Peniela (Story ya kijasusi)

Peniela (Story ya kijasusi)

SEASON 3

SEHEMU YA 10


MTUNZI 😛ATRICK.CK

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Nimefanikiwa kuonana tena na John na katika dakika zangu za mwisho nimejikuta nikishindwa kutekeleza mpango wangu wa kulipiza kisasi.Hali yake nilivyoiona jana ilikuwa mbaya na mimi mwenyewe nikamuonea huruma .Alikiri kosa lake na nikakubali kumsamehe.John alinieleza mambo makubwa na mazito sana na ninapaswa kumshukuru sana kwa kunichagua mimi niyafahamu mambo yale.Amekufa na siri nyingi kubwa kubwa na laiti kama ningepata muda wa kutosha wa kuongea naye angeweza kunieleza mambo mengi makubwa zaidi lakini ninashukuru hata kwa hili alilonieleza.Kitu kingine kizuri ni kwamba katika dakika za mwisho za uhai wake alipata huduma ya kiroho na kama maandiko yanavyosema hata kama tukiwa na dhambi nyingi kiasi gani tukifanya toba ya dhati Mungu hutuondolea dhambi zote na kutufanya wapya tena.Mungu amrehemu na ampe pumziko la milele” akawaza Mathew wakati akikaribia sana kufika katika baa ya Eva



ENDELEA…………………………….



Mathew aliwasili katika baa ya Eva.Watu hawakuwa wengi sana.Wengi wa waliokuwepo hapa mida hii walikuwa wakipata supu,kwani sifa nyingine ya baa hii ni kuwa na supu nzuri .Mathew aksshuka garini na moja kwa moja akelekea katika ofisi ya Eva,akagonga mlango , Eva akamruhusu aingie.
“ Hallow Eva” akasema Mathew

“ Karibu sana Mathew.” Akasema Eva
“ Ahsante Eva..Niambie kuna kitu chochote ulichokipata? akauliza Mathew huku akivuta kiti na kuketi.Eva akasubiri hadi Mathew alipoketi na kutulia kisha akasema
“ Ulipoondoka niliacha shughuli zote na kulishughulikia lile suala uliloniomba.Kuna jambo nimeligunuda ambalo linaweza kuwezesha kupata nafasi ya kuingia ndani ya nyumba ya Rosemary na ukafanya uchunguzi wako.” Akasema Eva
“ Ahsante sana Eva.Umegundua nini? akaulzia Mathew kwa shauku ya kutaka kulifahamu jambo hilo.
“ Baada ya kuachana na Mzee Deus Mkozumi,Rosemary aliingia katika mahusiano ya kimapenzi na mmoja wa aliyewahi kuwa waziri wa kilimo katika serikali ya Deus Mkozumi anaitwa Henry Alois Chibuma.” Akanyamaza kidogo kisha akaendelea
“ Henry Chibuma ni mmoja kati ya waliokuwa mawaziri vijana sana katika serikali iliyopita na anasemekana kuwa na utrajiri mkubwa.Katika uchunguzi wangu nimegundua kwamba mke wa ndoa wa henry alikwisha farikiki dunia na ana mtoto wake mmoja tu aitwaye Naomi.Huyu ni muathirika wa dawa za kulevya na kwa sasa anafungiwa ndani ya jumba kubwa lenye ulinzi mkali ili asiweze kutoka wala kuonekana.Taarifa zinasema kwamba Henry ndiye chanzo cha mwanae kuathirika na dawa hizo kwani yeye pia alikuwa ni muingizaji na mtumiaji mkubwa wa dawa hizo .Nina hakika tukimpata Naomi tukaongea naye tunaweza kufahamu mambo mengi sana na hii inaweza ikawa ni njia rahisi ya kumpata Henry atakayetupeleka kwa Rosemary..” Akasema Eva.
“ Unasema waziri Henry naye ni muingizaji na mtumiaji wa dawa za kulevya? Akauliza Mathew
“ Ni kweli Mathew.Henry ni muingizaji mkubwa sana wa dawa za kulevya hapa nchini lakini nakuwa vigumu kumtia nguvuni kutokana na mtandao walio nao.Ndiyo maana nilikutahadharisha toka awali kwamba watu hawa ni hatari sana.Hata wakati akiwa wazidi alikuwa akijihusisha na biashara hii” akasema Eva
“ Huyu Naomi umeweza kuipata historia yake japo kwa ufupi? Akauliza Mathew
“ Ndiyo nilifanikwa kupata historia yake.Ni binti wa miaka kumi na tisa sasa na inasemekana alishindwa kuendelea na masomo kutokana na kuathirika na dawa hizo.Pili rafiki yake wa kiume alipigwa risasi na watu wasiojulikana.Inaaminika aliuawa kwa amri ya Henry. Naomi anaishi maisha ya upweke mkubwa ndaniya jumba hilo alimofungiwa.Nina hakika tukienda kuonana naye atatusikia na atakubali kushirikiana nasi.Nimefanikiwa kupata hadi jina la Daktari anayemtibu anaitwa Dr Marina.Huyu ni daktari toka hospitali kuu ya taifa kitengo cha kuwahudumia waathirika wa dawa za kulevya. ” Akasema Eva.Mathew kama kawaida yake hutumia muda kidogo kutafakari kila jambo kabla ya kufanya maamuzi akainama akatafakari na kusema
“ Sawa Eva twende tukaonane na Naomi.Lakini kabla ya kwenda huko lazima tuhakikishe tumejiandaa vya kutosha kwani kama ulivyosema kuna ulinzi katika jumba hilo.Nina hakika hatutaruhusiwa kuonana na Naomi kwa hiyo tunaweza kulazimika kutumia nguvu.” Akasema Mathew.Naomi akainuka akafungua kasiki lake lililoko ukutani ambalo huhifadhia silaha kwa matumizi ya dharura akamuita Mathew aangalie silaha ambazo zingeweza kuwasaidia.Mathew akachagua silaha na vifaa ambavyo vingeweza kuwasadia halafu bila kupoteza muda wakaingia katika gari la Mathew na safari ya kuelekea kwa Naomi ikaanza.
“ Nadhani sasa umeanza kupata picha ya watu wanaomzunguka Rosemary ni watu wa namna gani.Mtandao wao ni mkubwa na hatari.Henry anajihusisha na biashara nyingi haramu ikiwemo uingizaji wa dawa za kulevya lakini kumtia hatiani inakuwa ni mtihani mgumu kwa sababu wamezishika karibu sekta zote muhimu.Wana watu wao ndani ya jeshi la polisi,hata ndani ya usalama wa taifa kuna watu wao kwa hiyo ni rahisi sana kwao kujua chochote kinachoendelea dhidi yao na wakajihami.Ndiyo maana nilikutahadharisha toka mapema kwamba unatakiwa uwe makini sana unapomfuatilia Rose .” akasema Eva

“ Nimeamni maneno yako Eva,lakini dhumuni kuu la kazi yetu ni kushughulika na watu kama hawa. Hatupaswi kuwaogopa hata kidogo.Lazima tuhakikishe watu kama hawa ambao wanakwenda kinyume na taratibu na sheria za nchi wanafikishwa katika vyombo husika.Endapo tukiogopa kupambana nao siku moja nchi hii itashindwa kukalika kwani itakuwa ikiongozwa na genge la wahuni na wahalifu.Wewe mwenyewe uliniambia kwamba Rosemary anafikiria kuwania urais.Kwa nguvu ya pesa,ushawishi na mtandao mkubwa alio nao akipata nafasi hiyo ya kugombea anaweza akawa rais,sasa hebu pata picha mtu kama Rosemary akiwa rais wa nchi hii nini kitatokea? Hatupaswi hata kidogo kuacha jambo kama hilo likatokea.Lazima tupambane naye kwa kila nguvu na uwezo tulio nao.Binafsi nina roho ngumu kama jiwe na huwa siogopi kitu chochote zaidi ya Mungu pekee” akasema Mathew.Eva akatabasamu na baada ya muda akasema
“ Mathew naomba nikuulize kitu na tafadhali naomba unijibu”

“ Uliza va usijali”
“ Ni jambo gani ambalo unalichunguza?

“ Eva , mimi na wewe tumekuwa karibu kwa muda mrefu sana na kila pale ninapokuwa na tatizo nimekuwa nikikukimbilia wewe kwa msaada.Natamani sana nikueleze nini ninachokichunguza lakini ninaomba unipe muda kidogo ili niliweke vizuri suala hili na kisha nitakueleza kila kitu.” Akasema Mathew

“ Don’t you trust me? Akauliza Eva
“ I do trust you with my life Eva” akasema

“ No you don’t.Kama unegkuwa unaniamini usingesita kunieleza kile unachokichunguza.Mathew ninaweza kuwa na msaada mkubwa sana kwako tofauti na unavyodhani.Au unahisi kwamba ukinieleza jambo hilo ninaweza kuvujisha siri na kuharibu uchunguzi wako? Akauliza Eva
“ Si hivyo Eva.Ninakuamini sana na ndiyo maana nimekwambia kwamba nipe muda kidogo na nitakueleza kila kitu .Naomba ufahamu vile vile kwamba bado ninahitaji sana msaada wako.” Akasema Mathew aliyekuwa makini katika usukani
“ Sawa Mathew..” akajibu Eva kwa shingo upande na safari ikaendelea kimya kimya.Baada ya muda Eva akauliza

“ That woman,Anitha is she your girlfried? Akauliza Eva na kumfanya Mathew atabasamu
“ Kwa nini umeuliza ?
“ Nimehisi tu kwamba anaweza akawa ni mchumba wako kwa namna mnavyopendana.” Akasema Eva na Mathew akatoa kicheko
“ Anitha si mpenzi wangu na wala hatuna mahusiano yoyote mengine zaidi ya kazi.Unaponiona mimi na Anitha tuko mahala basi ujue ni kazi tu inafanyika na hakuna lingine.Mimi ni kazi tu mambo hayo ya mapenzi nilikwisha achana nayo muda mrefu.Toka familia yangu ilipoteketea sitaki tena kuijingiza katika mahusiano mengine.” Akasema Mathew
“ Mathew ni miaka sasa imepita toka litokee tukio lile.Usiendelee kujitesa tafadhali.You have to move on.Au bado una mpango wa kulipa kisasi kwa waliofanya kitendo kile? Do you know them? Akauliza Eva.Mathew akanyamaza kidogo kisha akajibu
“ Ni kweli ni miaka mingi imepita sasa lakini bado picha za tukio lile zinanijia akilini kila siku na ninaona ni kama tukio lile limetokea jana.Nimejitahidi sana kulisahau tukio lile lakini nimeshindwa.Bado linanitesa na nitateseka hadi siku ninaingia kaburini.Kuhusu kulipiza kisasi ni kweli nilikuwa na mpango huo lakini kwa sasa nimeachana nao.Sintolipiza kisasi kwani aliyefanya kitendo kile tayari amekwisha fariki dunia na ni Mungu pekee atakayemuhukumu” akasema Mathew
“ Kwa hiyo ulimfahamu? Ni nani huyo shetani? Akauliza Eva

“ It doesn’t matter for now.Eva kama hutajali naomba tusiendelee kuliongelea suala hilo”

“ Sawa Mathew na samahani kwa kukukumbusha mbali lakini kuhusu kuingia katika mahusiano mengine hili sintaacha kukukumbusha kwani umri unakwenda sana.Promise me you’ll think about that” akasema Eva.Mathew akatabasamu na kusema

“ Ok Eva.I’ll think about it” akajibu Mathew na safari ikaendelea.
Waliwasili katika mtaa lilipo jumba analoishi Naomi.Ni jumba kubwa lililozungushiwa ukuta mkubwa wa rangi nyeupe.Haikuwa rahisi kwa mtu aliyeko nje kuona chochote kilichomo ndani ya jumba lile kutokana na ukuta ule mkubwa.Kilichoonekana ukiwa nje ni bati zuri la rangi ya bluu.
“ Ni hapa” akasema Eva.Mathew akalitazama jumba lile na kupunguza mwendo wa gari na kusimama katika geti.Wakashuka na kubonyeza kengele na mlango mdogo wa geti ukafunguliwa na mtu mmoja aliyevaa mavazi meusi aliyeonekana kushangazwa sana na ujio wa akina Mathew
“ Habari zenu? Akawasalimu

“ Nzuri.Habari za hapa? Wakajibu Mathew na Eva kwa pamoja
“ Niwasaidie nini ? Akauliza Yule jamaa.
“ Sisi ni wanasihi tumetoka katika hospitali ya taifa kitengo cha kuhudumia waathirika wa dawa za kulevya.Tumetumwa hapa na Dr Marina kwa ajili ya kumfabnyia unasihi Naomi.” Akasema Mathew.Yule jamaa akastuka kidogo
“ Ninamfahamu Dr Naomi lakini mbona hakunitaarifu kama kuna watu watakuja hapa leo?Isitoshe huwa anakuja mwenyewe iweje leo atume watu wengine?

“ Una namba zake za simu? Akauliza Mathew

“ Ndiyo ninazo.” Akajibu Yule jamaa
“ mpigie na atakupa maelekezo.” Akasema Mathew na yule jamaa akaingiza mkono mfukoni akatoa simu na kuanza kuzitafuta namba za Dr Marina.Wakati ameiinamia simu yake Mathew akamfanyia ishara Eva na kwa kasi ya umeme Eva akampiga Yule jamaa pigo moja la haraka na kumpeleka chini.Mathew akamuwahi pale chini na kumkaba kabala hadi akapoteza fahamu.Eva akachungulia ndani na hakuona mtu mwingine yeyote.
“ Its clear.No body is here! Akasema Eva kisha Mathew akamvuta Yule jamaa na kumuigiza ndani akamficha katika maua.Akaichukua simu ya yule jamaa kisha wakaelekea katika mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni.Wakagonga lakini hakuna mtu aliyejibu.Wakagonga tena na safari hii mlango ukafunguliwa na msichana mmoja aliyeonekana kama ni mfanyakazi za ndani.Alistuka sana alipowaona akina Mathew akawasalimu kwa uoga.
“ Naomi yuko wapi? Akauliza Mathew
“ Yuko chumbani kwake” akajibu Yule msichana
“ Tupeleke haraka chumbani kwake.” Akasema Mathew kwa ukali na yule msichana akawaongoza hadi katika mlango wa chumba cha Naomi
“ Chumba cha Naomi ni hiki hapa.” Akasema Yule msichana na mara sauti ikasikika toka ndani
“ Chiku unaongea na nani huko ?
Yule msichana akawafanyia akina Mathew ishara kwamba sauti ile ni ya Naomi.
“ Naomi kuna wageni wamekuja kukutembelea.” Akasema Chiku
“ Waambie waondoke.Sihitaji kuonana na mtu yeyote Yule.Nani kawaruhusu waingie humu? Akauliza Naomi kwa ukali toka ndani.Eva akamnong’oneza jambo Chiku akasema
“ Naomi ni watu toka hospitali wanataka kukuona”
“ Nimekwambia waambie waondoke zao.Leo si siku ya tiba” akasema Naomi

“ Eva she’s not going to open” akasema Mathew na kuupiga teke mlango ukafunguka wakaingia ndani.Naomi alistushwa sana na kitendo kile akapiga ukulele mkubwa.Mathew akamfuata na kumtuliza
“ Naomi naomba tafadhali usipige kelele.Hatuko hapa kwa ajili ya kukudhuru.Tuko hapa kwa ajili ya kukusaidia” akasema Mathew.Naomi akawatazama Mathew na Eva halafu akauliza

“ Kwani ninyi ni akina nani?
Mathew akamgeukia Eva aliyekuwa amemshikilia Chiku Yule mtumishi wa ndani

“ Mfungie bafuni huyo” akasema Mathew na Eva akamchukua Chiku akaenda kumfungia katika bafu la Naomi,akamsachi na kuhakikisha hana simu wala kifaa chochote cha mawasiliano .
“ Naomi naomba usituogope tafadhali.Sisi si wanasihi kama tulivyojitambulisha.Sisi ni maafisa toka idara ya usalama wa taifa.Ninaitwa Mathew na Yule dada anaitwa Eva.Tumekuja hapa kuzungumza nawe mambo kadhaa lakini dhumuni kubwa likiwa ni kukusaidia” akasema Mathew

“ Nitaaminije kama unasema kweli? Ninyi si watu wa mtandao wa baba?
“ Hapana sisi si watu wa mtandao baba yako.Tuamini Naomi tuko hapa kwa lengo la kukusaidia.Lakini tutakusaidia endapo na wewe utakuwa tayari kutusadia.” Akasema Mathew
“ Mnataka kunisaidia kivipi? Akauliza Naomi

“ Tunataka kukutoa katika maisha haya unayoishi sasa na kukusadia kuanza maisha mapya na uweze kutimiza ndoto zako za maisha.Naomi tunafahamu kila kitu kuhusu historia yako .Ulikuwa ni msichana mwenye akili sana darasani na ulikuwa na malengo mengi ya maisha yako kwa siku za usoni lakini malengo na ndoto zote za maisha yako zilikatishwa baada ya kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.Tunafahamu ni baba yako ndiye aliyesababisha haya yote yatokee.Tunafahamu anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya . Tunafahamu amekufungia humu ndani na hataki utoke kabisa nje ili watu wafahamu hali yako.Unaishi maisha ya upweke mkubwa humu ndani.Naomi tunataka kukusaidia ili uweze kuachana na maisha haya upate tiba upone na uendelee kutimiza ndoto zako.” Akasema Mathew.Naomi akashindwa kujizuia akaanza kulia.Eva akamfuata akakaa pembeni yake na kumbembeleza.

