PENIELA SEASON 3
SEHEMU YA 24
MTUNZI😛ATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Jaji yuko wapi ?Mbna nasikia sauti kubwa ya muziki ? akauliza Anitha
“ Inawezekana amepitiwa na usingizi” akasema Mathew kisha wote wakingia ndani.
Anitha na kwenda kupunguza sauti kubwa ya muziki .Baada ya kupunguza sauti wakasikia sauti ya kilio cha mtu.
“ Who is that? Akauliza Peniela
Mathew akatoa bastora yake na kuanza kufuatilia ilikotoka sauti ile ya mwanamke huku Anitha na Peniela wakiwa nyuma yake.Sauti ile ilitoka katika chumba cha jai Elibariki.Ilikuwa ni sauti ya Naomi.Haikuwa siri tena kwani sauti ilionyesha kwamba Jaji Elibariki na Naomi walikuwa wanafanya mapenzi.
“ Peniela,Anitha nendeni ofisini ninakuja muda si mrefu” akasema Mathew
“ No Mathew ! I want to see everything
“ akasema Peniela kwani alikwisha jua nini kilichokuwa kinaendelea mle chumbani.
ENDELEA…………………….
Mathew akavuta pumzi ndefu na kisha akagonga mlango lakini ilionekana waliokuwemo mle chumbani hawakusikia,akagonga tena safari hii kwa nguvu zaidi na ghafla kukawa kimya.Mathew akagonga tena na baada ya sekunde kadhaa mlango ukafunguliwa na jaji Elibariki ambaye licha ya kjaribukujifuta jasho bado liliendelea kumtiririka usoni..Alipatwa na mstuko mkubwa baada ya kukuta watu wote wako pale mlangoni wakimtazama akiwamo Peniela..
“ Mathew !.I can Explain this !!akasema jaji Elibariki huku akimtazama Peniela aliyekuwa anamuangalia kwa macho makali sana.
“ I can..I can explain this..akajitetea.
“ tell her to go to her room” Mathew akamwambia jaji Elibariki.Akaufunga mlango na kukasikika mabishano mle chumbani kati yakena Naomi na baada ya dakika mbili mlango ukafunguliwa na Naomi akatoka akiwa amejifunika shuka.uso wake ulijaa aibu.Alipotazamana na Mathew akarudi tena ndani na kuufunga mlango.Michirizi ya machozi ikaonekana machoni mwa Peniela ,akaondoka kwa kasi kuelekea sebuleni,Mathew akamfanyia ishara Anitha amfuate halafu akaufungua mlango na kuingia mle chumbani.Naomi alijibanza pembeni ya kabati na jaji Elibariki alikuwa amejinamia kitandani .
“ Mathew naomba unisamehe ..”akasema Naomi.
“ Naomi nenda chumbani kwako haraka sana”akasema Mathew..Naomi akatoka na kuchungulia nje kama akina Peniela wapo pale mlangoni kisha akatoka mbio kuelekea chumbani kwake.Mathew na Elibariki wakatazamana..
“ Mathew I can explain this..”akasema jaji Elibariki
“ Explain? Akasema Mathew ambaye hakuonekana kufurahishwa na kitendo kile
“ Sikutegemea kabisa kama unaweza ukafanya kitendo kama hiki Elibariki.na hasa kwa wakati huu zaidi ya yote na Naomi ”
“ Mathew najua nimechafua taswira yangu kwenu lakini naomba unielewe ndugu yangu kwamba sikufanya hivi kwa ridhaa yangu..”akasema jaji Elibariki na kumfanya Mathew acheke kidogo
“ Hukufanya kwa ridhaa yako? Unataka kuniambia kwamba Naomi alikubaka? Akauliza Mathew
“Mathew ni hadidthi ndefu na ninaomba tafadhali unipe nafasi nikueleze kila kitu” akasema jaji Elibariki
“ Elibariki mimi sina haja ya simulia yako unayetakiwa kumueleza ni Peniela na si mimi.Umemuumiza sana mtu ambaye tunamtegemea katika kazi yetu.Nenda kamueleze hayo unayaotaka kunieleza ”akasema Mathew na kutoka akaelekea katika chumba cha Naomi akagonga mlango Naomi akafungua.Uso wake ulijaa aibu na hakuthubutu kumtazama Mathew usoni
“ Mathew naomba unisamehe kaka yangu.Ni shetani tu alitupitia tukashindwa kujizuia” akasema Naomi huku akilia machozi
“ Isingekuwa kama nilikuahidi kukusaidia basi usiku huu huu ningekutimulia mbali.Kwa nini ukakubali kufanya uchafu ule katika nyumba yangu Naomi ?
