SEASON 2
SEHEMU YA 32
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Mtaona hapa kwamba Elibariki ni mtu sahihi kwa sababu kwanza hana kundi lolote katika chama na pili hana kashfa yoyote,na vile vile kitendo atakachokuwa amekifanya cha kufichua maovu ya Dr Joshua kitamuweka katika nafasi nzuri kuchaguliwa kwani kumg’oa rais madarakani si kitu chepesi.Sifa nyingine Elibariki bado kijana na ana nguvu za kutosha kwa hiyo atapata uungwaji mkono mkubwa sana toka kwa vijana.Ndugu zangu chama kinahitaji mageuzi makubwa na mageuzi haya yataanzia kwa kumuweka madarakani rais kijana kama Elibariki.Najua kila mmoja wenu akilitafakari suala hili kwa makini sana atakiona kile ninachomaanisha.” Akasema Mzee Deus na kikao kikaendelea hadi usiku mwingi na kisha wakatawanyika kwa makubaliano ya kukutana tena siku nyingine kulijadili kwa upana wake suala lile alilolipendekeza mzee Deus.
ENDELEA……………….
Peniela aliwasili nyumbani kwa Mathew,mlinzi akampigia sImu Mathew na kumfahamisha kwamba peniela amewasili akamruhusu amfungulie geti aingie ndani.
“ Its hard to do this but I hve to.lazima niwaeleze ukweli akina Elibariki.Bila kufanya hivyo sintaweza kabisa kujitoa katika team SC41 na maisha yangu hayataweza kamwe kubadilika” akawaza Peniela na kushuka garini akaelekea mlangoni akabonyeza kengele .Katika chumba cha kazi kilichokuwa na mitambo na luninga kubwa tatu ukutani,Mathew na Anitha walikuwa walimkagua Peniela kupitia katika kifaa kilichofungwa pale mlangoniili kukagua kama ana silaha amakitu chochote kinachoweza kuwa kinarusha mawasiliano na kuyapeleka sehemu nyingine.
“ She’s clean” akasema Anitha baada ya kuridhika kwamba Peniela hakuwa na silaha walakitu chochote cha kurusha mawasilianokupeleka sehemu nyingine. Mathew akatoka na kwenda mlangoni kumlaki Peniela
“ karibu Peniela” akasema Mathew
“ Ahsante sana Mathew. Samahani kwa kuwasumbua usiku huu” akasema Peniela
“ usijali P eniela ,unakaribishwa muda wote.katika nyumba hii watu hawalali “ akasema Mathew na kumkaribisha Peniela sebuleni walikokuwa wamekaa jaji Elibariki na Jason.Mtu wa kwanza kusalimiana naye alikuwa ni jaji Elibariki ambaye alimfuata na kumbusu halafu akamsalimu na Jason kwa kumpa mkono kisha akaketi kitini
“ Samahani sana kwa kuwaweka hadi mida hii.Nilikuwa na shughuli moja ya muhimu sana iliyonichelewesha ” akasema Peniela
“Usijali Peniela,hata kama ungekuja asubuhi lazima tungekusubiri tu” akasema jaji Elibariki na wote wakacheka.
“ Ok.Mmeshindaje toka muda ule nilipowaacha? Are you ok now? Akauliza Peniela ambaye uso na sauti yake vilionyesha kwamba hakuwa akihitaji mzaha wowote
“ We’re good.Tuko sawa.Tumeongea na tumeyamaliza yale mambo” akasema Jason
“ Good..I’m so happy for that.You are real men” akasema Peniela na mara akatokea Anitha wakasalimiana.
