PENIELA SEASON 3
SEHEMU YA 33
MTUNZI😛ATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Usiongelee kabisa suala la mimi na wewe kuwa washirika.Siwezi kamwe kushirikiana na mtu kama wewe ambaye nimekushuhudia ukiwasaliti wenzako.Kwa ajili ya maslahi yako unaweza ukamsaliti mtu yeyote Yule.Wewe si mtu wa kuamini hata kidogo lakini hata hivyo itakusaidia ingawa kwa sharti moja kubwa.”
“ Sharti gani hilo Rose? akauliza Elibariki
“ Promise me that you will help me find Mathew”akasema Rose
Bila kupepesa macho jaji Elibariki akasema
“ I will help you find Mathew.I promise”akasema jaji Elibariki.
“ Thank you.I will help you.Dr Joshua atakapomaliza mazishi ya mwanae nitakukutanisha naye”akasema Rose
“ Naomba unisaidie suala hili kwa haraka zaidi ili niweze kushiriki mazishi ya mke wangu Flaviana” akaomba Elibariki
“ Nitajitahidi kadiri nitakavyoweza “
“Fernando I’m done with Mr Judge,Take me to the next room to see that woman ” akasema Rose na kisha Fernando akamsaidia kuinuka akamshika mkono akamsaidia kutembea wakatoka mle chumbani.
ENDELEA…………………
Mlango wa chumba alimofungiwa Anitha ukafunguliwa ,Rosemary Mkozumi akaingia akiwa ameongozana na mlinzi wake Fernando.Anitha alikuwa amekaa kitandani amefungwa pingu mikononi ,alikuwa anatetemeka mwili mzima.Tukio lililotokea chumbani alimowekwa jaji Elbariki muda mfupi uliopita lilimuogopesha mno.Akainua uso na kumtazama Rose,macho yake yalijaa machozi
“ Nilidhani ninyi ni mashujaa na hamuogopi kufa kwa ajili ya kuitetea nchi yenu.!! Sasa mona unalia? akasema Rosemary Mkozumi huku akicheka kwa dharau .Anitha hakuongea kitu akabaki anamtazama kwa jicho la chuki.
“ whats your name ? akauliza Rose.Anitha hakumjibu kitu
“ nakuuliza jina lako nani? Akauliza tena lakini bado Anitha hakujibu kitu
“ Wewe ni bubu hutaki kujibu?.”akasema Rose na Fernando akamsogelea Anitha
“ Umeulizwa jina lako nani? Akasema Fernando kwa ukali
“ Fernando leave her.Atasema tu yeye ni nani hata kama si sasa hivi lakini atasema tu”akasema Rose huku akimtazama anitha kwa hasira
“ Wewe na mwenzako Mathew ndiyo mashujaa wa nchi hii ambao mmekuwa mnawatuatilia watu migongoni mwao kujua wanafanya nini siyo? Hongereni sana vijana wenye uchungu na nchi hii lakini siku zote mashujaa huwa wa kwanza kufa na ndivyo itakavyokutokea kwako kama usiponipatia kile ninachokihitaji”akasema Rose na kuendelea kumtazama Anitha kwa jicho kali
“ Mwenzako Mathew aliingia ndani ya nyumba yangu,akamuua mpenzi wangu na kisha akaniteka na kunipekea nyumbani kwake,akanitesa sana .Ninataka kujua ni nani aliyewatuma kwangu? Nani aliyewapa habari zangu?akauliza Rose.Bado Anitha hakuthubutu kuufungua mdomowake.