“ Nisamehe Mathew, sintarudia tena” akalia Naomi.Mathew akamtazama kwa hasira.Na mara akakumbuka namna alivyoachia risasi zilizomuua Henry baba yake Naomi.
“ I killed her father.kwa namna yoyote ile natakiwa kumsaidia.Namuonea huruma sana huyu binti kwani hajui hata kama baba yake amefariki dunia..”akawaza Mathew na kumshika mkono Naomi akamuinua.Uso wake ulijaa machozi.
“ Naomi nimekusamehe kwa kitendo hiki cha leo lakini ninakuomba kitendo kama hiki kisijirudie tena.Mimi na wenzangu tumejitolea kukusaidia ili uweze kuanza upya maisha yako kwa hiyo tafadhali naomba sana jitahidi kutunza heshima yako.Wote unaowaona humu ndani ni watu na heshima zao na kwa kitendo ulichokifanya leo hii kimekushushia sana heshima thamani yako kwao kwa hiyo jitahidi kwa kila uwezavyo kuhakiksha wanakuamni tena.Tumeelewana Naomi? Akasema Mathew
“ Nimekuelewa Mathew.Ninakuahidi kwamba sintarudia tena kitendo kama hiki na ninaomba unisamehe sana na uniombee msamaha kwa dada Anitha na Peniela “
“ sawa nitajaribu kuwaelewesha .”akasema mathew na kutaka kutoka mle chumbani Naomi akamuita
“ Unasemaje Naomi ?akauliza Mathew
“ Mathew naomba msimlaumu jaji kwani ni mimi ndiye niliyemshawishi hadi akakubali kufanya name mapenzi.Hakuwa anataka kufanya jambo hilo ila mimi nilimlazimisha kwa kumpa vitisho ” akasema Naomi.Mathew akamuangalia na kutikisa kichwa
“ Mathew usinielwe vibaya kaka yangu lakini nilijikuta tu nikipatwa na tamaa baada ya kubaki sisi wawili tu humu ndani na kwa muda wa miaka zaidi ya minne sikuwa nimekutana na mwanaume yeyote Yule.Nisamehe sana mathew najua hata kama ni wewe au mtu mwingine yeyote angekuwa katika nafasi kama yangu nina hakika kabisa kwamba angeweza kufanya jambo kama nililolifanya”akasema Naomi.Mathew hakusema kitu akafungua mlango na kutoka akaelekea chumbani kwake akafungua kasiki lake na kurejesha silaha na baadhi ya vifaa alivyokuwa amevichukua kisha akaenda kukaa kitandani.Alionekana kuwa katika mawazo mengi sana.Mara mlango ukagongwa akaenda kufungua na kukutana na Anitha akamkaribisha ndani
“ Nimewapa nafasi Elibariki na Peniela ya kuzungumza kwa uhuru ila Peniela ameumizwa sana na kitendo cha aibu alichokifaya jaji Elibariki.Nilimuamini sana Eli na sikutegemea kama angeweza kufanya kitendo kama kile.” Akasema Anitha,Mathew akamtazama na kusema
“ Naomi alifungiwa ndani kwa zaidi ya miaka minne na kama binadamu wengine naye alikuwa na matamanio.Alipogundua kwamba amebaki yeye na jaji Elibariki pekee akaingiwa na tamaa na ndiyo yakatokea yale yaliyototokea.Nimeongea naye na amekiri kwamba ni yeye ndiye aliyemshawishi jaji Elibariki wakafanya mapenzi .”
“ Do you believe her?akauliza Anitha
“ yes I do .Hata hivyo Naomi bado anahitaji sana msaada wetu.Kazi kubwa inatakiwa kufanyika ili kumtoa katika maisha yake ya awali aliyokuwa akiishi na kumlata katika maisha ya kawaida.”akasema Mathew
“ Tayari umemfahamisha kuhusu kifo cha baba yake? akauliza Anitha
“ hapana bado sijamwambia.Ninasubiri muda muafaka ukifika nitamweleza.”akasema Mathew.
