani ya mahala
wanakoishi endapo nitahitaji kuwatafuta.Kwa bahati
mbaya…” Mathew akainaisha kichwa
“ bahati mbaya gani tena Mathew?
“ Its complicated” akasema Mathew
“ How ?
“ Mke wangu tayari amekwisha olewa na ana watoto
wengine wawili kwa mume wake wa sasa.”
“ Oh jamani….! Nimeishiwa maneno ya
kuongea.Dunia hii imejaa watu makatili sana.kwa nini
wakakufanyia hivi Mathew? I hope right now John Mwaulaya
is burning in hell for all that he did ” akasema Anitah kwa
hasira
“ Naye mkeo kwa nini alikubali kuolewa tena? Nini
hasa kilimshawishi afanye hivyo? Akauliza tena
“ John alikuwa ni mtu mwenye roho mbaya lakini
katika hili ninamshukuru kwani hakuiteketeza familia
yangu.Alikuwa na uwezo wa kuwateketeza wote lakini
akaingiwa na moyo wa huruma akawaacha hai na
kuwatafutia mahala kwingine kwa kuishi nje ya nchi ambako
wanaishi maisha yaliyojaa furaha hivi sasa.Mke wangu naye
sipaswi kumlaumu kwa sababu sielewi ni kitu gani hasa
kilichomfanya anisahau na aamue kuolewa tena” akasema
Mathew na kuinama chini.Anitha akasema
“ So what are you going to do? When this is over are
you going to find them?
“ I cant..They’ve moved on with their life and they
are happy.Sitaki kuyavuruga maisha yao ya furaha
waliyonayo sasa”
“ Mathew una hakika hutaki kuwatafuta na
kufahamu kilichosababisha mkeo aamue kuolewa tena?
“ Anitha kwa sasa tuna kazi moja tu kubwa iliyoko
mbele yetu,kirusi Aby kiko katika hatari ya kutua kwenye
mikono isiyo salama ya watu wenye lengo la kufanya
maangamizi makubwa .Me ,you,peniela and Anna we’re the
only people who can save the world.Tunatakiwa kufanya kila
tuliwezalo kuiokoa nchi yetu na dunia toka katika
maangamizi makubwa yanayoweza kutokea endapo kirusi
Aby kitasambaa hewani.Ni jukumu zito sana kutokana na
watu tunaopambana nao.Baada ya kulikamilisha jukumu hilo
ndipo hayo mambo mengine yatafuata ila kwa sasa nataka
akili yangu niielekeze sehemu moja tu mambo ya familia
yatafuata baadae kwa hiyo naomba tusiongee chochote
kuhusiana na suala hilo la familia.” Akasema Mathew
“ Sawa Mathew nimekuelewa ila naomba uniahidi
kwamba baada ya mambo haya kumalizika mimi na wewe
tutapata wasaa wa kuzungumzia suala hili “
“ sawa ninakuahidi hivyo Anitha”
“ Thank you.Now let us g to sleep.I’m sleeping with
you tonight”
“ Nini ? Mathew akashangaa
“ Mbona umeshangaa Mathew niliposema kwamba
nitalala nawe usiku wa leo?
“ Lazima nishangae Anitha.Kwa nini tulale wote
wakati k ila mmoja ana chumba chake?
“ Mathe I’m sorry to say this but you and I we’ve
been in a sea of loneliness.Toka tumefahamiana sijawahi
kukuona hata mara moja na mwanamke halikadhalika
hujawahi kuniona au kusikia nina mpenzi.Sote tulichagua
kuishi maisha haya ya upweke kutokana na mambo
tuliyoyapitia.Baada ya kifo cha Noah nilijifunza kwamba
maisha ni zawadi na ni mafupi sana.Noah died so yung.What
happened to Noah can happen to us at anytime”
“ Unamaanisha nini Anitha?
“ Ninamaanisha kwamba tumeelekeza nguvu na akili
zetu zote katka kazi na tumejisahau wenyewe.Kazi zetu zina
mafanikio na tunapata pesa nyingi za kutuwezesha kuishi
maisha mazuri but we’re not happy.All we think day and
night is work,work,work,nothing else.Kama si kwa nguvu ya
Mungu pengine hivi sasa ningekwisha kuwa
marehemu.Tayari Rosemary angekwisha niua.Baada ya
kunusurika katika mikono ya Yule shetani mla watu,
nimefanya maamuzi.” Akatulia kidogo na kuendelea
“ Baada ya mambo haya kukamilika vizuri na kama
tutajaaliwa kubaki salama nitaachana na hizi kazi.Nataka
kuanza aina mpya ya maisha .I’m dreaming to have a family
and be happy.”akasema Anitha.Ilimkuchukua Mathew zaidi
ya dakika moja kusema chochote kuhusiana na kauli ile ya
Anitha
“ I’m glad to hear that.Its a good idea.Unachokisema
ni cha kweli kabisa.Mawazo yako ni kama ya kwangu.Hata
: mimi zaidi ya mara moja nimekuwa nafikiria kuachana na
shughuli hizi na kuanza maisha mapya”
“ Wow Mathew.Ahsante sana kama nawe umeliona
hilo .We both need to be happy again.Kwa kuwa sote tuna
mawazo yanayofanana,tonight we’re going to sleep together
We weed to comfort each other.Please Mathew don’t say no
to this.I need someone to comfort me tonight so do you.I
need strong arms to hug me tight tonight and tell everything
will be ok.I need you Mathew” akasema Anitha.Mathew
akajikuta akishindwa kumkatalia Anitha kwani naye alihisi
kuhitaji faraja kwa usiku ule..
*******
Tayari usingizi ulikwishaanza kumchukua Peniela
lakini alifumbua macho baada ya kusikia mlio wa simu ya
mkononi mle chumbani.Akainuka na kumtazama Dr Joshua
aliyekuwa amelala fofofo anakoroma.Akainuka taratibu na
kuzifuata nguo za Dr Joshua ambako mlio ule wa simu
ulitokea.Ndani ya koti akatoa simu na ilionyeshga mpigaji
alikuwa ni Abel Mkokasule
“ Abel Mkokasule,ni nani h uyu? Akajiuliza Peniela na
kwenda kumuamsha Dr Joshua ambaye alifikicha macho na
kutazama katika kioo cha simu na alipoona jina la mpigaji
akainuka haraka haraka na kubonyeza kitufe cha kupokelea.
“ Hallow Abel” akasema Dr Joshua
“ Mzee samahani kwa usumbufu”
“ Bila samahani Abel”
 
Back
Top Bottom