SEHEM YA 4
“ Dah ! hatimaye nimefanikiwa kumteka akili huyu
mzee.Elibariki alifanya kosa kubwa sana
kutusaliti.Nitahakikisha anakosa kila kitu.Dr Joshua hana tena
kauli yoyote kwangu na lazima mipango yetu yote iende
kama tunavyotaka.Kwa kuwa amenitaka nisitoke nje ya
nyumba hii ngoja nimkubalie matakwa yake lakini natakiwa
kutafuta namna ili niweze kulichukua kasha langu na
kuwapelekea akina Mathew.Kitu kizuri ni kwamba anasema
Kareem ndiye atakayekuwa hapa nyumbani akihakikisha
ninakuwa salama.Kareem hana kauli kwangu atafanya kila
nitakachomuamuru kufanya.” Akawaza Peniela huku
akiendelea kumfanyia Dr Joshua utundu,ambaye alikuwa
anaguna kimahaba kwa mambo aliyofanywa na muda si
muda wakaingia katika mzunguko wa pili.Peniela akashika
usukani alimpeleka vilivyo Dr Joshua na kumfanya alalame
kama mtoto mdogo.Hadi mzunguko wa pili unamalizika Dr
Joshua alikuwa hoi amechoka kupita maelezo.
“ I swear Peniela sintamuacha hata itokee nini.Huyu
binti ananipa raha ambayo siwezi kupewa na mtu
yeote.Nitafanya kila linalowezekana hadi niw…..” Dr Joshua
akashindwa kuendelea kuwaza akapitiwa na usingzi.
“ Dr Joshua!!.Dr Joshua .!!” akaita Peniela lakini
tayari D Joshua alikuwa katika usingizi mzito.
“ Kwisha habari yake” akawaza Peniela na kuinuka
akaelekea chooni akakigonga kile kifaa cha kuwasiliana
alichokiweka sikioni.
“ Hallow Mathew,can you hear me?!!! Akauliza
Peniela.
“ Ndiyo Peniela.Tumesikia kila kilichoendelea hapo
ndani.Good job” akasema Mathew
“ Ahsante.Kama mlivyosikia huyu mzee hataki nitoke
humu ndani . What are we going to do? Tunatakiw akuonana
na Deus Mkozumi,right?
“ Usijali kuhusu hilo tutatafuta namna nyingine ya
kufanya kuweza kuonana na Deus Mkozumi ila kwa sasa
wewe endelea kukaa humo humo ndani kama
anavyotaka.Endelea kumfanya akuamini tena na wakati
ukiwa hapo ndani jaribu kutafuta chochote kinachoweza
kutusaidia katika mpango wetu wa kukipata kirusi Aby”
“ Sawa Mathew,nitafanya nhivyo ila kesho
nitamtuma Kareem alete ule mzigo hapo nyumbani.
Mathew,tutawasiliana kesho.Good night”akasema Peniela
na kurejea chumbani ambako Dr Joshua alikuwa amelala
fofofo.
“ Nini kinafuata baada ya hapa? Akauliza Anitha
wakiwa ndani ya gari baada ya Peniel kumaliza kuongea na
Mathew
“ Tunarudi nyumbani kwani Peniela hawezi kutoka
mle ndani leo,kwa hiyo hatuna haja ya kuendelea kukaa
hapa”
“ Are you sure she’ll be ok? Ninawasi wasi kidogo
kwani mchezo anaoucheza ni wa hatari sana.Anacheza na
akili ya Dr Joshua,unadhani nini kitatokea endapo dr Joshua
atagundua kuwa Peniela anamdanganya? Akauliza Anitha
“ Hilo haliwezi kutokea kabla hatujakamilisha
mpango wetu.Peniela ni mjanja mno.Akili yake inafanya kazi
haraka sana na anaweza kufanya jambo lolote muda
wowote.Amenishangaza sana kwa namna alivyoweza
kubadili upepo kati ya Dr Joshua na jaji Elibariki.Ameweza
kuuvaa vyema uhusika na mtu yeyote angeweza kumuamini
alichokisema” akasema Mathew kisha wakaondoka kurejea
nyumbani.