“ Ok tuachane na hayo..Usiku wa leo naweza kusema ni usiku mkubwa sana kwetu kwani tumefanikiwa kugundua suala kubwa na zito.hatimaye leo hii kitendwili kimeteguliwa.Tumefahamu nini kilichomo ndani ya hiyo package.Mathew mpaka sasa mwili wote bado unanitetemeka sana baada ya kufahamu pachage hiyo ina kitu gani ndani yake. Sikuwahi kuota kama kungekuwa na kitu kibaya na cha hatari kama hiki.”akasema Anitha .Akanyamaza kidogo na kuendelea
“ kwa hiyo nini kinafuata baada ya hapa?
Mathew akafikiri kidogo na kusema
“ Anitha kwanza kabisa ninapenda nikushukuru sana na kwa dhati kwa msaada mkubwa uliotuwezesha kufika hapa.Bila wewe juhudi zetu zote zingekuwa bure.Utaalamu wako wa hali ya juu wa teknolojia unaifanya kazi yetu isiwe ngumu sana.pamoja na hayo kuna jambo ninataka nikiri kwako na nina omba unisamehe kwa hilo”
“Ni jambo gani Mathew?akauliza Anitha kwa wasiwasi
“ I knew about that virus before”
Anitha akamtazama Mathew kwa sekunde kadhaa halafu akainuka na kujishika kiuno
“ You knew? And you didn’t tell me?
“ I’m sorry for that Anitha” akasema Mathew
“ Mathew sijui niseme nini lakini umenishangaza sana.Tunahangaika kila siku kutaka kujua nini kilichomo ndani ya package hiyo kumbe wewe unafahamu na hutaki kutueleza !! why Mathew why ?!!..Ulifurahi kumuona peniela akiuza utu wake kwa Dues wakati unafahamu alichokuwa anakitafuta?akauliza Anitha kwa ukali
“ Calm down anitha “akasema Mathew
“ John told me !..
“ John Mwaulaya? Akauliza Anitha
“Ndiyo.John mwaulaya ndiye aliyeniambia kuhusiana na suala hili.,Usiku ule aliponiita nikaonane naye hospitali alinieleza kila kitu kuhusiana na package hiyo na kwa nini ni kitu cha muhimu sana ambacho kwa namna yoyote ile hatupaswi kukiacha kitue mikononi mwa watu ambao wana lengo la kukitumia kwa matumizi yasiyofaa”akasema Mathew
“ Kwa nini basi hukutuambia?
“ Nilihitaji kupata uthibitisho kutoka kwa Deus.Sikumuamini John Mwaulaya mojakwa moja ”akasema Mathewm.Anitha akamtazama na kuuliza
“ Kitu gani kingine alikwambia na hujatuambia?akauliza Anitha
“ Ni hilo tu”
“ Are you sure?akauliza Anitha
“ Yes I’m sure.” Akajibu Mathew
“ Once I find out that you’ve been lying to me I’ll never forgive you Mathew.Why don’t you trust me? Akauliza Anitha..
“ Anitha I do trust you with my life..”akajibu Mathew na kumfanya Anitha atabasamu
“ So what’s next?
“ Tulikuwa tunapambana kuipata package ambayo hatukujua ina nini ndani yake.kwa sasa baada ya kufahamu kila kitu kuhusiana na package hiyo tunapaswa kuongeza nguvu na mikakati katika kuhasikisha kwamba kwa gharama yoyote ile tunaipata hiyo package.Vyovyote vile itakavyokuwa lakini tunatakiwa kuhakikisha kwamba Dr Joshua hafanikishi lengo lake la kuiuza package hiyo.Tutatumia kila aiana ya mbinu tuliyonayo katika kuhakikisha kwamba jambo hili halifanikiwa.Mtu wa muhimu sana ambaye atatusaidia katika kulifanikisha hili ni peniela pekee.Ndiyo maana sikufurahishwa kabisa na kitendo alichokifanya jaji Elibariki ambacho kimemuumiza sana Peniela na kumtoa nje ya mstari..She loves him so much .Kwa kitendo cha kumfumania na mwanamke mwingine kimemuumiza sana.Inatakiwa ifanyike juhudi ya makusudi kumrudisha Peniela katika hali yake ya kawaida ili tuweze kuifanya kazi.Dr Joshua anarejea kesho na kwa mujibu wa mawasiliano yake na Kigomba ni kwamba anataka jambo hili limalizike haraka iwezekanavyo kwani mchakato wake umeingiliwa na watu wengi.kwa mujibu wa maelekezo yake kwa Kigomba ni kwamba kesho atawasili Hussein ambaye nina uhakika mkubwa kwamba ndiye anayekuja kuuchukua mzigo huo na hivyo kumfanya kuwa mtu muhm,u sana kwetu ” akasema Mathew.
