PENIELA SEASON 3
SEHEMU YA 12
MTUNZI: PATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Haraka haraka Anitha akachomoa kila kitu alichokuwa amekichomeka katika kompyuta ya Rose na kisha Mathew akachomoa bastora yake na kumuelekezea Henry kichwani
“ Ukitaka uwe salama wewe na mwanao ,kaa pale mezani na ujifanye ulikuwa unafanya kazi zako na usimwambie chochote kuhusu uwepo wetu humu.Ukithubutu kumweleza chochote Rose kwamba tuko humu nitakufumua kwa risasi.Tumeelewana? akasema Mathew.
“ Tumeelewana” akasema Henry kwa wasiwasi.
Rosemary Mkozumi baada ya kushuka garini moja kwa moja akaelekea katika ofisi yake ambako aliamini ndiko aliko Henry.Mara tu alipofungua mlango wa ofisi yake kikatokea kitu ambacho hakuwa amekitarajia.Henry aliruka toka katika meza aliyokuwa amekaa na kupiga ukulele akimzuia Rosemary kutokuingia mle ofisini.Wakati Rosemary akishangaa kitendo kile ikasikika milio ya risasi zilizotoka katika bastora yenye kiwambo cha kuzua sauti na henry akaanguka chini akaanza kutapa tapa huku akivuja damu nyingi.Kutahamaki Rose akajikuta aakitazamana na basora mbili toka kwa Mathew na Anitha.Aliishiwa nguvu akaanguka chini.
ENDELEA………………………
Haraka haraka Mathew akamshika mkono Rosemary mkozumi na kumvuta akamuingiza mle ofisini kisha akafunga mlango.Akamfuata Henry pale chini alipolalia dimbwi la damu akamgeuza
“ Henry !! akaita Mathew.Henry hakuitika na alionekana kupumua kwa shida sana.
“ Henry ! henry !!.Mathew akamtikisa.Henry akafumbua macho na kwa sauti ndogo akasema
“ Nao..nao…Naom……!! akashindwa kumalizia alichotaka kukisema akakata roho.Anitha akafumba macho alisikia uchungu sana .Mathew akainuka na kumsogelea Anitha
“ He’s gone” akasema kwa sauti ndogo.
“ I’m so sorry” akajibu Anitha.Kwa sekunde kadhaa walibaki kimya wakimtazama Rosemary aliyekuwa amelala chini hana nguvu huku jasho likimtiririka
“ What are going to do? Akauliza Anitha
“ Mtu tuliyekuwa tunamuhitaji sana ni Rosemary ambaye amejileta mwenyewe na hatuwezi kumuacha.Lazima tuondoke naye.We must do something to get us out of here” akasema Mathew na kuchukua simu yake akampigia Eva akamfahamisha kilichotokea na kumuomba alete gari la wagonjwa haraka sana pale nyumbani kwa Rosemary .Kisha ongea na Eva akamgeukia Anitha
“ Eva anakuja na gari la wagonjwa.Najua kama gari lile la wagonjwa likifika hapa ni lazima walinzi watataka kujua kilichotokea kwa hiyo basi lazima tumtoe Rosemary humu ndani na tuifunge hii ofisi kwa nje .Mlango huu wa ofisi ukifungwa kwa nje ni watu wawili tu wanaoweza kuufungua.Rosemary na Henry pekee kwa hiyo hata walinzi wake hawataweza kuufungua huu mlango na kujua klichotokea humu hadi hapo tutakapoondoka na kuwapigia simu na kuwataarifu kuhusu Henry.“ akasema Mathew na kumshika mkono Rosemary ambaye hakuwa na nguvu hata kidogo akamvuta na kumtoa nje ya ofisi yake.Anitha akaichukua kompyuta ile ya Rosemary pamoja na simu yake kisha akatoka mle ofisini na kuufunga mlango.Taa nyekundu ikawaka juu ya mlango kuashiria kwamba hakuna anayeweza kuufungua tena mlango ule kutokea nje zaidi ya Henry na Rosemary pekee.
“ Is she going to be ok? Akauliza Anitha kwa wasi wasi akimtazama Rosemary aliyekuwa akihema kwa taabu na jasho jingi kumtirirka
“ Don’t worry .She’ll be ok.Anaonekana amepatwa na mstuko wa ghafla kwa hiyo anahitajika daktari haraka kuweza kumsaidia.Mungu atusadie tufanikiwe kumtoa mama huyu salama humu ndani” akasema Mathew .Anitha akapiga magoti na kumfuta Rosemary jasho lililokuwa linamtiririka.
Baada ya dakika kama ishirini hivi simu ya Mathew ikaita alikuwa ni Eva.
“ Mathew tumezuiliwa hapa getini na walinzi kwamba hakuna gari inayoruhusiwa kuingia hapa bila kibali cha bosi wao Rosemary na hawana taarifa zozote za kuitwa kwa gari la wagonjwa” akasema Eva.
