PENIELA SEASON 3
SEHEMU YA 27
MTUNZI 😛ATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ hallow Peniela” akasema Josh
“ Josh,is everything ok? Akauliza Peniela
“ Peniela you are being followed “ akasema Josh
“ Followed by whom? Peniela akashangaa
“ Ulionekana kupitia kamera zilizofungwa nyumbani kwako ukiingia kwako usiku huu ukiwa umeongozana na Mathew na hivyo wakatuma watu kuja kukuchunguza ulikuwa wapi na unafanya nini.Wako nyuma yako wanakufuatilia.Kuwa makini sana” akasema Josh
“ Ouh my gosh !! akasema Peniela
“ Peniela kuna nini?
“ Team SC41 wanatufuatilia” akasema Peniela.Nikweli kupitia kioo cha pembeni Mathew akagundua kwamba kuna gari lilikuwa linawafuatilia .
“ Hata mimi nilihisi kuna gari linatufuatilia toka tulipoondoka nyumbani kwako.Get ready.We must do something…” akasema Mathew na kuongeza mwendo wa gari.
ENDELEA…………………………….
“ Wewe na Amos mlikuwa ni watu muhimu na mnaotegemewa sana na Team Sc41 katika zoezio zima la kuipata package na baada ya Amos kuuawa ,umebaki peke yako .Uliondoka bila kuwaaga na hawajui umeelekea wapi .Tayari team SC41 wamekwisha anza kuwa na wasiwasi na wewe na ndiyo maana wanakufuatilia ili wazifahamu nyendo zako.Tayari wamehisi kuna kitu hakiko sawa ” Akasema Mathew
“ kwa hiyo tutafanya nini Mathew? Hata mimi nina wasiwasi kwamba tayari wamekwisha gundua kwamba nina shirikianananyi kwani Dr Martin aliwaambia wale madaktari waliotoka Marekani kwamba haliya John ilibadilika baada ya wewe kumtolea vitisho.Walitaka sana kukufahamu na wakamuhoji Josh maswalimengi kama anakufahamu lakini alikana kukujua na akasema kwamba mimi ndiye ninayekufahamu kwa hiyowalikuwa wanatafuta nafasi ya kunihoji.Nilipoondoka kule hospitali bila kuaga kumewapa maswali mengi na kuwafanya waamini kwamba ni kweli kuna watu ninashirikiana nao.Mathew watu hawa ni hataisana na tusipojitahidi wanaweza wakatuua.” Akasema Peniela kwa wasi wasi huku akilitazama gari lile lililokuwa linawafuata nyuma yao.
“ Siku zote usihofu unapokuwa karibu na mimi” akasema Mathew na kufungua droo ya gari kulikuwa na bastora nne.Peniela akachukua mbili na kumpatia Mathew mbili.
“ Utafuata kile nitakachokuelekeza sawa? Akasema Mathew
“ Sawa Mathew.” Akajibu Peniela lakini kabla hawajafanya lolote zikatokea gari mbili mbele yao ambazo zilikuwa zinakuja kwa kasi huku zikiwasha taa zote kubwa na kumfanya Mathew apate ugumu kuona mbele
“ Damn it !!..akasema Mathew na kufunga breki za ghafla ,akageuza shingo ili aweze kulitazama gari lile lililokuwa linawafuatilia nyuma,lilikuwa karibu sana.Pembeni ya bara bara kulikuwa na vibanda vitatu ambavyo vilionekana ni kama vya wafanya biashara ndogo ndogo.
“ Peniela nahisi hizi gari mbili zinazokuja mbele yetu ni za kwao pia.Hatuwezi kuendelea mbele wametudhibiti kila kona.Shuka garini nenda kajifiche katika kibanda kimoja wapo kuna kitu ninataka kufanya.” Akasema Mathew na bila kupoteza hata sekunde Peniela akafungua mlango na kukimbia hadi katika kibanda kimoja wapo akajificha.Mathew akaliona tofali pale karibu yake akafungua mlango na kulichukua tofali kisha akaiganzamiza pedeli ya mafuta kwa kutulia tofali lile na yeye akaruka nje.Gari ilifyatuka kwa mwendo mkali sana nazile gari mbilizilizokuwa zinakuja mbele yao zikasimama na haraka haraka milango ikafunguliwa watu wakashuka na mara ikaanza kusikika milio ya risasi ,wale jamaa walianza kulimiminia risasi gari la Mathew wakiamini kuna mtu ndani na ghafla kikasikika kishindo cha magari kugongana.Garila Mathew liligonga mojawapo ya zile gari mbili.