“ Katika hili“Mathew akaendelea
“ Peniela ana nafasi kubwa sana kwani tunatakiwa tumfahamu huyo Hussein ni nani na njia pekee ya kumfahamu Hussein ni kwa kuipata simu ya Dr Joshua na mwenye uwezo wa kuipata simu hiyo ni Peniela pekee.”
“ kesho mwili wa Flaviana utawasili kwa hiyo itakuwa ni siku yenye pilika pilika nyingi sana na wageni watakaofika kwa ajili ya kumpa pole Dr Joshua ni wengi na miongoni mwa wageni hao ni huyu Hussein ambaye tunatakiwa kumfahamu na hata kuipata sura yake ili tuweze kumfuatilia toka anapowasili uwanja wa ndege. Nina uhakika mkubwa kwamba huyu ndiye anayekuja kuuchukua mzigo huo kwa hiyo jicho letu halitakiwi kubanduka kabisa kwake”akasema Mathew
“ kama nilivyokwambia awali kwamba ni Peniela pekee anayeweza kutusaidia kulifanikisha hili suala.Ni yeye pekee anayeweza kuipata simu ya Dr Joshua” akasema Anitha
“ Nakubaliana nawe Anitha.Katika hili tunamuhitaji sana Peniela .Ngoja nikajaribu kuongea naye nimuweke sawa ili aweze kuirejesha akili yake katika jambo la msingi linalotukabili”akasema Mathew na kutoka mle chumbani akaelekea sebuleni lakini peniela hakuwepo.Akachungulia ofisini lakini hakuwepo pia akatoka nje na kumuona akiwa amekaa pembeni ya bwawa la kuogelea akamfuata na kuketi pembeni yake.Peniela alikuwa anatazama angani huku analia.Mathew akatoa kitamba cha mfukoni akampatia.
“ take this”akamwambia.paniela akastuka kidogo
“ Take it it’s clean.Futa machozi yote”akasema Mathew
“ Mathew why always me? Akauliza Peniela huku akishindwa kujizuia kulia kwa nguvu.Mathew akauzungusha mkono wake shingoni na kumkumbatia.Peniela akakilaza kichwa chake kifuani kwa Mathew na kuendelea kulia .
“ Its ok peniela..its enough now” akasema Mathew.
“ Inaniuma sana Mathew kwani nilimpenda sana Elibariki na niliamini kwamba ni mwanaume ambaye nitaanza naye maisha mapya baada ya skata hili kumalizika .Yeye ni sababu kubwa inayonifanya nipambane kufa na kupona katika kuhakikisha kwamba tunashinda vita hii na mimi kubaki huru but he did in return, he broke my heart!!..akasema Peniela kwa uchungu mkubwa
“ Peniela kitendo kile cha Elibariki kimetuudhi sisi sote lakini hta hivyo kwa sasa tuko kati kati ya vita na tunatakiwavkuishinda vita hii kwa hiyo ninakuomba japo kwa siku mbili tatu zilizobaki ,yaondoe mawazo yako kwa Elibariki na tuelekeze nguvu zetu katika suala zito lililoko mbele yetu.Baada ya kulimaliza suala hili tutapata wasaa wa kukaa na kuzungumza jambo lililotokea leo. Ninajua umeumia Peniela lakini maumivu haya yaelekeze katika jambo lililoko mbele yetu ambalo ili lifanikiwe linakuhitaji sana wewe.Kuna mambo mengi mazuri yanakuja mbele yako iwapo suala lililoko mbele yetu litafanikiwa kumalizika na sisi tukaibuka washindi.Ukumbuke vile vile kwamba kuna mpango mkubwa wa kukufanya mwanamke mwenye nguvu au the next first lady..”akasema Mathew.Peniela akamtazama na kusema
“ Mathew unaweza ukanieleza ukweli?