“ Naomba umpe simu mmoja wa walinzi niongee nao” akasema Mathew na baada ya sekunde kadhaa akasikia sauti nzito ya kiume ikiita
“ Hallow”
“ Hallow ndugu yangu kuna tatizo limetokea humu ndani.Rosemary amepatwa na na mstuko wa ghafla na anahitajika kukimbizwa hospitali haraka sana.”
“ Mstuko wa ghafla? Nini kimesababisha akapatwa na mstukohuo? Mbona amepita haap getinimuda mfupiuliopita akiwa mzima wa afya? Henry yuko wapi ? Yule mlinzi akaulzia maswali mfululizo.
“ Kumetokea kutokuelewana kati ya Henry na Rose na Rose alipatwa na tatizo hili.Sisi ni wale wageni tuliokuwa na Henry na hatufahamu mpaka sasa aliko Henry .Tafadhali naomba mliruhusu gari hilo haraka sana la wagonjwa ili tumkimbize Rose hospitali.Endapo mtaendelea kulizuia gari hilo na hali ikazidi kuwa mbaya lawama zote zitawaangukia ninyi” akasema Mathew na simu ikakatwa.
Baada ya dakika tano wakaingia kwa kasi walinzi watatu na nyuma yao wakafuata Eva na watu wengine wawili waliovaa makoti meupe wakiwa na machela .
“ Henry kaelekea wapi “akauliza mmoja wa walinzi
“ Stop asking questions.Tusaidiane kwanza kuokoa maisha ya bosi wenu” akasema Mathew wakasaidiana kumpakia Rosemary katika machela na kumshusha chini .Gari la wagonjwa likasogezwa karibu na mlango wakampakia Rose.Mathew akawagukia wale walinzi.
“Endeleeni kumtafuta Henry,sisi ngoja tumuwahishe mgonjwa.Tutawafahamisha maendeleo yake.” Akasema Mathew na kuingia katika gari lile la wagonjwa wakaondoka kwa kasi wakiwawaacha watumishi wakishangaa kilichotokea.Ndani ya gari madaktari wale wawili waliendelea kumpatia Rose .
“ Finally we got her” akawaza Mathew
“ Vyombo vya usalama vimekuwa vikimuogopa sana huyu mama lakini leo imefika arobaini yake.Ametua mikononi mwangu na lazima atanieleza kila kitu.Ni heri angekutana na shetani kuliko kukutana na mimi” akawaza Mathew.
“ Mathew tunaelekea hospitali gani? akauliza Eva
“ Eva we need to talk” akasema Mathew na kuwatazama wale madaktari
“ Samahani ndugu madaktari.Ninahitaji dakika mbili niongee faragha na Eva” akasema Mathew na mmoja wa wale madaktari akamuomba dereva asimamishe gari pembeni ya barabara,Mathew na Eva wakashuka
“ Mathew what happened? Akauliza Eva
“ Eva kulitokea rabsha kidogo na kusababisha Rose apatwe na mstuko huu.”
“ Henry yuko wapi?
“ Henry is dead”
“ Ouh my God!!.. Eva akastuka
“ Kwa hiyo tunaelekea wapi ? akauliza Eva
“ Tunaelekea nyumbani kwangu.”
“ No ! Mathew hali ya Rose ni kama unavyoiona si nzuri hata kidogo anatakiwa apelekwe hospitali akakae chini ya uangalizi wa madaktari.”
“ Eva,huyu mama ana taarifa za muhimu sana na kwa sasa ameua mikononi mwangu siwezi kumuachia hata sekunde moja.”
“ Mathew unarudia tena ubishi wako kama wa kipindi kile uliosababisha kifo cha Yule msichana.Nakushauri kama rafiki yangu tumpeleke Rosemary hospitali na hali yake ikiwa nzuri tutamchukua na kumuhoji kama unavyotaka lakini kwa sasa bado hali yake si nzuri na huwezi kumuhoji chochote” akasema Eva
“ Eva,siwezi kamwe kufanya kosa la kumpeleka Rose hospitali.Wewe mwenyewe ndiye uliyenihakikishia kwamba huyu mama ni hatari na ana mtandao wake mkubwa kwa hiyo basi kitendo cha kumpeleka hospitali tutampoteza na hatutaweza kumpata tena.This is the only chance we have and we cant loose it”
“ Mathew nakubaliana nawe lakini bado naendelea kukushauri kwamba tumpeleke hospitali.Hawa madaktari wote wanafanya kazi katika idara ya usalama wa taifa na tutampeleka Rose katika hospitali zetu ambazo huwa tunazitumia kuwahifadhi watu kama hawa wakahudumiwa bila ya mtu kufahamu .Please Mathew,naomba unisikilize na tukubaliane katika hili.” akasema Eva
“ Eva tusiendelee kupoteza muda.Rosemary anapelekwa nyumbani kwangu na atahudumiwa pale.”