“ Nyamaza kuliza Naomi.Historia yako inaumiza sana .Tutakusaidia Naomi ..Naomba usiendelee kulia ili tuongee kwani muda wetu ni mfupi sana hapa kwako.” Akasema Eva.Naomi akafuta machozi na kusema

“ Nawaona ninyi ni kama malaika mliokuja kunikomboa.Kwa miaka minne sasa nimekuwa nikiishi kama mfungwa ndani ya jumba hili.Sina hamu tena ya kuendelea kuishi kwani siioni tena thamani yangu.Hakuna mtu anayenipenda tena wala kunijali.Yote hii imesababishwa na mimi kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.” Akasema Naomi huku akiendelea kububujikwa na machozi
“ Ilikuaje ukajiingiza katika matumizi ya dawa hizi za kulevya? Akauliza Mathew.Naomi akamtazama na kusema
“ Ni frank.Huyu ndiye aliyenishawishi mimi kujiingiza katika dawa za kulevya.”
“ Frank ni nani?
“ Alikuwa boyfriend wangu,kwa sasa amekwisha fariki alipigwa risasi.”
“ Pole sana” akasema Eva
“ Haikuwa dhamira ya Frank mimi kujiingiza katika maisha haya ya dawa za kulevya kwani alikuwa ananipenda sana lakini huu ulikuwa ni mpango wa baba niwe hivi.”
“ Mpango wa baba yako? Kivipi? Akauliza Mathew

“ Baba alimtumia Frank aniingize katika matumizi ya dawa za kulevya.Niligundua kwamba baba alikuwa anamtumia Franki katika biashara ile kwa hiyo akamtumia yeye kunishawishi niingie katika matumizi hayo ya dawa za kulevya.”
“ Naomi tunafahamu kwamba baba yako anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya na ni mtumiaji pia lakini hatuelewi ni kwa nini akuingize na wewe katika matumizi haya ya dawa za kulevya wakati anazifahamu athari zake? Akauliza Mathew

“ Ni kwa sababu ninafahamu mambo yake mengi.Ninazifahamu siri zake nyingi.Baba alihusika katika kifo cha mama na nilipoligundua niliumia sana na nilimuweka wazi kwamba lazima nihakikishe ninamfikisha katika vyombo vya sheria.Hapo ndipo ugomvi kati yangu na baba ulipoanza na ndipo alipomtumia Frank kuningiza katka dawa za kulevya ili nichanganyikiwe akili yangu nisiweze kufanya kile nilichokusudia kukifanya.Baada ya kuona nimeathirika vibaya Frank aliumia sana na alikuwa tayari kwenda kutoa siri hii ndipo alipouawa kwa risasi na watu wa baba.Nilichukuliwa na kufungiwa humu ndani na katika miaka yote hii minne sijawahi kutoka kwenda nje ya nyumba hii.Nikitoka humu chumbani ninakaa hapo bustanini na si nje ya hapo. Baba amenitafutia daktari wa kunitibu na ameweka hadi walinzi na hakuna yeyote anayeruhusiwa kuingia ndani humu zaidi ya daktari wangu tu.Ninaishi maisha magumu sana na ndiyo maana ninawaona ninyi ni kama malaika mliokuja kunikomboa kama kweli lengo lenu ni hilo” akasema Naomi

“ Naomi sisi tutakusaidia kwa kila namna tuwezavyo ili uweze kurejea katika maisha yako ya kawaida.”
“ Tafadhali naombeni msiniache humu ndani.Mkiondoka ondokeni na mimi” akasema Naomi
“ usijali Naomi tutaondoka nawe.Lakini kabla ya yote kuna jambo ambalo tunahitaji sana msaada wako.” Akasema Mathdew
“Tunafahamu baba yako anajihusisha na mambo mengi ya haramu ikiwemo na biashara hii ya dawa za kulevya.Tumekuwa tukimfuatilia kwa muda na tumegundua kwamba anao mtandao mkubwa wa watu wanaojishughulisha na mambo mengi ya hatari. Kwa sasa baba yako na mtandao wake wanajihusisha na jambo moja kubwa na la hatari lenye kuhatarisha uhai wa mamilioni ya watu duniani.Tunatafuta namna ya kuweza kumzuia yeye na mtandao wake wasiweze kutekeleza mpango wao huo lakini njia pekee ya kufanya hivyo ni kwa kupitia kwako.” Akasema Mathew
“ NInamfahamu baba yangu .Ana roho ya kishetani.Ni mkatili kupindukia.Yeye ndiye aliyenifanya mimi kuishi maisha ya namna hii.Simpendi na ninatamani kama siku moja ningekuwa na uwezo ningemuua.”akasema kwa uchungu Naomi huku akilia

“ Basi usilie Naomi .Hili tutalimaliza.Tunachokuomba ni ushirikiano wako.Baba yako kwa sasa yuko katika mahusiano ya kimapenzi na mke wa rais mstaafu.nadhani unalifahamu hilo”
“ Ndiyo ninalifahamu hilo na kuna nyakati huwa wanakuja wote kunitazama” akajibu Naomi

“ Basi Yule mama ndiye kiongozi wa mtandao alimo baba yako.Mambo mengi anayoyafanya baba yako yanaratibiwa na Yule mama kwa hiyo tunataka kuingia ndani ya jumba la Yule mama na kufanya uchunguzi lakni mtu pekee anayeweza kutuingiza humo ni baba yako kwa hiyo tunaomba utusaidie tuweze kumpata baba yako”
“ Mnataka niwasaidiaje? Akauliza Naomi

“ Tunataka uwasiliane naye na kumtaka afike hapa nyumbani haraka sana kwamba una tatizo na akisha fika sisi tutamtia mikononi mwetu na atatupeleka katika jumba hilo la Rosemary kufanya uchunguzi wetu.Wewe tutakuchukua na kukupeleka sehemu salama,tutakutafutia tiba na tutakupatia ulinzi na tutakusaidia kwa kila namna tuwezavyo kuhakikisha kwamba unakuwa na maisha mazuri na ya uhuru” akasema Mathew

“ Kwa kweli natamani sana baba yangu akamatwe na afungwe gerezani maisha au ikiwezekana anyongwe kabisa lakini ninashindwa namna ya kuwasaidia.Kwanza mimi na baba yangu hatuna mahusiano mazuri na siwezi kuwasiliana naye kwa sababu sina mawasiliano yoyote humu ndani.Sina simu wala kitu chochote cha kuniwezesha kuwasiliana na watu huko nje.” Akasema Naomi.Mathew akatoa simu ya Yule mlinzi aliyepoteza fahamu

“ Simu hii ya mlinzi wa getini.Wasiliana na baba yako.Tafuta namna ya kumfanya aweze kufika hapa mara moja” akasema Mathew na Naomi akaishika ile simu huku mikono ikimtetemeka akazitafuta namba za baba yake na kupiga



MPANGO WA MATHEW UTAFANIKIWA ?
 
Mjinga sana yule dogo hajakomaa kiakil haoni mwenzake Jaj ametulia Japo anajua penuel anagongwa na raisi Dr.kigomba lakn amekaisha tu angekuwa Jasoni angeenda kutoa taarifa police kwamba raisi anakuja demu wangu
Yaani hii tabia ya kutoa taarifa polisi ndio nilipomuona bado mburura. Kwa mfano mara mwisho wamegombana na Matthew, akasusa akashuka kwenye. Nikasema atakwenda kushtaki tena. Ila sijamsikia kitambo sana
 
PENIELA SEASON 3


SEHEMU YA 11


ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Mnataka niwasaidiaje? Akauliza Naomi

“ Tunataka uwasiliane naye na kumtaka afike hapa nyumbani haraka sana kwamba una tatizo na akisha fika sisi tutamtia mikononi mwetu na atatupeleka katika jumba hilo la Rosemary kufanya uchunguzi wetu.Wewe tutakuchukua na kukupeleka sehemu salama,tutakutafutia tiba na tutakupatia ulinzi na tutakusaidia kwa kila namna tuwezavyo kuhakikisha kwamba unakuwa na maisha mazuri na ya uhuru” akasema Mathew

“ Kwa kweli natamani sana baba yangu akamatwe na afungwe gerezani maisha au ikiwezekana anyongwe kabisa lakini ninashindwa namna ya kuwasaidia.Kwanza mimi na baba yangu hatuna mahusiano mazuri na siwezi kuwasiliana naye kwa sababu sina mawasiliano yoyote humu ndani.Sina simu wala kitu chochote cha kuniwezesha kuwasiliana na watu huko nje.” Akasema Naomi.Mathew akatoa simu ya Yule mlinzi aliyepoteza fahamu

“ Simu hii ya mlinzi wa getini.Wasiliana na baba yako.Tafuta namna ya kumfanya aweze kufika hapa mara moja” akasema Mathew na Naomi akaishika ile simu huku mikono ikimtetemeka akazitafuta namba za baba yake na kupiga


ENDELEA……………………………..


Mathew akamuelekeza abonyeze kitufe kitakachowafanya wote wasikie kile watakachokiogea.Simu ikaita bila kupokelewa ikakatika.Akapiga tena na safari hii ikapokelewa

“ Hallo Francis”ikasema sauti ya upande wa pili

“ Hallow dady ni mimi Naomi” akasema Naomi na kumstua kidogo Henry

“ Naomi kwa nini umechukua simu ya Francis wakati nilikwisha kukanya kutumia simu? Akauliza Henry

“ Dady nimelazimika kumuomba mara moja simu yake niwasiliane nawe.”
“ Ok siku nyingine usirudie tena kuchukua simu ya Francis.Muda wowote kama una tatizo mwambie Francis na yeye ndiye atakayenitafuta .Haya niambie una tatizo gani?
“ dady nina tatzo kubwa nahitaji kukuona mara moja”
“ Una tatizo gani Naomi?
“ Dady siwezi kukueleza katika simu.Naomba uje mara moja “
“ Naomi kwa sasa siwezi kufika nina kazi ya muhimu sana.Nitafika baadae baada ya kumaliza kazi hiyo.kamakuna tatizo kubwa mweleze Francis tafadhali”
“ No Dady ! tafadhali achana na kila ulichonacho na uje mara moja.Siwezi kumweleza Francis matatizo yangu ya ndani .He’s not my father”
“ Naomi kama huwezi kumweleza Francis nieleze basi katika simu nijue una tatizo gani?
“ Dady sijawahi hata siku moja kukuomba ukatishe kazi zako uje unitazame.Leo nina tatizo kubwa na ninaomba uje unisikilze.Just this once can you be a father to me and listen to what I want? .Hakuna mwingine ninayeweza kumweleza tatizo langu zaidi yako” akasema Naomi.Kukawa kimya kidogo halafu Henry akasema

“ Sawa ninakuja sasa hivi.Naomba niongee na Francis” akasema Henry.
“ Francis !!.Francis !!!......Francis…!!!!!!!.akaita Naomi kwa nguvu

“ Dady inaonekana Francis ametoka nje nadhani ameenda kutafuta sigara.Nitamwambia akupigie simu akirejea.”

“ Sawa Naomi.Ninakuja sasa hivi” akasema Henry na kukata simu
“ Good.Umefanya vizuri sana Naomi. Ahsante sana kwa msaada wako huu mkubwa.Endapo jambo hili litafanikiwa basi utakuwa umechangia kuokoa maisha ya watu wengi.” Akasema Mathew

“ Nimefanya mlivyotaka nifanye ni zamu yenu sasa kutimiza kile mlichoniahidi.To get me out of here” akasema Naomi
“ Usihofu Naomi.Utapata kila ulichoahidiwa.Tutakutoa hapa na kukupeleka sehemu salama ambako utaishi na tutakusaidia kutimiza malengo yako” akasema Mathew
“ Wakati tukimsubiri baba yako afike,naomba utueleze kama kuna vitu vingine anavyofanya baba yako ambavyo unaona ni vyema tukavifahamu “ akasema Mathew.naomi akainamana kufuta machozi kisha akasema

“ I hate my father.Ni kwa sababu yake maisha yangu leo hii yameharibika na kufika hapa.I hate him so much.Baba yangu anajihusisha na mambo mengi sana haramu lakini leo hii nitakueleza kuhusu jambo moja.Baba na watu wake wana kiwanda cha kutengeneza pesa bandia.Chini ya jumba lake analoishi kuna kiwanda cha kutengeneza fedha bandia.Niliwahi kunyata siku moja na kuingia ndani yua kiwanda hicho wakati baba hayupo na nilifanikiwa kuchukua video ya kiwanda hicho ambayo ninayo na kuna sehemu nimeificha .Sikujua kama ndani ya kiwanda hicho kuna kamera zilizokuwa zinanichukua picha .Hili ni mojawapo ya mambo yaliyomfanya baba aamue kunifanya hivi.Kuna kitu niliwahi kumuomba na akanikatalia nikamtishia kuvujisha siri zake kwaniushahdi ninao kwamba ana kiwanda cha kutengeneza noti bandia akaogopa sana na kwa kuogopa kwamba siku moja ninaweza kuweka siri zake hadharani akaona njia pekee ya kunizuia nisiweze kufanya hivyo ni kuniharibu kwa dawaza kulevya.” akasema Naomi huku akilia kwa uchungu.Aliwaeleza akina Mathew mambo mengi anayoyafahamu kuhusiana na baba yake.Baada ya kuridhika na maelezo yale ya Naomi,Mathew akamchukua Eva pamoja na Yule msichana wa kazi wakaelekea getini kumsubiri Henry.

“ Ama kweli dunia hii inawatu makatili kupindukia.Yaani unadiriki kumfanya vile mtoto wako wa kumzaa mwenyewe ! akasema Eva kwa uchungu
“ Toobad.But Naomi will be fine.Ametupa msaada mkubwa sana na nitahakikisha anapona na kurejea katika hali yake ya kawaida.” Akasema Mathew
Baada ya dakika ishirini za kusubiri mara ikasikika honi nje ya geti.Mathew akamuelekeza Yule msichana wa kazi achungulie kama ni henryndiye aliyekuwa anapiga honi ile.Msichana yule akachungulia na kuwataarifu kwamba ni Henry.Wakajiweka tayari na kumwambia alifungue geti.Taratibu msichana Yule akalifungua geti na Henry akaingiza gari ndani.Alistushwa kidogonakufunguliwa geti na msichanawa kazi badala ya mlinzi.Akafungua mlango na kushuka akitaka kujua aliko Francis lakini ghafla akajikuta akitazamana na watu wawli waliomuelekezea bastora.Akastuka sana kwani hakuwa amelitegemea tukio kama lile.Haraka haraka Mathew akamuamuru ashuke garini na bila ubishi Henry akashuka garini .Mathew akamuongoza kuelekea ndani.
“ Who are you guys? Mnataka nini kwangu? Nani kawatuma kwangu? Akauliza henry huku akiwa ameinua mikono akielekea ndani.Waliingia sebuleni na Mathew akamuamuru aketi sofani.

“ kwa nini mnanifanyia hivi? Ninyi ni akina nani? Nani kawatuma mnifanyie hivi? Hamuogopi kwa hili mnalolifanya? Anawalipa shilingi ngapialiyewatuma?Akauliza Henry.