“Ukweli upi Peniela?
“ Ninataka unieleze ukweli bila kunificha.Ukiniangalai mimi unanionaje? Ninaonekanaje mbele zawatu? Ninaonekana kama kahaba? mwanamke nisiye na heshima yoyote,mwanamke ambaye kila mwanaume anaweza akamtumia? Akauliza Peniela.Mathew akamtazama kwa makini usoni
“ Tell me the truth Mathew “ akasema Peniela.mathew akakohoa kisogo na kusema
“ Mtazamo wangu kwako unawakilisha mtazamo wa watu wengi na si mtazamo tu bali ni ukweli halisi.Nikuonapo ninamuona mwanamke jasiri,mwenye ndoto na ambaye yuko tayari kwenda hadi ncha ya mwisho wa dunia ili azitimize ndoto zake,mwaname asiye kata tamaa ,mwanamke mwenye nguvu kubwa ndani yake licha ya mwili wake kuwa mdogo, mwanamkemwenye sauti laini lakini inayoweza kupenya hadi ndani ya mioyo ya watu wenye nguvu na wakavifunga vinywa vyao kumsikia,sifa ni nyingi za mwanamke ninayemuona nikuonapo lakini kubwa zaidi ya yote mwanamke mwenye uzuri wa asili wa ndani na wa nje ambao unaweza kujaza kitabu cha kurasa mia mbili kuuelezea. Huyu ndiye mwanamke ninayemuona nikikutazama.thats you Peniela.” Akasema Mathew.Uso wa Peniela ukatabasamu na kisha akasema
“ Ahsante Mathew kwa kunieleza ukweli.Kwa miaka mingi nilitafuta mwanaumeambaye atanieleza ukweli kuhusu mimi.Maneno uliyoyatamka yametoka ndani kabisa mwa moyo wako na ninayaamini ni sahihi na wala hujayatamka kwa kunifurahisha so thank you Mathew,thank you so much.I’m so lucky to have you..”akasema Peniela na kumbusu Mathew shavuni.
“ Now lets get back to work” akasema Peniela huku akiinuka na kumuacha Mathew bado amekaa katika bwawa akiwa ni kama vile amepigwa na butwaa .
“ Mathew we have a job waiting for us “ akasema Peniela na Mathew akainuka kisha wakaelekea katika chumba cha ofisi ambamo walimkuta Anitha
“ Elibariki yuko wapi? Akauliza Mathew
“ Yuko chumbani kwake”akajibu Anitha
"Go call him.we need him here”akasemaMathew na Anitha akatoka .Baada ya dakika mbili akarejea akiwa na Elibariki.
“ Jamani tumekutana tena hapa ili tuweze kujadiliana masuala ya muhimu kuhusiana na kile tulichokipata usiku huu..”Mathew akaanzisha maongezi lakini Elibariki akaingilia kati
“ Ndugu zangu kabla hatujaendelea naomba dakika kama mbili tu niweze kuwaelezea kile kilichotokea.” Akasema jaji Elibariki
“ Eli,utapata nafasi lakini si sasa.kwa wakati huu tuna masuala mazito yaliyoko mbele yetu”akasema Mathew.Akawatazama wote usoni halafu akaendela
“ usiku wa leo tunaweza kusema kwamba ni usiku wa kipekee kabisa kwa sababu tumefanikiwa kulifahamu jambo kubwa sana.Tumefahamu nini hasa hiyo package ambayo Dr Joshua anataka kuiuza.kwa vile sisi sote tayari tunafahamu,naomba nikufahamishe Elibariki kwamba kilichomo katika hiyo package ni kirusi hatari ambacho kinaitwa Aby 16.Hiki ni kirusi hatari sana na kinachoweza kusababisha maangamizi makubwa sana.” Mathew akaendelea kumuelezea Elibariki kila walichokipata toka kwa Deus kuhusiana na kirusi hicho.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO