Peniela (Story ya kijasusi)

Peniela (Story ya kijasusi)

PENIELA
SEASON 1
SEHEMU YA 26
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Mathew akachukua simu yake na mara picha ya Michael Jr akiwa ndani ya gari ikatokea,akampatia Dr Michael ile simu.Alistuka sana alipoiona sura ya mwanae.Mwili ukamtetemeka.
“ Huyu ni mtoto wangu Michael” akasema
“ Ndiyo ni mtoto wako lakini kwa sasa tunaye sisi “
“ Mnaye ninyi? Kivipi mko naye ninyi wakati yuko shule? Ninyi ni akina nani? Akaulzia Dr Michael kwa wasi wasi mwingi
“ Dr Michael mwanao tumemtoa shuleni,yuko nasi .Hatuna lengo baya na mwanao kama utatupa ushirikiano tunaoutaka” akasema Mathew
“ Mbona sikuelewi.Mwanangu yuko wapi? Akasema Dr Michael kwa hamaki na kutaka kuinuka
“ Shhhh..kaa hapo hapo ulipo na tafadhali usipaaze sauti.Ukitaka mwanao aendelee kuwa hai tafadhali fuata kile ninachokuelekeza kufanya” akasema Mathew kwa ukali
“ Ok Ok..niambie unataka nini? Tafadhali naomba msimuumize mwanangu wala kumfanya kitu chochote kibaya.Niko tayari kufanya unachokitaka” akasema Dr Michael kwa wasi wasi
“ Nataka unipeleke chumba PV2 – 78” akasema Mathew.Dr Michael macho yakamtoka pima.Alistuka mno.Midomo ikabaki ikimcheza.
ENDELEA…………………
Dr Michael alimuangalia Mathew kwa uoga mkubwa.
“ Unataka nikupeleke PV2 – 78? Akauliza
“ Ndiyo nataka unipeleke huko” akajibu Mathew.Dr Michael akamtazama kwa macho makali na kuuliza
“ Wewe ni nani? Unataka kwenda kufanya nini kule wakati si daktari?
“ Dr Michael naomba tusiendelee kupoteza wakati.Nimesema nipeleke PV2 – 78..!! Mathew akasema kwa ukali huku amemuelekezea Dr Mathew bastora.Dr Mathew akaogopa sana ,akamtazama Mathew machoni na kugundua hakuwa akihitaji masihara.Akajikaza na kusema
“ Samahani ndugu yangu ,naomba usikasirike na tunaweza tuaongea bila kunielekeza hiyo silaha mkononi.Mnaye mwanangu kwa hiyo sina ujanja tena nitafanya kila mtakachoniamuru kufanya kwa ajili ya kumuokoa .Nitakupekeka huko unakotaka lakini naomba unifahamishe mambo machache.” Akasema Dr Michael
“ Mambo gani unayohitaji kufahamu Dr Michael?
“ Ninahitaji kufahamu kuhusiana na mgonjwa aliyelazwa katika chumba unachohitaji nikupeleke kwa sababu sina mahala ninapoweza kwenda kuuliza chochote kuhusiana na mgonjwa yule.Mambo yanayotendeka mle si ya kawaida.”