“ Shut up !! akafoka Mathew na kumuamuru Eva akamchukue Naomi chumbani kwake.Baada ya dakika mbili Naomi akafika pale sebuleni.henry akashangaa sana akabaki mdomo wazi
“ I cant believe thisNaomi !!!...kumbe ni wewe uliyekubali kunisaliti mwanangu? Wamekulipa shilingi ngapi hawa na ukakubali kumsaliti baba yako mzazi? Jambo gani nimekukosea mwanangu kiasi cha kunisaliti namna hii? Akauliza Henry

“ Huyu ni mwanao? Akauliza Mathew

“ Ndiyo ni mwanangu” akajibu Henry
“ kwa nini umesababisha akawa hivi?
“ Amewaeleza kwamba mimi ni sababu ya yeye kuwa hivi? Si mimi niliyemfaya akawa hivi.Yeye mwenyewe alijiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya na ndiyo maana akafikia hali hii.Mimi sihusiki na hali hii kwa namna yoyote.Nimejitahidi kumlea kwa kadiri nilivyoweza lakini bado hakuridhika na akajiingiza katika starehe nadawa za kulevya” akasema Henry
“ Liar !!!..akapaaza sauti Naomi huku akilia
“ Henry hatuna muda mrefu wa kuongea nawe hapa.Tayari tunafahamu mambo yako mengi unayoyafanya ya haramu.Tunafahamu kuhusu biashara yako ya dawa za kulevya.Tunafahamu kuhusu kiwanda chako cha kutengeneza noti bandia chiniya nyumba yako.Tunafahamu kila kitu unachokifanya na ushahidi tunao wa kuweza kukutia hatiani wewe na mtandao wako wote.” Akasema Mathew na kumfanya Henry atetemeke.Mathew akaendelea
“ Henry tunafahamu mambo yako mengi sana na endapo utafikishwa mbele ya sheria huwezi kukwepa kifungo cha maisha gerezani kwa mambo unayoyafanya.Hata hivyo kwa sasa tunayaweka yote pembeni kwanza.Kuna jambo tunalitaka toka kwako na endapo utatupatia tunachohitaji basi tutakuacha uendelee na shughuli zako ila Naomi tutamchukua na kumpeleka katika tiba and She’ll never talk about anything she knows about you”akasema Mathew

“ Who are you guys? Ni jambo gani mnalitaka toka kwangu? Akauliza henry
“ Huna haja ya kutufahamu sisi ni akina nani lakini sisi ni watu wabaya sana na una bahat mbaya ukutana na sisi.We can destroy you in a second” akasema Mathew
“Nielezeni mnataka nini toka kwangu? Akauliza Henry .Mathew akamsogelea karibu na kumuwekea bastora kifuani

“ Tunafahamu kwa sasa una mahusiano ya kimapenzi na Rosemary Mkozumi.Ninataka uniingize ndani ya jumba la Rosemary Mkozumi kwani wewe pale ni kama kwako .Unaweza ukaingia na kutoka muda wowote unaotaka..” Akasema Mathew na kumstua sana Henry
“ What ?!!Unataka kuingia kwa Rosemary? Unataka kwenda kufanya nini?

“ Henry shida yetu si wewe ,shida yetu ni Rosemary.Kuna jambo ninalotaka kulichunguza katik a mawasiliano ya Rosemary ndiyo maana nikakwambia kwamba ukinisaidia kulifanikisha hilo sintakuwa na shida na wewe .”akasema mathew
“ Hapana sintaweza kufanya hivyo mnavyotaka nifanye.Hamumfahamu vizuri Rosemary ninyi.Nawaonya msithubutu kucheza na Yule mama.”akasema Henry
“ Henry utanipeleka ndani ya jumba hilo na utafanya kila nitakachokuamuru umesikia? Usipofanya hivyo ndani ya dakika chache zijazo wewe na mtandao wako wote akiwemo na mpenzi wako Rosemary mtajikuta katika nondo za gereza..Unataka tulifanye hilo? Do you want to go down? Unataka nchi yote ifahamu mambo mnayoyafanya wewe na mtandao wako?akasemamathew.Heny akaonekana kuingiwa na woga
“ Jamani naomba basi muweke silaha zenu chini ili tuongee kama watu wazima na tuelewane.Ninakubali mnafahamu mambo yangu mengi na mmekuja kwangu mkiwa na shida yenu ambayo ili ifanikiwe inanihitaji sana mimi.Ni kweli sitaki mambo yangu yajulikane kwani heshima yangu niliyoijenga ndani ya nchi hii itashuka sana na hii ni mbaya sana kwangu kisiasa.Niko tayari kuwasaidia kile mnchokitaka lakini kwa sharti kwamba binti yangu asiondolewe humu ndani ya hii nyumba kwani akitoka humu ataendelea na tabia yake ya kutumia dawa za kulevya.Huyu ni binti yangu wa pekee na sina tena mtoto mwingine na ndiyo maana ninafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba anakuwa salama na haijihusishi tena na dawa za kulevya.Ili niwasaidie ninaomba mnihakkishie hilo kwanza’ akasema Henry

“ Henry suala hilo halitawezekana kwani kwa miaka minne sasa umemfungia Naomi ndani ya jumbahili na kwa sasa anahitaji kuwa huru.Sisi tutamchukua na kumpeleka katika sehemu atakakopatiwa matibabu na usiwe na wasiwasi hatasema chochote kuhusu wewe na wala hataendelea tena kutumia dawa za kulevya.Naomba uniamini katika hilo’ akasema Mathew.Henry akafikiri kidogo kisha akasema

“Ni kitu gani unachotaka kwenda kukichunguza kwa Rosemary?

“ Nataka kuchunguza mawasiliano yake ya ndani na nje ya nchi” akasema Mathew
“ Nyumba ya Rosemary ina mfumo wa kisasa sana wa ulinzi na kuna baadhi ya vitu vyake kama vile komyuta zake au sehemu anakohifadhi nyaraka zake muhimu vikiwashwa basi taarifa inatumwa moja kwa moja katika simu yake ya mkononi.Kwa hiyo ni vigumu sana kuweza kuwasha kitu chochote cha Rosemary kilichomo katika ofisi yake.”akasema Henry
“ Henry will you take me there or not?akauliza Mathew.Henry akakaa kimya kidogo na kusema

“ sawa nitakupeleka huko lakini tafadhali tukubaliane kwanza kuhusu binti yangu.Haendi kokote”

“ Naomi is in safe hands.Usiogope.She’ll be fine” akasema Mathew

“ Dady fanya kama ulivyoombwa kufanya na ushofukuhusu mimi.I’m free now”akasema Naomi.Henry akamtazama kwa jicho kali
“ Henry muda unakwenda sana.Tuondoke sasa”akasema Mathew.Henry akainuka pale katika sofa
“ Eva mchukue Naomi kamuhifadhi kwa muda ofisini kwako hadi zoezi hili likamilike kisha tutamchukua na kumpeleka sehemu salama.Mimi nitaongozana na Henry kwenda nyumbani kwa Rose.”akasema Mathew

“ Are you sure yo want to go teher alone Mathew? Akauliza Eva
“ yes Eva..” Akasema Mathew na kisha akamgeukia Naomi
“ Naomi utachukua mizigo yako na utaongozana na Eva atakupeleka sehemu salama” akasema Mathew kisha akaongozana na henry wakatoka hadi katika gari la henry .Bado bastora ya Mathew ilikuwa mkononi.Henry akageuza gari wakaondoka pale nyumbani.Mathew akachukua simu na kumpigia Anitha

“ hallow Mathew”akasema Anitha baada ya kupokea simu
“ Anitha kuna habari zozote mpya ?
“ Hapana mpaka sasa hakuna habari mpya ,Dr Kigomba alikuwa anapiga sehemu mbalimbali kufanya maandalizi ya msiba wa Flaviana”
“ Ok good.Niko njiani hivi sasa ninaelekea kwa Rosemary Mkozumi.Inasemekana nyumbani kwa Rose kuna mfumo wa kisasa wa ulinzi na kwa hiyo si rahisi kuingia katika kompyuta ya Rose .Nadhani ingekuwa vizuri sana kama ningeongozana nawe ili uweze kunisaisia katika kazi hi.Ukiwa karibu tunaweza kufanya kazi kwa haraka zaidi.Tafadhali chukua vifaa unavyoona vinaweza kutusaidia na uchukue gari.Utatukuta tunakusubiri pale picha ya samaki ili tuongozane ” akasema Mathew

“ sawa Mathew.Nisubirihapo picha ya samaki ninakuja si muda mrefu.” Akasema Anitha
“ Who are you guys? Mnatafuta kitu gani kwa Rose? Akauliza Henry
“shut up !!akasema Mathew na mara simu ya Henry ikaita.
“ Nipe hiyo simu”akasema Mathew
“ Mmeniweka chIni ya ulInzi na mnanilazimisha nifanye kile mnachokitaka,lakini bado mnanizuia hadi kutumia simu yangu? Akafoka Henry
“ Nimesema nipe smu yako”akasema Mathew na Henry akaogopa kwa namna Mathew alivyokuwa anamaungalia akampatia simu yake ,akaizima nakutoa kabisa betri

“ Twende hadi picha ya samaki kuna mtu tukamsubiri pale.” Akaamuru Mathew
Walifika eneo la picha ya samaki wakaegesha gari wakimsubiri Anitha.Ilimchukua anitha zaidi ya dakika thelathini kuwasili eneo lile.Haraka haraka akiwa na begi lake lenye vifaa muhimu vinavyoweza kuwasaidia akashuka katika piki piki aliyokodi na kuingia katika gari walimokuwamo akina Mathew na safari ikaendelea.
Waliwaisli katika jumba la Rosemary Mkozumi lililojengwa ufukweni mwa bahari .Toka kwa mbali uzuri wa jumba hili ulionekana,barabara iliyoeleka katika jumba hili ilipandwa maua na miti mizuri ya kuvutia sana.Kulikuwa na ukimya mkubwa eneo hili
Wakafika katika geti kubwa jeusi Henry akasimamisha gari.Getni pale walionekana walinzi wanne na wawili kati yao walikuwa na silaha.Walivaa sare za kampuni binafsi ya ulinzi.Mmoja wa walinzi wale akalisogelea gari,Henry akashusha kioo cha gari wakasalimiana halafu geti likafunguliwa na henry akapita.Hawaku muuliza maswali yoyote kwa kuwa walimfahamu.Baada ya kulivuka geti la kwanza wakakuta tena geti la pili,wakafunguliwa wakpita na mwisho wakalifikia geti la tatu nalo wakafunguliwa wakapita bila kuhojiwa.
“ Mhh kwa ulinzi ulioko hapa sina hakika kama ingekuwa rahisi kuingia.Huyu mama amejimarisha sana katika ulinzi.”akawaza Mathew
Kisha livuka geti la tatu lililokuwa na walinzi wawili,wakaanza kulitazama jumba kubwa la ghorofa nne.Lilikuwa ni jumba la kifahari mno.Henry akaegesha gari wakashuka na kuingia ndani.Aliwakaribisha ndani huku akitabsamu ili watumishi wasiweze kugundua chochote kilichokuwa kinaendelea.
Moja kwa moja henry akawapeleka Mathew na Anitha katika ofisi ya Rosemary.Juu ya mlango wa ofisi ile kulikuwa na taa nyekundu ikiwaka napembeni ya mlango ule kulikuwa na kijisanduku chenye namba.Henry ajkabonyeza namna kadhaa halafu akawekamkonokatika sehemu fulaniiliyowaka taa ya kijani na baada ya sekunde kadhaa yakatokea maandishi
“ Welcome Henry” na mlango akafunguka..
“ Hii ndiyo ofisi ya Rosemary lakinihata mimi huitumia pia.Kompyuta yake ile pale,na lile pale ni kabati ambalo huhifadhi nyaraka zake nyeti.Ili kufungua vitu vyake unahitaji namba za siri ambazo hata mimi sina.Ni yeye pekee anayezifahamu” akasema Henry.
Anitha akafungua begi lake akatoa vifaa Fulani akaviweka mezani akaiwasha kompyuta yake ndogo ,halafu akachukua kifaa kingine kidogo akakichomeka nyuma ya kompyuta ya Rose.Akakaa katika komyuta yake na kuanza kubonyeza bonyeza kompyuta yake kwa takribani dakika saba hivi huku Mathew na Henry wakimshangaa wasielwe alichokuwa anakifanya.Akainuka tena na kwenda kuiwasha kompyuta ya Rosemary na kisha akarejea tena katika kompyuta yake. Akaanza kubonyeza tena na baadaya dakika tano akasema

“ Done,we’re in…”
Henry akabaki anashangaa

“ Thank you anitha.You are always the best” akasema Mathew
“ Progarmu hii niliyoiweka inatengua mfumo huu wa usalama aliouweka Rose kwa muda wa dakika thelathini kwa hiyo tufanye haraka kutafuta kile tunachokitaka” akasema Anitha na kumuelekeza Anitha aanze kupekua katika mawasiliano ya barua pepe kama anaweza akapata mawasiliano kati ya Rose na Habib
Anitha akaanza kupekua mawasiliano ya Rose na watu kadhaa lakini ghafla akasimama

“ I think I’ve got something “akasema Anitha na kumuonyesha Mathew barua pepe ile ambayo Rosemary alimwandikia mtu mmoja anaitwa Samir hasaad.
Katika barua pepe hiyo Rose alimfahamisha Samir kwamba wanategemea kuupata mzigo muda wowote kwani wanaye mtu wa karibu sana na rais na ambaye anawapa taarifa zenye uhakika kuhusu mzigo huo kwa hiyo wana hakiak wa kuupata muda wowote”.

“ Samir hasaad ni nani? Mathew akamuuliza henry
“ Mimi simfahamu.Hao ni watu wa Rose ambao mimi sihusiani nao.Kuna mambo ambayo mimi na Rose tuna mashrikiano na kuna mambo ambayo hatuna mashirikiano.kwa ufupi simfahamu huyo Samir “ akasema henry
“ Nimzigo gani ambao Rose anamuhakikishia Samir kwamba wanategemea kuupata? Na zaidi anamuhakikishia kwamba wana mtu wa karibu sana na rais ambaye anawapa taarifa zenye uhakika ni nani huyo? Akauliza Mathew
Ghafla Henry aliyekuwa ameelekeza macho dirishani akaonekana kustushwa sana na jambo.Mathew akaligundua hilo na kumuuliza
“ Vipi? Mbona umestuka sana?
“ Rose amerudi.Tayari amejua ofisi yake imefunguliwa”
“ What ?! amejua vipi? akauliza Mathew huku naye akichungulia nje.Ni kweli mwanamama mmoja mnene alishuka katika gari akaanza kupiga hatua kwa kasi kuelekea ndani.

“Ofisi hii ina mfumo wake maalumwa ulinzi na wenye uwezo wa kuufungua mlango wa ofisi hii ni mmi na Rose pekee.Mlango ukifunguliwa lazima itaonyesha katika simu ya Rose .”akasema Henry
Haraka haraka Anitha akachomoa kila kitu alichokuwa amekichomeka katika kompyuta ya Rose na kisha Mathew akachomoa bastora yake na kumuelekezea Henry kichwani
“ Ukitaka uwe salama wewe na mwanao ,kaa pale mezani na ujifanye ulikuwa unafanya kazi zako na usimwambie chochote kuhusu uwepo wetu humu.Ukithubutu kumweleza chochote Rose kwamba tuko humu nitakufumua kwa risasi.Tumeelewana? akasema Mathew.
“ Tumeelewana” akasema Henry kwa wasiwasi.
Rosemary Mkozumi baada ya kushuka garini moja kwa moja akaelekea katika ofisi yake ambako aliamini ndiko aliko Henry.Mara tu alipofungua mlango wa ofisi yake kikatokea kitu ambacho hakuwa amekitarajia.Henry aliruka toka katika meza aliyokuwa amekaa na kupiga ukulele akimzuia Rosemary kutokuingia mle ofisini.Wakati Rosemary akishangaa kitendo kile ikasikika milio ya risasi zilizotoka katika bastora yenye kiwambo cha kuzua sauti na henry akaanguka chini akaanza kutapa tapa huku akivuja damu nyingi.Kutahamaki Rose akajikuta aakitazamana na basora mbili toka kwa Mathew na Anitha.Aliishiwa nguvu akaanguka chini.



TUKUTANE SEHEMU IJAYO…
 
PENIELA SEASON 3

SEHEMU YA 12

MTUNZI: PATRICK.CK


ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Haraka haraka Anitha akachomoa kila kitu alichokuwa amekichomeka katika kompyuta ya Rose na kisha Mathew akachomoa bastora yake na kumuelekezea Henry kichwani
“ Ukitaka uwe salama wewe na mwanao ,kaa pale mezani na ujifanye ulikuwa unafanya kazi zako na usimwambie chochote kuhusu uwepo wetu humu.Ukithubutu kumweleza chochote Rose kwamba tuko humu nitakufumua kwa risasi.Tumeelewana? akasema Mathew.
“ Tumeelewana” akasema Henry kwa wasiwasi.
Rosemary Mkozumi baada ya kushuka garini moja kwa moja akaelekea katika ofisi yake ambako aliamini ndiko aliko Henry.Mara tu alipofungua mlango wa ofisi yake kikatokea kitu ambacho hakuwa amekitarajia.Henry aliruka toka katika meza aliyokuwa amekaa na kupiga ukulele akimzuia Rosemary kutokuingia mle ofisini.Wakati Rosemary akishangaa kitendo kile ikasikika milio ya risasi zilizotoka katika bastora yenye kiwambo cha kuzua sauti na henry akaanguka chini akaanza kutapa tapa huku akivuja damu nyingi.Kutahamaki Rose akajikuta aakitazamana na basora mbili toka kwa Mathew na Anitha.Aliishiwa nguvu akaanguka chini.