.Mathew alitoka mtaroni alikoangukia mara aliporuka garini na kuelekea nyuma ya kibanda alichokuwa amejibanza Peniela.Baada ya kishindo kile wale jamaa wakalizunguka gari la Mathew an kuchungulia ndani lakini hakukuwa na mtu yeyote.Lile gari lililokuwa likiwafuata nyuma akinamathew likasimamana wakashuka watu wanne na kuanza kukimbia kuelekea mahala walipokuwa wenzao.walijadiliana kwa sekunde kadhaa kisha wakaanza kuwatafuta akina Mathew.
“ Hawako mbali na hapa.lazima watakuwa maeneo ya karibu i”akasema mmoja wao
“Wanatutafuta.Tunatakiwa tuwastukize “akasema Mathew na kisha akainuakichwa na kuchungulia nakwa kasi ya ajabu wote wawili wakasimama na kuanza kuwachafua wale jamaa kwa risasi.lilikuwa ni shambulio ambalo hawakulitarajia ,watu wanne wakaanguka chini .
“ Tayari wamekwisha tuona tulipokaa,let us get out of here”akasema Mathew na kabla
na hawajaondoka akapigwa risasi akaanguka chini
“ Aaaaaghhhhh !!!..akatoa mguno na kuanguka chini,
“ Mathew ! Mathew !..akaita Peniela huku akimtingisha Mathew aliyekuwa akigala gala kwa maumivu .
“ Nyuma yako Penny!!!.” Mathew akapaaza sauti.Penny akageuka na kumuona mtu mmoja akiwa amesimama nyuma yao akiwa amewaelekezea bastora.
Kwa kasi ya aina yake ambayo Mathew hakuitarajia Peniela akanyakua bastora yake na kumchakaza Yule jamaa kwa risasi akaanguka chini.Mivumo ya risasi ikaanza kusikika kuelekea kule mahala waliko.Mathew akainuka na kuegemea kibanda ,Peniela akamsaidia kuinuka wakaenda kujificha nyuma ya kizimbacha kuusanyia taka taka.
“ Mathew are you hurt? Akauliza Peniela
“ I’m ok Peniela.Risasi haijagusa mfupa imepita kwenye nyama” akasema Mathew na mara gari tatu nyingine zikawasili
"wanaongezeka.Bastora yangu imebakiza riasi chache sana” akasema Mathew
“ Me too.. I’m empty” akasema Peniela
“ we have to get out of here.Tusipo harakisha kutoka eneo hili wanaweza wakatuua hawa jamaa.Risasi tulizo nazo hazitoshi kupambana nao.Tuitumie nafasi hii ambayo wanajipanga tuondoke eneo hili” akasema Mathew kisha akachungulia na kwa msaada wa taa ya gari akaweza kuwaona watu zaidi ya sita wakiwa wamesimama wakijadiliana jambo
“ Mathew jereha lako linatoa damu nyingi,kutoka hapa hadi nyumbani kwangu hakuna umbali mrefu.Turejee nyumbani tukatibu jeraha hilo na kuchukua silaha .Ninazo silaha pale ndani”akashauri Peniela.Mathew akamtazama na kusema
“ Tutambae chini ya mtaro tutokee upande wa pili hahafu tupotee kabisa eneo hili.Tangulia.I’ll cover you” akasema Peniela akaanza kutambaa taratibu na kuingia mtaroni Mathew naye akafuata.Bado wale jamaa walikuwa wamesimama wakijadiliana jambo yawezekana hawakuwa wametegemea kupata upinzani mkali kiasi kile.
Mathew na Peniela wakatambaa katika mtaro ule wa maji machafu yaliyokuwa na harufu kali na kutokea upande wa pili wa bara bara kisha wakaambaa ambaa na mtaro hadi usawa wa nyumba moja kubwa nyeupe .Wakatoka mtaroni na kupita katika uchochoro uliokuwa pembeni ya nyumba ile kisha wakaanza kukimbia na kutokea katika mtaa wa pili .
