Peniela (Story ya kijasusi)

PENELA SEASON 3

SEHEMU YA 28

MTUNZI : PATRICK.CK

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

“Hii ni nafasi ambayo natakiwa kuitumia vizuri”akawaza Elibariki na kwa kasi ya aina yake akakinyakua chungu cha maua kilichokuwa karibu yake na kumpiga nacho Anitha Kichwani akaanguka na kupoteza fahamu.Akaikanyaga kanyaga simu ile akakimbia hadi katika mlango wa chumba cha Mathew na kujaribu kuufungua.Ulikuwa umefungwa.Akarudi nyuma hatua kadhaa na kuurukia teke mlango ule ukafunguka akaingia ndani na moja kwa moja akaeleka katika kile kisanduku chenye namba.Akabonyeza namba alizozikumbuka lakini mlango haukufunguka.
“ C’mon nimekosea wapi? Mbona namba alizobonyeza Mathew ni hizi hizi? Akajaribu tena lakini bado mlango haukufunguka
“Nimekumbuka kulikuwa na namba mbili mwisho nasi namba tano.”
Akarudia tena kubonyeza na safari hii kabati kubwa la ukutani likasogea pembeni na mlango ukafunguka kwa akaanza kushuka kuelekea chini



ENDELEA………………………



Jaji Elibariki akaufunguua mlango wa chumba alimowekwa Rosemary akaingia.Tayari Rosemary alikwisha pitiwa na usingizi. Elibariki akamuamsha.Rose akafumbua macho na kupatwa na mshangao mkubwa kwa kumuona Elibariki mle chumbani
“ Jaji ?!! akashangaa Rose
“ Rosemary amka” akasema Elibariki
“ jaji unafanya nini huku?
“ Rose I’ve come to free you” akasema jaji Elibariki huku akiangaza angaza kama angeweza kupata kitu chochote cha kumuwezesha kufungulia pingu alizofungwa Rosemary
“ You want to free me?akauliza Rosemary kwa mshangao
“ Ndiyo.Nataka nikuondoe hapa.”akajibu jaji Elibariki

“ jaji mbona sikuelewi? Unataka kunifungua? Unataka kunipeleka wapi?

“ Sikiliza Rose,hatuna muda mrefu hapa.Elibariki anaweza akatokea muda wowote na akinikuta huku tumekwisha kwa hiyo acha kuuliza maswali na unisadie mawazo namna ya kufungua pingu hizi ulizofungwa” akasema Elibariki

“ Hebu subiri kwanza jaji .Bado sijakuelewa unataka kufanya nini.Umesema unataka kunifungua? Unataka kunipeleka wapi? Akauliza Rose

“ Mathew hajanituma nikufungue lakini nimeamua mimi mwenyewe nikusaidie uweze kutoka humu ndani.Mathew hafahamu chochote juu ya hiki ninachokifanya”
“ Mathew hayupo?akauliza Rose

“Mathew hayupo ndiyo maana nimepata nafasi ya kuja humu.Unadhani angekuwepo ungeniona humu? Akauliza jaji Elibariki

“ jaji natamani sana nikuamini lakini ninasita.Wewe ni mshirika mkubwa wa Mathew unanishangaza sana kwa kitu unachotaka kukifanya.Are you betraying your friends? Akauliza Rose.Jaji Elibariki akavuta pumzi ndefu na kusema

“ Rose acha kuuliza maswali mengi .Ninataka nikutoe humu.Unahakika Mathew atakuachia? Nakuhakikishia kwamba hanampango wowote wa kukuachia huru kwa hiyo naomba tafadhali ukubali nikusaidie.”akasema Elibariki.
“ kwa nini unafany ahivi Elibariki? Kwa niniunawasaliti wenzako kwa sababu yangu? Akauliza Rosemary.
“ Rose nina tatizo kubwa na nimeona ni wewe pekee unayeweza kunisaidia ndiyo maana nimelazimika kufanya hivi ..Kabla sijakufungua ninataka unihakikishie kwamba utanisaidia tatizo langu.”
“Ni tatizo gani ulilonalo na unalotaka nikusaidie?akauliza Rose
“ hatuna muda wa kupoteza Rose.Mathew anaweza akatokea hapa muda wowote kwa hiyo nitakueleza baada ya kuwa tumetoka hapa.”akasema jaji Elibariki.

“ Ok jaji tafuta kitu kidogo kama waya au sindano nikuonyeshe namna ya kufungua” akasema Rose.jaji Elibariki akatoka kwa kasi mle chumbani hadi katika chumba cha Mathew akaanza kupekua sehemu mbali mbali akitafuta kitu cha kumuwezesha kufungua pingu zile alizofungwa Rose.Katika mojwapo ya droo akaziona funguo ambazo alihisi zinaweza kuwa ni zakufungulia pingu zile.Kwa kasi akarejea chini na kweli kama alivyokuwa amehisi funguo zile ziliweza kufungua pingu na Rosemary akabaki huru.Alikuwa amechubukana mwli wake wote umatapakaa damu.
“ I’m free now”akasema Rosemary.

“ Lets get out of here” akasema jaji Elibariki akamsaidia Rose kushka katika kitanda hlafu akamtegemeza wakatoka mle ndani.Rosemary alikuwa akihisimaumivu makali kutokanna kukatwa vidole na Mathew.Walielekea hadi katika chumba cha ofisi.Rosemary akastuka alipomuna Anitha amelala sakafuni hana fahamu

“ Na huyu naye vipi?akauliza
“ Huyu ndiye aliyekuwepo humu ndani na alikuwa ni kikwazo kikubwa kwangu hivyo nikampiga na mtungi wa maua kichwani akazimia.Tusipoteze muda wapigie watu wako waje watuchukue haraka kabla Mathew hajarejea.” Akasema Elibariki huku akichukua waya na kumfunga Anitha miguu na mikono
Juu ya meza Rose akaiona simu yake pamoja na kompyuta yake akaichukua simu akaiwasha na kuongeana mtufulani simuni akamuhakikshia kwamaba yuko salama na akamuomba waje haraak wamchukue.Rose hakuwa akipafahamu mahala walipo,hivyo akampa Elibariki simu ili amuelekeze Yule jamaa..
“Mathew kaenda wapi? Akauliza Rose
“ Aliondoka na Peniela na sijui wameelekea wapi.” Akajibu Elibariki.
“ watu wako watachukua muda gani kufika hapa?akauliza Elibariki

“ Sijui watatumia muda gani lakini watajitahidi sana kufika ndaniya muda mfupi.” Akasema Rose huku akiichukua kompyuta yake

“ washenzi sana hawa vijana.Sintawasamehe kabisa kwa jambo walilonifanyia. “ akasema Rose
“ jaji kwa kitendo hiki ulichokifanya ujue umewasaliti wenzako na watakutafuta kila kona ya nchi hadi wahakikishe wamekupata.Una hakika kwamba unataka kufanya jambo hili? Akauliza Rose

“ Najua nimefanya jambo baya la kuwasaliti wenzangu lakini sina namna nyingine ya kufanya kutokana na matatizo niliyonayo ndiyo manaa nikaamua kukusaida kuwa huru ili na wewe unisaidie.”akasema Elibariki
“ Jaji umenifanyia jambo kubwa sana na lazima na mimi nikusaidiae katika matatizo yako.Watu wangu wanaweza kufika hapa muda wowote kwa hiyo nenda getini ukawasubiri ili wasipotea” akasema Rose na Elbariki akatoka mle ndani akaenda getini.