ENDELEA………………………



Haraka haraka Mathew akamshika mkono Rosemary mkozumi na kumvuta akamuingiza mle ofisini kisha akafunga mlango.Akamfuata Henry pale chini alipolalia dimbwi la damu akamgeuza
“ Henry !! akaita Mathew.Henry hakuitika na alionekana kupumua kwa shida sana.
“ Henry ! henry !!.Mathew akamtikisa.Henry akafumbua macho na kwa sauti ndogo akasema
“ Nao..nao…Naom……!! akashindwa kumalizia alichotaka kukisema akakata roho.Anitha akafumba macho alisikia uchungu sana .Mathew akainuka na kumsogelea Anitha
“ He’s gone” akasema kwa sauti ndogo.

“ I’m so sorry” akajibu Anitha.Kwa sekunde kadhaa walibaki kimya wakimtazama Rosemary aliyekuwa amelala chini hana nguvu huku jasho likimtiririka
“ What are going to do? Akauliza Anitha
“ Mtu tuliyekuwa tunamuhitaji sana ni Rosemary ambaye amejileta mwenyewe na hatuwezi kumuacha.Lazima tuondoke naye.We must do something to get us out of here” akasema Mathew na kuchukua simu yake akampigia Eva akamfahamisha kilichotokea na kumuomba alete gari la wagonjwa haraka sana pale nyumbani kwa Rosemary .Kisha ongea na Eva akamgeukia Anitha
“ Eva anakuja na gari la wagonjwa.Najua kama gari lile la wagonjwa likifika hapa ni lazima walinzi watataka kujua kilichotokea kwa hiyo basi lazima tumtoe Rosemary humu ndani na tuifunge hii ofisi kwa nje .Mlango huu wa ofisi ukifungwa kwa nje ni watu wawili tu wanaoweza kuufungua.Rosemary na Henry pekee kwa hiyo hata walinzi wake hawataweza kuufungua huu mlango na kujua klichotokea humu hadi hapo tutakapoondoka na kuwapigia simu na kuwataarifu kuhusu Henry.“ akasema Mathew na kumshika mkono Rosemary ambaye hakuwa na nguvu hata kidogo akamvuta na kumtoa nje ya ofisi yake.Anitha akaichukua kompyuta ile ya Rosemary pamoja na simu yake kisha akatoka mle ofisini na kuufunga mlango.Taa nyekundu ikawaka juu ya mlango kuashiria kwamba hakuna anayeweza kuufungua tena mlango ule kutokea nje zaidi ya Henry na Rosemary pekee.
“ Is she going to be ok? Akauliza Anitha kwa wasi wasi akimtazama Rosemary aliyekuwa akihema kwa taabu na jasho jingi kumtirirka
“ Don’t worry .She’ll be ok.Anaonekana amepatwa na mstuko wa ghafla kwa hiyo anahitajika daktari haraka kuweza kumsaidia.Mungu atusadie tufanikiwe kumtoa mama huyu salama humu ndani” akasema Mathew .Anitha akapiga magoti na kumfuta Rosemary jasho lililokuwa linamtiririka.
Baada ya dakika kama ishirini hivi simu ya Mathew ikaita alikuwa ni Eva.
“ Mathew tumezuiliwa hapa getini na walinzi kwamba hakuna gari inayoruhusiwa kuingia hapa bila kibali cha bosi wao Rosemary na hawana taarifa zozote za kuitwa kwa gari la wagonjwa” akasema Eva.
“ Naomba umpe simu mmoja wa walinzi niongee nao” akasema Mathew na baada ya sekunde kadhaa akasikia sauti nzito ya kiume ikiita
“ Hallow”
“ Hallow ndugu yangu kuna tatizo limetokea humu ndani.Rosemary amepatwa na na mstuko wa ghafla na anahitajika kukimbizwa hospitali haraka sana.”

“ Mstuko wa ghafla? Nini kimesababisha akapatwa na mstukohuo? Mbona amepita haap getinimuda mfupiuliopita akiwa mzima wa afya? Henry yuko wapi ? Yule mlinzi akaulzia maswali mfululizo.
“ Kumetokea kutokuelewana kati ya Henry na Rose na Rose alipatwa na tatizo hili.Sisi ni wale wageni tuliokuwa na Henry na hatufahamu mpaka sasa aliko Henry .Tafadhali naomba mliruhusu gari hilo haraka sana la wagonjwa ili tumkimbize Rose hospitali.Endapo mtaendelea kulizuia gari hilo na hali ikazidi kuwa mbaya lawama zote zitawaangukia ninyi” akasema Mathew na simu ikakatwa.
Baada ya dakika tano wakaingia kwa kasi walinzi watatu na nyuma yao wakafuata Eva na watu wengine wawili waliovaa makoti meupe wakiwa na machela .
“ Henry kaelekea wapi “akauliza mmoja wa walinzi
“ Stop asking questions.Tusaidiane kwanza kuokoa maisha ya bosi wenu” akasema Mathew wakasaidiana kumpakia Rosemary katika machela na kumshusha chini .Gari la wagonjwa likasogezwa karibu na mlango wakampakia Rose.Mathew akawagukia wale walinzi.
“Endeleeni kumtafuta Henry,sisi ngoja tumuwahishe mgonjwa.Tutawafahamisha maendeleo yake.” Akasema Mathew na kuingia katika gari lile la wagonjwa wakaondoka kwa kasi wakiwawaacha watumishi wakishangaa kilichotokea.Ndani ya gari madaktari wale wawili waliendelea kumpatia Rose .
“ Finally we got her” akawaza Mathew

“ Vyombo vya usalama vimekuwa vikimuogopa sana huyu mama lakini leo imefika arobaini yake.Ametua mikononi mwangu na lazima atanieleza kila kitu.Ni heri angekutana na shetani kuliko kukutana na mimi” akawaza Mathew.

“ Mathew tunaelekea hospitali gani? akauliza Eva
“ Eva we need to talk” akasema Mathew na kuwatazama wale madaktari
“ Samahani ndugu madaktari.Ninahitaji dakika mbili niongee faragha na Eva” akasema Mathew na mmoja wa wale madaktari akamuomba dereva asimamishe gari pembeni ya barabara,Mathew na Eva wakashuka
“ Mathew what happened? Akauliza Eva

“ Eva kulitokea rabsha kidogo na kusababisha Rose apatwe na mstuko huu.”

“ Henry yuko wapi?
“ Henry is dead”
“ Ouh my God!!.. Eva akastuka
“ Kwa hiyo tunaelekea wapi ? akauliza Eva
“ Tunaelekea nyumbani kwangu.”
“ No ! Mathew hali ya Rose ni kama unavyoiona si nzuri hata kidogo anatakiwa apelekwe hospitali akakae chini ya uangalizi wa madaktari.”
“ Eva,huyu mama ana taarifa za muhimu sana na kwa sasa ameua mikononi mwangu siwezi kumuachia hata sekunde moja.”
“ Mathew unarudia tena ubishi wako kama wa kipindi kile uliosababisha kifo cha Yule msichana.Nakushauri kama rafiki yangu tumpeleke Rosemary hospitali na hali yake ikiwa nzuri tutamchukua na kumuhoji kama unavyotaka lakini kwa sasa bado hali yake si nzuri na huwezi kumuhoji chochote” akasema Eva

“ Eva,siwezi kamwe kufanya kosa la kumpeleka Rose hospitali.Wewe mwenyewe ndiye uliyenihakikishia kwamba huyu mama ni hatari na ana mtandao wake mkubwa kwa hiyo basi kitendo cha kumpeleka hospitali tutampoteza na hatutaweza kumpata tena.This is the only chance we have and we cant loose it”
“ Mathew nakubaliana nawe lakini bado naendelea kukushauri kwamba tumpeleke hospitali.Hawa madaktari wote wanafanya kazi katika idara ya usalama wa taifa na tutampeleka Rose katika hospitali zetu ambazo huwa tunazitumia kuwahifadhi watu kama hawa wakahudumiwa bila ya mtu kufahamu .Please Mathew,naomba unisikilize na tukubaliane katika hili.” akasema Eva
“ Eva tusiendelee kupoteza muda.Rosemary anapelekwa nyumbani kwangu na atahudumiwa pale.”
“ Itakuwaje iwapo atapoteza maisha akiwa nyumbani kwako? Mathew suala hili ni la hatari kubwa sana .Muda si mrefu itagundulika kwamba Rosemary ametoweka na utaanza msako mkali sana wa kumtafuta.Hii itakuwa mbaya sana kwako Mathew” Akasema Eva

“ That’s the risk I have to take Eva.Ikitokea hivyo I’ll know what I’ll do .Get in the car” akasema Mathew wakangia garini na safari ikaendelea

“ Katu siwezi kumpa nafasi huyu mama ya kutoroka japokuwa haliyakeni mbaya ,lakini kumpeleka hospitali hata kama inamilikiwa na usalama wa taifa bado ni kumpa nafasi ya kutoroka kwani kwa mujibu wa Eva hata ndani ya idara ya usalama wa taifa mtandao wa Rose umekita mizizi yake .I have to take this risk.Kama akipoteza maisha nitajua nini cha kufanya lakini naomba Mungu jambo hilo lisitokee kwa sasa “ akawaza Mathew .Anitha aliyekuwa amekaa mbele na dereva akamuelekeza njia ya kupita hadi walipofika nyumbani kwa Mathew.Rosemary akashushwa na kuingizwa katika chumba kimoja kikubwa ambacho kina vitanda vitatu kama vya hospitali na vifaa mbalimbali vya tiba.Chumbakile kilionekana kama zahanati ndogo.Rose akalazwa katika mojawapo ya vitanda vile .Madaktari wale wakaelekeza baadhi ya vitu vinavyotakiwa kupatikana haraka ili kufanikishamatibabu ya Rose.
Gari lile la wagonjwa lililotumika kumbeba Rose likabadilishwa namba ili kuzuia kutambulika kisha Eva na dereva wa lile gari wakaondoka .Eva alikwenda kutafuta baadhi ya vifaa vilivyohitajika . Mathew alimkumbusha pia kumchukua Naomi na kumleta pale nyumbani.Wakati madaktari wale wawili wakiwa na Rosemary wakimuhudumia,Anitha akaelekea ofisini kuendelea kuifanyia upekuzi kompyuta ya Rose,Mathew akamfuata Elibariki chumbani.
“ Hallow Elibariki.Unaendeleaje? akauliza Mathew

“ Ninajitahidi Mathew lakini bado kichwa changu kizito sana.Nimekuwa na mawazo mengi mno nahisi kama ninataka kuchanganyikiwa.Kuna taarifa zozote mpya kuhusiana na msiba wa Flaviana?
“ Anitha yuko ofisini sasa hivi akiangalia kama kuna taarifa yoyote mpya.” Akasema Mathew
“ Nini kinaendelea sasa hivi Mathew? Akauliza jaji Elibariki

“ Tumefanikiwa kumpata Rosemary Mkozumi.”
“ Mmefanikiwa kumpata? Hongereni sana.”
“ Ahsante sana Jaji lakini hali yake si nzuri sana na madaktari wako naye chumbani wakimuhudumia na hali yake itakapokuwa nzuri tutamfanyia mahojiano .Tutafahamu mambo mengi kutoka kwake.” Akasema Jaji Elibariki na mara Anitha akaingia mle chumbani
“ Mathew kuna kitu nimekigundua..” akasema Anitha

“ Umegundua nini Anitha? Akauliza Mathew huku akiinuka na kuongozana na Anitha kuelekea ofisini.

“ Wakati nikipekua kompyuta ya Rose nimekutana na barua pepe hii ambayo inaonyesha Rose alimtumia mtu anayeitwa Captain Amos akimtaka ampatie taarifa zenye uhakika kwani anategemea kwenda kuonana na Samir Asaad aliyefikia 7 angels hotel.Kilichonistua ni kwamba Peniela aliwahi kumtaja Captain Amos ambaye naye ni mshirika wa karibu sana wa rais na ambaye pamoja na Dr Kigomba wanashirikiana katika biashara ya hiyo package .” akasema Anitha

“ Ni kweli Anitha.Rais Dr Joshua anashirikiana na watu wawili katika biashara ile.Kuna Dr Kigomba na huyu Captain Amos.Kama utakumbuka katika ile barua pepe ambayo Rosemary alimuandikia Samir alimueleza kwamba anategemea kuupata mzigo muda wowote kwani ana mtu wa karibu sana na rais.Ni kweli Captain Amos ni mtu wa karibu sana na Rais na kwa maana hiyo basi picha ya haraka tunayoipata hapa ni kwamba Rose na Captain Amos ni washirika na nina wasiwasi kwamba huo mzigo anaouongelea Rose kwamba wana hakika ya kuupata wakati wowote ni hiyo package ambayo Dr Joshua anataka kuiuza.”
“ Exactly!! Akasema Anitha
“ Hakuna ubishi kwamba mzigo huo anaouongelea Rose ni hii package ambayo Dr Joshua na wenzake wanataka kuiuza.” Akasema Anitha
“ Ukumbuke vile vile Captain Amos yuko pia Team SC41 na wanamtegemea sana katika kupata package hiyo.Anaonekana ni mtu mwenye tamaa sana ya fedha kwani anachukua fedha toka Team SC41,anachukiua fedha kwa Rose na bado anategemea mgawo mkubwa wa fedha toka kwa Dr Joshua .Huyu ni mtu hatari sana na tunatakiwa kumpata haraka sana."

“ Hiyo package ina kitu gani ndani kiasi cha watu wengi namna hii kuitaka? Halafu kwa nini wanunuzi wake wengi wanatokea katika nchi za kiarabu? Akauliza Anitha

“ Nadhani Rose anaweza kutupa majibu ya nini kilichomo katika hiyo package lakini kwa sasa tunatakiwa kumpata Captain Amos.Endapo Amos akipotea ghafla basi Team SC41 na hata huyu Rose hawataweza kupata taarifa zozote kuhusiana na package kwa hiyo sisi tutapata nafasi nzuri ya kuweza kuichukua.” Akasema Mathew
“ Ni Peniela pekee anayeweza kutuelekeza mahala pa kumpata Amos.Nashangaa mpaka mida hii hajanipigia simu wakati nilimuachia maagizo Josh kwamba mara tu atakapozinduka anitafute .” akasema Mathew huku akiitoa sumu yake mfukoni na mara kengele ya getini ikalia.

“ Ngoja nikaangalie yawezekana Eva amerudi.” Akasema Mathew huku akitoka kwenda getini

“ Baada ya kazi hii kukamilika itanilazimu niwarudishe wale walinzi wa getini walikuwa wananisaidia sana
“ akawaza wakati akielekea getini.Alifungua geti na kukutana na Peniela
“ Peniela !! akasema Mathew kwa mshangao kidogo

“ Hello Mathew.Mbona umestuka?
“ Tulikuwa tunakuongelea sasa hivi hapo ndani kumbe uko getini.Mbona silioni gari lako? Umekuja kwa miguu? Akauliza Mathew
“ Nimekuja na taksi.Sikutaka watu wafahamu mahala ninakoenda.” Akasema peniela na mathew akamkaribisha ndani
“ Pole sana Peniela.Unajisikiaje sasa hivi? Nilishindwa kuonana nawe tena baada ya watu ambao nahisi ni Team SC41 kuwasili pale hospitali” akasema Mathew.
“ Kifo cha John kimenipa simanzi kubwa lakini baada ya kuzinduka nikakumbuka kuna jambo zito linalotukabili na ndiyo maana nimekuja hapa ili tujue kinachoendelea.”
“ Pole sana Peniela.Una hakika una nguvu za kutosha kuweza kuendelea na mapambano? akauliza Mathew
“ John amekwenda na maisha lazima yaendelee.Jambo kubwa lililoko akilini mwangu kwa sasa ni kuhakikisha package inapatikana kwa gharama zozote na kisha kuifunga kabisa Team SC41.Kukujibu swali lako ni kweli nina nguvu za kutosha kuendelea kupambana hadi mwisho.” Akasema Peniela
“ Good.Nafurahi kusikia hivyo.” Akasema Mathew

“ Elibariki yuko wapi? Akauliza Peniela
“ Peniela kuna jambo sikuwa nimekufahamisha .Nikiwa pale hospitali nilipigiwa simu na Anitha akanifahamisha kwamba Dr Joshua amempigia simu Dr Kigomba na kumfahamisha kwamba Flaviana amefariki dunia.”
“ What ?!!! Peniela akastuka sana
“ Flaviana amefariki dunia.” Akasema Mathew

“ Oh my God ! Yuko wapi Elibariki? Akauliza Peniela
“ Elibariki yuko chumbani anapumzika kwa mstuko alioupata” akajibu Mathew na bila kupoteza muda Peniela akainuka na kuelekea chumbani kwa jaji Elibariki akaufungua mlango na kuingia ndani.Elibariki alikuwa amekaa kitandani amejiinamia akiwaza na mara tu alipomuona Peniela akajikuta akipata nguvu na kusimama.Wakakumbatana kwa nguvu.