“ Mathew unavuja damu sana.” Akasema Peniela.
“UsijaliPeniela.” akasema Mathew wakaendelea kutembea kwa kasi kubwa.Ni sauti za mbwa ndizo zilisikika.Ghafla Peniela akasimama baada ya kuona miale mikubwa ya moto katika mtaa unaofuata iliko nyumba yake.
“ Mathew kuna moto mkubwa unaonekana mtaa wa pili”akasema peniela.
“ Yawezekana kuna nyumba inaungua”akasema Mathew kisha wakapita katika nyumba moja yenye maduka manne na kutokea katika mtaa iliko nyumbaya Peniela.Taratibu Peniela akaishiwa nguvu na kuanguka chini.Nyumba ya Peniela ilikuwa inawaka moto
“ Peniela ! peniela ! akaita Mathew…
******
Jaji Elibariki alikaa kitandani na kuinamisha kichwa halafu akasimama akaenda dirishani akachungulia nje.Kulikuwa kimya kabisa.Akarudi kukaa kitandani
“ Lazima nikubaliane na ukweli kwamba maisha yangu tayari yame haribika .Sifahamu ni lini nitatoka humu ndani na hata kama nikitoka sijui hatima yangu ni nini kwani tayari jina langu limekwisha chafuka na ninasakwa kila kona ya nchi hii kwakosa la kusababisha mauaji .Mathew anajitahidi sana kuhakikisha suala hili linafika mwisho lakini kila anapopiga hatua fulani jambo lingine linaibuka.”akawaza na akainuka tena na kusimama dirishani.
“ maisha yangu yameharibika .Nimempoteza mke wangu,nimepoteza kazi,nimepoteza kila kitu.Sina tena muelekeo katika maisha yangu .Kinachoniumiza zaidi ni kitendo cha kukutwa na Naomi .Sijui ni shetani gani alinipitia na nikajisahau kabisa hadinikakutwa na akinaMathew.Heshima yangu imeshuka mbele ya Peniela kwa sababu ya huyu kahaba Naomi.Ninampenda sana penela na tayari nilikuwa na mipango naye mingi tu baada ya mambo haya kumalizika lakini sina hakika tena kama kuna kitu kitakachoendelea tena kati yetu baada ya tukio la leo.Nimejidhalilisha sana kwa watu walioniheshimu na kunithamini ,walioyatoa maisha yao kunisaidia.Hakuna namna ninayoweza kuwaeleza na wakanielewa kwamba haikuwa ridhaa yangu mimi kufanya vile na kujishushai heshima kiasi hiki. “akaendelea kuwaza jaji Elibariki.
“ Mathew alisema kwamba Deus Mkozumi alikuwa na mpango mkubwa juu yangu na hakunieleza kwa kina ni mpango gani huo ila alisema kwamba ni mpango wa kutufanya mimi na Peniela wenye nguvu.Mpango huu utawezekanaje wakati ninaishi kama mfungwa.Natamani sana kuufahamu mpango huo , anaMathew ameonekana kama vile hataki kunieleza na kwa kuw ampangohuo unatuhusu mimi na peniela sidhani kama mpangohuo utawezekana tena kwani Peniela amekwisha vunja rasmi mahusiano yangu na yeye.Natakiwa kuonana na Deus mkozumi mimi mwenyewe ili aniambie ana mpango gani kuhusu mimi.Natakiwa kutafuta namna ya kutokahumu ndani ili ili niweze kunana na Deus nijue ana mipango gani juu yangu. “ akawaza Elibariki
“ Ninahitaji kumpata mtu ambaye atanisaidia kutoka hapa nilipo ,niweze kusafisha jna langu na mwisho maisha yangu yaweze kurejea kama awali.Ni nani ambaye anaweza akanisaidia katika jambo hili? Akaendelea kujiuliza na kushindwa kupata jibu akaenda kukaa kitandani