“ Nimewasaliti rafiki zangu .Nimefanya jambo baya sana lakini sina namna nyingine ya kufanya zaidi ya hivi nilivyofanya.Siwezi kukubali maisha yangu yawe niya kujificha humu ndani.”akawaza jaji Elibariki.
“ Katika maisha yangu sijawahi kukutana na vijana washenzi kama hawa.Bado sielewi mpaka leo hii wamewezaje kufanikiwa kunitia mikononi mwao.Tayari wamekwisha fahamu mambo mengi kuhusu mimi na kila ninachokifanya.Wameipekua kompyuta yangu kila mahala na wamegundua mambo mengi sana.Wamefahamu mambo yangu mengi ninayoyafanya,wamewafahamu washirika wangu wote.Ninaapa sintawasamehe hata kdogo.lazima niwafanyie kitu kibaya sana.Wameuwasha moto wenyewe na hawatauzima tena.Ni nani yuko nyuma yao? Lazima kuna mtu ambaye anawapa nguvu ya kuweza kufanya haya yote.Nina wasi wasi na Deus.Mimi na yeye kwa sasa ni maadui wakubwa na ninahisi yeye ndiye atakayekuwa nyuma ya hawa vijana na anawapa habari zangu kisha wakanivamia na kunishikilia.”akawaza Rose huku uso wake ukiwa umejikunja kwa hasira.Akaitazama mikono yake namna ilivyoumizwa ,akaviangalia vidole vyake vya miguu akakumbuka namna Mathew alivyovikata bila huruma..
“ Yule kijana amenisababishia ulemavu kwa kunikata vidolevyangu viwili.Amenitesa sana na kwa hili ninaapa sintomsamehe.Nitamsaka kila kona ya nchi hadi nihakikishe nimempata naye nimtese kama alivyonitesa mimi.Hataweza kunikimhia nina hakika ndaniyamuda mfupi nitakuwa nimempata.Mtandao wangu ni mkubwa na umesambaa kila kona.Nitampata tu.”akaendelea kuwaza Rose na kuketi kitini kwani alianza kuhisi maumivu mguuni.Akachukua simu yake na kuwapigia tena vijana wake kujua wamefika wapi na wakamuhakikishia kwamba wako karibu sana kufika.
“ Leo ninaiteketeza nyumba hii na watakaporejea watakuta imebaki majivu matupu na kila kitu chao kimeteketea .Lazima niwaonyeshe nguvu zangu.Wao na huyo anayewatuma watanitambua mimi ni nani.Watajuta kwa hiliwalilolianzisha .”akawaza Rose.
Baada ya dakika ishirini jaji Elibariki akaingia ofisini alimokuwa amekaa Rose akiwa ameongozana na vijana sita wakiwa na silaha.Vijana wale walistuka sana kwa haliwaliyomkuta nayo Rose.

“Pole sana madam.Who did this to you? Akauliza kijana mmoja aliyekuwa ameshika bastora na aliyeonekana ni kiongozi wa vijana wale.Rose akamtazama Elibariki kisha akatoa maelekezo kwa wale vijana wake

“Mkamateni huyo jamaa mfungeni,tunaondoka naye.Nimtu muhimu sana kwetu.Mwagieni petrol nyumba nzima na kisha tuichome moto nyumba yote.”akasema Rose na kisha akamuaangalia Anitha aliyekuwa amelala pale chini.
“Mchukueni hata huyu pia.Tunaondoka naye” akasema

“ Rose what is the meaning of this? We had an agreements!!!..jaji Elibariki akashangaa.
Rose akainuka akajitahidi kutembea kwa shida halafu akamnasa kofi.
“ You’ve betrayed your friends do you think I can believe you? Take him away ”Rose akawaamuru vijana wake.jaji Elibariki akafungwa pingu na kuanza kutolewa mle ndani.
“ Rose hivi sivyo tulivyokubaliana” akasema jaji Elibariki kwa nguvu lakini vijana wale wenye miili iliyojengeka wakamchukua kwa nguvu na kumfunga na kamba wakamrushia ndani ya gari.Anitha naye akachukuliwa na kurushwa ndani ya gari pamoja na Elibariki
“ Rose anafanya nini tena? Mbona anafanya kinyume na tulivyokubaliana?.Nimemsaidia kumuokoa lakini amenigeuka.Sikupaswa kabisa kumuamini huyu mwanamke.Maskini nyumba ya Mathew inataka kuteketezwa kwa moto.Sikujua kama huyu mwanamke ni mnyama kiasi hiki.”Mathew akastuliwa mawazoni na mlango uliofunguliwa na Naomi akarushwa ndani.

“ jaji nini kinaendelea? hawa watu ni akina nani? Tumevamiwa? mathew yuko wapi? Akauliza Naomi.
Vijana wawili wakamtegemeza Rose kwani alikuwa akisikia maumivu makali ya miguu kwa sababu ya vidole alivyokatwa na Mathew,wakampeleka katika gari.
Mlango wa nyumba ambayo Mathew huhifadhia magari yake ukavunjwa mle ndani yakakutwa magaloni manne ya mafuta ya akiba wakayachukua na kuyamimina ndani ya nyumba halafu wakapanda katika magari yao .Mmoja wao akawasha kiberiti akakirushia ndani na nyumba ikaanza kuwaka moto kisha wakaondoka.
“This is just the beginning .Wamenichokoza wao wenyewe na sasa ni zamu yangu kuwaonyesha mimi ni nani.Vijana wadogo kama wale hawawezi wakanifanya mimi namna hii.Wamenivamia nyumbani kwangu,wakamuua mpenzi wangu kwa risasi,wakaniteka na kunificha humu katika nyumba yao,wamenitesa mno na katu siwezi kukubali kuteswa na vijana wadogo kama hawa wasiokuwa na adabu hata chembe.Nitawasaka kila mahala na kuhakikisha nimewapata na mimi niwakate vidole vyao kama walivyonikata vyangu.Nitamsaka pia na anayewatumia ili kupambana na mimi ambaye nina hakika lazima atakuwa ni Deus.”akawaza Rosemary Mkozumi

.


*******



“ Peniela!..Peniela !!!..”akaita Mathew lakini Peniela hakuwa na nguvu kabisa.Umati wa watu ulianza kuongezeka katika mtaa ule wakija kushuhudia tukio lile la nyumba ya Peniela kuwaka moto .
Mathew akautazama moto ule mkubwa akavuta pumzi ndefu.
“ Hili si eneo salama tena.Team SC41 wameamua kuichoma nyumba ya Peniela kwa makusudi.They did this to me also and killed my wife.I have to save Peniela”akawaza Mathew na kumuinua Peniela akamuweka begani na kuondoka naye akapita kichochoro kadhaa na kutokea sehemu moja iliyokuwa na nyumba inayoendelea kujengwa akaingia ndani na kumlaza Peniela katika mojawapo ya chumba.Jasho jingi lilikuwa linamtoka akavua shati. Na kuanza kumpepea Peniela
“ Nilifanya vizuri kukataa kukaa pale kwa Peniela kama alivyokuwa ameniomba.Kumbe Team SC41 walikuwa wanamfuatilia kwa karibu sana kutaka kufahamu yuko wapi ,yuko na nani na anafanya nini.Hawa jamaa watamtafuta Peniela kila kona hadi wahakikishe wamempata kwani tayari wamekwisha gundua kwamba amewasaliti.Masikini Peniela jumba lake lote limeteketea kwa moto.Namuonea huruma sana kwa namna anavyoteseka.Ninaapa lazima nihakikishe kwamba ninamlinda kwa kila namna ninavyoweza.”akawaza Mathew na kisha akamuinamia peniea

“ Peniela ! Peniela..”akamtikisa kidogo na Peniela akafumba macho.

“ Ahsante Mungu:”akasema Mathew na kumuegemeza Peniela ukutani..

“ Unajisikiaje Peniela?akauliza Mathew

“ Mwili wote hauna nguvu kabisa.”akajbu Peniela
“Peniela.Jikaze kidogo na tondoke eneo hili.Eneo hili si salama kabisa kwetu kwa sasa”akasema Mathew

“ Mathew wamechoma nyumba yangu.Wameunguza nyumba yangu !! Peniela akaangua kilio
“ Shhh !!Peniela usilie tafadhali.Huu si wakati wa kulia”akasema Mathew

“ Mathew kila kitu changu wamekiteketeza.kwa nini wanifanyie hivi? Nimewafanyia mambo mangapi mazuri hadi wanifanyie hivi? akauliza Peniela huku machozi yakimwagika

“ peniela nadhani sasa umeelewa kwamba Team SC 41 si watu wazuri hata kidogo.Hata uwafanyie nini hawatakuthamini .Tunachotakiwa kufanya kwa sasa ni kuelekeza nguvu katika kuhakikisha kwamba tunaipata package kutoka kwa Dr Joshua na baada ya hapo tutawageukia Team SC41.Ninakuhakikishia Peniela kwamba nitapambana hadi nihakikishe tumelifyeka kabisa kundi lote la Team Sc41 hapa nchini .Usijali kuhsu vitu vyako vilivyoungua.Utavipata vingine” akasema Mathew.