“ Peniela unatumia kinywaji gani? Akauliza Anitha
“ Ahsante sana Anitha,naomba kama una whsky yoyote tafadhali” akasema Peniela Anitha akaenda kumletea mvinyo ,akanywa funda kubwa.Watu wote pale sebuleni walikuwa kimya wakisubiri kusikia Peniela anataka kuwaambia kitu gani
“ Ninashukuru kwamba ninyi nyote mko hapa .Nilikuwa nawahitaji sana nyote muwepo ili tuongee jambo moja muhimu sana” akaanzisha mazungumzo Peniela bila kupoteza wakati
“ Kwanza kabisa ninakushukuru Mathew kwa kunikaribisha hapa kwako .Ninashukuru vile vile kwa kuendelea kuhakikisha usalama wa Elibariki”akanyamaza na kunywa funda moja la mvinyo
“ Nina mambo mengi sana ambayo ningependa kuwaeleza usiku huu lakini kutokana na muda nitawaeleza mambo mawili au matatu makubwa ya muhimu kwa sasa.” Akanyamaza tena akawaangalia akina Mathew kisha akaendelea
“ Nadhani nyote mnafahamu kuhusiana na kesi ya mauaji iliyokuwa ikinikabili.Ninawashukuru sana Jason wakili wangu na jaji Elibariki kwa kunipigania na hatimaye nikawa huru.Baada ya kesi ile kumalizika jaji Elibariki na Jason walitaka kwenda ndani zaidi kulichimba suala lile na kumfahamu muuaji.Leo hii naomba niwaeleze ukweli kwamba sikutaka jambo lile lifanyike kwani tayari nilikuwa nikimfahamu muuaji.”akasema Peniela na wote mle ndani wakastushwa na kauli ile isipokuwa Mathew
“ Ulifahamu aliyemuua Edfson? Akauliza Jason
“ ndiyo nilifahamu mtu aliyemuua Edson na sikutaka kufumbua mdomo wangu kusema .Niliogopa ningeuawa kwani ni mtu mzito na mwenye nguvu” akasema Peniela
“ Who is that? Akauliza Jason.Peniela akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Ni mheshimiwa rais”
Kimya kifupi kikapita mle ndani na baada ya sekunde kadhaa akasema
“ Ulijuaje kama rais ndiye aliyemuua Edson? Akauliza jaji Elibariki
“ Nimekuja hapa kuwaelezeni ukweli wa kila kitu kwa hiyo msihofu nitawaeleza kila kitu kilivyo.”akasema na kukaa kimya kidogo akaendelea
“ Kabla sijaingia katika mahusiano ya kimapenzi na Edson ,tayari alikuwa katika mahusiano na mtoto wa rais aitwaye Anna na wakati huo mimi nilikuwa na mahusiano ya siri na mheshimiwa rais” akasema Peniela.Uso wa jaji Elibariki ukabadilika.Hakuwa ametegemea kusikia jambo kama lile.
“ Unasema ulikuwa na mahusiano na nani? Akauliza jaji Elibariki
“ Tafadhali usihamaki Elibariki utafahamu kila kitu hatua kwa hatua.Usikuhuu ni usiku utakaojaa ukwelimtupu wa kila jambo.Nilikuwa katika mahusiano na rais Dr Joshua na mpaka sasa bado niko katika mahusiano naye “
“ Shetan…..” jaji Elibariki alipandwana hasira za ghafla akainuka na kutaka kumfuata Peniela lakini Mathew akawahikumdaka akamzuia
“ Elibariki please calm down.Msikilize kwanza Peniela anataka kutueleza jambo gani.Tafadhali naomba usihamaki “akasema Mathew
“ Ahsante sana Mathew.Nafahamu umekasirika kwa sababu unanipenda,lakini naomba utulie na usikie kila kitu ninachotaka kuwaeleza” akasema Peniela
“ Endelea peniela” akasema Mathew
“ Wakati nikiwa katika mahusiano na mheshimiwa rais, siku moja alinialika katika sherehe moja kubwa iliyokuwa ikifanyika ikulu .Katika sherehe hiyo ndipo nilipokutana na Edson na urafiki wetu ukaanzia hapo na baadae tukawa wapenzi.Dr Joshau aligundua kuhusu mahusiano yangu na Edson na alikasirika sana na kupanga mpango ule wa kumuua Edson na mimi nikabebeshwa mzigo ule wa kesi, lengo lake likiwa ni kuniangamiza kabisa.Japo nilimfahamu muuaji lakini sikuthubutu kufumbua mdomo wangu kusema chochote kwa sababu endapo ningethubutu kufanya hivyo basi ningeuawa mara moja ”akasema Peniela na kukaa kimya kidogo huku Elibariki akiendelea kumuangalia kwa macho makali ya hasira
“ Ilitokeaje wewe na rais mkaingia katika mahusiano ya kimapenzi? akauliza Anitha
“ Ni hadithi ndefu kidogo ila nitawaeleza hilo baadae lakini kwa sasa naomba mniruhusu niwaeleze kile nilichokusudia kuwaeleza usiku huu ” akasema Peniela akawaangalia watu wote mle sebuleni na wote walikuwa kimya wakimtazama,akaendelea .