“ Kwa nini unasema hivyo? Akauliza Mathew
“ Kuna mambo yanayoendelea yasiyo ya kawaida kuhusiana na Yule mgonjwa.Ni mgonjwa anayeonekana kufichwa fichwa sana na hata ugonjwa wake unatibiwa kwa siri.Matibabu yake ni ya siri na nilipewa jukumu la kumuhudumia mgonjwa Yule kwa sharti maalum kwamba mtu yeyote asifahamu kinachoendelea kuhusiana na ugonjwa wake .Katika chumba kile si rahisi kwa mtu ambaye si daktari au hafahamiki na vijana wanaomlinda mtu Yule kuingia ndani ya kile chumba.Kuna vijana wanaomlinda kwa saa ishirini na nne.Nimewachunguza vizuri sana wale vijana wana vifaa maalum vya mawasiliano na wanatembea na bastora.Naomba unieleze mtu Yule ni nani? Ni kiongozi wa serikali? Nina wasi wasi pengine ninawea kuwa ninamuhudumia mtu hatari bila kujua” Akaulzia Dr Michael
“ Dr Michael swali lako kwa sasa ni gumu kulijibu .Naomba tusiendelee kupoteza wakati nipeleke mara moja mahala ninakotaka unipeleke.” Akasema Mathew.Dr Michael akavuta pumzi ndefu na kumuangalia Mathew kwa macho makali akasema
“ Mmemteka mwanangu na kwa sasa umenielekezea silaha huku ukiniamuru nifanye unavyotaka .Naomba ufahamu kwamba mgonjwa Yule yuko chini yangu na nilikabidhiwa kwa sharti kwamba chochote kitakachomtokea kitakuwa ni juu yangu kwa hiyo nina haki ya kufahamu.Kama una jibu la swali langu tafadhali ninaomba unipatie kwa sababu hakuna mahala ninakoweza kuuliza na kupata majibu kuusiana na mgonjwa Yule.Nina mashaka mno na maisha yangu yanaweza kuwa hatarini kutokana na mazingira yaliyomzunguka Yule mgonjwa na endapo nikifanya hata kosa moja ninaweza kujikuta katika hatari kubwa.” Akasema Dr Michael,Mathew akamtazama na kusema
“ Nitakueleza kila kitu lakini kwanza nipeleke katika chumba hicho”
“ Ninaogopa sana endapo wale vijana wanaopeana zamu kumlinda Yule mgonjwa watagundua kwamba wewe si daktari,nitakuwa nimejitafutia matatizo mimi mwenyewe na wanaweza wakanifanyia kitu kibaya”
“ Dr Michael hii ni kauli yangu ya mwisho Naomba unipeleke katika chumba hicho haraka.Ninafahamu kwamba siwezi kuingia kule bila ya wewe na ndiyo maana nimekuja hapa.Usinilzimishe nitumie nguvu.Kumbuka tunaye mwanao na kauli yangu moja tu mwanao hutamuona tena.Kwa hiyo naomba tuachane na mabishano na ufanye kile ninachokitaka ukifanye !! akafoka Mathew..Dr Michael hakutaka tena mabishano akafungua kabati lake na kumpatia Mathew koti jeupe
“ Vaa koti hili uonekane kama daktari.Vijana wale hawawezi kukuruhusu uingie kama wakigundua wewe si daktari.Kitu kingine ni kwamba hautakiwi uingie na silaha mle ndani kwani kabla ya kuniruhusu nianze kumtibu mgonjwa wao huwa wananikagua kwanza na chombo maalum kuhakisha kwamba sina silaha ya aina yoyote ile na hata dawa ninazompatia huwa wanazikagua kama zina sumu au kitu chochote cha hatari.Ndiyo maana nina maswali mengi sana kuhusiana na mgonjwa Yule ni nani? Akauliza Dr Michael.Mathew hakumjibu kitu akavaa koti lile akaonekana kama daktari halisi
“ Ok twende unipeleke , na tafadhali usijaribu kluonyesha dalili zozote kama nimekulazimisha kitu.Nataka watu watuone kama ni watu tunaofanya kazi pamoja.Nakukumbusha tena kosa moja tu na mwanao hutamuona tena” akaamuru Mathew .Dr Mathew hakujibu kitu akafungua mlango na kutoka Mathew akamfuata
“ We’re on move” Mathew akawataarifu akina Anitha
“ Ok Mathew ,tunakufuatilia kwa karibu sana,mpaka sasa hatujaona bado hatari yoyote” akasema Anitha
Hakuna aliyeweza kuhisi chochote kilichokuwa kinaendelea baina ya Dr Michael na Mathew.Walionekana kama ni madaktari waliokuwa katika shughuli zao za kawaida.Walitembea kwa haraka hadi walipolifikia jengo ilimo wadi PV2 – 78
“ Tunaingia ndani ya jengo la wadi” akasema Mathew akiwapa taarifa wenzake.Walipanda lifti hadi ghorofa ya nne wakashuka na kuelekea moja kwa moja chumba PV2 – 78.Dr Michael alionekana wazi kuwa na wasi wasi mwingi sana.Mathew yeye hakuwa na wasi wasi sana na alikwisha jiandaa kwa lolote
Waliufikia mlango wa chumba PV2 – 78 wakasimama.Dr Michael akasita kidogo.Mathew akamkata jicho kali Dr Michael akaogopa na kugonga mlango mara tatu.Sekunde zilikatika bila ya mlango kufunguliwa akagonga tena na safari hii pia hakukuwa na majibu yoyote.Hakuna mtu aliyejitokeza kuufungua mlango.