“ Mathew siwezi kukuficha nimeishiwa nguvu kabisa.Sikuwahi kuhisi kama team Sc41 wanaweza wakafikia hatua ya kunifanyia kitu kama hiki na kusahau mambo yote mazuri niliyowafanyia.Kama wameweza kunichomea nyumba yangu na kila kitu changu basi dakika yote wakinipata wataniua.Nitafanya nini Mathew?akauliza Peniela
“Peniela nitakulinda .Niamini nikwambiavyo kwamba nitakulinda” akasema Mathew

“ Mathew I don’t know if I can do this anymore”akasema Peniela.mathew akamuangalia
“Peniela anahitaji muda wa kutuliza akili yake.Tukio lile la kuishuhudia nyumba yake inateketekea limemuumiza sana” akawaza Mathew halafu akapapasa katika mifuko yake akachukua simu yake akaitazama kama iko salama

“ Thanks God simu yangu iko salama hata baada ya rabsha zile zote”akawaza Mathew na kuzitafuta namba za simu za Anitha akampigia.

“Hallow Mathew .What happened? Akauliza Anitha
“ Anitha tumepatwa na matatizo.Nahitaji msaada.Nataka uchukue gari utufuate sehemu nitakayokuelekeza ili uje utuchukue kwani Peniela hawezi kutembea.” Akasema Mathew lakini hakusikia Anitha akimjibu
“Anitha umenisikia? Akauliza lakini bado kulikuwa kimya na mara simu katika.Akapiga tena lakini simu ya Anitha haikuwa ikipatikana,akapiga namba nyingine za simu zilizomo mle ofisini lakini zote hazikupokelewa.

“ What happened? Kwa nini Anitha hataki kupokea simu? Akajiuliza

“ Nimeanza kuwa na hisia mbaya kwanini Anitha akatike ghafla simuni? Anyway ngoja nitafute msaada sehemu nyingine tena.Nani anayeweza kunisaidia muda huu? Akajiuliza Mathew

“ jason !..japokuwa mara ya mwisho tulikwaruzana lakini nina hakika akisikia kuhusu peniela lazima atakuwa tayari kumsaidia”akawaza Mathew na kuzitafuta namba za simu za Jason akampigia .Simu ikaita mara ya kwanza na kukatika.Ikaita mara ya pili ikapokelewa
“ Hallow Mathew” akasema jason

“ Jason samahani kwa kukupigia usiku huu.Nina shida nahitaji msaada wako.”

“Mathew I cant help you .Mara ya mwisho tulipoachana wakati tukitoka kwa John mwaulaya ulinitamkia maneno mabaya sana ya dharau . Siwezi kukusaidia Mathew hata iweje” akasema Jason
“ Josh its peniela.If you cant help me then help her” akasema Mathew
“ Peniela kafanya nini?

“Amepatwa na tatizo na anahitaji msaada”
Jason alipotajiwa jina la Peniela alishindwa kukataa,Mathew akamuelekeza sehemu ambayo atawakuta .
“ peniela nimempigia simu jason anatufuata .Jikaze tuondoke tuelekee sehemu ambayo tutakutana.” akasema Mathew akamuinua peniela wakatoka nje ya lile jumba.




TUKUTANE SEHEMU IJAYO………
 
PENIELA SEASON 3

SEHEMU YA 29

MTUNZI : PATRICK.CK

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

“ jason !..japokuwa mara ya mwisho tulikwaruzana lakini nina hakika akisikia kuhusu peniela lazima atakuwa tayari kumsaidia”akawaza Mathew na kuzitafuta namba za simu za Jason akampigia .Simu ikaita mara ya kwanza na kukatika.Ikaita mara ya pili ikapokelewa
“ Hallow Mathew” akasema jason

“ Jason samahani kwa kukupigia usiku huu.Nina shida nahitaji msaada wako.”

“Mathew I cant help you .Mara ya mwisho tulipoachana wakati tukitoka kwa John mwaulaya ulinitamkia maneno mabaya sana ya dharau . Siwezi kukusaidia Mathew hata iweje” akasema Jason

“ Josh its peniela.If you cant help me then help her” akasema Mathew

“ Peniela kafanya nini?

“Amepatwa na tatizo na anahitaji msaada”
Jason alipotajiwa jina la Peniela alishindwa kukataa,Mathew akamuelekeza sehemu ambayo atawakuta .
“ peniela nimempigia simu jason anatufuata .Jikaze tuondoke tuelekee sehemu ambayo tutakutana.” akasema Mathew akamuinua peniela wakatoka nje ya lile jumba.




ENDELEA……………………………..




Moto ule mkubwa uliokuwa unaiteketeza nyumba ya Peniela uliwafanya watu wengi waamke na kutoka katika nyumba zao wakaelekea katika eneo la tukio ili kujaribu kutoa msaada wa uokoaji.Ndani ya kipindi kifupi baada ya kupewa taarifa kikosi cha zimamoto kikawasili wakiwa na gari tatu kubwa zilizojaa maji na kuanza kuuzima ule moto wakisadiana na wananchi.Askari polisi pia walifika mahala pale kwa ajili ya kusaida katika uokoaji na ulinzi wa mali na usalama wa watu.Moto ulikuwa mkubwa sana na moshi mwingi ukaonekana angani.
Wakati jitihada za kuuzima moto ule zikiendelea kati ya kikosi cha zimamoto na wananchi,Mathew na Peniela walikuwa wanajikongoja kuelekea mahala ambako walipanga kukutana na Jason.Peniela hakuwa na nguvu za kutosha kutembea haraka ili kuwahi hivyo kuna nyakati ilimlazimu Mathew kumbeba mgongoni.Walifika katika sehemu ambayo walipanga wakutane na Jason.Ni katika kituo cha basi cha Msagaweni.Mathew akamkalisha Peniela katika kiti cha kupumzikia abiria .
“ Mathew thank you so much.Sintausahau usiku wa leo kwa namna ulivyonisaidia” akasema Peniela kwa sauti dhaifu.Mathew akamtazama na kusema

“ Usijali Peniela.Nilikuahidi kukulinda na nitafanya hivyo siku zote hata kama nitajiweka mimi hatarini ili wewe uwe salama.Tafadhali pumzika wakati tunamsubiri Jaso….”Ghafla akastuliwa na watu watatu waliotokea ghafla wakiwa na mapanga mikononi na kuwaamuru kusalimisha kila walichokuwa nacho.Peniela akatetemeka sana .Ghafla bila kutarajia Mathew akaichomoa bastora yake na kuwalekezea watu wale na kuwataka watimue mbio haraka sana.Kufumba na kufumbua vibaka wale wakatawanyika haraka sana kila mmoja na njia yake.Hawakutarajia kabisa kama Mathew alikuwa na bastora.
“ Mathew,eneo hili si salama hata kidogo .Kama usingekuwa na hiyo silaha vibaka hawa wangetuumza sana.” akasema Peniela kwa uoga..
“ Usiogope Peniela hakuna kibaka anayeweza kutufanya lolote.Nina risasi chache zimebaki katika bastora yangu zinatosha kutulinda” akasema Mathew na kuchukua simu yake akampigia Jason akamfahamisha kwamba tayari wamekwisha wasili katika eneo walilopanga wakutane.Baada ya kuwasiliana na Jason,akampigia tena Anitha lakini bado simu yake haikupatikana na kingine kilichomstua zaid hata zile simu zake nyingine ambazo huzitumia ofisini kwake hazikupatikana tena.

“ Whats going on? Kwa nini simu zote hata zile za ofisini hazipatikani ghafla? Hii haijawahi kutokea hata mara moja.Kuna kitu hakiko sawa hapa “ akawaza Mathew na kuchkua simu akapiga tena lakini hakukuwa na mabadiliko.Simu hazikupatikana.
“ Natakiwa kwenda nyumbani haraka.Something is wrong there” akawaza Mathew halafu akamgeukia Peniela
“ Peniela !!..unajisikiaje?

