Peniela (Story ya kijasusi)

Peniela (Story ya kijasusi)

mkuu humu tupo tofauti sana .wengine sio kwamba mda wote tunakuwa hewani harafu hizi story zipo huko kwenye ma group yao ya fb na watsapp.mm niliona sio mbaya na wapenda story wenzangu mkifaidi.hivyo ninapopata mda naiweka.au nkuu unataka nilale hapa na kushinda hapa
Mkuu watu hawana kazi, ni kulia ila tu, imefika muda haya mastory ndio yamegeuka faraja kwao, ukimwambia mtu walau hata auze nyanya au kufungua mradi wa ku brush viatu, hayo matusi utakayochezea ni Mungu nisaidie, watu huku hawajui Hatma zao kumaisha, wapo bora kumekucha.
Huyu jamaa mpaka amalize msimu wake, watu watakua wameisha saga meno vya kutosha.
 
Unaona wengine wameenda mbali mpaka wanajiona wamekuwa Mathew, na Peniela humu, wakati kushinda kitandani/ubarazani mpaka siku inaisha pasipo kuingiza kitu.
 
Mkuu watu hawana kazi, ni kulia ila tu, imefika muda haya mastory ndio yamegeuka faraja kwao, ukimwambia mtu walau hata auze nyanya au kufungua mradi wa ku brush viatu, hayo matusi utakayochezea ni Mungu nisaidie, watu huku hawajui Hatma zao kumaisha, wapo bora kumekucha.
Huyu jamaa mpaka amalize msimu wake, watu watakua wameisha saga meno vya kutosha.

Kweli mkuu,baada ya miangaiko ya siku nzima tunakuja kujiliwaza na hii stori. Majukwaa mengine hayashikiki,ukienda jukwaa la siasa ni vilio,jukwaa la MMU ndio usiseme kila mtu analia,ukienda jukwaa la michezo hasa sisi mashabiki wa Man Utd ndio vilio. Yani hii stori ndio imekua kimbilio
 
PENIELA SEASON 3

SEHEMU YA 23

MTUNZI 😛ATRICK.CK



ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ peniela mkubalie lakini mwambie na wewe kuna kitu unataka kutoka kwake” amathew akamwambai peniela
“ Ouh Deus ,utaniweza mtu kama mimi..?akaulzia Peniela
“ kwa nininisikuweze peniela?

“ Ok tutaona lakini mimi niko tayari kukuachia mwili wangu but I also need onething in return”akasema peniela
“ What do you need beautiful angel?
“ mwambie akwambie nini kilichomondani ya package” akasema Mathew

“ I want you to tell me whats in the package”

“ peniela ! peniela..nimekwisha kwambia kwamba hii ni siri yangu hadi siku ninaingia kaburini.tafadhaliombakitu kingine chochote na si hicho.Katu sintaweza kukuambia” akasema dues

“ peniela wakati wa kuondoka sasa.”Mathew akamwambia peniela
“ Deus ninashukur sana kwa kuipata nafasi hii ya kukaa nawe japo wa dakika chache.Ninashukuru kwa ushirikiano wako na kama Mungu akipenda tutaonana tena.Niko tayari kukaa nawe hata kwa usiku mzima lakini hadi pale tu utakaponieleza kuhusu kilichomo ndaniya package.” Akasema peniela huku akiinukana kuuchukua mkobawake tayari kwa kuondoka.




ENDELEA………………………………




“ Peniela not so fast my lady ! akasema Deus huku akitabasamu

“ Deus we’re done in here so I have to go” akasema Peniela
“ Not yet Peniela.The night is still so young.Tunahitaji kufahamiana zaidi hasa kwa usiku huu wa kwanza mimi na wewe kukutana.Dont you want to spend time with the person who wants to make you the next first lady? Akauliza Deus.Peniela akatabasamu
“ Deus tumekwisha fahamiana vya kutosha tayari . Tutatafuta tena siku nyingine ambayo tutakutana na kuendelea kufahamiana zaidi.” Akasema Peniela akionekana kuushikilia msimamo wake wa kutaka kuondoka.Deus akanywa whisky kidogo na kusema

“ Peniela unajua sisi tuliobobea katika masuala ya siasa we’re not good in convincing women and tonght I don’t know how to convince you to spend the night with me.” Akasema Deus Peniela akamtazama na kutabasamu

“ Peniela mwambie uko tayari kwa kile alichokiomba lakini mpaka akwambie kile kilichomo katika package ” Mathew akampa maelekezo.Peniela akasita kidogo
“ Peniela do it ! akasema Mathew.Peniela akasema

“ Deus , I would like to spend the night with you “ akasema Peniela na kuuweka mkoba wake chini akamfuata akaupeleka mkono wake shavuni kwa Deus akambusu kisha akamtazama na kusema

“ I’m ready to give you what you want,but you’ll have to tell me what is in that package ? akasema Peniela. Deus akaiweka mezani glasi yake ya mvinyo na kumtazama
“ Kwa nini unataka kufahamu kilichomo ndani ya hiyo package ?

“ Kwa sababu mimi na wewe tuna lengo moja la kuhakikisha kiwamba package hiyo haitui mikononi mwa watu wabaya kwa hiyo ninahitaki kufahamu ni kitu gani kiko ndani ya hiyo package na kwanini watu wamekuwa wakiitafuta kwa pesa nyingi kiasi hiki? Is it a bomb? I want to know Deus”
Peniela akamkumbatia tena na kuanza kumchezea Deus maeneo nyeti ambayo ghafla yakafura kwa hasira kali.
“ I know This is what you want Deus so tell me everything that I want to know and I’ll be yours tonight and many nights to come “ akasema Peniela na kumchanganya zaidi Deus

“ Peniela kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nimekutana na mwanamke ambaye amenifanya niende nje ya msimamo na kiapo changu.Nitakueleza kila kitu,lakini tafadhali naomba uniahidi kwamba hii itabaki kuwa ni siri yako na hatafahamu mtu mwingine yeyote Yule.What am about to tell you it’s a very very big secret.” Akasema Deus.Peniela akamsogelea akamkumbatia na kuanza kumpapasa maungoni

“ That secret is safe with me.” Akasema Peniela na kuipeleka ncha ya ulimi wake katika sikio la Deus na kumfanya atoe mguno kwa msisimko alioupata.Deus akamuinua Peniela kwa nguvu na kumtupa kitandani kisha akaanza kuvua nguo zake haraka haraka na kupanda kitandani.
“ Peniela kuwa makini sana na Deus.Usifanye naye chochote kabla hajakueleza kile tunachokitaka” Mathew akamuelekeza Peniela.Deus akaanza kumbusu Peniela kila sehemu
“ Ouh C’mon Deus not so fast my dear. First thing first Mr President.Why don’t you start by telling me what I want to know before I undress ? Akasema Peniela kisha akamvuta Deus na kumbusu huku akiendelea kumpapasa sehemu mbali mbali za mwili wake.
“ She’s so good at this “ Anitha akamwambia Mathew wakiwa garini wakiendelea kufuatilia kila kinachoendelea kati ya Deus na Peniela
“ yah .She good.Very good.” Akasema Mathew.Anitha akamtazama kwa makini na kusema
“ Mathew can I ask you something?
“ Yes ask”
“ Unakumbuka tukiwa nyumbani nilikuelekeza kwamba uende chumbani ukamtazame Peniela kama amemaliza kuvaa.What happened in there?
“ kwa nini umeuliza hivyo Anitha?
“ Ninahitaji tu kufahamu kwa sababu baada ya kutoka kule chumbani ulionekana tofauti kidogo,the way you were looking at her..tell me, did something happen in there? Akauliza Anitha.Mathew akatabasamu na kusema

“ Nothing happened”
Anitha akamtazama tena usoni na kutabasamu kisha akasema
“ You saw her naked right? Do you like her? Akauliza Anitha

“ Anitha lets not talk about that” akasema Mathew

“ Mathew wewe ni rafiki yangu na ninakupenda na ndiyo maana ninataka kukupa ushauri mdogo.Tafadhali ifute kabisa picha ya Peniela kichwani kwako.She’s not good for you..”akasema Anitha

“ Deus anataka kumweleza kitu Peniela
“ Mathew akamwambia Anitha wote wakaelekeza macho katika kompyuta kusikiliza kile ambacho Deus anataka kumweleza Peniela
“ Ok Peniela you won .I’m going to tell you what’s in there” akasema Deus akamtazama Peniela kwa sekunde kadhaa na kusema
“ Kilichomo ndani ya hiyo inayoitwa package ni kirusi kilichopewa jina la Aby 16.”
“ A virus ?!!! Peniela akashangaa
“ Yes it’s a virus and not only a virus but a very very very dangerous virus ever made by a man” akasema Deus.
“ ouh my gosh ! akasema Peniela

“ Kirusi hiki kama kitaachiwa husambaa kwa njia ya hewa na ndani ya dakika kinaweza kusambaa kwa maelfu ya watu na kusababisha homa kali ambayo mgonjwa asipotibiwa ndani ya saa moja toka alipopatwa na ugonjwa huo atapoteza maisha.Kibaya zaidi ni kwamba mpaka hivi sasa kirusi hicho hakijawahi kupatiwa kinga yake kwa hiyo ni kitu hatari sana kwa usalama wa nchi yetu na dunia kwa ujumla na ndiyo maana kinahifadhiwa ikulu mahala ambako hakuna mtu wa kawaida anaweza akapafikia.Kwa bahati mbaya taarifa za uwepo wa kirusi hiki katika Ikulu ya Dar es salaam zimevuja na hivyo kuyavutia sana mataifa mbalimbali kutaka kukipata kirusi hiki kwa gharma zozote zile.Serikali ya Marekani inakitumia kikundi cha Team SC41 ili kuweza kukipata kirusi hicho lakini kibaya zaidi ni kwamba hata mitandao ya kigaidi wamekuwa wakikitafuta kirusi hiki kwa nguvu sana ili kuweza kukitumia katika mashambulio yao ya kigaidi.Mataifa makubwa yenye viwanda vikubwa vya kutengeneza dawa nao pia wanakitafuta kirusi hiki kwa udi na uvumba ili waweze kutafuta dawa yake na kisha kukiachia ili wafanye biashra ya dawa.Kwa bahati mbaya sana Dr Joshua ameingiwa na tamaa ya pesa nyingi na ndiyo maana anataka kukiuza kirusi hicho kwa namna yoyote ile bila kujali madhara yake.Wakati wa uongozi wangu hata mimi nimeshawishiwa sana kuuza package hiyo kwa matrilioni ya pesa lakini sikuwa na tamaa na pesa .” akasema Deus.Kikapita kimya kifupi Peniela akauliza
“ Deus hebu nifafanulie kirusi hicho kimefikaje katika ikulu yetu ya Dar es salaama ? Nani alikitengeneza? Yuko wapi? Karatasi zile zilizoibwa ikulu na akina Rosemary na kutaka kuuzwa kwa magaidi zinahusiana kwa namna yoyote na kirusi hiki?

“ Peniela ulitaka kufahamu kuhusiana na pachage hiyo anayotaka kuiuza Dr Joshua ina nini ndani yake na nimekueleza kilichomo kwa hiyo nadhani nimejibu swali lako .Kuhusu kimetoka wapi na nani aliyetengeneza kwa kweli sintaweza kukujibu kwa sababu hata mimi sifahamu.Mimi pia nilikabidhiwa bila kupewa historia yoyote ile.Kuhusu karatasi zile kama zinahusiana na kirusi kile jibu ni ndiyo.Kanuni zile ndizo zinazoelekeza namna ya kukitenegeneza kirusi hicho lakini bado hazijakamilika ,bado kuna karatasi nyingine zimehifadhiwa sehemu nyingine na ili uweze kukamilisha kutengenza kirusi kamili unatakiwa uzipate karatasi hizo zote.” Akasema Deus

“ Peniela nadhani sasa umefahamu ni kwa nini watu wanaitafuta package hiyo kwa udi na uvumba.Kwa nini watu wako tayari kutoa pesa nyingi mno kwa ajili ya kukipata kirusi hicho .Ninakuhakikishia kwamba endapo kirusi hicho kikifanikiwa kutoka mahala kilipohifadhiwa na kutua mikononi mwa watu wenye uchu wa kukipata dunia haitakuwa sehemu salama tena .Hili si suala dogo kama unavyodhani . Kitu anachotaka kukifanya Dr Joshua kwa tamaa ya fedha ni kitu kinachoweza kusababisha maangamzi makubwa sana duniani.Endapo kirusi hicho kikitua mikononi mwa mitandao ya kigaidi unadhani nini kitakwenda kutokea? Yatakuwa ni maangamizi makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika historia ya dunia.Endapo kirusi hiki kitatua katika mikono ya mataifa makubwa yenye viwanda vikubwa vya kutengeneza dawa lazima watakuja kukitupa kirusi hiki huku Afrika kwa ajili ya kufanya majaribio na kuuza dawa zao.Watu wengi sana watapoteza maisha yao kwa hiyo kirusi hiki hatari kinatakiwa kuendelea kuhifadhiwa katika sehemu salama” akasema Deus.
Ndani ya gari Mathew akachukua kitambaa na kujifuta jasho.Mambo waliyoyasikia toka kwa Deus yalimsisimua sana.
“ Peniela ,nadhani Deus hataweza kutoa tena maelezo mengine zaidi ya hayo aliyoyatoa.Mpatie anachokihitaji halafu uondoke “ akasema Mathew
“ Deus thank you for this information.Sikuwahi kuhisi kabisa kama package hiyo itakuwa na kitu cha muhimu kama hiki.Nikuahidi nitahakikisha haitui katika mikono ya mtu yeyote Yule mwenye nia mbaya na itaendelea kuwa salama”

“ Thank you Peniela.Thank you so much” akasema Deus

“ Now come here and get what you need” akasema Peniela huku akilipandisha juu gauni lake na nguo yake ya ndani ikaonekena.Deus akaonekana kuchanganyikiwa.Taratibu Peniela akaanza kuishusha nguo ile ya ndani, na kuiweka pembeni akamfanyia ishara Deus amsogelee.
“ Switch it off “ akasema Mathew ndani ya gari
“ kwa nini Mathew? Lazima tuangalie kila kinachoendelea mle ndani ili tujue kama Peniela yuko salama “ akasema Anitha

“ Japokuwa tumepata taarifa tulizokuwa tunazihitaji lakini sifurahii na njia tuliyoitumia kuzipata.” akasema Mathew.
“ Usijali Mathew .Kitu cha msingi ni kwamba tumefanikiwa kupata taarifa muhimu.” akasema Anitha.
Ndani ya chumba haikuchukua zaidi ya dakika sita Deus kufika mshindo akaanguka pembeni.
“ Gosh ! mzee mwenyewe hajiwezi halafu anataka kukesha na mimi .Dakika tano tu ameanguka kama kuku “ akawaza Peniela huku akivaa nguo yake ya ndani akambusu Deus na kusema

“ Deus nadhani tayari umekipata kile ulichokuwa unakihitaji.I can go now. ” akasema Peniela
“ Ouh Peniela I’m so sorry kwa hali hii.Leo siko vizuri na ndiyo maana sijaweza kwenda mwendo mrefu” akasema Deus

“ Its ok Deus.I’ll call you again” akasema Peniela.
“ Ngoja kwanza Peniela niwaite walinzi wakuongoze kutoka humu ndani” akasema Deus na kuvaa kisha akabonyeza kitufe Fulani na mara mlango ukafunguka akaingia mtu mmoja aliyevalia nadhifu suti nyeusi.Deus akampa maelekezo amuongoze Peniela hadi katika gari lake .
“ Nimemaliza kazi and now I’m on my way out
“ Peniela akawataarifu akina Mathew baada ya kuingia garini

“ Thank you Peniela and good job.” Akasema Mathew.Peniela akawasha gari na kuondoka



********


Peniela ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwasili nyumbani kwa Mathew na baada ya dakika mbili wakawasili Mathew na Anitha.Mathew akashuka garini na kwenda kulifungua geti

“ Elibariki amepitiwa na usingizi ? Mbona hafungui geti “ Akauliza Mathew.

“ Sielewi kwa sabau nimejaribu kupiga honi mara kadhaa hakuna aliyejitokeza kufungua geti” akasema Peniela
. Kwa kutumia remote control Mathew akalifungua geti na magari yakaingizwa ndani .Mara tu Peniela aliposhuka garini Mathew akamfuata na kumkumbatia.
“ Peniela you did a good job today.Bila wewe katu tusingeweza kuzipata taarifa zile nzito” akasema Mathew.Peniela akatabasamu

“ Ahsanteni pia kwani tumeifanya kazi hii pamoja.Bila ninyi hakuna kitu kingeweza kufanikiwa.” Akasema Peniela halafu wakatazamana kwa sekunde kadhaa wakastuliwa na Anitha

“ Jaji yuko wapi ?Mbna nasikia sauti kubwa ya muziki ? akauliza Anitha

“ Inawezekana amepitiwa na usingizi” akasema Mathew kisha wote wakingia ndani.
Anitha na kwenda kupunguza sauti kubwa ya muziki .Baada ya kupunguza sauti wakasikia sauti ya kilio cha mtu.

“ Who is that? Akauliza Peniela
Mathew akatoa bastora yake na kuanza kufuatilia ilikotoka sauti ile ya mwanamke huku Anitha na Peniela wakiwa nyuma yake.Sauti ile ilitoka katika chumba cha jai Elibariki.Ilikuwa ni sauti ya Naomi.Haikuwa siri tena kwani sauti ilionyesha kwamba Jaji Elibariki na Naomi walikuwa wanafanya mapenzi.
“ Peniela,Anitha nendeni ofisini ninakuja muda si mrefu” akasema Mathew
“ No Mathew ! I want to see everything “ akasema Peniela kwani alikwisha jua nini kilichokuwa kinaendelea mle chumbani.



TUKUTANE SEHEMU IJAYO……
 
PENIELA SEASON 3


SEHEMU YA 24

MTUNZI😛ATRICK.CK



ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Jaji yuko wapi ?Mbna nasikia sauti kubwa ya muziki ? akauliza Anitha
“ Inawezekana amepitiwa na usingizi” akasema Mathew kisha wote wakingia ndani.
Anitha na kwenda kupunguza sauti kubwa ya muziki .Baada ya kupunguza sauti wakasikia sauti ya kilio cha mtu.

“ Who is that? Akauliza Peniela
Mathew akatoa bastora yake na kuanza kufuatilia ilikotoka sauti ile ya mwanamke huku Anitha na Peniela wakiwa nyuma yake.Sauti ile ilitoka katika chumba cha jai Elibariki.Ilikuwa ni sauti ya Naomi.Haikuwa siri tena kwani sauti ilionyesha kwamba Jaji Elibariki na Naomi walikuwa wanafanya mapenzi.
“ Peniela,Anitha nendeni ofisini ninakuja muda si mrefu” akasema Mathew

“ No Mathew ! I want to see everything
“ akasema Peniela kwani alikwisha jua nini kilichokuwa kinaendelea mle chumbani.



ENDELEA…………………….



Mathew akavuta pumzi ndefu na kisha akagonga mlango lakini ilionekana waliokuwemo mle chumbani hawakusikia,akagonga tena safari hii kwa nguvu zaidi na ghafla kukawa kimya.Mathew akagonga tena na baada ya sekunde kadhaa mlango ukafunguliwa na jaji Elibariki ambaye licha ya kjaribukujifuta jasho bado liliendelea kumtiririka usoni..Alipatwa na mstuko mkubwa baada ya kukuta watu wote wako pale mlangoni wakimtazama akiwamo Peniela..
“ Mathew !.I can Explain this !!akasema jaji Elibariki huku akimtazama Peniela aliyekuwa anamuangalia kwa macho makali sana.
“ I can..I can explain this..akajitetea.

“ tell her to go to her room” Mathew akamwambia jaji Elibariki.Akaufunga mlango na kukasikika mabishano mle chumbani kati yakena Naomi na baada ya dakika mbili mlango ukafunguliwa na Naomi akatoka akiwa amejifunika shuka.uso wake ulijaa aibu.Alipotazamana na Mathew akarudi tena ndani na kuufunga mlango.Michirizi ya machozi ikaonekana machoni mwa Peniela ,akaondoka kwa kasi kuelekea sebuleni,Mathew akamfanyia ishara Anitha amfuate halafu akaufungua mlango na kuingia mle chumbani.Naomi alijibanza pembeni ya kabati na jaji Elibariki alikuwa amejinamia kitandani .
“ Mathew naomba unisamehe ..”akasema Naomi.
“ Naomi nenda chumbani kwako haraka sana”akasema Mathew..Naomi akatoka na kuchungulia nje kama akina Peniela wapo pale mlangoni kisha akatoka mbio kuelekea chumbani kwake.Mathew na Elibariki wakatazamana..

“ Mathew I can explain this..”akasema jaji Elibariki

“ Explain? Akasema Mathew ambaye hakuonekana kufurahishwa na kitendo kile
“ Sikutegemea kabisa kama unaweza ukafanya kitendo kama hiki Elibariki.na hasa kwa wakati huu zaidi ya yote na Naomi ”
“ Mathew najua nimechafua taswira yangu kwenu lakini naomba unielewe ndugu yangu kwamba sikufanya hivi kwa ridhaa yangu..”akasema jaji Elibariki na kumfanya Mathew acheke kidogo
“ Hukufanya kwa ridhaa yako? Unataka kuniambia kwamba Naomi alikubaka? Akauliza Mathew

“Mathew ni hadidthi ndefu na ninaomba tafadhali unipe nafasi nikueleze kila kitu” akasema jaji Elibariki

“ Elibariki mimi sina haja ya simulia yako unayetakiwa kumueleza ni Peniela na si mimi.Umemuumiza sana mtu ambaye tunamtegemea katika kazi yetu.Nenda kamueleze hayo unayaotaka kunieleza ”akasema Mathew na kutoka akaelekea katika chumba cha Naomi akagonga mlango Naomi akafungua.Uso wake ulijaa aibu na hakuthubutu kumtazama Mathew usoni

“ Mathew naomba unisamehe kaka yangu.Ni shetani tu alitupitia tukashindwa kujizuia” akasema Naomi huku akilia machozi

“ Isingekuwa kama nilikuahidi kukusaidia basi usiku huu huu ningekutimulia mbali.Kwa nini ukakubali kufanya uchafu ule katika nyumba yangu Naomi ?
“ Nisamehe Mathew, sintarudia tena” akalia Naomi.Mathew akamtazama kwa hasira.Na mara akakumbuka namna alivyoachia risasi zilizomuua Henry baba yake Naomi.
“ I killed her father.kwa namna yoyote ile natakiwa kumsaidia.Namuonea huruma sana huyu binti kwani hajui hata kama baba yake amefariki dunia..”akawaza Mathew na kumshika mkono Naomi akamuinua.Uso wake ulijaa machozi.
“ Naomi nimekusamehe kwa kitendo hiki cha leo lakini ninakuomba kitendo kama hiki kisijirudie tena.Mimi na wenzangu tumejitolea kukusaidia ili uweze kuanza upya maisha yako kwa hiyo tafadhali naomba sana jitahidi kutunza heshima yako.Wote unaowaona humu ndani ni watu na heshima zao na kwa kitendo ulichokifanya leo hii kimekushushia sana heshima thamani yako kwao kwa hiyo jitahidi kwa kila uwezavyo kuhakiksha wanakuamni tena.Tumeelewana Naomi? Akasema Mathew
“ Nimekuelewa Mathew.Ninakuahidi kwamba sintarudia tena kitendo kama hiki na ninaomba unisamehe sana na uniombee msamaha kwa dada Anitha na Peniela “
“ sawa nitajaribu kuwaelewesha .”akasema mathew na kutaka kutoka mle chumbani Naomi akamuita

“ Unasemaje Naomi ?akauliza Mathew

“ Mathew naomba msimlaumu jaji kwani ni mimi ndiye niliyemshawishi hadi akakubali kufanya name mapenzi.Hakuwa anataka kufanya jambo hilo ila mimi nilimlazimisha kwa kumpa vitisho ” akasema Naomi.Mathew akamuangalia na kutikisa kichwa

“ Mathew usinielwe vibaya kaka yangu lakini nilijikuta tu nikipatwa na tamaa baada ya kubaki sisi wawili tu humu ndani na kwa muda wa miaka zaidi ya minne sikuwa nimekutana na mwanaume yeyote Yule.Nisamehe sana mathew najua hata kama ni wewe au mtu mwingine yeyote angekuwa katika nafasi kama yangu nina hakika kabisa kwamba angeweza kufanya jambo kama nililolifanya”akasema Naomi.Mathew hakusema kitu akafungua mlango na kutoka akaelekea chumbani kwake akafungua kasiki lake na kurejesha silaha na baadhi ya vifaa alivyokuwa amevichukua kisha akaenda kukaa kitandani.Alionekana kuwa katika mawazo mengi sana.Mara mlango ukagongwa akaenda kufungua na kukutana na Anitha akamkaribisha ndani
“ Nimewapa nafasi Elibariki na Peniela ya kuzungumza kwa uhuru ila Peniela ameumizwa sana na kitendo cha aibu alichokifaya jaji Elibariki.Nilimuamini sana Eli na sikutegemea kama angeweza kufanya kitendo kama kile.” Akasema Anitha,Mathew akamtazama na kusema

“ Naomi alifungiwa ndani kwa zaidi ya miaka minne na kama binadamu wengine naye alikuwa na matamanio.Alipogundua kwamba amebaki yeye na jaji Elibariki pekee akaingiwa na tamaa na ndiyo yakatokea yale yaliyototokea.Nimeongea naye na amekiri kwamba ni yeye ndiye aliyemshawishi jaji Elibariki wakafanya mapenzi .”
“ Do you believe her?akauliza Anitha
“ yes I do .Hata hivyo Naomi bado anahitaji sana msaada wetu.Kazi kubwa inatakiwa kufanyika ili kumtoa katika maisha yake ya awali aliyokuwa akiishi na kumlata katika maisha ya kawaida.”akasema Mathew

“ Tayari umemfahamisha kuhusu kifo cha baba yake? akauliza Anitha
“ hapana bado sijamwambia.Ninasubiri muda muafaka ukifika nitamweleza.”akasema Mathew.

“ Ok tuachane na hayo..Usiku wa leo naweza kusema ni usiku mkubwa sana kwetu kwani tumefanikiwa kugundua suala kubwa na zito.hatimaye leo hii kitendwili kimeteguliwa.Tumefahamu nini kilichomo ndani ya hiyo package.Mathew mpaka sasa mwili wote bado unanitetemeka sana baada ya kufahamu pachage hiyo ina kitu gani ndani yake. Sikuwahi kuota kama kungekuwa na kitu kibaya na cha hatari kama hiki.”akasema Anitha .Akanyamaza kidogo na kuendelea
“ kwa hiyo nini kinafuata baada ya hapa?
Mathew akafikiri kidogo na kusema
“ Anitha kwanza kabisa ninapenda nikushukuru sana na kwa dhati kwa msaada mkubwa uliotuwezesha kufika hapa.Bila wewe juhudi zetu zote zingekuwa bure.Utaalamu wako wa hali ya juu wa teknolojia unaifanya kazi yetu isiwe ngumu sana.pamoja na hayo kuna jambo ninataka nikiri kwako na nina omba unisamehe kwa hilo”
“Ni jambo gani Mathew?akauliza Anitha kwa wasiwasi
“ I knew about that virus before”
Anitha akamtazama Mathew kwa sekunde kadhaa halafu akainuka na kujishika kiuno

“ You knew? And you didn’t tell me?
“ I’m sorry for that Anitha” akasema Mathew
“ Mathew sijui niseme nini lakini umenishangaza sana.Tunahangaika kila siku kutaka kujua nini kilichomo ndani ya package hiyo kumbe wewe unafahamu na hutaki kutueleza !! why Mathew why ?!!..Ulifurahi kumuona peniela akiuza utu wake kwa Dues wakati unafahamu alichokuwa anakitafuta?akauliza Anitha kwa ukali

“ Calm down anitha “akasema Mathew

“ John told me !..
“ John Mwaulaya? Akauliza Anitha
“Ndiyo.John mwaulaya ndiye aliyeniambia kuhusiana na suala hili.,Usiku ule aliponiita nikaonane naye hospitali alinieleza kila kitu kuhusiana na package hiyo na kwa nini ni kitu cha muhimu sana ambacho kwa namna yoyote ile hatupaswi kukiacha kitue mikononi mwa watu ambao wana lengo la kukitumia kwa matumizi yasiyofaa”akasema Mathew

“ Kwa nini basi hukutuambia?
“ Nilihitaji kupata uthibitisho kutoka kwa Deus.Sikumuamini John Mwaulaya mojakwa moja ”akasema Mathewm.Anitha akamtazama na kuuliza

“ Kitu gani kingine alikwambia na hujatuambia?akauliza Anitha
“ Ni hilo tu”

“ Are you sure?akauliza Anitha

“ Yes I’m sure.” Akajibu Mathew

“ Once I find out that you’ve been lying to me I’ll never forgive you Mathew.Why don’t you trust me? Akauliza Anitha..
“ Anitha I do trust you with my life..”akajibu Mathew na kumfanya Anitha atabasamu

“ So what’s next?
“ Tulikuwa tunapambana kuipata package ambayo hatukujua ina nini ndani yake.kwa sasa baada ya kufahamu kila kitu kuhusiana na package hiyo tunapaswa kuongeza nguvu na mikakati katika kuhasikisha kwamba kwa gharama yoyote ile tunaipata hiyo package.Vyovyote vile itakavyokuwa lakini tunatakiwa kuhakikisha kwamba Dr Joshua hafanikishi lengo lake la kuiuza package hiyo.Tutatumia kila aiana ya mbinu tuliyonayo katika kuhakikisha kwamba jambo hili halifanikiwa.Mtu wa muhimu sana ambaye atatusaidia katika kulifanikisha hili ni peniela pekee.Ndiyo maana sikufurahishwa kabisa na kitendo alichokifanya jaji Elibariki ambacho kimemuumiza sana Peniela na kumtoa nje ya mstari..She loves him so much .Kwa kitendo cha kumfumania na mwanamke mwingine kimemuumiza sana.Inatakiwa ifanyike juhudi ya makusudi kumrudisha Peniela katika hali yake ya kawaida ili tuweze kuifanya kazi.Dr Joshua anarejea kesho na kwa mujibu wa mawasiliano yake na Kigomba ni kwamba anataka jambo hili limalizike haraka iwezekanavyo kwani mchakato wake umeingiliwa na watu wengi.kwa mujibu wa maelekezo yake kwa Kigomba ni kwamba kesho atawasili Hussein ambaye nina uhakika mkubwa kwamba ndiye anayekuja kuuchukua mzigo huo na hivyo kumfanya kuwa mtu muhm,u sana kwetu ” akasema Mathew.
“ Katika hili“Mathew akaendelea
“ Peniela ana nafasi kubwa sana kwani tunatakiwa tumfahamu huyo Hussein ni nani na njia pekee ya kumfahamu Hussein ni kwa kuipata simu ya Dr Joshua na mwenye uwezo wa kuipata simu hiyo ni Peniela pekee.”

“ kesho mwili wa Flaviana utawasili kwa hiyo itakuwa ni siku yenye pilika pilika nyingi sana na wageni watakaofika kwa ajili ya kumpa pole Dr Joshua ni wengi na miongoni mwa wageni hao ni huyu Hussein ambaye tunatakiwa kumfahamu na hata kuipata sura yake ili tuweze kumfuatilia toka anapowasili uwanja wa ndege. Nina uhakika mkubwa kwamba huyu ndiye anayekuja kuuchukua mzigo huo kwa hiyo jicho letu halitakiwi kubanduka kabisa kwake”akasema Mathew
“ kama nilivyokwambia awali kwamba ni Peniela pekee anayeweza kutusaidia kulifanikisha hili suala.Ni yeye pekee anayeweza kuipata simu ya Dr Joshua” akasema Anitha
“ Nakubaliana nawe Anitha.Katika hili tunamuhitaji sana Peniela .Ngoja nikajaribu kuongea naye nimuweke sawa ili aweze kuirejesha akili yake katika jambo la msingi linalotukabili”akasema Mathew na kutoka mle chumbani akaelekea sebuleni lakini peniela hakuwepo.Akachungulia ofisini lakini hakuwepo pia akatoka nje na kumuona akiwa amekaa pembeni ya bwawa la kuogelea akamfuata na kuketi pembeni yake.Peniela alikuwa anatazama angani huku analia.Mathew akatoa kitamba cha mfukoni akampatia.
“ take this”akamwambia.paniela akastuka kidogo
“ Take it it’s clean.Futa machozi yote”akasema Mathew

“ Mathew why always me? Akauliza Peniela huku akishindwa kujizuia kulia kwa nguvu.Mathew akauzungusha mkono wake shingoni na kumkumbatia.Peniela akakilaza kichwa chake kifuani kwa Mathew na kuendelea kulia .

“ Its ok peniela..its enough now” akasema Mathew.

“ Inaniuma sana Mathew kwani nilimpenda sana Elibariki na niliamini kwamba ni mwanaume ambaye nitaanza naye maisha mapya baada ya skata hili kumalizika .Yeye ni sababu kubwa inayonifanya nipambane kufa na kupona katika kuhakikisha kwamba tunashinda vita hii na mimi kubaki huru but he did in return, he broke my heart!!..akasema Peniela kwa uchungu mkubwa
“ Peniela kitendo kile cha Elibariki kimetuudhi sisi sote lakini hta hivyo kwa sasa tuko kati kati ya vita na tunatakiwavkuishinda vita hii kwa hiyo ninakuomba japo kwa siku mbili tatu zilizobaki ,yaondoe mawazo yako kwa Elibariki na tuelekeze nguvu zetu katika suala zito lililoko mbele yetu.Baada ya kulimaliza suala hili tutapata wasaa wa kukaa na kuzungumza jambo lililotokea leo. Ninajua umeumia Peniela lakini maumivu haya yaelekeze katika jambo lililoko mbele yetu ambalo ili lifanikiwe linakuhitaji sana wewe.Kuna mambo mengi mazuri yanakuja mbele yako iwapo suala lililoko mbele yetu litafanikiwa kumalizika na sisi tukaibuka washindi.Ukumbuke vile vile kwamba kuna mpango mkubwa wa kukufanya mwanamke mwenye nguvu au the next first lady..”akasema Mathew.Peniela akamtazama na kusema
“ Mathew unaweza ukanieleza ukweli?
“Ukweli upi Peniela?
“ Ninataka unieleze ukweli bila kunificha.Ukiniangalai mimi unanionaje? Ninaonekanaje mbele zawatu? Ninaonekana kama kahaba? mwanamke nisiye na heshima yoyote,mwanamke ambaye kila mwanaume anaweza akamtumia? Akauliza Peniela.Mathew akamtazama kwa makini usoni
“ Tell me the truth Mathew “ akasema Peniela.mathew akakohoa kisogo na kusema
“ Mtazamo wangu kwako unawakilisha mtazamo wa watu wengi na si mtazamo tu bali ni ukweli halisi.Nikuonapo ninamuona mwanamke jasiri,mwenye ndoto na ambaye yuko tayari kwenda hadi ncha ya mwisho wa dunia ili azitimize ndoto zake,mwaname asiye kata tamaa ,mwanamke mwenye nguvu kubwa ndani yake licha ya mwili wake kuwa mdogo, mwanamkemwenye sauti laini lakini inayoweza kupenya hadi ndani ya mioyo ya watu wenye nguvu na wakavifunga vinywa vyao kumsikia,sifa ni nyingi za mwanamke ninayemuona nikuonapo lakini kubwa zaidi ya yote mwanamke mwenye uzuri wa asili wa ndani na wa nje ambao unaweza kujaza kitabu cha kurasa mia mbili kuuelezea. Huyu ndiye mwanamke ninayemuona nikikutazama.thats you Peniela.” Akasema Mathew.Uso wa Peniela ukatabasamu na kisha akasema

“ Ahsante Mathew kwa kunieleza ukweli.Kwa miaka mingi nilitafuta mwanaumeambaye atanieleza ukweli kuhusu mimi.Maneno uliyoyatamka yametoka ndani kabisa mwa moyo wako na ninayaamini ni sahihi na wala hujayatamka kwa kunifurahisha so thank you Mathew,thank you so much.I’m so lucky to have you..”akasema Peniela na kumbusu Mathew shavuni.

“ Now lets get back to work” akasema Peniela huku akiinuka na kumuacha Mathew bado amekaa katika bwawa akiwa ni kama vile amepigwa na butwaa .
“ Mathew we have a job waiting for us “ akasema Peniela na Mathew akainuka kisha wakaelekea katika chumba cha ofisi ambamo walimkuta Anitha

“ Elibariki yuko wapi? Akauliza Mathew

“ Yuko chumbani kwake”akajibu Anitha

"Go call him.we need him here”akasemaMathew na Anitha akatoka .Baada ya dakika mbili akarejea akiwa na Elibariki.
“ Jamani tumekutana tena hapa ili tuweze kujadiliana masuala ya muhimu kuhusiana na kile tulichokipata usiku huu..”Mathew akaanzisha maongezi lakini Elibariki akaingilia kati

“ Ndugu zangu kabla hatujaendelea naomba dakika kama mbili tu niweze kuwaelezea kile kilichotokea.” Akasema jaji Elibariki
“ Eli,utapata nafasi lakini si sasa.kwa wakati huu tuna masuala mazito yaliyoko mbele yetu”akasema Mathew.Akawatazama wote usoni halafu akaendela
“ usiku wa leo tunaweza kusema kwamba ni usiku wa kipekee kabisa kwa sababu tumefanikiwa kulifahamu jambo kubwa sana.Tumefahamu nini hasa hiyo package ambayo Dr Joshua anataka kuiuza.kwa vile sisi sote tayari tunafahamu,naomba nikufahamishe Elibariki kwamba kilichomo katika hiyo package ni kirusi hatari ambacho kinaitwa Aby 16.Hiki ni kirusi hatari sana na kinachoweza kusababisha maangamizi makubwa sana.” Mathew akaendelea kumuelezea Elibariki kila walichokipata toka kwa Deus kuhusiana na kirusi hicho.


TUKUTANE SEHEMU IJAYO
 
PENIELA SEASON 3

SEHEMU YA 25

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Elibariki yuko wapi? Akauliza Mathew

“ Yuko chumbani kwake”akajibu Anitha
‘Go call him.we need him here”akasemaMathew na Anitha akatoka .Baada ya dakika mbili akarejea akiwa na Elibariki.

“ Jamani tumekutana tena hapa ili tuweze kujadiliana masuala ya muhimu kuhusiana na kile tulichokipata usiku huu..”Mathew akaanzisha maongezi lakini Elibariki akaingilia kati
“ Ndugu zangu kabla hatujaendelea naomba dakika kama mbili tu niweze kuwaelezea kile kilichotokea.” Akasema jaji Elibariki
“ Eli,utapata nafasi lakini si sasa.kwa wakati huu tuna masuala mazito yaliyoko mbele yetu”akasema Mathew.Akawatazama wote usoni halafu akaendela

“ usiku wa leo tunaweza kusema kwamba ni usiku wa kipekee kabisa kwa sababu tumefanikiwa kulifahamu jambo kubwa sana.Tumefahamu nini hasa hiyo package ambayo Dr Joshua anataka kuiuza.kwa vile sisi sote tayari tunafahamu,naomba nikufahamishe Elibariki kwamba kilichomo katika hiyo package ni kirusi hatari ambacho kinaitwa Aby 16.Hiki ni kirusi hatari sana na kinachoweza kusababisha maangamizi makubwa sana.” Mathew akaendelea kumuelezea Elibariki kila walichokipata toka kwa Deus kuhusiana na kirusi hicho.




ENDELEA……………………..




Jaji Elibariki alibaki kinywa wazi baada ya maelezo yale ya Mathew.Akashusha pumzi

“ Kwa hiyo maelezo yale ya Josh Yule rafiki yako wa Israel kuhusiana na kirusi kile yalikuwa sahihi kabisa .” akasema Elibariki
“ Ndiyo Eli. Josh alikuwa sahihi kabisa .Kilichoandikwa katika nyaraka zile ni kanuni za kutengeneza kirusi Aby 16.Kwa bahati mbaya kirusi hicho tayari kimekwisha tengenezwa na kinahifadhiwa katika ikuluya dare s salaam na kwa hivi sasa kinagombaniwa na watu mbali mbali na wengi kati yao ni watu wenye nia ovu na wanaotaka kukitumia kusababisha maangamizi makubwa ” Akasema Mathew
“ Mathew ambacho bado sijakielewa mpaka sasa na sijasikia ukikisema.Kirusi hicho hakikujitengeneza na wala hakikujileta chenyewe pale ikulu bali kimetengenezwa na mtu na kikafikishwa pale ikulu na mtu.Ninachotaka kufahamu ni nani aliyekitengeneza na yuko wapi? Kilifikaje pale ikulu ? Akauliza jaji Elibariki
“ Elibariki maswali hayo ni magumu hakuna anayeweza kutupa majibu yake kwa sasa.Kilichopo mbele yetu baada ya kufahamu kwamba package tunayoitafuta ni kirusi Aby 16 ni kuhakikisha kwamba tunakipata kirusi hicho kwa gharama zozote zile.Tukirejea mazungumzo ya Dr Joshua na Kigomba ni kwamba wanataka kulimaliza suala hili haraka kwani tayari limekwishaanza kuiingiliwa na watu wengi.Kesho mwili wa Flaviana utarejeshwa nyumbani kutokea afrika ya kusini kwa hiyo itakuwa nisiku yenye shughuli nyingi kwa Dr Joshua na sina hakika kama ataweza kushughulika na suala hili.Nina hakika baada ya shughuli za mazishi kukamilika basi wataifanya biashara hi haraka sana.” Akasema Mathew akanyamaza kidogohalafu akaendelea.
“ Dr Joshua alimtaarifu Dr Kigomba kuhusu kuwasili kwa mtu aliyemtaja wka jina moja tu la Hussein.Si mara ya kwanza kwa Dr Joshua akumtaja mtu huyu mtu na nina hisi kwamba ana nafasi kubwa sana katika jambo hili.Hussien anategemea kuwasili kesho jioni .Hatufahamu ni raia wa nchi gani na hata sura yake hatuifahamu lakini ni mtu muhimu sana ambaye tunatakiwa kumfahamu na kumfuatilia kwa karibu sana toka dakika ambayo ataingia nchini.Nina uhakika mkubwa kwamba mtu huyu kama si yeye aliyekuja kuuchukua mzigo huo basi ni wakala kwa hiyo jicho letu halitakiwi kubanduka kwake.” Mathew akanyamaza akawatazama wenzake waliokuwa kimya wakimsikiliza kisha akaendelea.
“ ili kumfahamu Hussein ni nani tunapaswa kuipata namba yake ya simu toka katika simu ya Dr Joshua na anayeweza kuipata simu ya Dr Joshua na akatupatia namba ya Hussein ni Peniela pekee.Zoezi la kuipata namba hiyoya simu toka katika simu ya Dr Joshua linatakiwa lifanyike kesho ili tuweze kumfahamau Hussein na kumfuatailia toka dakiak ya kwanza anapoingia nchini.Unasemaje kuhusu hilo peniela linaweza ufanyika kesho? Akauliza Mathew
“ Usihofu Mathew,ninaweza kuifanya kazihiyokesho.Najua Dr Joshua kwa siku ya kesho atakuwa na pilika nyingi za msiba lakininitahakiksha kwamba ninakutana naye na ninaipata simuyake na kuichukua hiyo namba ya Hussein tunayoitaka” akasema peniela
“ Are you sure peniela? Hatutaki kukuweka katika hatari” akasema Mathew

“ Usiogope Mathew.Nitakupatia hiyo namba kesho..” Akasema peniela

“ Thankyou so much Peniela “ akasema Mathew

“ Nini kitafuata baada ya kumfahamu Hussein? Akauliza Peniela
“ Kama nilivyosema awali kwamba Dr Joshua amemtaja Hussein zaidi ya mara moja kuhusiana na mpangohuu.Mara ya kwanza alimfahamisha Kigomba kwamba amezungumza na Hussein na amemfahamisha kwamba tayari pesa imekwisha ingizwa katika akaunti walizofungua nje ya nchi.Katika maelezo mengine Dr Joshua amemtaarifu Kigomba kwamba Hussein atawasili kesho na inaonyesha wazi kwamba ujio wake huu ni wa kuja kukamilisha biashara yao na ikiwezekana kuondoka kabisa na kirusi hicho. Dr Joshua atamkabidhi Kigomba package hiyo na ambaye ndiye atakayefanya makabidhiano na wanunuzi .Nina hakika kabisa kwamba makabidhiano hayo yatafanyika sehemu fulani ambako wanunuzi itawalazimu wahakikishe kwamba kitu walichouziwa ni chenyewe .Hili litafanyika sehemuya siri sana .Kwa kuwa sisi tayari tunamfuatilia Kigomba kila aendako basi itakuwa rahisi kujua yuko wapi na tutamdhibiti na kuichukua hiyo package. Wakati huo huo Hussein naye atadhibitiwa kikamilifu ili asije akatoroka kwani mtandao huu wote unatakiwa utiwe nguvuni.Huo utakuw amwisho wa mchezo.”Mathew akasema halafu akafikiri kidogo na kusema

“ Kwa namna yoyote ile nilazima tupate mtu ambaye anaweza akatusaidia kwa upande wa kumdhibiti Hussein.Ni nyakati kamahizi ninakumbuka sana Noah”akasema Mathew

“ Josh can do that”akasema Peniela
“Josh ?!
“ Ndiyo .Ni kijana mwenye uwezo mkubwa sana anafuata maelekezo na anaweza akaifanya kazi hii bila matatzo”
“ Are yu sure we can trust him? Akauliza Mathew

“ Bila wasiwasi.Josh aliaminiwa sana na John Mwaulaya na alikuwa akimtumia sana katika shughuli zake mbali mbali na kama alikuwa akihitaji kumshughulikia mtu Fulani basi alikuwa akimtumia josh.NI kijana ambaye ana malengo ya kuachana na team SC41 na kuanza maisha mapya kwa hiyo anaweza akatufaa sana” akasema Peniela

“sawa.Tutampataje Josh?akauliza Mathew
“kesho asubuhi nitalazimika kwenda nyumbani kwa John kuonana na Team SC41 na kujua ni kitu gani ambacho wamekipanga kuhusianana na msiba wa john.Nina hakika mpaka mida hiii watakuwa wamejiuliza maswali mengi sana kuhusiana na kutoonekana kwangu.Baada ya kifo cha amos ,mimindiye wananitegemea sana katika suala hii.Ninataka nifahamu pia kuhusiana na mipango yao ya kuipata package na nitawataarifu ” Akasema Peniela
“ Ok jamani nadhani tumeelewanatutapanga zaidi kesho.Siku ya leo imekuwa ni ndefu sana kwetu kwa hiyo niwakatiwa kwenda kupumzika na kujiandaa kwa ajili ya kesho.” Akasema Mathew

“ Kabla hatujaondoka humu kuna suala ninataka kuuliza”akasema jaji Elibariki

“ Uliza Eli” akasema mathew
“ Tunaye Rosemary Mkozumi humu ndani tunaendelea kumshikilia ,nini hatima yake? Suala lake linashughulikiwa vipi?

“ Suala la Rosemary ni kubwa na linatakiwa kushughulikiwa kwa upana wake.Tumeliweka pembeni kidogo tumalize kwanza suala la Dr Joshua na ndipo tutaendelea na suala la Rose.Tutaendelea kumshikilia hapa ambayo ni sehemu salama zaidi.Vile vile kuna suala la Deus alilomweleza Peniela kuhusiana na mipango waliyonayo juu yako Elibariki na Peniela.Yote haya tutayaweka pembeni kwa muda ili tushughulikie kwanza hili kubwa “ akasema Mathew
“ Mathew mimi sintalala hapa ninaomba niondoke niende nyumbani nikapumzike ili kesho niamkie katika masuala mengine.Tutawasiliana kuhusiana na kinachoendelea..” akasema Peniela.
“ Hapana peniela.Tayari umekwisha kuwa usiku mwingi.Hapa kuna nafasi ya kutosha na zaidi sana ni sehemu salama .Utalala hapa” akasema Mathew
“ Mathew dhumuni la kutaka kwenda nyumbani ninataka kufanya mawasiliano na Dr Joshua usiku huu .Simu ninayotumia kuwasiliana naye iko nyumbani so I must go there” akasema Peniela.
“ Ok sawa.Kama umesisitiza kwamba unataka kwenda basi nitakupeleka ukaichukue hiyo simu kisha tutarejea hapa.Peniela wewe ni mtu muhimu sana kwa sasa na siko tayari upatwe na tatizo lolote.” Akasema Mathew.Peniela akatabasamu na kutikisa kichwa kukubalianana Mathew kisha wakaingia katika gari la Mathew na kuondoka kuelekea nyumbani kwa Peniela
“Mathew imekuwa vizuri sana nimepata nafasi hii ya kuwa nawe kuna mambo mawili ninataka tuyajadili.” Akasema peniela
“Nakusikiliza Penny”akasema Mathew.
“usijali Mathew tutajadili tukifika nyumbani” akasema Peniela kisha wakaendelea na safari.
“ Mathew kwa nini hukutaka nije kulala nyumbani kwangu wakati unafahamu kabisa kwamba ni vigumu tena mimi kuwa karibu na Elibariki hasa kwa kitendo alichokifanya? Akauliza Peniela.

“ Peniela tulikubaliana kwamba masuala yale yaliytokea yawekwe pembeni kwanza kwa muda hadi tutakapomaliza masuala mazito yanayotukabili”akasema Mathew.Peniela akamtazama na kuuliza
“ Mathew toka alipofariki mkeo,have you ever been in love?
“ There is only one woman I Ever loved on earth.Thats my wife ..She died with all the love I had inside me so my heart is empty.Kujibu swali lako ni kwamba sijawahi kuzama mapenzini kwa mwanamke yeyote Yule toka alipofariki mke wangu”akasema Mathew

“ That’s why you don’t know the pain I’m feeling right now.” akasema Peniela.
“Umesemaje?!! Akauliza Mathew
“ Nimesema kwamba bado huyafahamu maumivu ya kumpenda mtu halafu akakufanyia kama alivyonifanyia Elibariki” akasema Peniela
“ Peniela nimepitia mambo mengi zaidi yako.Ninayafahamu mapenzi zaidi ya unavyoyafahamu wewe.Nimeumizwa na mapenzi zaidi ya ulivyowahi kuumizwa wewe na ndiyo maana nikasema kwamba suala lako na Elibariki nisuala dogo na linaweza kumalizika.Are you sure that you love him? Are you sure that he loves you? Unatakiwa ujiulize maswali haya kabla ya kuuruhusu moyo wako uumie kwa sababu ya mtu Fulani.Anastahili machozi mtu Yule ambaye una hakika kwamba uko tayari hata kufa kwa ajili yake lakini kama huna uhakika na hilo just let this go” Akasema Mathew
“ Do you think it’s easy to let this go Mathew? I love Elibariki with all my heart na ndiyo maana nimeumia sana kwa kitu alichonifanyia.Sikutegemea kama angeweza kunifanyia kitu kama kile.” Akasema Peniela.
“ Peniela forget what happened and move on.Thats my advice to you”akasema Mathew
“ I don’t know if I’ll move on without him.I love him so much”

“ If you do love him that much then forgive him” akasema Mathew kisha safari ikaendelea kimya kimya.Baada ya muda Penieal akasema
“ Mathew kuna jambo lingine nataka kukuuliza “ akasema Peniela
“ Uliza peniela hii ni fursa yako” akajibu Mathew

“ wakati tukijiandaa kwenda kwa Deus usiku huu ,ulikuja chumbani kwa Anitha na ukafungua mlango ukanikuta nikiwa mtupu ninavaa .Nilijua ni bahati mbaya labda hukujua kama ninavaa na nilitegemea ungefunga mlango mara moja na kuondoka na baadae ungeniomba samahani lakini hukufanya hivyo badala yake ukaendelea kusimama pale mlangoni unanitazama .Nilikuona na sikutaka kukusemesha.Nataka kujua Mathew kwa nini ulifanya vile? akauliza peniela.
“ I’m sorry for that peniela.Sikujua kama ulikuwa unavaa” Akajibu Mathew

“ Mathew si suala la kuomba msamaha na wala hii si kesi.Ninachotka kusikia toka kwako ni kwa nini baada ya kunikuta ninavaa hukuufunga mlango na kuondoka badala yake ukabaki unanitazama? Mathew ninakuamini wewe ni muwazi na huwezi kunificha kuhusu hili.Be honest with me” akasema peniela
“ Kumbe aliniona?!!..dah !aibu gani hii..” akawaza Mathew
“peniela naomba tafadhali tusiongele suala lile la aibu.Samahani sana kwa kitendo kile cha aibu nilichokifanya and please don’t tell anyone” akasema Mathew

“ Mathew naona hujanielewa.Ni kwamba sikulaumu kwa kitendo kile na wala sijakasirika na wala sioni aibu kwa sababu najua mwili wangu wote umekwisha uona ukiwa mtupu. Ninachotaka kufahamu ni kwa nini ulisimama mlangoni na kunitazama? Do you like my body when naked? Akauliza Peniela na kumpa wakati mgumu Mathew kujibu.
“ peniela naomba tafadhali tusiliongelee suala hilo” akasema Mathew.Peniela akatabasamu na kusema
“ Mathew ninajua unachokiogopa kukisema.Let me answer for you.You liked me ,right? Akasema peniela Mathew akabaki kimya.

“ Ever since we met I knew you liked me but you are scared to let me know.Ulitakiwa kuniambia ukweli wako Mathew because even me I’ve started to like you” akasema peniela.

“ Peniela tafadhali naomba tuachane na mambo hayo.”akasema Mathew

“ I’ve been in many places around the world and I’ve met so many guys lakini sijawahi kukutana na mtu kama wewe Mathew.You are a real gentleman.”akasema peniela .
“ peniela ni mwanmke mwenye majaribu makubwa sana.Ana maneno matamu ambayo yanaweza kukufanya akili yako yote isiwaze kitu kingine chochote zaidi yake yeye tu. Nimekwisha fahamu anachokitaka na siwezi kumpa nafasi. “ akawaza Mathew

“ Pamoja na hayo lazima nikiri kwamba Peniela amependelewa uzuri wa kipekee kabisa.Anasisimua mno na ndiyo maana nilipomkuta akiwa mtupu mle chumbani nilijikuta nikisisimkwa na nikashindwa kubandua mguu pale mlangoni..She’s hot” akawaza Mathew
Walifika nyumbani kwa Peniela wakaingia ndani.Nyumba ilikuwa tulivu sana

“ Home sweet home.I missed my house so much”akasema Peniela na kumkaribisha Mathew sofani.Peniela akafungua kabati kubwa ambalo hulitumia kuhifadhia mvinyo akatoa chupa kubwa ya mvinyo na kuiweka mezani

“ Mathew imekuwa ni siku ndefu sana na mambo mengi yametokea siku ya leo.Kwa nini tusiitumie nafasi hii kutuliza akili wakati tukijiandaa na kesho?akasema Peniela huku akimimina mvinyo katika glasi na kumpatia Mathew
“ Ulisema kuna mambo ambayo unataka kuniuliza ? akauliza Mathew

“ Ndiyo Mathew but before that I’m hungry ,why don’t we make something to eat? Aren’t you hungry? Akauliza Peniela

“ hata mimi ninahisi njaa” akasema Mathew.

“ Wakati ninaandaa chakula kwa nini usiende kuoga na upunguze uchovu? Akasema Peniela
“ Hilo ni wazo la msingi .Ninahisi uchovu mwingi sana.” Akasema Mathew.
Penela akamshika mkono Mathew na kumuogoza hadi chumbani kwake akamuingiza katika bafu lake kubwa na zuri akamuacha humo kisha akaenda jikoni kuendelea kuandaa chakula.

“ Elibariki amenifanyia kitendo cha aibu sana na ameniumiza mno.Nilimpenda sana lakini kwa kitendo alichokifanya sitaki tena kuendelea naye.Nimeanza kuvutiwa na Mathew.Ni kijana mzuri anajitambua na kujiheshimu tofauti na Elibariki ambaye anaonekana kuwa na tamaa.Mathew anaonekana ni mtu mwenye msimamo kwani toka mke wake alipofariki hajawahi kujiingiza tena katika mapenzi na mwanamke mwingine .Sina hakika kama ananipenda lakini nina hakika na kitu kimoja kwamba ana hisa Fulani juu yangu.Nina uhakika huo kutokana na namna alivyokuwa ananiangalia .Hii ni sehemu nzuri kwa kuanzia .” akawaza Peniela.
Aliandaa chakula chepesi haraka haraka kisha akarejea chumbani .Bado Mathew alikuwa amekaa katika jaccuzi akioga.Kichwa chake kilijaa mawazomengi sana.Mara mlango wa bafu ukafunguliwa akaingia peniela akiwa amejifunga taulo.Mathew macho yakamtoka pima.Peniela akamtazama akatabasamu na kusema
“ Mbona umestuka Mathew? Umestuka kuniona hivi? Akauliza Peniela huku akitoa kichekokidogo
“ Usiogope Mathew kwani hakuna kitu ambcho hujakiona.”akasema Peniela na kuliangusha taulo akabaki mtupu.



TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………………..
 
mkuu humu tupo tofauti sana .wengine sio kwamba mda wote tunakuwa hewani harafu hizi story zipo huko kwenye ma group yao ya fb na watsapp.mm niliona sio mbaya na wapenda story wenzangu mkifaidi.hivyo ninapopata mda naiweka.au nkuu unataka nilale hapa na kushinda hapa
Achana nae mkuu mtu ambae hana shukran unavyojitoa bure ili nasi tupate burudan wengine atupo uko fb wala kwenye ayo magroup
 
Kweli mkuu,baada ya miangaiko ya siku nzima tunakuja kujiliwaza na hii stori. Majukwaa mengine hayashikiki,ukienda jukwaa la siasa ni vilio,jukwaa la MMU ndio usiseme kila mtu analia,ukienda jukwaa la michezo hasa sisi mashabiki wa Man Utd ndio vilio. Yani hii stori ndio imekua kimbilio
Hahahhhhh
 
Elli..ni mdhaifu bhana....hivi ktk akiri ya kawaida mashtaka ya naomi kutaka kubakwa na elli nani atamuamini na uteja wake...???....kutanuliwa mapaja tuuu...baaaasiiiii......na mwenzake ana ugumu wa 4yrs...migundi ya kumwaga....
 
Mkuki kwa nguruwe kumbe kwa paniela.....kasahau kwamba alimsababishia eli.apasuke kichwa alivyowagonganisha na jason.....???...na kama papuchi ingalikuwa inaisha kama sabuni..?..ya paniela ingebaki kiselema cha kuoshea vyombo......
 
Ukisikia Eli anatema Big G kwa karanga ya kuonjeshwa....
Ila ataendelea na Naomi alishajua utamu wake then kwa Madam Rose kama akitaka kubadilisha mboga
 
Daahh...mama weee...!!!!....mathew kaingia kwenye mtego wa penny.....kazi inaharibika sasa........
 
Back
Top Bottom