“ Hii si kawaida yao.Siku zote ninapogonga mara tatu hunifungulia mlango ,sielewi leo nini kimetokea” akasema Dr Michael kwa wasi wasi
“ Gonga tena” akasema Mathew na Dr Michael akafuata maelekezo akagonga tena lakini bado hakukuwa na majibu.Kengele ya hatari ikagonga kichwani kwa Mathew,akaupeleka mkono ilipo bastora yake na kuishika.Akamwambia Dr Michael akinyonge kitasa na kuufungua mlango.Taratibu na kwa uoga mwingi akakinyonga kitasa na mlango ukafunguka wakaingia ndani.Dr Michael alipatwa na mshangao wa mwaka,alihisi miguu ikimuisha nguvu.Kitu cha ajabu kilikuwa kimetokea.John Mwaulaya hakuwepo mle chumbani.Chumba kilikuwa kitupu.
************
Kila mtu katika ofisi ile ya wanasheria aliiona furaha aliyokuwa nayo Jason.Toka amefika ofisini alikuwa mchangamfu sana na uso wake ulitawaliwa na tabasamu muda wote.Alisalimiana na kila mtu kwa furaha na utani mwingi kitu ambacho hakikuwa kawaida yake kwani siku zote Jason huwa ni mtu mwenye pilika pilika nyingi hivyo hakuwa akitaniana na wenzake.
Aliingia ofisini kwake ,akavua koti halafu akalegeza tai na kujimiminia mvinyo kidogo katika glasi akanywa na kukaa juu ya meza.Ni picha moja tu iliyokuwa imekitawala kichwa chake kwa wakati huo.Picha ya msichana mrefu wastani ,mwenye umbo la kuvutia na tabasamu la kimalaika,iliufanya uso wake usikaukiwe na tabasamu
“ peniela..!!..” akasema kwa sauti ndogo halafu akamalizia mvinyo katika glasi
“ Bado siamini kama ndoto yangu ya siku nyingi imetimia.Peniela alikuwa akilini mwangu kwa muda mrefu sana.Toka nilipoonana naye tukafahamiana nilianza kumpenda.Moyo wangu umekuwa ukiugulia ni lini nitampata malaika Yule lakini hatimaye sasa ndoto imekuwa kweli.Peniela ana kila kitu ninachokihitaji kwa mwanamke wa maisha yangu.” Akawaza halafu akainuka na kwenda kuketi kitini,bado mawazo yakiendelea kumuandama
“ Nakiri katika maisha yangu sijawahi kukutana na mwanamke aliyenipa raha na kuufanya moyo wangu uwe na furaha kama Peniela.Anayafahamu mapenzi,anajua mwanaume anahitaji nini,.Ouh gosh ! usiku wa jana ni usiku wa kihistoria kwangu .Nilijivinjari nitakavyo na Peniela mwanamke asiyeisha hamu.Kila baada ya mzunguko nilijikuta nikihitaji tena na tena.Dah !..sintausahau usiku ule” akaendelea kuwaza
Picha ya mambo waliyoyafanya na Penny usiku ikamjia kichwani na mara akahisi ikulu imeanza kukasirika na kufura .Mwili wote ulikuwa unamsisimka.