“ Mathew sina nguvu kabisa.Mwili wote hauna nguvu hata kidogo” akasema Peniela
“ usijali Peniela.Nimeongoea na Jason amesema yuko karibu sana kufika.”
Baada ya kama dakika kumi hivi kwa mbali likaonekana gari linakuja upande ule.Mathew akaweka bastora yake tayari halafu akamuamsha Peniela
“ Peniela kuna gari linakuja upande huu.Inawezekana akawa ni Jason au hata Team Sc41.Inuka tujiweke tayari” akasema Mathew na kumsaidia Peniela kuinuka kisha wakajibanza katika kona ya kituo.Gari lille lilikuwa linakuja kwa mwendo mkali sana na baada ya muda likawasili pale kituoni na kusimama.Mathew bastora ilikuwa mkononi tayari kukabiliana na lolote lile ambalo lingejitokeza lakini kupitia mwangaza wa taa ya gari akamuona Jason akishuka,akashusha pumzi.

“ Peniela Jason amefika” akasema Mathew halafu akajitokeza na kumuita Jason aliyekuwa akiangaza angaza akiwatafuta.Jason akawakimbilia na moja kwa moja akamuinamia Peniela
“ Peniela ! Peniela !..nini kimetokea? Akauliza Jason

“ Jason we need to get out of here fast” akasema Mathew na kusaidiana na Jason kumuinua Peniela hadi ndani ya gari kisha wakaondoka
“ Mathew nini kimetokea? Mbona unavuja damu kiasi hicho? Mmeshambuliwa? Akaulizia Jason kwa wasi wasi baada ya kumuona Mathew namna alivyochafuka damu
“ Jason kuna tukio limetokea usiku huu baya sana.” akasema Mathew na kumsimulia Jason kila kitu kilichotokea usiku ule.Jason akaogopa sana.
“ Mathew mnatakiwa mpelekwe kwanza hospitali mkapate matibabu.Jeraha lako linavuja damu nyingi.Hata Peniela naye anaonekana kuwa katika mshtuko mkubwa sana.Ouh maskini Peniela kwa nini ni yeye kila wakati anakutwa na mambo mabaya? Akasema Jason
“ Hapana Jason nipeleke kwanza nyumbani nikaangalie kama kuna usalama.Nina wasiwasi ana na usalama wa watu niliowaacha kule .” Akasema Mathew

” Sawa Mathew lakini kwa hali hii ulitakiwa kwanza matibabu”
“ Usijali Jason nipeleke kwanza nyumbani.Nina wasi wasi mkubwa kama nyumbani kwangu kuko salama” akasema Mathew akageuka na kumtazama Peniela aliyekuwa amelala katika kiti cha nyuma.
“ Jason samahani sana kwa kilichotokea siku ile.Nilikutamkia maneno ya kuudhi lakini nilifanya vile kwa ajili ya kukulinda wewe mwenyewe kwani nilifahamu ulichokuwa unataka kukifanya ni hatari sana kwa maisha yako.John mwaulaya japkuwa amefariki lakini alikuwa ni mtu hatari sana na mtandao wake pia ni hatari.Umeona kilichomtokea Peniela leo.Amewafanyia Team Sc41mambo mengi lakini hivi sasa wanamsaka kwa udi na uvumba na nyumba yake wameiwasha moto.” Akasema Mathew

“ John mwaulaya amefariki dunia? Akauliza Jason
“ Ndiyo Jason” akajibu Mathew

“ Ouh thank you Lord ! akasema Jason akionekana kufurahia kifo kile cha John lakini Mathew akamgusa na kumfanyia ishara kwamba hatakiwi kufurahia kifo kile cha John mbele ya Peniela.
“Mathew, mimi ndiye ninayepaswa kusema samahani kwa kitendo cha kukukosea heshima kwa maneno niliyoyatamka .Nilikutamkia maneno ambayo sikupaswa kukutamkia mtu kama wewe.Sikujua nini nilikuwa ninakiongea kwani niliongozwa na hisia zangu zaidi kutaka kufanya kitu ambacho sikuwa nakijua undani wake.Samahani sana Mathew naomba tusahau yaliyopita na tushikamane kwa ajili ya Peniela.Kama kuna jambo lolote ambalo unaona ninaweza kusaidia tafadhali usisite kunitaarifu” akasema Jason
“ Ahsante sana Jason.” Akasema Mathew na kuegemea kiti huku akiitumia fulana yake kugandamiza sehemu yenye jeraha kuzuia damu kuendelea kuvuja.
“ Nilichokuwa nataka kukifanya siku ile ni kitu cha kijinga sana.Nashukuru kwa Mathew kunitamkia maneno yale yaliyonifanya nikasirike na nisifanye kile ambacho nilikusudia kukifanya.Nilikuwa najipeleka katika mdomo wa mamba mimi mwenyewe.Hiki kilichomkuta Peniela leo kingeweza hata kunikuta mimi” akawaza Jason.

“ Nadhani ni wakati wa Peniela kuachana na kundi hili analoshirikiana nalo.Si watu wazuri hata kidogo na asipoangalia wanaweza hata kumuua.” Akaendelea kuwaza Jason wakati wakipana kilima na mara walipofika juu ya kilima akastuka baada ya kuuona moto mkubwa ukiwaka kutokea sehemu walikokuwa wanakwenda.
“ Mathew kuna moto mkubwa unawaka maeneo ya kule unakoishi” akasema Jason na kumstua Mathew aliyekuwa amefumba macho akitafakari.

“ ouh my God ! moto ule ni mkubwa sana lazima kuna nyumba nyumba itakuwa inaungua moto” akasema Mathew aliyestuka sana baada ya kuona moto ule

“ Yale ni maeneo ninapoishi kwani ni karibu na ule mnara wa simu.Pale jirani yangu kuna nyumba za wazungu wawili na nyingine za waswahili wenzangu.Ni nyumba ipi itakuwa inawaka moto? Akawaza Mathew

“ Usiku huu tayari nimekwisha ushuhudia moto mkubwa ukiteketeza nyumba ya Peniela na huku tena kuna mto unawaka, tena karibu na eneo ninaloishi.Mbona matukio ya moto yametawala usiku huu? Akajiuliza Mathew

“ Bado taswira ya ule ya moto mkubwa ukiiteketeza nyumba na familia yangu inanijia kila usiku na baada ya kuuona moto ule mkubwa ukiiteketeza nyumba ya Peniela ,umekitonesha tena kidonda changu kilichokwisha anza kupona.Ninajiuliza nini lengo la kuichoma nyumba moto nyumba ya Peniela na kumkosesha makazi? Nitawasaka washenzi hawa wote na kuwashikisha adabu.Huu ni unyama uliopitiliza sana .” Akawaza Mathew huku wakikaribia sana maeneo anakoishi.Miale ya magari ya zimamoto ilionekana na ving’ora vya magari ya polisi yakiendelea kuja kwa kasi eneo lile vikasikika.Kadiri walivyozidi kusogea ndivyo moto ulivyoonekana kuwa mkubwa na mara wakakutana na kizuizi cha askari wakasimamishwa.Kulikuwa na magari ya polisi na mengine yameegeshwa pembeni..Askari mmoja mwenye silaha akawafuata na kuwasalimu na kuwaambia
“ Ndugu njia iimefungwa hakuna mtu anayeruhusiwa kupita mtaa huu.Kuna nyumba inaungua na kwa bahati mbaya ndani ya nyumba hiyo inasadikiwa kulikuwa na milipuko kwani baada ya moto kuanza imetokea milipuko mikubwa minne ambayo tunahisi yanaweza kuwa ni mabomu .Hali hiyo imefanya juhudi za kuuzima moto huo kushindikana kwani hatujui kama ndani ya nyumba hiyo kunaweza kuwa na milipuko zaidi ama vipi.Tunachokifanya kwa sasa ni kujitahidi kuzuia moto ule usiweze kusambaa katika nyumba za jirani na kusababisha maafa zaidi ” akasema Yule askari.Kwa mara ya kwanza Mathew alihisi miguu yake inaisha nguvu baada ya kusikia maneno yale ya askari.