“ Nisipofanya bidii nitakwama hapa nilipo na maisha yangu yatahamia ndani ya nyumba hii.Dr Joshua na wenzake wamenitengenezea kesi mbaya sana ya kusababisha kifo cha Flaviana na kwa vyovyote vile endapo nitakamatwa hata kama sina hatia nilazima nitasota gerezani kwa kipindi kirefu kwani watu wanaonitafuta niwatu wenye nguvu sana na watatengeneza kila aina ya ushahidi mpaka wahakikshe nimekutw ana hatia na kufungwa.. Lazima nikiri kwamba hapa sina ujanja tena kwani siwezi kuepuka kukaa gerezani .Jaji wa mahakama kuu na mwenye heshima kubwa sana nchini,nitatuhumiwa na kesi ya kumuua mke wangu tena mtotowa rais.Dah ! balaa gani hili” akaendelea kuwazua jaji Elibariki
“ Naona akili yangu imefikia mwisho wake wa kufanya kazi na sioni msaada wowote tena ambao unaweza ukanitoa hapa nilipo na kunirudisha katika maisha yangu ya kawaida.Najuta ni kwa nini nilijiingiza katika mambo haya.Awali nilikuwa na maisha mazuri tu na kama nisingejingiza katika masuala haya basi nisingefika hapa nilipofika sasa hivi.Lakini haya yote yamesababishwa na Peniela.Nilitaka nimtafute muuaji wa Edson ili nimuonyesha peniela ni namna gani ninamjali na ili niweze kulisafisha jina lake katika jamii.Nilimpenda Peniela na ndiyo maana nikajitolea kufanya haya yote kwa ajili yake lakini mambo yamebadilika.Peniela nimemkosa na jina langu limechafuka na sijui nitumie njia gani kulisafisha tena.Najuta sana kujiingiza katika mapaambanohaya na watu wenye nguvu..” akatoka mle chumbani na kuelekea jikoni katika kabati ambalo huhifadhiwa chupa za pombe akafungua na kuchukua moja.wakati anatoka mle chumbani akakutana na Anitha
“ Elibariki hujalaa bado? Akauliza Anitha
” Hapana Anitha ,nimekosa usingizi kabisa .Nataka nipate mvino kidogo labda ninaweza kupata usingizi” akasema jaji Elibariki na kuelekea chumbani kwake akaanza kunywa pombe ile kali
“ Kuna wazo limenijia ,kwa nini nisitafute muafaka na rais? Akasimama na kutabasamu
“ Hili ni wazo zuri sana.Hakuna ubaya wowote kama nikijishusha na kuomba msamaha kwa rais na mambo haya yakaisha.Bila ya kufanya hivyo katu hakutakuwa na muafaka wowote ule.kwa kuwa yeye ndiye aliyeviagiza vyombo vya usalama vinisake kila kona ya nchi anaweza akaviamuru viachane na msako huo ,kesiyangu ikafutwa na jinalangu likasafishwa.Nitarejea kazini na maisha yangu yataendelea kuwa ya kawaida kama zaman japokuwa nitakuwa na maumivu ya kumpoteza mke wangu Flaviana na peniela pia.” Uso wa jaji Elibariki ukapambwa na tabasamu baada ya kupata wazo lile.Akachukua chupa ya mvinyo akanywa kidogo
“ hakuna ujanja mwingine , lazima nionane na Dr Joshua nimuombe msamaha ili mambo haya yamalizike.Natumai endapo nikimuangukia na kumuomba msamaha atanielewa na anaweza akanisamehe na mambo haya yatakwisha.Lakini endapo nikionana na Dr Joshua ina maana lazima niwasaliti wenzangu kwa kuianika mipango yao yote wanayoipanga kwa Dr Joshua ili aweze kuniamini . Huu ni usaliti mkubwa sana lakini nitafanya nini? Sina namna nyingine ya kufanya.” Akaendelea kuwaza.
“ Elibariki na wenzake wamenifanyia mambo mengi makubwa hadi hapa tulipofika na kuwasaliti itakuwa ni dhambi mbaya sana.lakini nitaendelea kukaa humu ndani hadi lini? Nitaendelea kujificha hadi lini wakati sina kosa? Nitakubali maisha yangu yaharibike na niendelee kuwa mkimbizi hadi lini? Elibariki akachukua mvinyo akanywa na kuendelea kutafakari
“ Hapana siwezi kukubali maisha yangu yaharibike kiasi hiki.I must do something to save myself.Hakuna ambaye atanisaidia kunikwamua ..Mathew ana mambo mengi sana ya kushughulikia na nisipo jihangaikia mwenywe nitaozea humu ndani.Ni lazima nifanye maamuzi magumu kwa ajili ya mustakabali mzima wa maisha yangu ya sasa na yajayo.”akaenda dirishani akatazama nje
“ Moyo unaniuma sana lakini nitafanya nini wakati sina ujanja tena .Nililianzisha jambo hili na mimi ndiye nitakayelimaliza na ili kulimaliza hakuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya kutafuta muafaka na Dr Joshua.Tayari amekwishanizidi nguvu na sina namna ya kupambana naye tena.Ninafahamu maovu yake ,ninafahamu kamuua mke wake,na amesababisha kifo cha mkewangu Flaviana lakini sina namna zaidi ya kumuangukia kwani nikiendelea kupambana naye ni sawa na kupambana na ukuta nitajiumiza mwenyewe.Potelea mbali litakalokuwa na liwe tu lakini sitaki tena kuendelea kuishi maisha haya.Acha tu niibebe dhambi hii ya usaliti lakini lazima nirejee katika maisha yangu ya kawaida.” Akawaza Elibariki
“ Lakini nitaonana vipi na Dr Joshua? Si rahisi kuonana naye hivi hivi lazimaawepo mtu wa kuniunganisha naye .Ni nani basi ambaye anaweza kunisaidia kwa hili? Akajiuliza na kutafakari kwa sekunde kadhaa halafu akapata wazo
“ Rosemary Mkozumi.Huyu anaweza akanisaidia sana kuniunganisha na Dr johua.Huyu mwanamke ana mtandao mkubwa wa watu na anaweza kuwa na msaada mkubwa kwangu.lakini ili anisaidie lazima nimfungue kule chini alikofungwa.Nafahamu Rosemary ni mtu hatari sana na anashirikiana na magaidi lakini sina namna nyingine ya kufanya zaidi ya kumuachia huru ili aweze kunisaidia.Ninakumbuka kila kitu alichokifanya Mathew wakati tunamuingiza Rosemary kule chini.Ninazikumbuka namba alizobonyeza na mlango ukafunguka.Ninachotakiwa kufanya ni kumdhibiti kwanza Anitha “
Jaji Elibariki akaufungua mlango akachungulia nje.Nyumba yote ilikuwa kimya kabisa akatoka akaelekea katika chumba cha ofisi akachungulia na kumuona Anitha amekaa akiendelea na kazi akaufungu amlango na kuingia mle ofisini.Anitha akastuka
“ Jaji hulali leo? Akauliza
“ Nimekosa usingizi kabisa.Mathew na Peniela hawajarejea?
“ Hapana bado hawajarejea.Kuna tatizo limetokea”
“ Pole sana Anitha.let me make you a coffee”akasema Mathew
“ No thankyou Elibariki.situmii kahawa tafadhali” akasema Anitha na mara simu ikaita..
“halow Mathew.What happened? akasema Anitha kwa wasi wasi
“Hii ni nafasi ambayo natakiwa kuitumia vizuri”akawaza Elibariki na kwa kasi ya aina yake akakinyakua chungu cha maua kilichokuwa karibu yake na kumpiga nacho Anitha Kichwani akaanguka na kupoteza fahamu.Akaikanyaga kanyaga simu ile akakimbia hadi katika mlango wa chumba cha Mathew na kujaribu kuufungua.Ulikuwa umefungwa.Akarudi nyuma hatua kadhaa na kuurukia teke mlango ule ukafunguka akaingia ndani na moja kwa moja akaeleka katika kile kisanduku chenye namba.Akabonyeza namba alizozikumbuka lakini mlango haukufunguka.
“ C’mon nimekosea wapi? Mbona namba alizobonyeza Mathew ni hizi hizi? Akajaribu tena lakini bado mlango haukufunguka
“Nimekumbuka kulikuwa na namba mbili mwisho nasi namba tano.”
Akarudia tena kubonyeza na safari hii kabati kubwa la ukutani likasogea pembeni na mlango ukafunguka kwa akaanza kushuka kuelekea chini