“ Peniela amekiteka kichwa changu.Akili yangu yote inamuwaza yeye tu.Sina hamu ya kufanya chochote leo,nahitaji kuwa naye tu karibu.Natamani muda huu angekuwa mikononi mwangu nikimbembeleza kama mtoto mdogo,huku nikiisikia miguno yake.Sauti yake laini anapolalama kwa raha inanichanganya mno.Natamani msisimko ule ninaoupata pale anapozigusisha chuchu zake kifuani kwangu.Peniela yuko tofauti na wanawake wengine wote,ana mvuto wa ajabu mno na amebarikiwa vitu vya kipekee ambavyo ni vigumu hata kuvielezea.Kitu kingine kinachonipa furaha ni kwamba hata yeye mwenyewe ameonekana kuwa na hisia kwangu.Nalisubiri kwa hamu sana jibu lake.Nina hakika hataweza kusema hapana.Kuna kila dalili kwamba mimi na yeye tuliumbwa tuwe pamoja .Ni kwa maongozi ya Mungu tumekutana .Ngoja kwanza nimpigie simu “ akachukua simu na kumpigia .Simu ikaita na kukatika bila kupokelewa,akapiga tena na safari hii ikapokewa
“ Hallow Jason” Sauti laini ya Penny iliyoonyesha uchovu ikasikika
“ Hallow my angel Peniela how are you? Akauliza Jason
“ I’m ok Jason.How are you?
“ I’m ok Penny.Umelala?
“ Nilikuwa nimelala .Mwili umechoka sana.Shughuli ya jana haikuwa ndogo” akasema Penny kwa sauti iliyojaa uchovu
“ Pole sana Penny
“ Pole ya nini Jason?
“ Kwa uchovu unaousikia”
Penny akacheka kidogo na kusema
“ You don’t know how much I miss you Jason.Sijawahi kuwa na usiku mzuri kama wa jana.Naomba nikiri kwamba sijawahi kukutana na mwanaume kama wewe.Nakupigia saluti Jason wewe ni wa kipekee kabisa.Mwanamke yeyote Yule ambaye utamgusa hatakubali kamwe kukuachia kama vile ambavyo mimi sitaki kukuacha. Natamani niwe nawe kila wakati.Natamani nikichezee kifua chako ,natamani nipapaswe na mikonoyako yenye nguvu” akasema Penny.Maneno yale ya Penny yakazidi kumpandisha mzuka Jason na ikulu yake nayo ikaonekana kuzidi kuchachamaa.Akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Penny maneno matamu uliyoniambia nayarudisha tena kwako.Wewe ni wa kipekee kabisa.Hakuna kama wewe katika hii dunia.Ni vigumu mno kuielezea raha niliyoipata jana kwa kuwa pembeni ya malaika kama wewe ,natamani usiku ule ujirudie tena na tena “
“ Usihofu Jason.Hata mimi natamani iwe hivyo.Hata mimi nakutamani sana.Naomba uje tena kwangu usiku wa leo.Please don’t say No Jason” akasema Penny .Uso wa Jason ukachanua kwa tabasamu pana
“ Peniela ,Kwako wewe ulimi wangu hauwezi kutamka neno hapana.Dakika nitakayotamka neno hilo nitakuwa nimelaaniwa.Kwako kila utakachoniambia nitakuwa na jibu moja tu la Ndiyo.Nitakuwa na matatizo ya akili endapo nitakataa kuupitisha usiku wangu nikiwa na malaika kama wewe.Nitafika Penny ,si leo tu bali kila mara utakaponihitaji”
“ Nafurahi sana kusikia kauli hiyo Jason.Ndiyo maana nikakwambia kwamba katika dunia hii hakuna mwanaume wa kulinganishwa na wewe.Nitakusubiri kuanzia mida ya saa tatu.Ukifika hauna haja ya kugonga geti litakuwa wazi,pita ndani moja kwa moja”
“ Ahsante sana Penny.Ahsante sana malaika wangu.Nitafika mida hiyo usijali” akasema Jason
“ Ahsante Jason.Kwa sasa ngoja nipumzike tutaonana baadae”
“ Penny naomba usikate simu kwanza..!! Akasema Jason
“ Unasemaje Jason?
“ Nataka tu kukukumbusha kwamba ninakupenda sana kuliko chochote katika hii dunia”
“ Nafurahi kusikia hivyo” akajibu Penny na kukata simu
Hata baada ya kumaliza kuongea na Peniela simuni ,bado uso wa Jason uliendelea kupambwa na tabasamu zito sana.