“ Afande kuna mtu yeyote ameokolewa kutoka katika nyumba hiyo inayoungua? Akauliza Jason

“ Kwa mujibu wa watu waliowahi kufika eneo la tukio baada ya moto kuanza wanasema kwamba hawakuwahi kuokoa kitu chochote kile na hawajui kama ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na mtu .Eneo hili ni jipya na bado halina wakazi wengi kwa hiyo wengi walistuka kama kuna moto baada ya mlipuko wa kwanza kutokea na wakati huo tayari moto ulikwisha sambaa nyumba nzima kwa hiyo hakuna walichofanikiwa kuokoa zaidi ya kukimbia kujinusuru” akasema Yule askari na kuondoka
“ Mathew kuna nini? Mbona naona magari ya askari polisi na kule kuna moto mkubwa unawak? Akauliza Peniela kwa wasi wasi baada ya kuzinduka toka kwa wasiwasi

“ Peniela huku ni nyumbani kwangu.Kuna nyumba inaungua mta huu ndiyo maana tumezuiliwa hapa.” akasema Mathew huku sauti yake ikionyesha kitetemeshi ,aliogopa sana
“ Jason kwa maelezo ya Yule askari nina wasi wasi sana yawezekana ni nyumba yangu ndiyo inaungua kwa sababu nimehifadhi mabomu matano ya kutupa kwa mkono mle ndani na kuna silaha nyinginezo ambazo zinaweza kusababisha mlipuko” akasema Mathew huku akiufungua mlango na kutaka kushuka.
“ No Mathew usishuke.Umechafuka damu sana na eneo lote limetapakaa askari wanaweza wakataka kufahamu jeraha hili umelipata wapi.Ngona mimi nishuke nikajaribu kufanya uchunguzi nijue ni nyumba ipi inaungua.” Akasema Jason na kushuka

“ Mathew bado jeraha linavuja damu.Tutafanya nini kuzia damu hii isiendelee kutoka? Akauliza Peniela lakini Mathew hakumjibu kitu alikuwa anatetemeka kwa ndani
“ Mungu asaidie nyumba hiyo inayoteketea isiwe ni ya kwangu.” Akawaza.

“ Kama ni ya kwangu sijui nitafanya nini ” akaendelea kuwaza Mathew na kuchukua simu yake akapiga namba za Anitha na zile za nyumbani kwake lakini hakuna simu iliyopatikana akazidi kuogopa
“ Yawezekana Anitha na jaji Elibariki watakuwa wamekimbia na kujificha mahala baada ya moto huo kutokea katika nyumba ya jirani na yawezekana hii ni sababu iliyomfanya Anitha azime kila kitu hata simu zote.Kama ni hivyo watakuwa wapi? Jaji Elibariki anatafutwa na hatakiwi kuonekana hovyo hadharani.Nahisi watakuwa wamejificha mahala Fulani mbali kidogo na hapa ili kuepuka kuonekana.Halafu kule nyumba ya chini alikuwemo Rosemary lakini yeye simuhofii sana kwani hakuna anayeweza kufahamu kama kule chini kuna nyumba .Hata hivyo natakiwa kufahamu mahala walipojificha Anitha ,jaji Elibariki na Naomi na kama wako salama ama vipi” akawaza Mathew huku akiendelea kuangaza angaza kama angeweza kumuona Antha kutoka katika kundi la watu waliokuwepo eneo lile.
Ghafla Jason akarejea mbio na kuingia ndani ya gari akafunga mkanda na kumtaka Mathew naye afunge mkanda kisha akawasha gari.
“ Jason kuna nini ? Mbona umerudi mbio namna hiyo? Akauliza Mathew kwa wasi wasi huku akiufunga mkanda.Jason hakujbu kitu akawasha gari na kugeuza kisha akaondoka kwa kasi
“ Jason kuna nini? Mbona hivyo? Umeona nini kimekustua? Akauliza tena Mathew lakini jason hakujibu kitu akaongeza mwendo.Alionekana kama kuchanganyikiwa hali iliyozidi kumuogopesha Mathew.
“ Jason mbona hutaki kutueleza umeona nini? Tueleze tafadhali nini umeona kilichokustua? Akauliza Mathew
“ Jason kweli unatuogopesha sana.Tueleze ukweli nini umekiona kimekustua hivyo” Peniela naye akasisitiza lakini bado Jason hakuwa tayari kusema chochote bali aliendesha gari kwa mwendo mkali sana
“ Jason !! akaita Mathew kwa ukali lakini bado Jason hakugeuza hata shingo kumtazama bali aliendelea kuwa makini katika usukani.Uso wake ulionekana kuloa jasho .

“ Jason whats wrong with you?? Akauliza Peniela.

“ Something is not right!! Akawaza Mathew
“ Kuna kitu alichoona Jason na ndiyo maana amestuka na hataki kusema chochote.Akili yangu inanituma niamini kwamba yawezekana ni nyumba yangu ndiyo inateketekea na anaogopa kunieleza ukweli.Please help me God isiwe ni nyumba yangu” Akawaza Mathew na kumgeukia Jason

“ Jason stop the car and tell me the truth.!!! Akasema Mathew kwa ukali
“ Mathew not now “ akasema Jason.
“ Jason simamisha gari na utueleze nini umeona kilichokustua .? Naomba hii iwe ni mara ya mwisho sitaki kukuuliza tena.Kama hutasimamisha nitasimamisha mimi mwenyewe,” Akasema Mathew Kwa ukali.
Jason akaogopa namna Mathew alivyobadilika na kusimamisha gari pembeni ya barabara kisha akavuta pumzi ndefu na kusema

“ Mathew ni nyumba yako ndiyo iliyoungua”
“ Ouh My god !!!....
Haya ndiyo maneno aliyoweza kutamka Mathew huku ameiweka mikono yake kichwani.Mstuko alioupata ulikuwa ni mkubwa sana .
“ Mathew !!.mathew !! akaita Peniela lakini Mathew hakuitika.

“ Mathew ! .akaita tena peniela lakini Mathew hakuitika.bado mikono iliendelea kuwa kichwani.

“ Mungu wangu nini kimemtokea Mathew? Hii ndiyo sababu sikutaka kumueleza pale karibu na eneo la tuo kwani niliogopa lazima angepatw ana mstuko mkubwa na lazima angefanya fujo na angekamatwa na askari wale kwani wangetaka kufahamu milipuko ile iliyotokea ndani ya nyumba yake ameitoa wapi.Mambo yangekuwa magumu sana kwa Mathew “ akawaza Jason na kumgeukia Mathew

“ Mathew are you ok? Akauliza Jason lakini Mathew hakujibu kitu.Jason akawasha taa ya ndani ya gari ili kumtazama Mathew .Michirizi ya machozi ikaonekana machoni pake.Ilikuw ani mara ya kwanza kwa Peniela kumshuhudia Mathew akimwaga machozi. Aliogopa sana

“ Nimekutana na mambo mengi ya hatari nikiwa na Team Sc41 lakini sijawahi kukutana na matukio ya hatari yaliyoniogopesha kama ya usiku wa leo.Ni nani ameichoma nyumba ya Mathew? Ni team SC41? Anitha na jaji Elibariki wako wapi? Wameteketea ndani ya nyumba au wamekimbia ? Rosemary mkozumi je yuko wapi? Kwa sababu nakumbuka Mathew alimchukua na kwenda kumuhifadhi mahala pa siri” Akajiuliza Peniela na kuzidi kuogopa naye pia machozi yakaanza kumtoka.
Iliwachukua zaidi ya robo saa wakiwa pale pembeni ya bara bara na Mathew hakuwa ameongea chochote.Bado mikono ilikua kichwani na michirizi ya machozi ilionekana machoni pake.

“ Mathew !!..akaita Jason lakini Mathew hakujibu kitu.Katika kiti cha nyuma Peniela naye akasikika analia.Jason akashindwa afanye nini .
“ Mathew please talk to me” akasema Jason.Bado Mathew aliendelea kuiweka mikono kichwani na machozi kuendelea kumdondoka.
Baada ya dakika ishirini Mathew akatoa mikono kichwani akafuta machozi na kuingiza mkono mfukoni akachukua simu yake akaitazama halafu akatafuta namba Fulani katika simu yake akapiga,akaiweka simu sikioni kisha akafungua mlango wa gari akashuka.Jason akaogopa sana na kutaka kushuka garini lakini Mathew akamfanyia ishara kwamba asishuke garini.Mathew akaenda umbali wa hatua kadhaa ili aweze kuongea na Yule aliyempigia simu bila ya akina Jason kusikia.
“ Jason kwa nini umemuacha Mathew asuke garini? Akauliza Peniela uso wake ukiwa umejaa machozi
“ Kwa sasa amechanganyikiwa na hajui anachokifanya” akasema Peniela
“ Wait Peniela ! akasema Jason huku akimuangalia Mathew kwa makni.Baada ya kama dakika tano hivi Mathew akarejea garini

“ Twende Jamaica night club” akasema Mathew huku akiufunga mkanda .Jason akawasha gari wakaondoka
“ Are you ok Mathew “ akauliza Peniela
“ Yes ! I’m ok” akajibu Mathew
“ He’s not ok.Nmemfahamu Mathew ndani ya kipindi kifupi sana lakini ni mwanaume jasiri mno na asiyeogopa kitu chochote.Kwa mara ya kwanza nimemuona akidondosha machozi hii inaonyesha ni namna gani alivyoumizwa na hiki kilichotokea usiku huu.He’s badly hurt.Ni nani lakini ambaye amefanya jambo hili? Ni Team SC41 au nani? Akajiuliza Peniela

“ Ni vigumu sana kufahamu ni nani aliyefanya kitendo hiki .Nini kitafuata baada ya hapa? Je mipango yetu yote imefikia mwisho wake? Akaendelea kujiuliza Peniela na machozi mengi yakaendelea kumdondoka

“ Tumepambana sana lakini mambo yamekuja kuharibika mwishoni kabisa.Inaniuma sana.Kwa nini iwe hivi? Akashindwa kujizuia na kuanza kulia kwa kwikwi,Mathew akageuza shingo akamtazama na kusema
“ Usilie Peniela.This isn’t over yet” akasema na kisha akafuta machozi.Peniela hakujibu kitu zaidi ya kuendelea kulia.
Safari iliendelea hadi walipofika Jamaica nigt club.Mathew akamuelekeza Jason sehemu ya kuegesha.Jamaica night club ni mojawapo ya kumbi za burudani inayotoa burudani kwa saa ishirini na nne.Gari zilikuwa zinaingia na kutoka.Walikaa mle garini kwa takribani dakika saba mara ikaja gari moja nyeusi mbele yao na kusimama kisha taa kubwa zikazimwa na kuwashwa haraka haraka mara tatu.Mathew akamgeukia Peniela.
“ Peniela we have to go” akasema na kumshangaza Jason

“ Mathew mnakwenda wapi? Akauliza
“ Jason ahsante sana kwa msaada wako mkubwa.Siwezi kukusahau kwa msaada huu mkubwa ulioutaidia kwa usiku huu wa leo.Muda wowote nikihitaji tena msaada nitakupigia.Tafadhali kuwa muangalifu sana” akasema Mathew na kuufungua mlango wa gari akashuka ,akamfungulia Peniela mlango akashuka ,akamshika mkono akamuongoza hadi katika lile gari lililosimama mbele yao wakaingia na gari likaondoka.Jason akabaki amepigwa na butwaa.

“ wanakwenda wapi? Gari ile iliyokuj akuwachukua ni ya nani? Akajiuliza Jason bila kupata jibu




MATHEW NA PENIELA WAMEKWEND WAPI?
 
naona story inaanza upya tena bado mbichi sana mapambano yanaanza upyaa maana wamerudishwa kwenye 0.na mda ndio huo wajipange ne kuzuia dili la package.

ni ngumu sana hii story kuitabili kuwa sehem ijayo itakuwa hivi au vile
 
PENIELA SEASON 3

SEHEMU YA 30

MTUNZI😛ATRICK.CK


ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Safari iliendelea hadi walipofika Jamaica nigt club.Mathew akamuelekeza Jason sehemu ya kuegesha.Jamaica night club ni mojawapo ya kumbi za burudani inayotoa burudani kwa saa ishirini na nne.Gari zilikuwa zinaingia na kutoka.Walikaa mle garini kwa takribani dakika saba mara ikaja gari moja nyeusi mbele yao na kusimama kisha taa kubwa zikazimwa na kuwashwa haraka haraka mara tatu.Mathew akamgeukia Peniela.

“ Peniela we have to go” akasema na kumshangaza Jason
“ Mathew mnakwenda wapi? Akauliza
“ Jason ahsante sana kwa msaada wako mkubwa.Siwezi kukusahau kwa msaada huu mkubwa ulioutaidia kwa usiku huu wa leo.Muda wowote nikihitaji tena msaada nitakupigia.Tafadhali kuwa muangalifu sana” akasema Mathew na kuufungua mlango wa gari akashuka ,akamfungulia Peniela mlango akashuka ,akamshika mkono akamuongoza hadi katika lile gari lililosimama mbele yao wakaingia na gari likaondoka.Jason akabaki amepigwa na butwaa.

“ wanakwenda wapi? Gari ile iliyokuj akuwachukua ni ya nani? Akajiuliza Jason bila kupata jibu



ENDELEA………………………………..



“ Karibu tena nyumbani madam.” Mmoja wa walinzi wa Rosemary Mkozumi akamwambia Rose huku akimfungulia mlango.Rose akasaidiwa na walinzi wake kushuka ndani ya gari na kuingia sebuleni akakalishwa katika sofa.

“ Ahsanteni sana vijana.Mmefanya kazi nzuri usiku waleo.” Akasema Rose

“ madam kwa niaba ya wenzangu wote ninaomba samahani sana kwa tukio lile lililotokea.Sisi hatukujua kama watu wale walioongozana na Henry ni watu wabaya namna hii.” Akasema Yule mlinzi.

“ Fernando haya mambo si wakati wake sasa,nitakuwa na maongezi na ninyi.Hebu nieleze kuna habari gani hapa nyumbani katika muda wote ambao sikuwepo?

“ Baada ya wewe kuchukuliwa katika lile gari la wagonjwa ,tulipigiwa simu na watu wakatuarifu kwamba kuna mwili wa Henry mle ofisini kwako tuliwasiliana na polisi ambao walifika hapa wakafanya uchunguzi wao wakavunja mlango na kuondoka na mwili wa Henry.Hiyo ndiyo habari kubwa iliyopo.Zaidi ya hiyo hakuna tena habari nyingine yoyote” akasema Fernando.
“ Ok safi sana.Imarisheni ulinzi na kuanzia sasa mtu yeyote asiingie humu ndani bila ruhusa yangu na yeyote atakayeingia humu hata kama ameruhusiwa lazima apekuliwe ili kujua kama hana silaha ya aina yoyote ile.Nitaongea zaidi na ninyi kesho “ akasema Rose

“ lakini madam ni nani aliyefanya ukatili huu ? Huyu aliyefanya hivi anatakiwa asakwe hadi apatikane na afundishwe adabu “Akauliza Fernando.
“ usijali Fernando.Atasakwa na atapatikana tu.kwa sasa wale wote watu tuliowachukua kule wafungieni kila mmoja katika chumba chake.Nitakuwa na maongezi nao nao mmoja mmoja asubuhi.Kwa sasa naombeni mnipeleke chumbani kwangu” akasema Rose na walinzi wake wakambeba hadi chumbani kwake.
“ Ok ahsanteni sana vijana.Naombeni mniache sasa ninahitaji kuwa mwenyewe.”akasema Rose na walinzi wake wakaondoka wakamuacha mwenyewe.Akampigia simu mfanyakazi wake wa ndani akamuomba amtengenezee supu kwani hakuwa ameweka chochote tumboni.Alihisi maumivu makali sana kila sehemu ya mwili wake.Mlango ukagongwa akaingia Dr Imelda daktari binafsi wa Rosemary .

“ madam pole sana kwa mkasa huu.Nani kakufanya hivi? Imelda akashangaa

“ Imelda nashukuru sana umefika kwa wakati.Hali yangu ni kama unavyoniona.Si nzuri hata kidopo”akasema Rose.Dr Imelda akamchunguza Rose majeraha yake halafu akasema
“ Inabidi kabla ya kuanza kutibu nikusafishe kwanza majeraha yote ili tujue ukubwa wake.Can you walk?akauliza Imelda.Rose akasimama na kuuma meno kwa maumivu aliyokuwa akiyasikia.Imelda akamsaidia akamuingiza bafuni na kumuogesha kwani hakuwa akitazamika kwa damu iliyomtapakaa kila mahala.Baada ya kuhakikisha amekuwa safi akamrudisha chumbani na kumlaza kitandani akaanza kumtibu majeraha akianzia na yale makubwa ya miguuni ya kukatwa vidole.
“ Ni katili gani ambaye alifanya hivi madam? Mtu huyu aliyefanya hivi hana roho ya ubinadamu hata chembe. Lengo lake lilikuwa ni kukuua” akasema Dr Imelda wakati akitibu majeraha ya miguuni.
“ Imelda katika hii dunia tunaishi na maadui wengi sana na waliofanya hivi ni watu wenye visasi na mimi na lengo lao ni kuniua.” Akasema Rosemary.

“ Inasikitisha sana kwa ukatili huu kufanyiwa mtu mkubwa kama wewe.Yeyote aliyefanya hivi anatakiwa kuozea gerezani.Alichokufanyia kinatisha sana” akasema Imelda na machozi yakaonekana machoni kwa Rosemary

“ They will all pay..!!..They must pay ! ..akasema Rose.
Dr Imelda akaendelea kumganga Rose majeraha yake na wakati wanaendelea simu ya Rose ikaita matibabu yakasimama kidogo ili aweze kuongea na simu ile kwani alisema ni ya muhimu sana

“ hallow Rose”ikasema sauti ya upande wa pili baada ya Rose kupokea simu

“ Hallow Vincent !!!
“Rose ninataka kuripoti ukosefu wa adabu wanaonifanyia hawa walinzi wako.Dont they know who I am? Akauliza Vincent
“I’m sorry Vincent.Ni mimi ndiye niliyewapa maagizo ya kuhakikisha kwamba kila mtu anayeingia hapa anapekuliwa ili kuhakikisha hana silaha yoyote.I don’t trust anyone right now.Nipe kiongozi wao niongee naye” akasema Rose na baada ya sekunde kadhaa akasikia sauti ya Fernando
“ hallow Madam”
“ Fernando mruhusuni Vincent apite moja kwa moja”akasema Rose na kukata simu na matibabu yakaendelea.
Baada ya dakika kumi mlango ukagongwa Dr Imelda akaenda kuangalia ni nani aliyekuwa anagonga akakutana na Vincent akamueleza aketi sofani katika sebule ya Rose asubiri hadi amalize kazi aliyokuwa anaifanya.
Baada ya saa nzima Dr Imelda akamaliza kumtibu Rose majeraha yake halafu akamchoma sindano na kutoka mle chumbani ili kumpa nafasi Rose ya kuongea na mgeni wake.Vincent akastuka sana baada ya kumuona Rose akiwa na majeraha
“ Ouh my God ! who did this to you Rose? Vincent akashangaa

“ I have so many enemies Vincent” akasema Rose
“ Pole sana Rose.Whoever did this to you,must be pay.Umekwisha mfahamu ni nani aliyefanya unyama huu?akauliza Vincent
“ Tayari nimewajua walionifanya hivi na hata aliyewatuma wanifanyie hivi” akasema Rose.
“ Good.Its pay back time..”akasema Vincent kwa hasira
“ Not so fast Vincent.Wameuwasha moto wenyewe sasa watakosa maji ya kuuzimia.Nitapambana nao taratibu na kuwafyeka mmoja baada ya mwingine. Kwa bahati mbaya waliotumwa wanifanyie hivi hawakutaarifiwa kwamba Rosemary ni nani na sasa watakwenda kunifahamu mimi ni nani.Ninakuhakikishia Vincent yeyote ambaye ana mkono wakekatika jambo hili lazima atalipa.Hakuna atakayesalimika hata kama ni nani.Tuachane na hayo nimekuita hapa kwanza kukujulisha kwamba nimerejea nyumbani ingawa nimechakazwa kila sehemu ya mwili wangu.Nilivamiwa na kutekwa na watu ambao walimuua pia Henry.Watu hao wamenitesa sana kama hivi unavyoona.”
“ Dah ! pole sana Rose.” Akasema Vincent kw masikitiko

“ Ahsante Vicent.” Akasema Rose na kugugumia kwa maumivu kisha akasema

“Jambo la pili ninalotaka ulifahamu wewe kama mshirika wangu ni kwamba kuanzia sasa tuko vitani.Watu hawa walioniteka tayari wanafahamu mambo mengi sana kuhusu mimi na hata wale ambao ninashirikiana nao...”akasema Rosemary na kumfanya Vincent astuke

“ They know ?!! akauliza

“ Ndiyo Vincent.wanafahamu kila kitu kuhusu mimi,wamepekua kompyuta yangu,simu zangu,wamefahamu mambo mengi sana kwa hiyo nimekuita ili kukupa taarifa hizi ili unisaidie kupambana na watu hawa.” akasema Rose.
“ Ni nani hawa watu? Nani kawatuma? Halafu tukio hili lilitokeaje? Akauliza Vincent
“Henry alikuja na watu hao na sifahamu alitoka nao wapi .Kuna kitu nilisahau hivyo nikarejea mara moja ndipo nilipotaarifiwa kwamba Henry amekuja na wageni.Moja kwa moja nikaja mpaka ofisini ili niwafahamu wageni hao ni akina nani na mara tu nilipoingia ofisini Henry akaruka ili anipe taarifa kwamba nisingiie mle ofisini lakini watu wale wakamuwahi na kumpiga risasi akafariki pale pale.Ouh masikini Henry wamemuua mpenzi wangu jamani !!..Rose akasema kwa uchungu mkubwa na kushindwa kuyazuia machozi kumtoka.

“ Pole sana Rose.”akasema Vincent.Rose akafuta machozi na kuendelea.

“ Watu wale sifahamu walitoka wapi na Henry lakini ninachoweza kusema kwamba walimtumia Henry ili kuingia hapa ndani. Ninamfahamu Henry vizuri kwa namna yoyote ili asingeweza kuwaleta hapa kwangu watu ambao anajua ni hatari .Watu wale hadi wakamtumia Henry ni watu ambao tayari wamenifahamu kwa undani na wanajua kila kitu kuhusu mimi na yeye.Wamepekua kila mahala wamechukua kila taarifa waliyokuwa wanaitaka na huko walikonipeleka wamenitesa sana ili niwaeleze baadhi ya mambo “ akasema Rose

“ Dah pole sana Rose.” Akasema Vincent

“ Ahsante sana Vincent.Lakini nimegundua aliyewatuma watu hawa lazima atakuwa ni mmoja wa washindani wangu wa kisiasa na hili ni jaribio lao la kutaka kuizima ndoto yangu ya kugombea urais lakini nakuhakikishia kwamba hawataweza.Nitagombea urais na nitashinda tu”akasema Rose
“ Nakubaliana nawe Rose unapoingia katika siasa na hasa katika jambo kubwa kama kugombea urais lazima utapata maadui wengi na vikwazo vingi.Lakini ni nani basi ambaye unahisi ameianzisha vita hii ? akauliza Vincent

“ Ni Deus “ akasema Rose na kumstua sana Vincent
“ Deus ? akauliza Vinmcnet

“ Ndiyo ni Deus.My x husband”

“ Are you sure Rose? Akauliza Vincent
“ Ndiyo nina hakika kabisa ni yeye.Toka tulipoachana amekuwa ni adui yangu mkubwa na aliposikia kwamba nina nia ya kuwani aurais amekuwa ni mpinzani wangu mkubwa .Nina hakika kabisa kwamba ni yeye ndiye aliyewatuma vijana wale wanifanyie hivi.Lakini ninakuhakikishia Vincent kwamba simuogopi Deus na nitamuonyesha kwamba mimi ni nani.Safari hii ataifahamu nguvu yangu” akasema Rose.Vincent akamtazama Rose na kusema.
“ Rose kuna kitu ninataka kukuuliza.Una hakika gani kwamba ni Dues ndiye aliyewatuma watu hao kwako ?