“ Wewe ni bubu? Akauliza Rose akionyesha kukerwa na tabia ile ya Anitha kukaa kimya kila alipoulizwa
“ Sikiliza binti,kwa hivi sasa hatima ya maisha yako iko mikononi mwangu na endapo ukinipa ushirikiano ninaoutaka basi ninaweza kukuachia huru lakini ukiendelea na tabia yako ya kiburi ninakuapia kwamba hutaliona tena jua la kesho.Mpaka sasa wewe na mwenzako Mathew ni maadui zangu wakubwa sana na huyu mwenzako nitamsaka kwa udi na uvumba hadi nihakikishe nimemtia mikononi na kumuonyesha mimi ni nani.Nataka liwe fundisho kwenu na kwa wenzenu ili mjue kwamba Tanzania hii ina wenyewe.Kwa taarifa yako ile nyumba yenu mliyokuwa mnaitumia kuwatesea watu nimeiteketeza kwa moto jana usiku.Kila kitucheni hivi sasa ni majivu ”akasema Rosemary na kumstua sana Anitha ambaye aliinuka ghafla na kutaka kumvamia Rose lakini Fernando akawahi kumdaka
“ You devil ! I swear you’ll pay for this Rose..You will pay !! akasema kwa hasira Anitha.
“ Ouh kumbe unaweza kuongea vizuri,basi baadae mchana nitakapomaliza mkutano wangu na waandishi wa habari nitapata nafasi ya kuongea nawe.fernando I need her later in room five” Rosemary akamuelekeza Fernando.
“ Brave woman,me and you we’ll meet later.We’’ hve a nice talk. “ akasema Rose
“ you go to hell !! akasema Anitha kwa ukali.Rose akamsogelea
“ You’ll see how hell looks like,very soon..”akasema Rose.Anitha akamtemea mate usoni na kabla hajakaa sawa Fernando akamnasa kibao kikali kilichompekea chini
“ Thank you brave woman,tutaonana baadae na nitakutemea lita kadhaa za mate “ akasema Rose kisha wakatoka mle ofisini.
“ This woman is brave..haonekani kuogopa hata kidogo.Anaonekana ni mtu mzoefu sana katika shughuli hizi “akasema Rose
“ Ni kweli madam.Anaonekana jasiri sanamlakini akiminywa atasema kila kitu”
“ Ok tutaonana naye baadae.Huyu lazima atuonyeshe mahala alipo mwenzake.Watu hawa ni hatari sana kwetu” akasema Fernando.
Bado Anitha aliendelea kutweta kwa hasira baada ya Rosemary kutoka mle chumbani.Alikuwana hasira kali sana.
“ Ama kweli hawakukosea waliosema ni heri kumfadhili Mbuzi kuliko binadamu.Elibarki anawezaje kweli leo hii kutifanyia sisi namna hii? Tumefanya mambo mengi kwa ajili yake lakini haya ndiyo malipo yake...Mhh !Elibariki !! bado siamini ”akawaza Anitha huku machozi yakimtoka kwa hasira alizokuwa nazo
"Aaaaagghhhh!!!..akapiga ukelele mkubwa.
“ Tulifanya kila tuliloweza kumsaidia na hata Noah akapoteza uhai kwa ajili ya kumuokoa yeye lakini haya yote hayana thamani tena kwake na badala yake amediriki kutusaliti tena kwa mtu ambaye ni hatari sana.Amemuachia huru mtu ambaye anashirikiana na magaidi.Ouh Elibariki kwa nini lakini umefanya hivi?Jitihada zetu zote ni kazi bure.Hatutaweza tena kukipata kirusi kile hatari !! Aaaaghhh !!...akaendelea kulia kwa uchungu.
“ Sipati picha Mathew atakuwa katika hali gani hivi sasa baada ya nyumba yake kuteteketezwa kwa moto.Kama kila kitu kimeungua basi tutakuwa tumerudi nyuma sana na kazi ya kukipata kirusi Aby itakuw angumu sana kwani kila kitu amacho tulikitegemea katika operesheni hii kilikuwamo mle ndani.I must get out of here.I must help Mathew.lakini nitatokajehapa? akajiuliza
Baada ya kutoka chumbani kwa Anitha Rose akaelekea katika chumba alimofungiwa Naomi.Akapata mstuko mkubwa baada ya kugundua msichana aliyefungwa mle ni Naomi.
“ Naomi ?!! akasema kwa mshangao
“ Aunt Rose? Naomi naye akashangaa
“Umejuaje kama niko hapa aunt Rose? Akauliza
Naomi
“ Hapa ni nyumbani kwangu.Ulifikaje kwa Mathew ?Alikuteka nyara? Akauliza Rose
“ Kwa hiyo wewe ndiye uliyetuteka pale kwa Mathew mimi jaji na Aunt Anitha?
“ Naomi nieleze ulifikaje pale kwa Mathew? Alikuteka na kukuchukau kwa nguvu? Akauliza Rose
“ Hapana aunt,Mathew hakuniteka bali ndiye aliyenisaidia kunitoa katika lile jumba baba alimokuwa ananifungia kwa zaidi ya miaka minne na kuniweka huru..”
“Mathew alikusaidia? Rose akashangaa
“ Ndiye aliyenisaidia kutoka ndani ya jumba lile” akasema Naomi bila wasiwasi
“ Naomi hebu nieleze vizuri ilikuajehadi akamuamini Mathew ? Unafahamiana naye? Nieleze vizuri tafadhali”akasema Rose.
Naomi akamsimulia kila kitu kilivyokuwa hadi akafanikiwa kutoka mle ndani na kuishi nyumbani kwa Mathew
“ Naomi ulifanya kosa kubwa sana kumuamini Mathew na utalijutia kosa hili kwa siku zote za maisha yako.Mathew ni mtu mbaya sana na katili na hafai kuaminiwa hata idogo.kwa nini ulifanya vile lakini? Kwa nini ulimuamini? Kwa nini ulikubali akakundanganya kwamba atakupatia maisha mazuri na ukakubali kumuuza baba yako?
“ Aunt wewe mwenyewe unajua maisha yangu yalivyokuwa.Mara kadhaa Ulikuwa unakuja na baba na kunikuta namna nilivyokuwa ninateseka ndani ya lile jumba.Nimekaa kifungoni mle ndani kwa zaidi ya miaka minne na nimechoka .Nahitaji kuwa huru.Nimeteseka vya kutosha .Baba amenitesa mno na siwezi kuvumilia tena”akasema Naomi
“ Naomi unafahamu lakini athari za hiki ulichokifanya?akauliza Rose
“ I dont care aunt.Ninachohitaji ni mimi kuwa huru basi.Nimeteseka vya kutosha na siwezi tena kuendelea kuteseka.Aunt ninaomba uniache huru mimi niende zangu.Sitaki maswali zaidi” akasema Naomi
“ Naomi sikiliza.watu uliowaamini kwamba watakusadia si watu wazuri hata kidogo na hawana lengo wala nia ya kukusaidia,Unafahamu kwamba baba yako ameuawa?
“ Ameuawa? Naomi akashangaa
“Ndiyo kwani Mathew hajakueleza?
“ hapana hajaniambia chochote kuhusiana na baba yangu kuuawa”
“ Hawezi kukueleza kwa sababu ndiye aliyemuua baba yako.Baada ya kupata kile alichokuwa anakihitaji toka kwake alimpiga risasi humu humu ndani mwangu akamuua.Ndiyo maanan nilikuuliza awali kama unafahamu athari za hicho ulichokifanya..Baba yako amefariki dunia na hujui hata kinachoendelea.Masikini Naomi”akasema Rose.Naomi akamtazama Rose halafu akainua mikono na macho juu na kusema
“ Ouh ahsante Mungu.Ahsante kwa kumuondoa huyu mtu huku duniani.Hatimaye shetani karejea kuzimu”akasema Naomi na kumkasirisha sana Rose ambaye alimsogelea na kumnasa kibao kikali
“ Baba yako ameuawa na wewe unafurahia? Wewe ni mtoto wa namna gani? Nina mashaka kama akili yako iko sawasawa” akasema Rosemary kwa hasira
“ Akili yangu haiko sawasawa,kwani aliyeiharibu ni huyo huyo ambaye ambaye wewekwako unamuona ana thamani kubwa kwa sababu alikuwa mshirika wako katika biashara zenu za haramu.Ameniharibu kwa kuniingiza katika matumizi ya unga wa kulevya ,ndoto zangu zote za maisha zimepotea maisha yangu yote hayana muelekeo tena,unadhani nitampenda mtu kama huyo? Ninamsifu Mathew kwa kumuua na kama angechelewa ningemuua hata mimi mwenyewe.Mathew ni shujaa na anastahili pongezi kwa kitu alichokifanya cha kishujaa.Ninamchukia sana baba yangu na ninamuomba huko aliko Mungu amtupe katika moto.”akasema Naomi na kuzidi kumchafua Rose
“ Jaji na Aunt Anitha wako wapi? Jana tulipakiwa katika gari wote.Umewapeleka wapi? ” Akauliza Naomi
“ Naomi umenisikitisha sana .Nilikupenda sana kama binti yangu lakini leo umenisikitisha sana .Sina hakika kama kweli wewe ni mtoto wa Henry.”
“ Aunt Rose wewe na baba hamtofautiani na ndiyo maana mkawa wapenzi.Ninaomba unifungue humu nikamzike huyu anayeitwa baba yangu kisha niendelee na maisha yangu,.nahitaji pia kuonana na mathew nimpongeze kwa kitendo alichokifanya cha kumuua baba yangu."Akasema Naomi.Rose akamtazama kwa hasira halafu akamgeukia Fernando
“ Fernando let’s get out of here.Naomi utaendelea kukaa ndani ya chumba hiki na hutatoka kamwe mpaka hapo akili yako itakapokaa sawa”akasema Rose.Fernando akamfungulia mlango wakatoka mle ndani na kumuacha Naomi akipiga ukele mkubwa akitaka aachiwe huru.
“ dah ! nahisi nimeishiwa nguvu Fernando.Sikutegemea kabisa kama msichana Yule tuliyemchukua kule kwa Mathew ni Naomi. Huyu Mathew ni anapaswa kutafutwa haraka sana kwa kila namna anaonekana ni mtu anayenifahamu vyema.Alifahamu kwamba kuingia hapa nyumbani kwangu kuna ugumu kwa hiyo akaamua kumtumia Henry na ili kumpata henr ilimlazimu kumtumia binti yake Naomi.Dah ! huyu kijana ameniogopesha .”
“ Usijali Madam tutamtafuta huyu Mathew kwa kila namna tutakavyoweza na ninakuhakikishia kwamba tutampata tu.” Akasema Fernando.
Rose akarejea chumbani kwake na kuketi sofani akitafakari.
“ Kwa nini kijana mdogo kama huyu Mathew anataka kuninyima usingizi? Lakini hawezi kushindana na mimi kamwe.Nitamsaka kwa namna yoyote hadi nitampata tu. Nataka kabla ya kuanza kwa harakati zangu za urais niwe nimemtia mikononi huyu kijana na kumnyamazisha kimya kimya.Ni mtu ambaye anafahamu mambo yangu mengi sana na endapo nisipofanya jitihada za kumsaka anaweza akaniharibia kila kitu..lazima ndoto yangu itimie na ili kuitimiza sihitaji vikwazo vyovyote njiani.Nitakiondoa kila kikwazokitakachokuja mbele yangu na kikwazo cha kwanza ni huyu kijana Mathew.Atanitambua mimi ndiye Rosemary Mkozumi.!!akawaza Rosemary na kustuliwa na Celline katibu wake aliyeingia ghafla pale sebuleni.
“ celline siku nyingine ukiingia uwe unabisha hodi ,umenistua sana nilikuwa mbali kimawazo”akasema Rose
“ samahani madam.”akajibu Celline huku akitabasamu
“ madam nimekuja kukutaarifu kwamba lile zoezi limekamilika na mpaka sasa hivi tayari waandishi wa habari wamekwisha anza kuwasili.Kila kitu kitakwenda kama vile ulivyoagiza .Waandishi toka vyombo vyote vikubwa vya habari watakuwepo.kwa hiyo ninaomba sasa uingie ndani na uanze kujiandaa kwa ajili ya kuongea na waandishi wa habari.”akasema Cellne
“ Good Job celline.halafu bado kuna jambo moja ninataka ulifane.Ninataka niwasiliane na Dr Kigomba Yule katibu wa rais.” Akasema Rose
“ Sawa madam ngoja nimtafute simuni halafu nitakupa uongee naye” akasema Celline na kumsaidia Rosemary kunyanyuka akaelekea chumbani kwa ajili ya kujiandaa kuongea na waandishio wa habari
TUKUTANE SEHEMU IJAYO……