“ baada ya kesi ile iliyokuwa ikinikabili kumalizika na mahakama kuniachia huru,Jaji Elibariki na Jason waliamua kuanzisha uchunguzi ili kulichimba zaidi suala lile na kufahamu nani aliyemuua Edson kwani wote waliamini mimi si muuaji.Niliogopa kwa wao kujiingiza katika suala hili kwani Endapo wangelichimba jambo hili kwa ndani wangeweza kugundua kwamba rais ana mkono wake katika mauaji yale na wangekuwa katika hatari kubwa kwani ninamfahamu vizuri Dr Joshua .Elibariina Jason ni watu wangu wa karibu na wa muhimu sana.Wote wana nafasi kubwa sana ndani ya moyo wangu na katika maisha yangu kwa ujumla kwa hiyo sikuwa tayari kuwaona wakiingia katika matatizo makubwa na kuhatarisha maisha yao.Niliogopa kuwaeleza ukweli wa jambo hilo na kwa hiyo nikatafuta njia ya kuweza kuwavuruga wasiendelee na mpango wao na nikaamua kuwagombanisha.Wenyewe wanafahamu kitu kilichotokea na wakavurugana..Mtanisamehe sana Elibariki na Jason kwa nilichokifanya hadi mkagombana ,lakinisikuwa na njia nyingine ya kuweza kuwazuia msiendelee na mpango ule wa kulichimba kiundani suala la lile la mauaji ya Edson.” Akasema peniela .Elibariki alimuangalia Peniela kwa jicho kali.
“ Sikuwahi kuhisi kama Peniela anaweza kuwa namna hii.Dah ! ama kweli umdhaniaye siye,ndiye.Nilikuwa tayari kufanya kila linalowezekana iliniwe naye lakinikmbenilikuwa najiingiza katika mdomo wa joka kubwa bila kujua.Nilidanganywa na uzir wake wa nje lakini kumbe ndani hana hata chembe ya ubinadamu.Siku ile Jason aliponipiga na chupa kichwani ningeweza hata kupoteza maisha kumbe yote ilisababishwa na Peniela.”akawaza jaji Elibariki akiendela kumuangalia Peniela kwa chuki
“ Ulimuuliza Dr Joshua sababu ya kumuua Edson? Akauliza Mathew
“ Nilimuuliza na akaniambia kwamba alifikia maamuzi yake kutokana na mimi kumsaliti kwa kuanzisha mahusiano na Edson kwa hiyo alitaka wote wakose na mimi nikaozee gerezani na ndiyo maana nikabebeshwa mzigo wa ile kesi kubwa” akasema Peniela.Mathew akamtazama na kusema
“ Alikudanganya”
“ alinidanganya? Peniela akashangaa
“ Ndiyo.dr Joshua alikudanganya kuhusu sabau ya kumuua Edson”
“ Unajuaje kama alinidanganya? Akauliza Peniela
“Tayari tunafahamu kila kitu kuhusiana na kifo cha Edson na ninisababuya yeye kuuawa.”
“ You know? Peniela akazidi kushanga
“ How do you know? Who are you Mathew? Akauliza Peniela
“ Nadhani Elibariki ndiye anayeweza kukueleza kila kitu kuhusiana na mimi.Elibariki please tell Peniela everything’ akasema Mathew.Jaji Elibariki akamtazama Peniela na kusema
“ Kutokana na mambo mengi yasiyo ya kawaida niliyoyaona wakati wa usikilizwaji wa kesi iliyokuwa ikikukabili ,niliazimia kwamba lazima nilifanyie uchunguzi wa kina suala hili na nifahamu ukweli wake.Nilimshirikisha Jason wazo langu na kwa pamoja tukakubaliana kulifanyia uchunguzi suala hili.kwa kuwa sisi wawili hatuna ujuzi wowote wa kufanya mambo haya ya uchunguzi na sikutaka kulichunguza jambo hili kwa kutumia jeshi la polisi nililazimika kutafuta mtu ambaye ana ujuzi na uzoefu wa kutosha wa mambo haya na ndipo nilipomfuata Mathew na kumuomba msaada wake katika jambo hili.Mathew ni mzoefu wa siku nyingi katika kazi hizi,amekwisha fanya kazi katika idara ya ujasusi ya taifa na kwa sasa anafanya kazi zake binafsi” akasema jaji Elibariki na kuendelea
“ Mathew aliwaita wenzake wamsaidie kuifanya kazi hii na mmoja wao ni huyu hapa Anitha na Noah aliyepoteza maisha wakati akiniokoa katika lile shambulio . Kitendo cha Peniela kunivuruga mimi na Jason kwa kutugombanisha hakikuathiri chochote kuhusu mpango wetu wa kulichunguza sualahili ,kwahio Mathew na wenzakewaliendelea na uchunguzi wao.Ni hayo tu ninayoweza kusema kuhusiana na Mathew na kuhusu namna walivyochunguza atakueleza yeye mwenyewe” akasema Elibariki akionekana kuishiwa kabisa maneno ya kusema
“ Peniela nadhani sasa umenifahamu mimi ni nani na kazi yangu ni nini.” Akasema Mathew na Peniela akatingisha kichwa kukubaliana naye,Mathew akaendelea
“ Tumelichungza suala hili na tumegundua kwamba Edson aliuawa kwa amri ya rais lakini kilichopeleka auawe si kwa sababu ya wewe kuingia katika mahusiano naye bali ni kwa sababu nyingine kabisa.Tumegundua kwamba Edson alikuwa akishirikiana na watu Fulani ambao walimtumia katika kuiba nyaraka za siri Ikulu.Nyaraka hizo walipanga waziuze kwa mabilioni ya fedha.Kwa bahati mbaya yeye na watu wote aliokuwa akishirikiana nao wote wamekwisha fariki kwa sababu ya nyaraka hizo na kwa bahati nzuri nyaraka hizo tumezipata na kwa sasa tunazifanyia uchunguzi wa kina kuzifahamu zinahusianana na nini kwani zimeandikwa kwa lugha ya kisayansi na sisi hatuelewi ni kitu gani kilichoandikwamo.Nadhani sasa umeelewa sababu iliyopelekea kifocha Edson.” Akasema Mathew.Peniela alionekana kustushwa sana na taarifa ile.
“ sikuwa nikilifahamu jambohilohilo .Niliaminimanenoaliyoniambia Dr Joshua .Nashukuru kwa kunifahamisha ukweli.’ akasema Peniela.
“ Dr Joshua asingeweza kukueleza ukweli kwa sababu inaonekana nyaraka hizo zina kitu kikubwa sana ndani yake na ndiyo maana wote waliozishika wamepoteza maisha.” akasema Elibariki
Peniela akainama chini akaonekana kujawa na mawazo
“ Ilikuaje hadi ukaanzisha mahusiano na mheshimiwa rais?akauliza Mathew
“ Ni hadithi ndefu kidogo lakini nitawaeleza ukweli wa kila kitu kinachoendelea kwani nina hakika hata ninyi mpaka mmefikia hatua ya kufahamu kuhusiana na jambo hili basi mtakuwa mmekwisha fahamu mambo mengi”akasema Peniela.Akakaa kimyakidogona kuendelea
“ Mimi ni Team SC41.Sina hakika kama mnafahamu au mmekwisha sikia kuhusu Team SC41 “ akasema Peniela na kuzidi kuwachanga Elibariki na Jason ambao hawakuwa wakifahamu chochote kuhusiana na Team SC41.
“ we already know what team SC41 is” akasema Mathew
“ You know? Peniela akashangaa
“ Peniela we don’t know anthything.Kama Mathew anafahamu kuhusu hiyo team unayoisema ni yeye mwenyewe lakini sisi hatufahamu chochote kuhusianana hiyo team ” akasema jaji Elibariki
“ I’m sorry guys ,sikuwahi kuwaeleza chochote kwamba katika uchunguzi wetu tuligundua uwapo wa team SC41 lakini hakukuwa na ulazima wa kuwaeleza kwa sababu kikundi hiki hakikuhusika na kifo cha Edson ”akasema Mathew
“ Ulipaswa kutuweka wazi kuhusu kila kitu Elibariki. Kwa hiyo team SC41 ni akina nani? shughuli zao ni nini? Akauliza Elibariki.
“ Team SC41 ni kikundi cha siri kinachofanya kazi zake kwa siri hapa nchini na katika ukanda wa afrika mashariki.Kikundi hiki kilianzishwa kwa siri na serikali ya marekani kwa ajili ya kulinda maslahi yake katika ukanda huu wa afrika ya mashariki.Kazi kubwa ya kikundi hiki ni kuhakikisha kwamba maslahi ya Marekani yanalindwa na yanakuwa salama.Serikali ya Marekani imefanya uwekezaji mkubwa katika eneo la afrika mashariki kwa hiyo wameweka kikundi hiki makusudi ili kiwe ni kama jicho la kuhakikisha kwamba hakuna hatari yoyote katika uwekezaji wao.Team SC41 imekita mizizi yake ndani ya serikali na wanafahamu kila kinachoendelea ndani ya serikali na endapo kuna mpango wowote wa kuhujumu maslahi ya marekani basi watafahamu mara moja.Mimi ni mmoja wao japokuwa kazi yangu mimi ni tofauti na wengine.Kazi yangu mimi ni kutafuta taarifa Fulani toka kwa mtu.Endapo kuna mtu ambaye team SC41 wanahitaji kitu Fulani toka kwake basi hunitumia mimi.Hujenga mahusiano na mtu huyo na kisha huhakikisha kwamba nimekipata kitu hicho au taarifa hiyo inayotakiwa.” akasema Peniela
“ Kuingia katika mahusiano na Dr Joshua ulikuwa ni mpango wa team yako au ulipenda mwenyewe? Ama kuna kitu ulikuwa unakitafuta? Akauliza jaji Elibariki ambaye alionekana kuwa mkali sana.