“ Pole sana Elibariki.Pole sana my love”akasema peniela huku akimpiga piga mgongoni.
“ ahsante sana Peniela.Ahsante sana kwa kuja kunifariji.Pole nawe pia.Mathew ameniambia kwamba John amefariki dunia. “ akasema Elibariki

“ Ndiyo amefariki dunia.”
“ Pole sana Peniela.Kifo hakizoeleki hasa kwa mtu wako wa karibu lakini lazima maisha yaendelee.”
“ Ni kweli Elibariki na ndiyo maana nimekuja hapa ili kuweza kuendelea na mikakati yetu “ akasema Peniela. Mara Mathew akasimama mlangoni na kusema
“ Peniela kama hutajali nakuomba ofisini mara moja”akasema Mathew na Peniela na jaji Elibariki wote kwa pamoja wakaelekea ofisini kwa Mathew
“ Peniela kuna jambo limetokea asubuhi ya leo ambalo huna budi kulifahamu.Ni kwamba tumefanikiwa kumpata Rosemary Mkozumi mke wa rais wa zamani wa Tanzania.”

“ Roemary Mkozumi? Akauliza Peniela kwa mshangao

“ Ndiyo Peniela.Katika uchunguzi wetu tumegundua kwamba huyu mama amekuwa na mawasiliano ya karibu na Habib soud ambaye anatajwa kutaka kuzinunua karatasi zile ambazo Edson aliziiba ikulu.Tunaamini kwamba huyu mama ndiye aliyekuwa nyuma ya mpango ule na Edson alitumiwa tu katika kuziiba karatasi hizo.Tumekwenda mbali zaidi katika kumfanyia uchunguzi Rosemary na tumegundua kwamba amekuwa na mawasiliano na mtu mmoja anaitwa Samir asaad na katika mawasiliano hayo Rosemary anamuhakikishia Samir kwamba mzigo utapatikana muda wowote kwani tayari ana mawasiliano na mtu aliyeko karibu sana na rais.Tumeendelea kuchunguza na kugundua kwamba Rosemary amekuwa na mawasiliano na Captain amos.”

“ Captain Amos?!! Peniela akashangaa
“ Ndiyo peniela.”
“ This is weird. Captain Amos yuko team Sc41,kumbe anatumiwa tena na huyu mama? The whole game is full of betrayals” akasema peniela

“ We need to get him as soon as possible” akasema Mathew

“ Tukitaka kufanikiwa katika kuipata hiyo package lazima tumpate Captain Amos ili hao wanaomtumia wakose taarifa sahihi za kuhusiana na kinachoendelea katika biashara hiyo.Katika hili utatusaidia sana tuweze kumpata kwani wewe unaweza kuwasiliana naye muda wowote” akasema Mathew.Peniela akatoa simu yake na kuzitafuta namba za Amos akapiga
“ Hallow Peniela,pole sana na matatizo.Nimepata taarifa za kifo cha John.Zimenistua sana” akasema Amos

“ Amos uko wapi? I need to see you.” Akasema peniela
“ Kuna tatizo gani Peniela?
“ Kuna jambo la muhimu sana la kuongea nawe”

“ Cant we talk on phone?

“ No .I have to meet you face to face” akasema Peniela.Ukapita ukimya wa sekunde kadhaa kisha Amos akajibu

“ Tukutane pale Mlimba restaurant,upande wa nyuma kuna vyumba,nenda hadi chumba namba kumi na nne huwa ninakitumia kwa dharura.Sitaki watu wajue nina mawasiliano nawe” akasema Amos na kukata simu



TUKUTANE SEHEMU IJAYO……





PENIELA SEASON 3

SEHEMU YA 13


ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA


“ Tukitaka kufanikiwa katika kuipata hiyo package lazima tumpate Captain Amos ili hao wanaomtumia wakose taarifa sahihi za kuhusiana na kinachoendelea katika biashara hiyo.Katika hili utatusaidia sana tuweze kumpata kwani wewe unaweza kuwasiliana naye muda wowote” akasema Mathew.Peniela akatoa simu yake na kuzitafuta namba za Amos akapiga
“ Hallow Peniela,pole sana na matatizo.Nimepata taarifa za kifo cha John.Zimenistua sana” akasema Amos
“ Amos uko wapi? I need to see you.” Akasema peniela

“ Kuna tatizo gani Peniela?
“ Kuna jambo la muhimu sana la kuongea nawe”
“ Cant we talk on phone?

“ No .I have to meet you face to face” akasema Peniela.Ukapita ukimya wa sekunde kadhaa kisha Amos akajibu
“ Tukutane pale Mlimba restaurant,upande wa nyuma kuna vyumba,nenda hadi chumba namba kumi na nne huwa ninakitumia kwa dharura.Sitaki watu wajue nina mawasiliano nawe” akasema Amos na kukata simu


ENDELEA……………………………..


“ Anitha nitaongozana na Peniela kwenda Mlimba Lodge kumchukua Captain Amos.Wewe utabaki hapa kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri na kufuatilia mawasiliano yoyote kati ya Dr Joshua na Dr Kigomba.Vile vile endelea kufuatilia hali ya Rosemary Mkozumi .Eva ameenda kuvifuatilia baadhi ya vifaa na atarejea hapa muda si mrefu.Hakikisha unakuwa karibu na wale madaktari na kuhakikisha Rose anapata nafuu haraka kwa ajili ya kumfanyia mahojian😵ne more thing,usimruhusu Eva afahamu jambo lolote lile tunalolifuatilia na wala usimruhusu akaingia humu ofisini na wala asifahamu chochote kuhusu uwepo wa Elibariki hapa ndani” akasema Mathew

“ Who is this Eva? Akauliza jaji Elibariki
“ Ni rafiki yangu anafanya kazi usalama wa taifa” akajibu Mathew

“ Are you sure you want to go there alone? Akauliza tena jaji Elibariki

“ I’m not alone.Peniela will be there with me” akajibu Mathew.

“ Sawa Mathew,jitahidi kuwasiliana nasi mara kwa mara kutujulisha kila kinakachojiri ili kama kutahitajika msaada wa haraka basi tujue namna ya kujipanga” akasema Anitha
Jaji Elibariki na Peniela wakakumbatiana

“ Please take care Peniela” akasema jaji Elibariki
“ I will” akajibu Peniela halafu Mathew akatoka na kwenda katika chumba alimolazwa Rosemary Mkozumi ambaye kwa sasa hali yake ilianza kuleta matumaini.Mathew akatoka na kuingia chumbani kwake akachukua baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kumsaidia katika shughuli ile kisha akatoka na kuongozana na Anitha wakaingia garini kuelekea Mlimba Lodge.
“ Nilimuamini sana Captain Amos na kumuona kama mwenzangu ninayeweza kumtegemea kumbe ni mtu mbaya sana.Sikuwahi kufikiria kwamba anaweza akatumiwa pia na Rosemary Mkozumi . Kinachoniuma zaidi ni kwamba anatumiwa na Rosemary kupata taarifa za operesheni kubwa kama hii tunayoendelea nayo ya kuipata package toka kwa Dr Joshua.Amos ametuzunguka na kutoa taarifa kwa Rosemary ambaye naye pia anaonekana kuitafuta package hiyo.Jambo hili limeniumiza sana sana.Mathew nashukuru kwa kuligundua jambo hili mapema.Sisi tungeendelea na mipango yetu bila kujua kama mtu tunayedhani ni mwenzetu tayari ametuzunguka na anashirikiana na watu wengine ambao nao wanajipanga kwa ajili ya kuipata package hiyo na tungeweza hata kuuawa kwa kutolijua hili…Damn you Amos kwa nini ukatufanyia hivi? Akasema Peniela kwa hasira

“ Imekuwa vizuri sana tumewahi kulifahamu jambo hili mapema.Tusingeligundua hili mapema tungeweza kupata upinzani mkubwa sana toka kwa watu tusiowafahamu na hili lingetupa ugumu katika kuichukua hiyo package.Kwa sasa kwa kuwa tayari tunaye Rosemary Mkozumi ambaye naye anaitaka package hiyo basi tunatakiwa kwa kila namna tuweze kumpata pia Amos ambaye ndiye mtoa taarifa wake ili tuwe na uhakika kwamba kuna kundi moja tu ambalo tunapambana nao katika kuipata package hiyo nalo ni Team Sc41.Baada ya kumpata Amos kazi kubwa utakayobakiwa nayo peniela ni kuhakikisha unafahamu mikakati yote ya Team SC41 waliyoiweka katika kuhakikisha kwamba wanaipata hiyo package ili tuone namna ya kupambana nao na kuwawahi kabla hawajafanikiwa .” Akasema Mathew
“ Usihofu kuhusu hilo Mathew.Nitafalinyia kazi.Tutakuwa na kikao cha Team SC41 wote ili kujadili kuhusu suala hili nanitawafahamisheni kila kitu” akasema Peniela
“ Kuna chochote kilichopangwa kuhusiana na mazishi ya John Mwaulaya?

“ Mpaka sasa hakuna chochote kilichopangwa.Kutakuwa na kikao cha pamoja nadhani jioni ya leo kufahamishana kuhusu suala hili na hapo ndipo tutakapojua nini kinaendelea na namna tutakavyomzika John Mwaulaya” akasema Anitha

“ Ok Good ! akasema Mathew na kukawa kimya kidogo
“ Nilisikia ukimpa maelekezo Anitha kuhusiana na Eva.Who is she? Akauliza Peniela
“ Eva anafanya kazi katika idara ya usalama wa taifa na ndiye aliyenisaidia nikampata Rosemary Mkozumi.” Akasema Mathew
“ Don’t you trust her? Akauliza Peniela
“ Eva amekuwa ni msaada mkubwa sana kwangu na mara kwa mara amekuwa akinisaidia kufanikisha baadhi ya mambo lakini kusema ukweli bado sijafikia hatua ya kuweza kumuamini.” Akasema Mathew
“ Sawa Mathew,Kuna taarifa zozote kuhusiana na kinachoendelea katika msiba wa Flaviana?

“ Mpaka sasa hivi bado hatujapata taarifa za kinachoendelea ila nina hakika mpaka jioni tutajua nini kinachoendelea.” Akasema Mathew

“ Mathew now that John has gone,kuna mambo ambayo natakiwa niyakamilishe.Yeye mwenyewe alinipa maelekezo kwamba niyakamilisha pindi atakapokuwa amefariki.amenisisitiza sana nisiache kuyakamilisha” Akasema Peniela

“ Tutayakamilisha yote Peniela lakini kwa sasa kitu kikubwa ni kuelekeza nguvu katika suala hili lililoko mbele yetu .Tunatakiwa kwa kila tuwezavyo kuhakikisha kwamba package inatua mikononi mwetu ” akasema Mathew
Walikarbia sana kufika Mlimba Lodge,Mathew akasimamisha gari katika kituo cha basi na kusema
“ Peniela tumekaribia sana kufika.Kutokea hapa itakulazmu uchuke taksi hadi Mlimba lodge.Mimi nitakuwa ninakufuatilia kwa nyuma.Utakapoingia ndani kukutana na Amos tafadhali usionyeshe kwamba unafahamu mambo anayoyafanya.Tafuta namna ya kuongea naye ili kuvuta muda wakati nikijiandaa kuvamia ndaniya chumba ” Akasema Mathew na kufungua droo ya gari akatoa kijimtambo Fulani akakiwasha halafu akachomoa vidude viwili vidogo na kumpatia kimoja peniela akamwambia akiweke sikioni.
“ Hiki ni kifaa cha mawasilino .Nitasikia kila utakachoongea na Amos ” akasema Mathew halaf akampatia Peniela bastora iliyofungwa kiwambo cha sauti. Peniela akashuka garini na kuchukua taksi kuelekea Mlimba Lodge Mathew akafuata kwa nyuma.
Taksi alilopanda Peniela likafika katika megesho ya Mlimba Lodge akashuka na kupiga hatua za haraka haraka kuelekea katika chumba alichoelekezwa na Amos.

“ Ninaelekea chumbani kwa Amos” Peniela akamtaarifu Mathew
“Ninakutazama.Peniela be carefull,this man is very dangerous” akasema Mathew

“ I will” akajibu Peniela
Peniala akafika chumba namba kumi na nne akasima mlangoni kwa sekune kadhaa halafu taratibu akakinyonga kitasa cha mlango na kuingia ndani.Ndani ya chumba kile Captain Amos alikuwa amekaa katika sofa akiwa na chupa ya bia pembeni pamoja na bakuli la supu.
“ Peniela,karibu sana” akasema Amos huku akitabasamu.Peniela akageuka kwa dhumuila kuufunga mlango na ghafla akachomoa bastora na kumuelekezea Amos

“ I trusted you son of a bitch…why you did that ? Why you betrayed us Amos ? Akauliza Peniela huku uso wake ukiwa umejikunja kwa hasira.Captain Amos akabaki anashangaa.hakuwa ametegemea kitendo kile cha Peniela

“ Peniela !!..what happened? Please calm down ! Akasema Amos huku akijaribu kutaka kuinuka

“ Sit down Amos !! akasema kwa hasira Peniela na Amos akagundua kwamba peniela hakuwa akitania akaketi.
“ peniela !!.akataka kusema kitru amos lakini peniela akamzuia.
“ Shut up….!! Akafoka Peniela huku akimuangalia Amos kwa hasira kali.
“ why Amos ? Why you betrayed us? Akauliza Peniela
“ Peniela I dont understand what you are talking about”
“ You don’t know ?? akauliza Peniela kwa ukali
“ Peniela tafadhali weka silaha yako chini…tafadhali weka silaha tuongee..Sielewi unazungumzia kitu gani..”

“ Toka lini umekuwa ukishirikiana na Rosemary Mkozumi na kumpa habari zetu? Akauliza Peniela
Captan amos akastuka sana .
“ How do you know that? Akauliza Amos
“ Ulidhani hatutajua? Kwa nini Amos ukafanya vile? Kwa nini ukaingiwa na tamaa ya pesa kiasi hicho? You sold us all.Sote tungeuawa kwa sababu yako.Huna thamani tena kwangu Amos.!! I hate you !
“ Forgive me Peniela..I did that on purpose.!!

“ On Purpose? Hustahili msamaha kabisa mwanaharamu wewe.”akasema Peniela huku akiuma meno kwa harsira
“ Peniela ! Peniala! …..akaita Mathew kupitia kile kifaa kidogo Peniela alichokiweka sikioni.
“ Today you’ll tell me everything .Ukikataa kunieleza ninachokitaka I swear in heaven and earth I’m going to kill you with my own hand.!! akasema peniela.Captain Amos alogopa,hakuwahi kumuona Peniela akiwa amekasirika namna ile. Macho yake yalionyesha wazi kwamba alidhamiria kukifanya kile alichokuwa anakisema
“ peniela !! ..Peniela !!..akaita Mathew

“ Peniela don’t do that please! Don’t kill him , I’m on the way coming there.Dont shoot him.We need him alive”akasema Mathew .
“ Peniela don’t shoot me..If you do that,you’ll be doing a very big mistake..Me and you we’re all in the same team and everything I’m doing is for you peniela !” akasema Amos .

“ For me ?!! Kutoa siri za mipango yetu ndiyo kufanya jambo kwa ajili yangu? Akafoka peniela
“Peniela kuna mambo mengi ambayo bado huyafahamu but we want to make you and Elibariki very powerfull.. “ akasema Amos na kuzidi kumchanganya peniela.

“ You use the word We ? wewe na nani? Rosemary Mkozumi? Akauliza
“ Peniela najua sio wakati wake kukweleza kuhusu jambo hili lakini sina ujanja lazima nikueleze kila kitu kuhusiana na mipango iliyopo juu yako na Elibariki” akasema Amos lakini ghafla mlango ukapigwa teke na kufunguka,akatokea mwanamke mmoja aliyevaa mavazi meusi na miwani mikubwa myeusi kufunika macho yake ,aliyekuw ana bastora mbili mkononi zilizofungwa kiwambo cha kuzuia sauti .Kama chura Peniela akaruka na kujificha nyuma ya kabati na mwanamke yule akaanza kummiminia risasi Captain Amos.Peniela akaachia risasi mbili toka katika bastora yake kuelekea mlangoni lakini tayari mwanamke Yule alikwisha toweka na Captain Amos alikuwa amelala sakafuni damu nyingi ikimtoka.

“ Ouh My God !!..akasema Peniela kisha akamfuata Amos

“ Amos ! Amos !.akaita Peniela lakini tayari Amos alikwisha fariki kitambo na mara akaingia Mathew.
“ Peniela what happened? Akauliza Mathew huku naye akishangaa
“ Are you ok ? akauliza Mathew
“ I’m ok Mathew.” Akajibu peniela

“ He’s gone Mathew !..Amos is dead” akasema Peniela.
“What happened? Akauliza Mathew
“ Mlango ulipigwa teke ukafunguka ghafla na mwanamke mmoja aliyekuwa na bastora mbili akammiminia Amos risasi.Mathew I’m so scared” akasema Peniela.Mathew akamtazama Amos na kuhakikisha ni kweli amefariki akamsachi na kuchukua simu yake .Akaangaza angaza kwa haraka kuona kama kuna chochote wanachoweza kuondoka nacho hakukuwa na kingine zaidi ya mkoba wa kompyuta,Mathew akauweka begani .

“ Lets get out of here” akasema Mathew wakaufunga mlango na kutoka kwa kasi hadi katika gari wakaondoka

“ I’m sorry Mathew ,Amos ni mtu niliyemuamini kupita kiasi na siri zangu nyingi nilimweleza.Kitendo alichokifanya cha kutusaliti kimeniumza sana na ndiyo maana mara tu nilipomtia machoni nilipandwa na hasira kali na nikashindwa kuwa mstahimilivu nikamtolea bastora.I’m so sorry I failed you.” Akasema Peniela

“ Its ok peniela.Mambo kama haya hutokea.We wanted him alive na ndiyo maana baada ya kusikia maongezi yenu mle chumbani nikagundua ulipandwa na hasira na ukashindwa kujizuia naukiwa na hasira kitu chochote kingeweza kutokea ndiyo maana nikakuita ili kujaribu kukuzuia usifanye chochote.Kuna mambo mengi ambayo tulihitaji kuyafahamu kutoka kwake.” Akajibu Mathew

“ I’m so sorry Mathew.” Akasema Peniela
“ Usijilaumu sana Peniela.Imekwisha tokea na tuangalie yajayo.lakini bado najiuliza mwanamke Yule ni nani? Kwa nini kamuua Amos? Akasema Mathew

“ Inavyoonekana Yule mwanamke alikuwa karibu akifuatilia maongezi yetu mimi na Amos lakini nashindwa kuelewa ni kwa nini amuue Amos hasa pale ambapo alikuwa trayari kunieleza jambola muhimu?
“ Jibu hapa ni rahisi tu.hakutaka Amos akueleze kile alichotaka kukweleza na ndiyo maana suluhisho pekee lilikuwa ni kumuua.But this woman ,who is she? Anaonekana ni mwanamke hatari na mwenye ujuzi wa hali ya juu wa kutumia silaha.kwa namna alivyomuua Amos anaonekana ni muuaji mzoefu sana.We need to find out who is she? Katumwa na nani amuue captain Amos? Na kuna siri gani ambayohakutaka Amos akueleze? Akasema Mathew.
“ Ninaskitikika sana kwa amos kufa namna ile lakini ukweliutabaki wazi kwamba Amos hakuwa vile tulivyomdhania.Alikuwa na mtandao wake wa siri .Wait ! I remember something…..” Peniela akanyamaza ghafla kwamba kuna kitu alikikumbuka
“ Umekumbuka kitu gani? Akauliza Mathew
“ Nimekumbuka usiku ule Elibariki aliposhambuliwa nilipigiwa simu na mwanamke mmoja nisiyemfahamu na akanifahamisha kwamba nikutane naye ili nimchukue elibariki.Ulikuwa ni usiku na kichwani alivaa kofia lakini nilifanikiwa kuiona sura yake.Nimeikumbuka vyema ..Nihuyu mwanamke aliyemuua Amos...Yes it was her. Yule mwanamke aliyemuoka Elibariki ndiye huyu aliyemuua Amos” akasema Peniela

“ are you sure Peniela? Akauliza Mathew

“ I’m sure Mathew.Sura ile nimeikumbuka kabisa na hasa sehemuya mashavu...Its her” akasema Peniela.Mathew akafikiri kidogo na kusema

“ who exactly is this woman? Akauliza Mathew.

“ I don’t know her.Lakini nina hakika kabisa ndiye Yule ambaye alikuwa na Elibariki usiku ule aliposhambuliwa.”

“ Tunatakiwa tumfahamu mwanamke Yule na ndipo tutaweza kumfahamu yeye ni Nani.Anahusikaje katika shambulio lile la Elibariki na kwa nini amemuua Amos? Akasema Mathew
“ How are we going to find her” akauliza Peniela
“ I don’t know how but we must find her.Huu unaonekana ni mtandao hatari.Kama mwanamke Yule alikuwepo usiku ule Elibariki aliposhambuliwa basi yeye na mtandao wake wanafahamu mambo mengi na kuna sababu kubwa ya Amos kuuawa.Amos alikwamba kwamba wana mpango wa kuwafanya wewe na elibariki kuwa na nguvu kubwa.Ni mpango gani huo? Ni akina nani hawa wenye kupanga mipango hiyo ?

“ Mathew hili suala si la kupuuzia hata kidogo.Nina uhakika mkubwa kwamba ni kweli lazima kuna kuna jambo linaloendelea chini kwa chini kuhusiana na mimi na Elibariki.Ni jambo gani hilo na ni akina nani ambao wanapanga mipango hiyo ? Tunahitaji kulifahamu suala hili.Tukifanikiwa kumpata Yule mwanamke tutafahamu kila kitu”akasema Peniela.
Sura ya mwanamke Yule aliyepishana na Mathew huku akikimbia ikaendelea kuzunguka kichwani kwa Mathew.
“ who is this woman? Akajiuliza bila kupata jibu
“ anaonekana ni mwanamke mwenye kufahamu mambo mengi .Nakumbuka Elibariki aliniambia kwamba usiku ule lilipofanyika lile shambulio aliokolewa na mwanamke ambaye alimkabidhi kwa Peniela.kwa mujibu wa peniela ameikumbuka sura ya mwanamke Yule kwamba ni huyu aliyemuua Amos leo.Ninahakika mtandao aliomo utakuwa unafahamu mambo mengi sana kuhusiana na Elibariki na ninahisi kuna mambo mengi wanayafahamu pia kuhusiana na package ile toka kwa Dr Joshua.Lazima tumtafute mwanamke Yule kwa kila njia.Suala hili linazidi kuwa kubwa kila uchao” akawaza Mathew wakiwa garini
“ Unawaza nini Mathew? Akauliza Peniela.
“ Ninawaza mambo mengi sana na kubwa ni namna mambo mapya yanavyozidi kuibuka kila uchao..Hili la kuuawa amos limeniwashia taa nyekundu kuashiria kwamba mapambano haya kwa sasa yamefikia sehemu ya hatari zaidi” akasema Mathew

“ nakubaliana nawe Mathew.hata mimi sikutegemea kabisa kama suala hili lingeweza kufika hapa lilipofika.hata hivyo nawapongeza kwa hatua kubwa iliyofikiwa hadi hivi sasa.Mmegundua mambo mengi makubwa na mazito.Kinachotakiwa kwa sasa nikushirikiana kuhakikisha kwamba mambo haya yanafika mwisho na tunaizika kabisa mitandano hii ya hatari hapa nchini na hasa team SC41”

“Uko sawa Peniela lakini bado tuna kazi kubwa ya kufanya mbeleni.watu tunaopambana nao niwatu hatari na wenye nguvu lakinininwahakikishia kwamba tutapambana hadi tone la mwisho la damu na nitaongoza mapambano kuishinda vita hii” akasema Mathew safari ikaendelea hadi walipowasili nyumbani kwa Mathew.Anitha akawafungulia geti.
“ What happened? Kuna tatizo Mathew ?akauliza Anitha baada ya Mathew na Peniela kushuka garini
“ yes there is a problem.Eva amekwisha rejea?
“Ndiyo amerejea yuko na madaktari chumbani.”akasema Anitha.

“ Naomi yuko wapi? Akauliza Mathew

“ Yuko nyuma bustanini anapumzika.who is she? Akauliza Anitha

“ Nitakufahamisha baadae.kwa sasa muandalie chumba cha kulala ataishi nasi hapa.Vile vile mpeleke peniela chumba cha mapumziko akapumzike kwa muda.”akasema Mathew kisha akaongoza hadi katika chumba alimolazwa Rosemary Mkozumi.hali yake ilikuwa nzuri na alikuwa amekaa kitandani akionge ana madaktari wale wawili pamoja na Eva.Mara tu Rosemary alipomuona Mathew akamkumbuka

“Its you..Its you who shot henry..its you…!!..akapiga ukulele na kutaka kuinuka pale kitandani madaktari wakamzuia kwanialikuwa na pingu mguuni..

“ Anaendeleaje? Mathew akawauliza madkatari

‘Kwa sasa hali yake imetulia na anaendelea vizuri”
“kwa hiyo ninaweza kumfanyia mahojiano? Akauliza Mathew

“ Nadhani ungesubiri kidogo kabla ya kumfanyia mahojiano ili hadi hapo hali yake itakapokuwa nzuri kabisa. “akashauri mmoja wa wale madaktari

“ Thank you doctor ..we’ll take it from here” akasema Mathew
“ what ?! akauliza Eva

“Your job here is done you can go now.! Akasema Mathew
“ You are kidding Mathew.Huyu mama bado anahitaji usimamizi wa madaktari na hawezi kuhojiwa kwa sasa” akasema Eva

“ Thank you so much for your help but you job is done here too,so you can go now.Naomi atabaki hapa kwetu na kama kutakuwa na tatizo lolote nitakutaarifu” akasema Mathew.Eva akaonekana kukerwa sana na kauli ile ya Mathew akamtazama kwa hasira na kusema

“ Mathew can we talk for a minute?
Mathew na Eva wakatoka nje ya kile chumba
“What are you doing Mathew? Akauliza Eva
“ I’m doing my job Eva” akajibu Mathew

“ Mathew mbona unajiweka katika hatari kubwa . Huyu mama bado anaumwa na anatakiwa uangalizi wa madaktari kwa nini unakuwa mbishi Mathew?
“ Eva this is my job and I’m going to do it the way Iwant.Huyu mama ana taaifa za muhimu sana ambazo ni lazima tuzipate.we don’t have that time to wait so if you don’t mind can you please go and let me do my job? Akasema Mathew

“ Ok I’m going but don’t you ever find me again for any help” akasema Eva huku akiingia ndani ya kile chumba kwa hasira na kuwaomba wale madaktari waondoke zao.
Baada ya Eva na madaktarikuondoka Mathew akarejea ndani ya chumba alimokuwamo Rosemary mkozumi akamtazama kwa sekunde kadhaa

“ Now its just me and you..Today I’m your angel of death..” akawaza Mathew na kuufunga mlango akatoka



TUKUTANE SEHEMU IJAYO…
 
MKUU USIONDOKE NIMEFIKA nilikuwa zoezi kidogo .salama wakuu za j2 na week end??

nategeme week end ya leo itakuwa na kupofoa macho.
Safi mkuu. Tupe vitu tuendelee kula movie bila tabu. Ngoja nitafute wine ikae karibu ili nikianza kuburudika nisipoteze concentration
 
Yaani hii tabia ya kutoa taarifa polisi ndio nilipomuona bado mburura. Kwa mfano mara mwisho wamegombana na Matthew, akasusa akashuka kwenye. Nikasema atakwenda kushtaki tena. Ila sijamsikia kitambo sana
bora yake yy lkn sio mjinga elibariki
 
PENIELA SEASON 3

SEHEMU YA 14

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Mathew can we talk for a minute?
Mathew na Eva wakatoka nje ya kile chumba

“What are you doing Mathew? Akauliza Eva
“ I’m doing my job Eva” akajibu Mathew
“ Mathew mbona unajiweka katika hatari kubwa . Huyu mama bado anaumwa na anatakiwa uangalizi wa madaktari kwa nini unakuwa mbishi Mathew?
“ Eva this is my job and I’m going to do it the way Iwant.Huyu mama ana taaifa za muhimu sana ambazo ni lazima tuzipate.we don’t have that time to wait so if you don’t mind can you please go and let me do my job? Akasema Mathew
“ Ok I’m going but don’t you ever find me again for any help” akasema Eva huku akiingia ndani ya kile chumba kwa hasira na kuwaomba wale madaktari waondoke zao.
Baada ya Eva na madaktarikuondoka Mathew akarejea ndani ya chumba alimokuwamo Rosemary mkozumi akamtazama kwa sekunde kadhaa
“ Now its just me and you..Today I’m your angel of death..” akawaza Mathew na kuufunga mlango akatoka



ENDELEA………………….


Moja kwa moja akaelekea nyuma ya nyumba alikokuwa amekaa Naomi akipung a upepo.Mara tu alipomuona Mathew akainuka na kumfuata

“ Naomi karibu sana.Hapa ni nyumbani kwangu na wewe utaishi hapa pia.Nina rafiki zangu ambao ninaishi nao hapa ambao wengine tayari umekwisha onana nao.” Akasema Mathew

“ Nashukuru sana .Nimeipenda nyumba yako nzuri sana.Imetulia na sikamalile gereza nililokuwa nimefungiwa.Habari ya kule ulikokwenda? Ulifanikiwa kukipata ulichokuwa unakitafuta? Akauliza Naomi.Mathew akasita kidogo kumweleza chochote kuhusiana na kile kilichotokea kule nyumbani kwa Rsemary Mkozumi
“Naomi ninashukuru sana kwa msaada wako mkubwa .Ninaomba kama hutajali twende ndani tukaongee.Kuna mambo mengi ya kufahamishana ikiwamo kukufahamisha kwa watu ” akasema Mathew kisha akaongozana na Naomi hadi ndani Sebuleni akawaita Anitha ,Peniela na jaji Elibariki.
“ndugu zangu nimewaiteni hapa kuna mambo muhimu ninataka tuongee.Imekuwa ni bahati tumepata fursa nyingine ya kukutana sote pamoja.”akasema Mathew akanyamaza kidogo kisha akaendelea
“ Siku ya leo imekuwa ni siku ngumu na chungu sana kwetu sote.Tumewapoteza watu wetu wa muhimu katika maisha hyetu.Tukianza na Elbariki,umempoteza mkeo mpendwa Flaviana.Hili ni jambo zito sana na inauma sana japokuwa kama mwanaume lazima ujikaze na ukubaliane na hali halisi .Ninayafahamu machungu ya kuondokewa na Yule mtu w a karibu yako sana na uliyempenda kwani hata mimi niliwahi kuondokewa na familia yangu yote kwa hiyo ninafahamu jaji Elibariki anapitia kipindi gani kwa sasa.Msiba huu si wako peke yako ,ni wetu sote na sote tumeumizwa na jambo hili.kwa niaba yangu , Anitha na Peniela tunakupa pole sana na binafsi ninakuhakikishia kwamba sintalala usingizi hadi nihakikishe kwamba wale wote waliosababisha kifo cha mkeo Flaviana wanapatikana na kufikishwa mbele ya sheria ili haki itendeke.Ninachokuomba jipe moyo,tuko pamoja na tushirikiane katika jukumu zito lililoko mbele yetu na tuhakikishe kwamba tunaikamilisha kazi hii vizuri”akasema Mathew na kunyamza kidogo halafu akaendelea,
“ Peniela leo hii umempoteza mlezi wako ambaye alikuwa ni mtu wa muhimu sana katika maisha yako.Japokuwa alikuwa na matattizo yake ya kibinadamu lakini nina hakika kifo chake kimekuumiza sana .Kwa niaba yangu,Anitha na jaji Elibariki tunakupa pole nyingi sana kwa kumpoteza mtu wako wa muhimu sana na tunakuahidi ushirikiano mkubwa hasa katika kipindi hiki kigumu.Ulimpenda sana John na njia pekee ya kumuenzi kwa yale mema yote aliyokufanyia ni kwa kuhakikisha kwamba tunaikamilisha operesheni ya kuzuia uuzwaji wa package ya Dr Joshua na kuhakikisha inatua mikononi mwetu.Kabla ya kifo chake John alisisitiza sana kwamba lazima tuhakikishe jambo hili linafanikiwa kwa gharama zozote na tusiiache package hiyo ikachukuliwa .Kwa hali hiyo basi ninakuomba sana Peniela kwa muda huu mchache yasahau machungu yote ya kifo cha John na tuelekeze nguvu zote katika kuhakikisha tunaikamilisha operesheni hii.”akasema Mathew.
“ Mathew ninashukuru sana kwa kusimama pamoja nami katika wakati huu mgumu. Lakini pamoja na yote yaliyotokea ninawahakikishia kwamba niko imara na akili yangu yote nimeielekeza katika suala lililoko mbele yetu.Ni kweli john alikuwa mtu muhimu kwangu lakini kifo chake hakiwezi kunifanya nipoteze muelekeo katika suala zito linalotukabili.Naomba msiwe na shaka yoyote kuhusu mimi niko vizuri kabisa kuifanya kazi” akasema Peniela
“ Ahsante sana Peniela kwa kutuhakikishia kwamba uko imara.Binafsi ninawaahidi kwamba nitawongoza katika mapambano haya na tutashinda.” Akasema Mathew

“ jambo lingine ambalo ninataka niwafahamishe ni kwamba leo tumepata mgeni.Anaitwa Naomi.Huyu ni mtoto wa waziri wa zamani wa kilimo anaitwa Henry.Naomi ametoa mchango mkubwa sana sikuya leo katika kumpata Rosemary Mkozumi.Kwa hiyo basi kwa sasa ataendelea kukaa nasi hapa kwani bado anahitaji sana msaada wetu sisi ili aweze kuendelea na maisha yakeya kawaida.” Akasema Mathew kisha akamgeukia Naomi
“Naomi hawa uwaonao hapa ni wenzangu na wote shughuliyetu ni moja.Sisi ni watu tunaoshughulika na masuala ya usalama kwa hiyo kwa hapa uko sehemu salama kabisa.Mimi ninaitwa Mathew,Yule pale anaitwa jaji Elibariki,Yule pale ni Anitha na yule pale anaitwa Peniela.” Mathew akafanya utambulisho

“ Peniela ?!!..akasema Naomi huku akitabasamu

“ Sura yako si ngeni sana machoni pangu.Nilipokuona nilikuwa najiuliza nimewahi kukuona wapi nimekumbuka nilikuona katika Luninga .Uliwahi kuwa na kesi mahakamni na ukashinda ,right? Akauliza Naomi
“ Ndiyo Naomi” akajibu Peniela huku akitabasamu

“ nakumbuka pia uliwahi kuwa na maduka maarufu sana ya mavazi ?

“ Ndiyo Naomi niliwahi kuwa na maduka ya mavazi lakini baada ya kupatwa na yale matatizo ya ile kesi niliyafunga maduka yangu.”

“ Nilikuwa mnunuzi mzuri sana wa nguo navipodozi kutoka katika maduka yako.Leo nimefurahi sana kukuona Peniela.Kumbe ni mrembo hivi”akasema Naomi na wote pale sebuleni wakacheka.Naomi na peniela wakakumbatiana..
“ Naomi utakaa hapa pamoja na sisi kwa muda wakati tunaendelea kulifanyia kazi suala lako na chochote utakachohitaji usisite kutuambia.Kwa sasa Anitha atakupeleka chumbani kwako ukapumzike wakati sisi tunaendelea na maongezi yetu ya kikazi” akasema Mathew
“Nashukuru sana Mathew kwa msaada wako na kunitoa kule kifungoni.Hapa kwako nimekaa mwa muda mfupi lakini ninajiona ni mwenye furaha sana na amani tele moyoni mwangu.Nilipokuwa ndani ya lile jumba sikuwa na tumaini kama siku moja na mimi nitakuwa huru tena lakini Mungu ni mwema siku zote na amenikutanisha na ninyi watu wema.Ahsante sana.Endapo kuna lolote mnalotaka kulifahamu kuhusu baba yangu mimi niko tayari kuwasaidia muda wowote kwani ninayafahamu mambo yake mengi sana” akasema Naomi
“ Ahsnate sana Naomi.Tutakufahamisha tukihitaji msaada ako ”akajibu Mathew.
Anitha akainuka kwa lengo la kumpeleka Naomi chumbani lakini akakataa

“ Dada Anitha,Mimi nimekuwa kifungoni kwa miaka zaidi ya minne na sitaki tena kuendelea kukaa kaa chumbani .Nataka niyafurahie maisha ya uhuru hivyo ninakwenda kule nje kuogelea” akasema Naomi na kutoka nje.
“ She’s so happy” akasema Peniela baada ya Naomi kutoka

“ Naomi ni mtoto wa pekee wa Henry waziri wa zamaniwa kilimo ambaye kwa sasa ana mahusiano ya kimapenzi na Rosemary mkozumi.kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba Henry ndiye aliyesababisha yeye kujitumbukiza katika matumizi ya madawa ya kulevya.Naomi anadai kwamba anazifahamu siri nyingi za baba yake na aliwahi kumtisha kwamba siku moja anaweza akatoa siri zake jambo lililomuogopesha sana Henry na akaamua kumtumia kijana aliyekuwa katika mahusiano na Naomi ambaye alimshawishi na akakubali kujiingiza katika dawa za kulevya.lengo lilikuwa ni kumfanya Naomi aelekeze akili yake katika unga na asikumbuke chochote kuhusu mamboya baba yake. Naomi alijikuta akiboea katika madawa ya kulevya na maisha yake kuharibika kabisa.Baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya,Henry akamfungia ndani ya jumba na kumuwekea kila kitu na ulinzi mkali sana.kwa takribani zaidi ya miaka mine sasa Naomi hajawahi kutoka nje ya jumba almofungiwa.Tulimuahidi kumsaidia na kumtoa katika kifungo kile na ndiyo maana alikubali kwa moyo mmoja kushirikiana nasi na akatusaidia tukampata Henry ambaye alituingiza ndani ya jumba la Rosemary .Kwa hiyo Naomi anahitaji sana ushirikiano wetu sisi katika kumrejesha katika maisha yake ya awali.Kwa sasa amekwisha achana na matumizi ya dawa za kulevya na kinachofanyika sasa ni ingawa bado hajarejea katika ile hali yake aliyokuwa nayo awali i.” Akasema Mathew

“ usijali kuhusu hilo Mathew.Tutashirikiana kuhakiksha kwamba Naomi anarejea katika hali yake ya kawaida.Huyu ni mdogo wetu na hatuna budi kumsaidia.Baada ya kuikamilisha kazi hii iliyoko mbele yetu ninakuahidi kumshuguhulikia sana Naomi.”akasema Peniela.
“ Ahsante sana Peniela.Ila kuna jambo nimemficha na sijamweleza ukweli hadi hapo baadae.Her father is dead ”
“ henry is dead? How?
“ Alifariki katika purukushani iliyotokea nyumbani kwa Rose.Alijaribu kuzuia tusiweze kumpata Rose kwa hiyo sikuwa na namna nyingine ya kufanya.I shot him” akasema Mathew na sebule yote ikawa kimya

“ kwa sasa tusimweleze chochote hadi hapo baadae “akasema Mathwe
“ na vipi iwapo jambo hili litatangazwa katika luninga je itakuwaje? Akauliza Peniela

“ Tutamweleza ukweli wa kilichotokea na nina imani atatuelewa” akasema Mathew na kuendelea
“ Pamoja na siku ya leo kuanza vibaya lakini kuna mambo mazuri pia yametokea.Tumefanikiwa kumpata mtu ambaye tunadhani ndiye aliyekuwa nyuma ya wizi wa karatasizile zilizoibwa toka ikulu zenye kanuni za kutengeneza kirusi hatari.Rosemary natajwa kuwa na mawasiliano ya karibu na Habib Soud ambaye ndiye aliyetaka kuzinunua karatasizile na kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka wa mtu wangu ndani ya C.I.A ni kwamba Habib anachunguzwa na C.I.A kwa kufadhili makundi ya kigaidi.Ninahisi lengo lake la kutaka kununua karatasi zile ni kutumia kanuni zile kutengeneza kirusi ambacho wangeweza kukitumia katika mambo ya kigaidi.Rosemary amekuwa akipokea pesa nyingi kutoka kwa Habib na ninahisi kuna mambo mengi wanashirikiana na ninahisi kwamba yawezekana hata Rosemary naye pia akawa na mafungamano na makundi ya kigaidi.” akanyamaza kidogo na kuendelea
“ Rosemary pia amekuwa na mawasiliano na mtu mmoja aitwaye Samir asaad na katika mojawapo ya mawasiliano tuliyoyapata,Rosemary alimuhakikishia kwamba mzigo utapaatikana muda wowote kwani ana mawasiliano ya karibu sana na mtu aliye karibu na rais.Tulipochunguza zaidi tukagundua kwamba Rosemary alikuwa na mawasiliano ya karibu na Captain Amos ambaye ni mtu wa karibu sana na rais Dr Joshua.Hii inatupa picha kwamba mzigo ambao Rosemary alimuhakikishia Samir kuupata muda wowote ni hiyo package ambayo hata sisi tunaifuatilia.Tulitaka kupata uhakika toka kwa Captain Amos na tukaweka mtego wa kumpata ,tukaenda na Peniela kuonana naye mahala walikopanga wakutane.Peniela akaonana naye na baada ya kumbana na kumtolea vitisho Amos kuna mambo alitaka kuyasema kabla ya kuuawa.Peniela hebu simulia nini Amos alikisema?
“ Nilipokutanana Amos nilishindwa kujizuia nikapandwa na hasira na kumtolea bastora.Nilimtaka anieleze ni kwa nini alitusaliti na kutoa taarifa za kuhusiana na package kwa Rosemary ? aliniambia kwamba nikimuua nitafanya kosa kubwa sana kwani tayari wana mpango mkubwa kwa ajili yangu na Elibarii wa kutufanya wenye nguvu.Nilimuuliza yeye na nani ambao wana mpango huo na akawa tayari kunieleza lakini ghafla mlango ukapigwa teke na mwanamke mmoja akajitokeza akiwa na bastora mbili akamchakaza Amos kwa risasi kisha akatoweka.Lilikuwa ni shambulio la haraka sana na ambalo hatukuwa tumelitegemea.Captain Amos alifariki dunia palepale.Baada ya tukio lile nikaikumbuka sura ya Yule mwanamke.Ni Yule ambaye alikuwa na Elibariki usiku ule aliposhambuliwa.”

“ What ?! akauliza jaji Elibariki kwa mshangao.

“ Are you sure Peniela?

“ Ndiyo Elibariki.Japokuwa ulikuwa ni usiku lakini niliweza kumuona vyema Yule mwanamke sura yake na baada ya kumuona leo hii nimekumbuka ni Yule Yule uliyekuwa naye usiku ule”akasisitiza Peniela
“ Nikweli usiku ule niliokolewa na mwanamke ambaye aliniondoa toka pale kwenye eneo la tukio naakanikabidhi kwa Peniela..Hakunieleza jina lake na wala sababu ya kuniokoa.Nimestuka kidogo kusikia kwamba leo hii amejitokeza tena.Ni nani huyu mwanamke? Akauliza jaji Elibariki

“ Hilo ndilo swali tunalotakiwa kulitafutia majibu.Tunatakiwa kumfahamu Yule mwanamke ni nani .Inaonekana wazi kwamba kuna mpango Fulani unaandaliwa na watu au kikundi cha watu unaowahusisha jaji Elibariki na Peniela.” Akasema Mathew
“ Who are these people? How do they know about us? Akauliza jaji Elibariki
“ Kwa sasa ni mapema mno kulijibu swali lako lakini tunayo sehemu ya kuanzia kutafutia majibu yetu.Tunaye Rosemary Mkozumi.Huyu ana majibu ya maswali yetu mengi tu.Nadhani ni wakati sasa wa kuweza kuyapata majibu ya maswaliyetu.I’m going in there to find answers.Anitha wewe utaendelea kuifanyia uchunguzi simu na kompyuta ya Amos.Elibariki na peniela mnaweza kwenda kupumzika kwa muda .”akasema Mathew na kuinuka akaelekea chumbani kwake.
“ Namuonea huruma sana huyu Rosemary kukutana na Mathew.Kwa usalama wake ni bora akamueleza ukweli kwa kila atakachomuuliza bila ya kumficha.”akasema Anitha baada ya Mathew kuondoka pale sebuleni
“ Mathew hata mimi ninamuogopa sana.Ni mtu mzurilakini awapo kazinihuwa nimtu tofauti kabisa ”akasema jaji Elibariki

“ By the way ninaomba kukuuliza Peniela.Ulikuwa na Mathew siku alipoitwa na John Mwaulaya hospitali.unaweza kufahamu waliongea jambo gani? Akauliza Anitha

“ Kilichotokea usiku ule kilikuwa cha kushangaza sana.John aliomba aonane naMathew na maadui wa siku nyingiwalikutana na waliongea kana kwamba ni marafiki wa muda mrefu.Waliongea kwa zaidi ya dakika hamsini na mpaka leo hakuna anayefahamuwaliongea kitu gani.Mazungumzo yao yamebaki kuwa siri ya Mathew ”akasema Peniela.
“lazima kuna jambo zito waliongea na ninatumai iko siku Mathew atatueleza waliongea kitu gani”akasema Anitha kisha akainuka na kuelekea ofisini, jaji Elibariki akamshika mkono Peniela wakaelekea chumbani.




TUKTANE SEHEMUIJAYO………
 
PENIELA SEASON 3



SEHEMU YA 15

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

“ Mathew hata mimi ninamuogopa sana.Ni mtu mzurilakini awapo kazinihuwa nimtu tofauti kabisa ”akasema jaji Elibariki

“ By the way ninaomba kukuuliza Peniela.Ulikuwa na Mathew siku alipoitwa na John Mwaulaya hospitali.unaweza kufahamu waliongea jambo gani? Akauliza Anitha

“ Kilichotokea usiku ule kilikuwa cha kushangaza sana.John aliomba aonane naMathew na maadui wa siku nyingiwalikutana na waliongea kana kwamba ni marafiki wa muda mrefu.Waliongea kwa zaidi ya dakika hamsini na mpaka leo hakuna anayefahamuwaliongea kitu gani.Mazungumzo yao yamebaki kuwa siri ya Mathew ”akasema Peniela.
“lazima kuna jambo zito waliongea na ninatumai iko siku Mathew atatueleza waliongea kitu gani”akasema Anitha kisha akainuka na kuelekea ofisini, jaji Elibariki akamshika mkono Peniela wakaelekea chumbani.



ENDELEA……………………..



“ Pole sana Peniela kwa kilichotokea.Nimestuka sana kusikia kuhusu kilichotokea ulipokwenda kuonana na Amos.Sijui ningefanya nini kama kwa bahati mbaya ungeshambuliwa” akasema jaji Elibariki akiwa chumbani na Peniela.

“ Lilikuwa ni shambulo la ghafla sana ambalo hata sisi hatukulitarajia kabisa.Mini nilitanguliwa kuingia chumbani kuonana na Amos naMathew akabaki nje .Mara tu nilipoingia ndani na kukutana uso kwa uso na Amos hasira zikanipanda nikachomoa bastora nikamuuliza ni kwa nini anashirikiana na Rosemary Mkozumi na kutoa taarifa zetu? Amos akanijibu kama nilivyowaeleza na nilipomtisha zaidi alikuwa tayari kabisa kunieleza nimpango gani huo walio nao juu yetu na mara tu alipoanza kunieleza akatokea Yule mwanamke na kummiminia risasi.Shambulio lile limetokea kwa haraka sana na katika muda mfupi.Mwanamke Yule alikuwa katika nafasi nzuri sana ya kuweza hata kuniua na mimi kwani sikuwa nimejiandaa kwa rabsha zozote lakini aliniacha na inaonekana kabisa kwamba lengo lake lilikuwa ni kumuua Amos tu.”akasema peniela.jaji Elibariki akashika kichwa chake akatafakari kidogo na kusema
“lakini watu hawa ni akina nani? Wametufahamuje sisi? Wana mpango gani na sisi? Akauliza jaji Elibariki
“ kama alivyosema Mathew kwamba maswali hayo ni magumu sana kujibika kwa sasa hadi hapo utakapofanika uchunguzi na tutafahamu kila kitu lakini tukae kwa tahadhari kubwa kwanikuna watu wanaotufahamu na kutufuatilia na wana mipango juu yetu.Umakini mkubwa sanaunahitajika kwa kila tunachokifanya.Elibariki sikutegemea kabisa kama suala hili lingeweza kufika hapa lilipofika.Kuna wakati najikuta nikiogopa kutokana na namna jambo hili linavyochukua sura mpya kila uchao,namna mambo mazito yanavyoibuliwa kila siku.”akasema Peniela
“ Hata mimi sikufikiria kama tunaweza kufika hapa tulipofika.Nilimpa Mathew kazi ya kumtafuta muuaji wa Edson na nilitegemea kwa uwezo wa Mathew ingechukua siku chache tu kuikamilisha kazi ile na kumfahamu muuaji na nilifanya hivi kwa lengo la kulisafisha jina lako .Nilitaka muuaji halisi apatikane iliumma wote ujue kwmba ulisingiziwa ile kesi na kwamba sikukuachiahuru kwa makosa bali hukuwa na hatia,lakini mambo yaliyoibuliwa na yanaoendelea kuibuliwa katika uchunguzi huu yanaogopesha sana.Ni mambo mazito na sijui nini mwisho wake.Kila siku unalala hujui kesho nini kitaibuka.Sikuwahi kufahamu kama hapa nchini kuna kitu kinaitwa team SC41.Kuna mambo mengi ambayo sikuyafahamu hadi lilipoanza sakata hili.” Akasema jaji Elibariki
“ usihofu Elibariki kila kitu kitafika mwisho.Anyway tuachane na hayo,unaendeleaje? Akauliza peniela