“ Nina uhakika huo Vincent.Vijana wale walipokuwa wananitesa walitaka kufahamu kuhusu Hasheem Abullah.Ni Deus pekee ambaye anafahamu kuhusu mimi na Hasheem na hii ilikuwa ni sababu kubwa ya mimi na Deus kutengana. Nina hakika aliyewapa taarifa hizo zote ni Deus.Jambo hili ni la ndani sana na wasingeweza kulifahamu kama si kuambiwa na Deus.Kwa hiyo safari hii I swear nitamuonyesha mimi ni nani ” Akasema Rose.
“ Rose kabla hujafanya lolote nataka uwe na uhakika kama ni kweli Deus ndiye aliyekuwa nyuma ya hao watu,kama huna hakika na suala hilo naomba usifanye hilo tafadhali. “ akasema Vincent
“ Vincent nina uhakika mkubwa sana kwamba hakuna mtu mwingine anayeweza kunifanyia hivi zaidi yake.Deus hataki kuniona nyota yangu iking’aa kisiasa na ndiyo maana anafanya kila awezalo kuhakikisha kwamba mambo yangu hayafanikiwi na lengo la kuwatumia vijana wale ni ili kuweza kunivurugia mipango yangu wa kuwania urais kwani anajua kabisa kwamba nina watu wengi wanaoniunga mkono na kwamba lazima nitashinda tu na kuwa rais wa kwanza mwanamke Tanzania.Nimeishi na Deus na ninamfahamu vizuri sana kuliko mtu mwingine yeyote Yule.He’s a monster” Akasema Rose.Vincent akajiweka vizuri na kusema
“ Rose kuna mambo kadhaa ambayo ninataka uyafahamu kabla hujafanya hichounachotaka kukifanya.Kwanza kabisa…” akasema Vincent na simu ya Rose ikaita ikambidi asubiri hadi Rose alipomaliza kuongea akaendelea.

“ Kwanza kabisa ninataka ufahamu for years now I’ve been working with Deus.Mimi nay eye ni washirika wakubwa .”

“ What ?!..Rosemary akashangaa

“ Ina maana kwa muda huu wote umekuwa ukishirikiana na Deus bila ya kunitaarifu? You traitor !!“ akasema Rose kwa ukali
“ Rose tafadhali usihamaki.Nisikilize vizuri.Nimeamua kukueleza jambo hili kwa sababu sitaki ukurupuke katika maamuzi yako na uje kujutia baadae.NInataka kukusaidia kumfahamu muhusika halisi aliyefanya jambo hili.Mimi na Deus tumekuwa marafiki na washirika wakubwa kwa muda mrefu.Tuna kikundi cha watu wachache mabilionea wakubwa ambao tunakifadhili chama anachokiongoza Deus na nyakati ningine tunafanya hata maamuzi makubwa yanayohusu nchi.Hiki ni kikundi cha watu wenye nguvu ya kufanya jambo lolote katika nchi.It’s us who decides who is going to be the next president” akasema Vincent na kumfanya Rose azidi kumtumbulia macho
“ Nimekueleza haya yote ili kukupa picha kwamba katika vikao vyetu vya maamuzi hata siku moja hatujawahi kukuzungumzia wewe na hata siku moja sijawahi kumsikia Deus akikuzugumzia.Katika watu ambao wanazungumzwa kuwa na nguvu kubwa kisiasa na katika uchaguzi ujao wewe haumo hata kati ya tano bora kwa hiyo nina hakika kabisa kwamba Deus siye aliyewatuma hao watu wakufanyie hivyo kwa sababu hana shida na wewe . There is must be someone else behind this and not Deus. We have to find him” akasema Vincent.

“ Vincent umenisikitisha sana.Kumbe siku hizi zote umekuwa ni mtu wangu wa karibu unayeniunga mkono na kunisapoti katika mambo mengi kumbe umekuwa pia na ushirika na Deus? Umenisaliti Vincent na sitaki kabisa kukuona tena hapa kwangu.You traitor !! akasema kwa ukali Rosemary
“ Rosemary Calm down my dear.Nimeamua kukueleza ukweli ili kukusaidia kumtafuta mtu sahihi aliyekufanyia haya na si Deus. Yule ni mtu mkubwa sana na hana mpango wowote na wewe na usijaribu kabisa kucheza naye.Hata sisi pamoja na uwezo wetu mkubwa kifedha lakini tunamuogopa na tunatii kila atakachotuambia.Japokuwa amestaafu lakini bado ni mtu mwenye nguvu sana hapa nchini” Akasema Vincent.Rose alimuangalia Vincent kwa hasira kali
“ Vincent mimi na wewe tulikuwa marafiki wakubwa nilikuamini kwamba ni mtu ambaye ninaweza kukutegemea katika jambo lolote na hata kukupa siri zangu.Na hata usiku huu wewe ndiye uliyekuwa mtu wa kwanza kukupigia simu na kukufahamisha kwamba niko salama lakini sikujua kama una ushirika na Deus ambaye ni adui yangu mkubwa.Kwa kushirikiana na adui yangu ninakuweka nawe vile vile katika kundi la maadui zangu. From now on you are my enemy !!! akasema Rose.Vincent akacheka kidogo

“ Listen to me carefull woman.Dont you ever try to do anything to Deus.Atakumaliza ndani ya sekunde moja kama mbu anavyouliwa kwa kofi moja.Kwa Deus wewe bado ni mtu mdogo sana na anaweza akakufanya chochote muda wowote.There is one more thing I want to tell you.Mtu uliyemtegemea Captain Amos amefariki..!!..Taarifa ile ilimuingia Rosemary Mkozumi moyoni kama vile kitu chenye ncha kali na kwa dakika mbili hakuweza kusema chochote
“Ulimtegemea sana Amos katika mambo mengi lakini hukujua kwamba mtu ambaye ulimuamini kama mshirika wako alikuwa ni moja wa vijana wa Deus.Rose umewekwa kiganjani na Deus na kama angekuwa na shida ya kukudhuru wala asingewatumia hao vijana,angewatumia watu wako waliokuzunguka na wangekumaliza sekunde moja.Endapo utakayothubutu kujaribu kufanya chochote kwa Deus kama unavyofikiria nakuapia atakufinyanga kama udongo so don’t try him” akasema Vincent
“ Vincent please go away !! I’m surrounded by traitors !! Go away !! Akasema Rose huku akibubujikwa na machozi.

“ Rose you called me here because you need my help..Right now I’m the only friend you can count on” akasema Vincent
“ Go away Vincent .I’ll fight this war alone”
“ Rose huwezi kushinda vita hii.Let me help you to find who did this to you” akasema Vincent.Rose akamuangalia kwa jicho la chuki kisha akauliza
“ Who killed Amos and why? Akauliza Rose

“ Siwezi kukutajia ni nani aliyemuua lakini ninaweza kukwambia ni kwa nini aliuawa.Alikuwa tayari kuvujisha siri ambayo hakutakiwa kuitoa” akasema Vincent

“ Ouh Amos nitakulilia kilio gani mimi jamani..!!..akasema Rose huku akimwaga machozi
“ Rose ninadhani sintakuwa na jambo lingile la kuzungumza nawe kwa usiku huu. Endelea kupumzika na tafadhali zingatia hayo niliyokueleza.Dont start war with Deus.Nitakutembelea tena kujua hali yako” akasema Vincent

“ Vincent don’t show your face here again you monster !! akasema Rose kwa ukali .Vincent akaufungua mlango akatoka .

“ Aaaagggghhhh.!!!!! Akalia kwa uchungu Rose na mara Dr Imelda akaingia na kumchoma sindano ya usingizi ili aweze kulala





TUKUTANE SEHEMU IJAYO………
 
Mbona stori inaharibika yaani naye Mathew kafanya Yale Yale ya Elibarik kwa Penuel? Kah! Nimesikitika sana naye Penuel anatamaa sana si mwanamke wa kumuweka ndani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…