*******
Watu hawakuwa wengi nyumbani kwa rais usiku huu
uliko msiba wa Flaviana.Wengi wa waliobaki ni ndugu na
watu wa karibu na familia ya rais.Anna akamuulizia Jaji
Elibariki akaambiwa kwamba ameondoka ameelekea
nyumbani kwake kupumzika
“ Nitamfuata huko huko nyumbani kwake” akawaza
na bila kupoteza wakati akaelekea katika gari lake na
kuondoka kumfuata jaji Elibariki nyumbani kwake
“ Leo lazima nifahamu ni kitu gani kinachoendelea
kati ya baba na jaji Elibariki.Kama alivyonieleza Mathew
lazima kuna kitu kinachoendelea kati yao.I must find out”
akawaza na kuanza kuyakumbuka maneno aliyoambiwa na
Mathew
“ Kila nikiyakumbuka maneno ya Mathew kuhusu
baba,mwili wote unanisisimka.Ni mambo mazito mno.Hatua
aliyofikia baba si hatua ya ubinadamu.Amefikia hatua ya
ukatili uliopitiliza.Amebariki mke wake na mwanae wauawe
kwa sababu ya pesa???..!! Atapata raha gani kama atazipata
hizo pesa lakini hana mtu wa kutumia naye? Ni ujinga
: mtupu” akawaza Anna akiwa katika mwendo mkali akielekea
nyumbani kwa jaji Elibariki
“ Kwa kila nitakavyoweza lazima nimsaidie Mathew
kuhakikisha baba na genge lake wote wanafikishwa katika
vyombo vya sheria ili na kupata dhabu stahiki.Siwezi katu
kulifumbia macho suala hili kwa vile muhusika mkuu ni baba
yangu.Nitapambana bega kwa bega na Mathew mpaka
tuhakikishe tunashinda” akawaza Anna na sura ya Mathew
ikamjia kichwani
“ Mathew ni mtu shujaa ambaye anastahili sifa za
kipekee kabsa.Ameweza kufukunyua na kugundua mambo
mazito kama haya .Lazima nimuunge mkono.Nadhani nikiwa
karibu naye nitafahamu mambo mengi zaidi.Anaonekana ni
mtu anayefahamu mambo mengi sana mabaya
yanayofanywa na watu mbali mbali wa hapa nchini.Natakwa
kutafuta namna ya kumfanya aniamini.Halafu kuna kitu
Kareem aliniambia ,eti Mathew na Anitha ni mtu na mpenzi
wake.Kuna ukweli wowote katika hili? Nitamuuliza Mathew
nikionana naye” akawaza
“ Lakini kwa nini nifuatilie mambo binafsi ya Mathew
na Anitha? Kama ni wapenzi mimi inanihusu nini? Kazi yangu
mimi ni kumsaidia na kuhakikisha tunawafikisha mbele ya
sheria baba na mtandao wake.Lakini mhhh!!Mathew
amenivutia sana.He’s real a gentleman.Anajiamini na kwa
namna nilivyomsoma kwa haraka ni mwanaume ambaye
hana tamaa na wanawake kama hawa wanaume wengine ..”
Anna aliwaza mambo mengi sana akiwa njiani
kuelekea nyumbani kwa jaji Elibariki.Alifika katika makazi ya
jaji Elibariki ,akasimamishwa na askari wawili wenye silaha
..kulikuwa na ulinzi mkali eneo lile.Anna akawasalimu askari
wale na kujitambulisha kwao.Mmoja wa askari wale akaenda
kumfahamisha jaji Elibariki kuhusu ujio wa Anna.Jaji Elbariki
akatoa ruhusa Anna aruhusiwe kuingia ndani.Anna akashuka
garini na kulakiwa na jaji Elibariki akamkaribisha sebuleni.
“ I’m sorry Anna,sina kinywaji kingine chochote
kikubwa humu ndani zaidi ya hii whysky ninayokunywa”
akasema jaji Elibariki ambaye macho yake yalikuwa
mekundu kwani toka aliporejea amekuwa akinywa pombe
kali
“ Usijali Elibariki hata kama kungekuwa na vinywaji
nisingekunywa.Look,Im here for one reason only.I want to
know whats going on between you and my father? Akauliza
Anna.Elibariki akamtazama kwa sekunde kadhaa na kusema
“ Anna imekuwa vizuri umekuja .Kuna mambo
kadhaa ambayo nataka tuongee na itakuwa vyema kama
tutautumia usiku hu wa leo kuongea kila kile kinachotuhusu
lakini kabla sijasema chochote naomba kwanza nitumie
nafasi hii kukupa pole sana kwa kifo cha dada
yako.Nimeumizwa mno kwa kifo cha mke wangu” akasema
Elibariki na kuinamisha kichwa.
“ Elibariki I think you know me,huwa si mtu wa
kutaka hadithi nyingi.Nahitaji uende moja kwa moja kujibu
swali langu nililokuuliza,whats going on between you and my
father? Jeshi la polisi walitangaza msako mkali dhidi yako kwa
kusababisha kifo cha Flaviana.Nikiwa Afrika ya kusini
nilikupigia simu na ukanihakikishia kwamba hauhusiki kabisa
na hicho kinachodaiwa na jeshi la polisi halafu nikakuuliza
kama baba anahusika katika matukio ya vifo vya mama na
dada ukakubali kwamba ni kweli baba ndiye muhusika mkuu
wa vifo hivyo na kwamba hata wewe umejificha kuepuka
kuuawa kwa vile tayari unayafahamu madhambi ya
baba.Ghafla bila kutegemea umeibuka toka mafichoni na
unaonekana ukiwa umeongozana na baba mtu ambaye ulidai
anataka kukuua.Na kama haitoshi,jeshi la polisi lililokuwa
linakusaka kwa udi na uvumba wanadiriki kujitokeza mbele
ya watanzania na kukusafisha kwamba ulikuwa umetekwa na
majambazi na kwa hiyo tuhuma ulizokuwa ukitafutwa kwazo
hauhusiki nazo.Nataka uniondolee hizi picha picha kichwani
kwangu na unieleze ukweli wa nini kinaendelea kati yako na
baba? Nataka unieleze ukweli wote.You know I do trust you
with all my heart so tell me nothing but the truth.Nataka ukiri
tena ile kauli yako uliyonieleza kwamba baba anahusika na
vifo vya mama na dada.If you real love my sister you are
going to tell me the truth”
Jaji Elibariki akanywa whysky halafu akainamisha
kichwa na alionekana kuzama katika mawazo mengi.Baada ya
ya kufikiri kwa muda akasema
“ Ok I’m going to tell you the truth”
Jaji Elibariki akainamisha tena kichwa alionekana
kuwa katika majonzi mazito…
“ Anna kwanza kabisa nataka nikiri tena kwamba yale
maneno niliyokwambia ukiwa afrika kusini kuhusiana na
baba yako ni ya kweli kabisa.Yeye ndiye muhusika mkuu wa
vifo vya mama na dada yako.” Akanyamaza akainamisha
kichwa kidogo halafu akainua kichwa na kumuelea Anna kila
kitu kilichotokea toka mama yake alipofariki .Maneno
aliyoyasema jaji Elibariki ni sawa na yale yale kama Anna
aliyoambiwa na Mathew.
“Kwa hiyo Anna hivyo ndivyo ilivyokuwa” Mathew
akaendelea
“ Baada ya Dr Joshua na kundi lake kugundua
kwamba tayari nimefahamu wanahusika katika kifo cha Dr
Flora wakasuka mpangowaniue.Nilinusurika katika shambulio
lililoratibiwa na mtandao wa Dr Joshua.Nawashukuru sana
Mathew na wenzake kwa jitihada zao hadi leo niko hai”
akainama akawaza kidogo kisha akaendelea kumsimulia
Anna kila kitu bila kumficha.UKimya ukatanda pale
alipomaliza.Anna alimtazama Elibariki kwa jicho la chuki
“Kwa hiyo Anna baada ya matukio haya yote
nikajikuta maisha yangu yakibadilika ghafla” akaendelea jaji
Elibariki
“ Sikuwa na muelekeo na nilipoteza kila kitu katika
maisha yangu.Niliishi bila kuifahamu kesho yangu.Kwa ufupi
nilikuwa nimekwama na sikuwa na namna nyingine ya
kujikwamua ili maisha yangu yasonge mbele kwani nilikuwa
sawa na mtu asiye na uhai na ndipo nilipoamua kufanya
jambo ambalo kila ninapolifikiria nahisi kama moyo wangu
unakatwa katwa na kisu kikali” akasema jaji Elibariki na
kuinama akashika mahali ulipo moyo wake
“ Moyo unaniuma sana kwa jambo nililolifanya”
akasema jaji Elibariki
“ Ulifanya nini” akauliza Anna
“ Baada ya kuona nimekwama na maisha yangu
yamekwama nililazimika kutafuta namna ya kujikwamua na
njia pekee ya kurejesha tena maisha yangu ni kwa
kujisalimisha kwa Dr Joshua.Niliwasaliti wenzangu na kwa
kumtumia Rosemary Mkozumi ambaye nilimfungua toka
mahala pa siri alipokuwa amefichwa na Mathew,nilifanikiwa
kuonana na Dr Joshua ,nikaongea naye na ili anisamehe
nikalazimika kumueleza kila mpango mimi na wenzangu
tuliokuwa tumeupanga dhidhi yake.Dr Joshua alifurahi kwa
niliyomuleleza akanisameheh tukaufungua ukurasa mpya.I’m
free now”
Anna akamtazama kwa hasira na kusema
“ Hukupaswa hata kumuoa dada yangu mtu kama
wewe.Kwa nini ukafanya jambo kama hilo la kijinga Elibariki?
Baada ya kufahamu yote ambayo baba ameyafanya na hadi
kuhusika katika kusababisha kifo cha mkeo kwa nini badala
ya kumfikisha mbele za sheria ukawageuka wenzako na
kuungana na muuaji? Wewe na yeye nyote mko sawa..You
are both monsters!!! Akasema Anna
“ Yes I’m a monster!! Akasema kwa ukali jaji Elibariki.
“ I had no choice.Nilifanya kile ambacho mtu yeyote
kama angekuwa mahala pangu angekifanya.Hupaswi
kunilaumu mimi kwani ni Flaviana ndiye aliyeniingiza katika
vita dhdi ya rais na baada ya kufariki sikuona sababu ya
kuendeleza vita ile ambayo hata ningefanya nini
nisingeshinda,nikaamua kujisalimisha”
“Is that all you wanted ?only to be free” akauliza
Anna
Nilichokuwa nakihitaji sana nI kuwa huru ili
niendelee na maish a yangu ya kawaida lakini baada ya
kumueleza Dr Joshua mambo yale makubwa yaliyopangwa
dhidi yake amefanya maamuzi .Anataka niwe rais ajaYe wa
Tanzania baada ya yeye kumaliza muda wake wa uongozi”
akasema jaji Elibariki huku akitabasamu kidogo
“ What??!! Anna akapatwa na mshangao mkubwa
“ Tell me it’s a lie!! Akasema
“ Its true Anna.I’m going to be the next president”
Anna aliyekuwa amekunja sura akalazimika kutoa kicheko
kidogo.
“ Ama kweli dunia inaelekea ukingoni.You ?? Next
president?? That cant be” akasema Anna
“ Anna utake usitake nitakuwa rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania baada ya baba yako kumaliza muda
wake hiyo ni ahadi aliyonipa.Kwani siwezi kuongoza nchi?
Akauliza Elibariki
“ Kama umeshindwa kuvumilia na ukawasaliti
wenzako itakuwa nchi? Si utaiuza nchi na watu wake wewe??
Hebu acheni hayo masihara “
“ Si masihara Anna.Hili ni jambo la kweli na ndivyo
itakavyokuwa”
“ Hivyo ndivyo baba alivyokudanganya?
“ Hajanidanganya .He’s going to make me the next
president .Right now I’m the only one he trust the most”
“ Elibariki kitu gani kimekuingia kichwani na
kukubadilisha kiasi hiki? I know me and you we never seen
eye to eye but down deep I know you are a good guy,what
turns you to a monster?
“ I’m serving a monster so I have to be a monster
too!! Akasema jaji Elibariki kwa sauti ya juu akionekana
kukerwa na maneno yale ya Anna
“ Sikiliza Anna.Hakuna ubishi kwamba nitakuwa rais
ajaye wa Tanzania kwa hiyo badala ya kunikashifu na
kunivunja moyo unapaswa kuniunga mkono kwani mimi na
wewe tuna maisha marefu huko mbeleni”
“ What do you mean ?? akauliza Anna akimtazama
Elibariki kwa hasira
“ Sikiliza.Kwa sasa sisi sote tumewapoteza wapenzi
wetu.Umempoteza Edson na mimi nimempoteza Flaviana
hivyo basi kwa kuwa ninaelekea kushika wadhifa mkubwa na
wa juu katika uongozi nahitaji kuwa na mwenza na kwa vile
kwa sasa uko mwenyewe basi si vibaya kama tukianzisha
mahusiano na baada ya mimi kushika urais you are going to
be the first lady” ak asema Elibariki .Ana akamtazama kwa
hasira na kusema
“ You are sick Elibariki and you need treatment.Hivi
unathubutuje kutamka maneno kama hayo? Unafahamu
kabisa kwamba ninakuchukua sana sana na kwa hili
ulilolifanya limenifanya nikuchukie hata zaidi kwa hiyo
naomba usirudie tena kunitusi kwa kunitamkia maneno hayo
” akafoka Anna
“ Hata mimi si kwamba ninakupenda Anna bali huo
ni ushauri toka kwa baba yako na ndivyo anavyotaka