“ Ulikuwa ni mpango wa TeamSC41 wala haikuwa ni kwa mapenzi yangu.Kuna kitu walikuwa wanakihitaji toka kwake na ndiyo maana wakanitumia mimikuanzishamahusiano naye” Akasema Peniela
“ Ni kitu gani mnachokitafuta kwa Dr Joshua? Akauliza Mathew
“ Package E21” akajibu Peniela
“ Package E 21?.Ni kitu gani hicho? Akauliza Mathew
“ Hata mimi sifahamu ni kitu gani na hakuna aliyewahi kunieleza package hiyo ina nini lakini inaonekana ni kitu chenye thamani kubwa kwa sababu Package hiyo inafichwa ikulu na hata hapo ikulu kwenyewe anayefahamu mahala ilipo ni rais peke yake .Dr Joshua anataka kuiuza package hiyo kwa matrilioniya fedha.Dr Flora mke wa rais aligundua kuhusu jambo analotaka kulifanya mume wake na alijitajhidi sana kumsihi mume wake asiiuze package hiyo lakini bila mafanikio na ndipo alipoamua kuwaeleza wanae kile anachotaka kukifanya baba yao na mchana wa siku ambayo alipanga kuonana na wanae jioni ili awaeleze anachokifanya baba yao akafariki dunia.Aliuawa ili asiweze kutoa siri”
“ What ?! Dr Flora aliuawa kwa sababu ya hiyo Package? Akashangaa jaji Elibariki.
“ Ndiyo.Dr Flora aliuawa ili asiweze kutoa siri hiyo.”akasema Peniela.Kila mtu alikuwa kimya pale sebuleni.
“ Una uhakika gani kwamba Dr Flora aliuawa ili asiweze kutoa siri? Akauliza Mathew
“ katika biashara ya package hiyo Dr Joshua anashirikiana na watu wengine wawili.Katibu wake Dr Kigomba na daktari wa familia ya rais anaitwa Captain Amos.Hawa ndio wanaofahamu kila kitu kuhusianana biashara nzima ya package hiyo.Captain Amos naye yuko team SC41 na ndiye anayetupa taarifa zote kuhusiana na kila kinachoendelea ikulu.Captain Amos ndiye aliyemchoma sindano ya sumu Dr Flora kwa amri ya rais.” Akasema Peniela
“Mawazo yangu yalikuwa sawa kabisa kwamba Dr Flora aliuawa.Nilitegemea tu kwamba lazima kifo chake kitakuwa kimesbabishwa na jambo kubwa na kama anavyosema Peniela nikwamba aligundua kuhusiana na hiyo package anayotaka kuiuza Dr Joshua na ndipo alipouawa.Package hiyoni ya nini? Inamahusiano yoyote na hizi nyaraka alizoziiba Edson? Mhh! Mambo haya yanazidi kuwa magumu.” Akawaza Mathew.