“ Nilikuwa nikisikia kwamba kuna nyakati mapenzi yanaweza kukupa uendawazimu,nahisi hata mimi ninaelekea huko.Nina haki ya kuchanganyikiwa kwa mwanamke kama Peniela.Usiku wa leo nitampeleka tena katika sayari nyingine.Dah sipati picha namna itakavyokuwa usiku wa leo” akawaza huku akiinuka na kuvaa koti lake
“ Ninaanza kuwa na matumaini kwamba hata Peniela naye ananihitaji sana.Nina hakika hata jibu atakalonipa ni zuri kwani angekuwa hana hisia zozote kwangu basi asingenikubalia kirahisi namna hii” akawaza Jason huku akitoka ofisini kwake
*********
Baada ya kutoka nyumbani kwa Peniela Jaji Elibariki akaelekea nyumbani kwake kubadili nguo.Kichwa chake kilija mawazo mengi sana kuhusiana na kile alichokifanya na Penny
“ Mmhh ! sikujua kama Peniala ni msichana mtundu kiasi kile.Aliponipigia simu nilidhani ana tatizo kubwa sana lakini kumbe alikuwa na lake jambo “ akawaza huku akitabasamu
“ Nilihisi kuchanganyikiwa pale alipofungua mlango na kuingia bafuni.Mtoto ameumbika Yule.Kila nikiikumbuka picha ile mwili wote unanisisimka. Inaonekana upweke unamsumbua Penny,nitajitahidi kwa kadiri niwezavyo niweze kumuweka karibu na kumliwaza.Anahitaji faraja na hapa amefika.Kwa sasa Flaviana hataniumiza kichwa tena kwani tayari nina sehemu ya kupata kitulizo.” Akaendelea kuwaza.
Alifika nyumbani kwake na kufululiza moja kwa moja chumbani akabadili nguo haraka haraka
“Sikutegemea hata siku moja kama nitakuja kuisaliti ndoa yangu.Pamoja na misuko suko mingi ambayo tumeipata ndani ya ndoa yangu lakini nimesimama imara na hata mara moja sijawahi kutoka nje ya ndoa.Kwa mara ya kwanza nimeshindwa kuwa jasiri wa kukitetea kiapo changu cha ndoa mbele ya Peniela.Nahisi huyu mwanamke anaweza kuwa na dawa Fulani kwa sababu sijawahi kuchanganywa kichwa changu na mtoto wa kike kama inavyonitokea sasa. Nahisi kuanza kuchanganyikiwa na mambo aliyonifanyia Penny leo.Hata mke wangu hajawahi kunifanyia mambo kama yale na ndiyo maana Penny amekitawala kichwa changu.Ninaapa nitafanya kila ninachoweza kuhakikisha kwamba Penny anakuwa ni mwanamke mwenye furaha sana .Nitampatia kila anachokihitaji na kwa kuanzia nitafanya kila linalowezekana kulisafisha jina lake kutokana na tuhuma zile za mauaji.Nitahakikisha aliyefanya mauaji yale ya Edson na kumbambikia Peniela kesi ile anapatikana na jina la Penny linasafishwa.” Jaji Elibariki akastushwa na mlio wa simu.Alikuwa ni mke wake Flaviana.Akabonyeza kitufe cha kupokelea
“ Hallo Flaviana”
“ Hallo Eli,uko wapi? Ninakutafuta hapa sikuoni na simu yako imekuwa ikiita bila kupokelewa.”Akauliza Flaviana
“ Nimekuja nyumbani mara moja kubadili nguo.” Akajibu Elibariki
“ Ok Eli ukifika naomba unitafute kuna jambo ninahitaji kuongea nawe la muhimu sana”
“ Sawa Flaviana ninakuja sasa hivi” akasema Mathew na kukata simu moja kwa moja akapanda gari lake na kuelekea msibani.Baada ya kuwasili akamtafuta mkewe wakajitenga pembeni kidogo mahala kusikokuwa na watu
“ Eli kuna jambo ambalo nataka unisaidie” akasema Flaviana
“ Jambo gani Flaviana?