“ Kusema kweli sijielewi Peniela.Siwezi kusema kwamba ninaendelea vizuri wala vibaya,kiujumla naona akili yangu kama imefika kiwango cha mwisho cha kufikiri .Ninawaza mambo mengi sana .Hapa nilipo sifahamu hatima yangu ni nini..Sijui lini nitatoka ndani ya jumba hili na kuendelea na maisha yangu ya kawaida .sijfahamu maisha yangu yatakuaje baada ya kutoka humu ndani,ninawaza mambo mengi mno” akasema jaji Elibariki.Peniela akamtazama na kumuonea huruma sana.
“ Pole sana elibariki lakini nina kuhakikishia kwamba tutafanya kila linalowezekana ili kulifikisha mwisho suala hili na maisha yako yatarejea kuwa ya kawaida.” Akasema peniela
“ ahsante sanaPeniela.Ahsante kwa kunipa moyo.Vipi kuhusu wewe unaendelaje? Akauliza jaji Elibarki
“ John was a bastard na kifo chake kimeniumiza sana lakini kutokana na mambo yaliyoko mbele yangu nimeamua kuwa jasiri na kuendelea kukabiliana na mambo mazito yaliyoko mbele yetu.John is gone na maisha lazima yaendelee.Ni wakati wangu sasa wa kutafuta uhuru wangu.Nataka nihakikishe nimiangusha team SC41.Sitaki kusikia tena kikundi kama hiki kikiendelea.Nikifanikiwa jambo hili nitakuwa huru na nitaweza kuendelea namaisha yangu ya furaha .Nataka nianze upya maisha yangu nikiwa nawe Elibariki mwanaume wa maisha yangu ambaye ninakuwaza kila sekunde..”akasema Peniela na mara akastuka baada ya kukumbuka kitu
“ Elibariki I’m so sorry.Nimebebwa na hisia na kutamka maneno ambayo sikupaswa kuyatamka kwa wakati huu ambao unaomboleza kifo cha mkeo.Nisamehe sana Elibariki sitaki nionekane kwamba nimefurahia kifo cha Flaviana ” akasema Peniela
“Peniela ulichokisema ni ukweli ulio wazi na hakuna sababu ya kuficha.Sifurahii kwa kifo cha mke wangu Flavana lakini kwa vile kimetokea basi hii ni fursa yetu sisi kuweza kuikamilisha mipango yetu ya kuwa pamoja.Wanasema kwamba kila jambo hutokea kwa sababu maalum na inawezekana kabisa hata suala hili la kifo cha Flaviana limetokea kwa sababu maalum na sababu yenyewe ni mimi na wewe kuwa pamoja.” Akasema jaji Elibariki

“ Elbariki usiseme hivyo tafadhali.Haipendezi kuongelea masuala haya kwa wakati huu wa majonzi tunapoomboleza kifo cha Flaviana.”akasema Peniela
“ Peniela hakuna ubaya wowote wa kuliongelea suala hili.Flavana is gone and she will never come back.Hakuna ubaya kwa sisi kuanza kuyapanga maisha yetu ya mbele.Tunapendana kwa dhati na hakuna sababu ya kuficha tena kuhusu suala hili.” Akasema jaji Elibariki.Peniela akamtazama akatabasamu na kusema

“ usijali jaji Elibariki .Tutapata muda mzuriwa kuongea kuhusu mambo haya lakini kwa sasa tuelekeze nguvu katika suala lililoko mbele yetu ili tuhakikishe kwamba tunapoanza maisha mapya tunakuwa huru na hatufungwi na kitu chochote”akasema Peniela
“ Uko sawa peniela.Vipi kuhusu John mwaulaya anazikwa lini?

“ Mpaka sasa bado hatujaamua atazikwa lini na wapi .”akasema peniela.Jaji Elibariki akainama na kuzama mawazoni
“ unawaza nini Elibariki?

“ Peniela najitahidi sana kujizuia nisiwe na mawazo lakini ninashindwa.Kuna mambo yanaumiza mno,kwa mfano sintaweza kuhudhuria mazishi ya mke wangu.Jambo hili linaniumiza mno.” Akasema jaji Elibariki

“ Ni kweli inauma sana lakini nitakwenda mimi kukuwakilisha na nitahakikisha nimetupia ua kwa niaba yako.Ntasema maneno yale ambayo ungetamka wewe kwa mdomowako kama ungekuwepo wakati Flaviana akizikwa “ akasema peniela
“ Ahsante sana peniela”



*******



Geti jesi linafunguliwa katika jumba moja kubwa la ghorofa tatu na gari nyeusi aina ya BMW likaingia kisha geti likafungwa.Toka ndani ya gari lile msichana mmoja mwenye mavazi meusi akashuka garini akavua miwani yake na kisha akaanza kutembea kiukakamavu kuelekea ndani ya lile jumba.Mbele ya mlango wa kuingilia ndani walisimama walinzi wawili waliovaa suti nyeusi .Yule msichana akasalimiana nao na kisha mmoja wao akamfungulia mlango na kumuongoza ndani,wakapanda hadi juu kabisa ya ghorofa ambako kulikuwa na sehemu nzuri sana ya kupumzikia .Mlinzi akamuelekeza Yule msichana sehemu ya kukaa na kisha akafika msichana mmoja aliyevaa suruali nyeusi na shati jeupe aliyeonekana kama mtumishi wa ndani akamsalimu Yule dada kwa adabu na kumuuliza kinywaji anachotumia.Yule dada akagiza mvinyo wowote mkali .Baada ya dakika kama nne mvinyo ukaletwa na Yule dada akanywa funda kubwa.Akatoa pakiti ya sigara na kuchomoa moja akaiwasha akavuta huku akipuliza moshi mwingi .Baada ya dakika kama kumi hivi akatokea mzee mmoja mwenye umbo kubwa aliyevaa shati refu jeupe lililofingwa nusu na kukiachawazikifua chake kikubwa kilichoibeba mikufu miwilimikubwa ya dhahabu..
“ Jesica ! akasema Yule mzee aliyekuwa na sauti ndogo tofauti na mwili wake

“ Hallo Vincent” akasema Jesica huku akisimama na kusalimiana na Yule mzee

“ Karibu sana Jessica” akasema Vincent
“ Nashukur u sana Vincent.” Akasema Jesica
“ Sikutegemea kabisa kama ningeweza kukuona hapa mida hii.Kuna tatizo lolote Jesica? Akauliza Vincent
“ Vincent Kuna jambo limetokea “

“ Jambo gani Jesica?
“ Amos is dead..I shot him” akasema Jessica,Vincent akamtazama kwa makini na kusema
“ How it happened?
“ They discovered him.Peniela na kundi lake la Team SC41 tayari wamegundua kwamba Amos amewasaliti.Wamegundua mawasiliano yake na Rosemary Mkozumi na kwamba alikuwa akitumiwa na Rose kupata taarifa za kuhusiana na package iliyoko ikulu inayotaka kuuzwa na Dr Joshua.Nilipata taarifa ambazonadhanihata wewe tayari umekwisha zipata kuhusu tukio lililotokea nyumbani kwa Rosemary Mkozumi ambapo Henry waziri wa zamani wa kilimo ambaye kwa sasa ana mahusiano ya kimapenzi na Rose amepigwa risasi na kufariki na Rosemary Mkozumi bado hajulikani alipo.Baadae Amos alinipigia simu na kunieleza kwamba Peniela amempigia simu na kumtaka waonane kuna jambo la dharura hivyo Amos akanitaka tuongozane wote mpaka Mlimba lodge kwenda kuonana na peniela na baada ya hapo tuelekee hospitali tukafahamu nini kinachoendelea kuhusiana na msiba wa John Mwaulaya. Kwa kuwa ninafahamu ushirika wa Rosemary na Amos,na tayari nilifahamu kilichotokea kwa Rose nilihisi lazima kuna jambo lisilo la kawaida katika mwito ule.Nilikuwa sahihi kumbe Team SC41 waligundua kwamba Amos na Rosemary ni washirika.Peniela alifanikiwa kumuweka Amos chini ya ulinzi na sikutegemea kabisa kama Amos anaweza kuwa muoga kiasi kile kwani alipotishwa kidogo tu akataka kuanza kutoa siri.Nilikuwa mlangoni na niliyasikia maongezi yao yote na Amos alianza kumueleza Peniela kuhusu mipango inaopangwa juu yake yeye na Elibariki .kwa kuelekezewa bastora tu Amos alikuwa tayari kutoa siri nikaogopa iwapo angeteswa angeweza kusema kila kitu na hata kuhusu sisi hivyo nikaona njia pekee ni kumuua tu.” akasema Jesica.Vincent akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Congratulations Jesica.You did a wonderfull job.Ulifanya vizuri sana kumuua Amos.kwa ufupi hata mimi na wenzangu ambao ni wafadhili wakuu wa chama tulikuwa na mpango kama huo kwani hatujaridhishwa kabisa na maamuzi ya Deus Mkozumi kutaka kumuweka mtu kama Elibariki kugombea nafasi kubwa ya urais.Sisi tuna mtu wetu ambaye tuna imani endapo akishika madaraka atatusaidia sana lakini Deus amekuwa akishikilia msimamo wake wa kutaka kumpigania jaji Elbariki agombee urais kupitia chama chetu .Anataka kumtumia Elibariki kwa manufaa yake mwenyewe.Hatuko tayari kwa hilo na jambo hili ulilolifanya leo umeturahisishia sana kazi yetu kwani Deus alikuwa anamtegemea sana Amos kwa hiyo kama Amos amefariki sina hakika kama Deus atakuwa na nguvu ya kutosha kuweza kuikamilisha ndoto yake kwani ni Amos pekee aliyekuwa na uwezo wa kumunganisha na Elibariki..By the way hukuacha nyayo zozote katika eneo la tukio kwa sababu nina hakika lazima uchunguzi utafanyika.”

“ Hapana hakuna nyayo yoyote iliyoachwa.Nilifanya jambo hili kitaalamu sana”.

“ Good.Umefanya vizuri sana. “ akasema Vincent na kumuita mlinzi wake aliyekuwa amesimama mbali kidogo na pale walipokuwa wamekaa,akafika haraka akamnong’oneza jambo na Yule mlinzi akaondoka
“.Jesica kuna jambo nataka kulifahamu , ukiacha John Mwaulaya na Amos kuna mtu mwingine ambaye anafahamu kwamba wewe uko team Sc41? Akauliza Vincent

“ Niliingizwa Team SC41 na Amos na nilitaka ushiriki wangu uwe ni wa siri kwa hiyo wanaofahamu ushiriki wangu katika kundi hili ni hao wawili tu.Japokuwa nimemuua lakini Amos alikuwa mtu wangu wa karibu sana na nilijiunga na Team Sc41 kwa sababu yake baada ya kuniomba niwe nikimsaidia katika baadhi ya majukumu yake aliyokabidhiwa na Team SC41.Nilimsaidia kazi kadhaa na mojawapo kubwa ilikuwa ni ile niliyomuokoa jaji Elibariki usiku ule alipotaka kuuawa.Baada ya watu hao wote wawili wawili kufariki ambao ndio waliokuwa wakinilipa I’m no longer a part of Team SC41. ”
“ Good ! nimefurahi kusikia hivyo.” akasema Vincent

“ Kwa hiyo Vincent nini kitafuata bada ya hapa? Akauliza Jesica

“ Kwa sasa endelea na kazi zako kama kawaida wakati tunaangalia upepo unavyokwenda baada ya kifo hiki cha Amos.Unajua Yule alikuwa mtu mkubwa alikuwa daktari w a familia ya rais kwa hiyo lazima uchunguzi utafanyika kubaini sababu ya kifo chake na aliyemuua lakini usihofu endapo kamakutakuw ana hatari yoyote sisi tutashughulika nayo.Nchi hii ni ya kwetu.” akasema Vincent.Mlinzi wake akareje ana kitabu ,akakichukua na kuandika cheki akampatia Jesica.
“ Nitakuwa nikikufahamisha kila kitu kuhusiana na kinachoendelea lakini kuna jambo nitaomba ulifanyie uchunguzi.Ninataka unisaidie kufanya utafiti Rosemary Mkozumi yuko wapi ? Idara yenu ya usalama wa taifa mnazo nyenzo za kuweza kupata taarifa mapema sana kwa hiyo nisaidie kufahamu mahala aliko Rosemary .Can you do that for me? Akauliza Vincent
“ Niachie suala hilo nitalifanyia kazi .Nitafuatilia ofisini ili nione kama kuna taarifa zozote zimepatikana kuhusu mahala alipo Rose.” akasema Jesica

“ Ahsante sana Jesica.Lifanyie kazi suala hilo kwani nina wasiwasi sana na kutoweka huku kwa kutatanisha kwa Rose .Yule ni mtu anayetufahamu sana sisi na anayafahamumamboyetu mengi kamasisi tunavyoyafahamu yak wake “: akasema Vincent akaagana na Jesica.

“ Sasa kidogo ninaweza kuvuta pumzi baada ya kuwa na uhakika Amos ametoweka.Huyu alikuwa ni mtu muhimu mno kwa Deus na ndiye alikuwa anamtegemea sana katika mpango wake.Kwa sasa mipango yake haitaweza kufanikiwa tena na ni nafasi yetu kumuandaa mtu wetu ambaye atatusaidia sana endapoatashika madaraka “ akawaza Vincent.



TUKUTANE SEHEMU IJAYO…
 
Ww miaka iyo ukuwa na simu wala kujua kama ipo kutokana na umasikin wako team SC 41 na pia viongoz wakubwa serkalin kama alivyokua baba yake peniela cm haikua tatizo walikua nazo za kutosha pia ww unaiona iyo laki mbili nyingi tatizo ni lile la umeskin wanajeshi wakubwa walikua na ela za kutosha kama uyo aliyemlea john
Unajua Mobile phones ziliingia sokoni miaka gani? Na hiyo laki mbili ya kumpa mtoto kwa miaka hiyo ya 1940 unaona ipo sawa? Na hiyo form four? Maana Back then kulikua na middle schools tu,. Vipi kuhusu huyo askari wa JWTZ kwa miaka hiyo, maana haikuwepo na badala yake tulikua na King African Riffle (KAR).
Inawezekana unayejaribu kunijibisha na kunibishia hapa ni kitukuu wangu.
 
Ungeweza kumueleza vzr kuwa simu zilikuwepo zamani bila kumuambia yeye masikini. Neno.. "umasikini wako" hapo limetumika viabaya..
Ndiyo matajiri wetu hao mkuu. Inabidi tuwavumilie tu ili maisha yaendelee.
 
Mkuu hadithi ni masilimulizi, au tuchukulie mfano mdogo wa muziki, kile wanachoimba sio kwamba wako hivyo. Mtu anaimba hajala siku 3, lakini hapo anasema kwa jinsi nilivyoshiba hata kucheza siwezi. Kwa wale waelewa wa hadithi, hii ni aina ya hadithi ambazo husoma huku nikitengeneza movie kichwani kwangu.
Nimejaribu kuanisha hayo kwa sababu ya umakini alioutumia mwandishi. Nimejaribu kumkumbusha namna ya kutumia mazingira na nyakati.
Mrejesho ni kitu muhimu sana kwa ajili ya maboresho.
Najua hadithi hii imevuta hisia za wengi, yote ni kwa sababu ya mirejesho ambayo Mtunzi aliwahi kupewa kwenye hadithi zake za mwanzo ambapo akaja kufanya maboresho ambayo yamemuimarisha yeye na kazi zake kiasi cha kuvuta hisia za wengi.
Kama tutasoma bila ya kutoa mirejesho tutakua hatutendi haki. Msanii anahitaji kukua na ili akue ni lazima tushiriki katika kumkuza, kimawazo, kihali na kiuchumi.
 
marhabaa, nafurahi kulitambua hilo, ila raha ya sie vibabu unaijua? Nina kabinti kabichii kamenigandaaaaa hako, acha kabisa, manake nakapigia singeli sio za kitoto

cc gwijimimi na kisukari kwa ushauri, huyu shunie nimtendeje?
Raha ya vibabu ipoje au kujua kulea au kuna lingine zaidi ya hilo
 
Mjinga sana yule dogo hajakomaa kiakil haoni mwenzake Jaj ametulia Japo anajua penuel anagongwa na raisi Dr.kigomba lakn amekaisha tu angekuwa Jasoni angeenda kutoa taarifa police kwamba raisi anakuja demu wangu
Hahhhhaah
 
Unajua Mobile phones ziliingia sokoni miaka gani? Na hiyo laki mbili ya kumpa mtoto kwa miaka hiyo ya 1940 unaona ipo sawa? Na hiyo form four? Maana Back then kulikua na middle schools tu,. Vipi kuhusu huyo askari wa JWTZ kwa miaka hiyo, maana haikuwepo na badala yake tulikua na King African Riffle (KAR).
Inawezekana unayejaribu kunijibisha na kunibishia hapa ni kitukuu wangu.
mkuu naungana na ww na hiki ulichokisema kwa waandishi makini na wenye uelewa na wanao dhamini fani yao huwa wanafurahia sana kukosolewa au kuonyeshwa makosa kama ulivyofanya ww.sababu ulichokifanya na kukisema ni huduma ambayo wao hulipia pesa nyingi sana ili waweze kuipata.lakini ww umetoa bure.wengi huwa wanasoma story na kuipotezea tuu.lkn ww umeona makosa hayo.
 
Back
Top Bottom