Jaji Elibariki alikuwa ameinama amekishika kichwa chake
“ Ouh Mungu wangu ! akasema Elibariki halafu akainua kichwa akasema
“Mathew tulikuwa sahihi kabisa kuhisi kwamba Dr Joshua atakuwa akihusika na kifo cha mkewe na ndiyo maana nguvu kubwa ikatumika kuhakikisha sababu ya kifo cha Dr flora haijulikani.Kumbe tulipompelekea ile taarifa yetu ya uchunguzi iliyobainishakwamba dr Flora aliuawa kwa sumu tulikuwa tunajipalia makaa ”akasema Elibariki na kumstua peniela
“ Mlifahamu kilichomuua Dr Flora? Akauliza Peniela
“Ndiyo tulifahamu kila kitu.”akasema Mathew
“ Badaa ya kifo cha Dr Flora ilitolewa taarifa kwamba mwili wake usifanyiwe uchunguzi wowote kubainisababuya kifo chake na badala yake ikatolewasababu ya jumla kwamba kilichomuua ni shinikizo la damu. Mke wa Elibariki aliingiwa na hofu kuhusu kifocha mama yake namazingira kilivyotokea hivyo akamuomba mume wake amsaidie kuweza kuufahamu ukweli.Elibariki likuja kwangu akaniomba nimsaidie kufanya uchunguzi wa kubaini kilichomuua Dr Florana nusura tungepoteze maisha yetu wakati wa kufanya uchunguzi huo lakini mwishowe tuliubaini ukweli .Tuligundua hadi aina ya sumu iliyomuua Dr Flora .Baada ya hapo Elibariki alimpelekea mheshmwia rais majibu yale ili ayafanyie kazi bila ya kufahamu kwamba ni yeye ndiye aliyekuwa nyuma ya yale mauaji”akasema Mathew
“I’m impressed with you guys.Namna mnavyofanya kazi zenu mmenifurahisha sana” akasema Peniela
“ Baada ya Dr Joshua kugundua kwamba tayari Elibariki amegundua kilichosababisha kifo cha dr Flora aliamuru auawe na ndipo lilipopangwa lile shambulio ambalo alinusurika kuuawa”akasemaMathew.Jaji Elibariki naye akasema
“ Katika shambulio lile alitokea mwanamke mmoja na kunichukua toka eneo la tukio na akanikabidhi kwako.Mpaka leo sijamfahamu mwanamke yule ni nani na kwa nini aliniokoa.Hakutak……”kabla Elibariihajaendelea Penielaakaingilia kati
“That’s Jessica.Naye ni team SC41.Alipewa maagizo ya kukuokoa na Amos .”akasema Peniela.
“ Dah ! nimechoka kwa kweli.Hawa team SC41 wako kila mahala ,but why they saved me? Akauliza Elibariki.Kabla Peniela hajajibu kitu Mathew akauliza
“ John mwaulaya anaendeleaje?
Swalilile lilimstua mno Peniela.Hakuwa ametegemea kama Mathew anamfahamu John
“ Umesema John mwaulaya? Akauliza peniela
“ Ndiyo.John Mwaulaya.is he ok? Akauliza Mathew
“ Do you know him?
“ yes I know him” akasema Mathew
“ John mwaulaya ni nani? Akauliza jaji elibariki
“ Ni kiongozi wa team SC41”akajibu mathew
“ Unafahamiana na kiongozi wa team SC41? akauliza Elibariki kwa mshangao
“ Ndiyo ninamfahamu.Japokuwa si marafiki lakini mimi na yeye tun historia .Nitawaeleza siku nyingine ninamfahamuje John mwaulaya lakini usiku huu ni usiku wa peniela ,ametueleza mambo makubwa kabisa na kutufunulia mambo mengi mazito.Peniela endelea kutueleza kile ulichokusudia kutueleza” akasema Mathew,Penielaakaendelea
“ baada ya kunusurika katika ajali ile ,Elbariki alikuja nyumbani kwangu kwani aliamini ni sehemu salama.Ni kweli ni sehemu salama na alikuwa salama hadi pale Jason alipokwenda kutoa taarifa polisi kwamba Elibariki yuko kwangu.Taarifa zile zilimfikia Amos naye akamtaarifu kiongozi wangu John mwaulaya aliyeamuru Jason akamatwe na aeleze kwa nini alitoa taarifa zile kwa jeshi la polisi.Alikuwa na wasi wasi kwamba yawezekana Jason akawa anafahamu mambo mengi kuhusu team SC41.Walimteka Jason na kumtesa na ndipo alipopata nafasi ya kunipigia simu na kunifahamisha kwamba ametekwa.Nilichukizwa mno na kitendo kile cha kuwateka na kuwatesa watu wangu wa karibu na hiyo ndiyo sababu niko hapa nikiwaeleza haya yote niliyowaeleza ambayo sikupaswa kuwaelezakitendo kile na hii ndiyo sababu niko hapa kwenu mida hii nikiwaeleza haya yote niliyowaeleza na nikihitaji msaada wenu.” akasema Peniela akaak kimya kidogona kusema tena
“ I need your help guys”
“Our help? Akauliza Mathew
“ yes. Your help.”
“ Unahitaji msaada gani? Akauliza Mathew
“ To take down Team SC41”
TUKUTANE SEHEMU IJAYO…