“ Ni kuhusu kilichomuua mama.Mpaka sasa hivi hakuna kitu kilichowekwa wazi nini kilimuua mama.Hata sisi watoto wake hatufahamu kitu gani kilimuua ghafla namna ile.”
“ Baba yako anasemaje kuhusu hilo? Mmekwisha muuliza kma kuna taarifa yoyote aliyoipokea ? Akauliza jaji Elibariki
“ Baba hajasema chochote mpaka sasa. Kuna daktari mmoja katika hospitali ile ya jeshi ambaye ninafahamiana naye nilimpigia simu na kumuuliza kuhusiana na uchunguzi wa kifo cha mama alinipa jibu la kushangaza sana.”
“ Alisemaje?
“ Alisema kwamba wakiwa katika harakati za kufanya uchunguzi wa kifo cha mama walipokea simu kwamba wasiendelee na kufanya uchunguzi huo”
“ What ?!! Jaji Elibariki akashangaa
“ Amri hiyo walipewa na nani?
“ Sifahamu Eli,sifahamu nani aliyewapa amri hiyo na kwa nini walifanya hivyo.Daktari huyo hakuwa tayari kusema ni nani aliyewapa taarifa hiyo ya kutokuendelea na uchunguzi wa kifo cha mama”
Jaji Elibariki akainama akazama katika mawazo
“ Unajua hainiingii akilini kwamba kwa mtu mkubwa kama mke wa rais afariki ghafla halafu kusifanyike uchunguzi wowote wa kuhusiana na kifo chake.”
“ Hata mimi nimeshindwa kuelewa Eli na ndiyo maana nikakuita hapa ili unisaidie”
“ Unataja nifanye nini?
“ Naomba unisaidie kufahamu nini kilimuua mama”
“ What ? akauliza Jaji Elibariki kwa mshangao
“ Naomba unisadie kuupata ukweli wa nini kilisababisha kifo cha mama”
“ Flaviana nitawezaje kufanya hivyo wakati mimi si daktari?
“ I don’t know Eli but find a way.I know you must have a way to find the truth.”
Jaji Elibariki alihisi kama kitu kizito kimegonga kichwa chake.Flaviana akauona mstuko alioupata mumewe akamshika mkono na kusema
“ Elibariki mume wangu najua hili si suala rahisi lakini sina mwingine ambaye anaweza akanisaidia katika hili zaidi yako.Please help me.Nahitaji sana kufahamu nini kilimuua mama.Sielewi ni kwa nini moyo wangu unajikuta ukitaka kufahamu sababu ya kifo cha mama.Elibariki najua wewe una njia nyingi za kuweza kufanya ukaipata.You have many connections so please my love do it for me.Najua nimekukosea sana mambo mengi lakini tafadhali naomba tofauti zetu tuziweke kando kwa sasa na tulishughulikie suala hili.Ni muhimu sana kwangu ” Akasema Flaviana.Jaji Elibariki akainama akawaza halafu akainua kichwa na kusema
“ Ok my love.I’ll do it for you”
Wakakumbatiana na Flaviana akaondoka.Kichwa cha Jaji Elibariki kilikuwa kizito kama kimefungwa jiwe.Alihisi kuchanganyikiwa,hakujua angewezaje kuipata ripoti ile aliyoitaka mke wake.Alibaki ameegemea mti kwa dakika kadhaa akiwaza
“ How am I going to do it? Nahisi kuchanganyikiwa sielewi nitafanya vipi kufahamu nini kilimuua Dr Flora.”
Kwa takribani dakika kumi alikuwa amezama katika mawazo na mwishowe akachukua simu yake na kuzitafuta namba za simu za Mathew
“ I need Mathew.” Akasema na kumpigia.Simu ikaita bila kupokelewa.Akapiga tena lakini bado simu haikupokelewa ,akahisi kuchanganyikiwa
TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………………
 
Kitu kimenoga ase, mkuu tunakuomba utundoshee
 
Back
Top Bottom