“ Itakuwaje iwapo atapoteza maisha akiwa nyumbani kwako? Mathew suala hili ni la hatari kubwa sana .Muda si mrefu itagundulika kwamba Rosemary ametoweka na utaanza msako mkali sana wa kumtafuta.Hii itakuwa mbaya sana kwako Mathew” Akasema Eva
“ That’s the risk I have to take Eva.Ikitokea hivyo I’ll know what I’ll do .Get in the car” akasema Mathew wakangia garini na safari ikaendelea
“ Katu siwezi kumpa nafasi huyu mama ya kutoroka japokuwa haliyakeni mbaya ,lakini kumpeleka hospitali hata kama inamilikiwa na usalama wa taifa bado ni kumpa nafasi ya kutoroka kwani kwa mujibu wa Eva hata ndani ya idara ya usalama wa taifa mtandao wa Rose umekita mizizi yake .I have to take this risk.Kama akipoteza maisha nitajua nini cha kufanya lakini naomba Mungu jambo hilo lisitokee kwa sasa “ akawaza Mathew .Anitha aliyekuwa amekaa mbele na dereva akamuelekeza njia ya kupita hadi walipofika nyumbani kwa Mathew.Rosemary akashushwa na kuingizwa katika chumba kimoja kikubwa ambacho kina vitanda vitatu kama vya hospitali na vifaa mbalimbali vya tiba.Chumbakile kilionekana kama zahanati ndogo.Rose akalazwa katika mojawapo ya vitanda vile .Madaktari wale wakaelekeza baadhi ya vitu vinavyotakiwa kupatikana haraka ili kufanikishamatibabu ya Rose.
Gari lile la wagonjwa lililotumika kumbeba Rose likabadilishwa namba ili kuzuia kutambulika kisha Eva na dereva wa lile gari wakaondoka .Eva alikwenda kutafuta baadhi ya vifaa vilivyohitajika . Mathew alimkumbusha pia kumchukua Naomi na kumleta pale nyumbani.Wakati madaktari wale wawili wakiwa na Rosemary wakimuhudumia,Anitha akaelekea ofisini kuendelea kuifanyia upekuzi kompyuta ya Rose,Mathew akamfuata Elibariki chumbani.
“ Hallow Elibariki.Unaendeleaje? akauliza Mathew
“ Ninajitahidi Mathew lakini bado kichwa changu kizito sana.Nimekuwa na mawazo mengi mno nahisi kama ninataka kuchanganyikiwa.Kuna taarifa zozote mpya kuhusiana na msiba wa Flaviana?
“ Anitha yuko ofisini sasa hivi akiangalia kama kuna taarifa yoyote mpya.” Akasema Mathew
“ Nini kinaendelea sasa hivi Mathew? Akauliza jaji Elibariki
“ Tumefanikiwa kumpata Rosemary Mkozumi.”
“ Mmefanikiwa kumpata? Hongereni sana.”
“ Ahsante sana Jaji lakini hali yake si nzuri sana na madaktari wako naye chumbani wakimuhudumia na hali yake itakapokuwa nzuri tutamfanyia mahojiano .Tutafahamu mambo mengi kutoka kwake.” Akasema Jaji Elibariki na mara Anitha akaingia mle chumbani
“ Mathew kuna kitu nimekigundua..” akasema Anitha
“ Umegundua nini Anitha? Akauliza Mathew huku akiinuka na kuongozana na Anitha kuelekea ofisini.
“ Wakati nikipekua kompyuta ya Rose nimekutana na barua pepe hii ambayo inaonyesha Rose alimtumia mtu anayeitwa Captain Amos akimtaka ampatie taarifa zenye uhakika kwani anategemea kwenda kuonana na Samir Asaad aliyefikia 7 angels hotel.Kilichonistua ni kwamba Peniela aliwahi kumtaja Captain Amos ambaye naye ni mshirika wa karibu sana wa rais na ambaye pamoja na Dr Kigomba wanashirikiana katika biashara ya hiyo package .” akasema Anitha
“ Ni kweli Anitha.Rais Dr Joshua anashirikiana na watu wawili katika biashara ile.Kuna Dr Kigomba na huyu Captain Amos.Kama utakumbuka katika ile barua pepe ambayo Rosemary alimuandikia Samir alimueleza kwamba anategemea kuupata mzigo muda wowote kwani ana mtu wa karibu sana na rais.Ni kweli Captain Amos ni mtu wa karibu sana na Rais na kwa maana hiyo basi picha ya haraka tunayoipata hapa ni kwamba Rose na Captain Amos ni washirika na nina wasiwasi kwamba huo mzigo anaouongelea Rose kwamba wana hakika ya kuupata wakati wowote ni hiyo package ambayo Dr Joshua anataka kuiuza.”
“ Exactly!! Akasema Anitha
“ Hakuna ubishi kwamba mzigo huo anaouongelea Rose ni hii package ambayo Dr Joshua na wenzake wanataka kuiuza.” Akasema Anitha
“ Ukumbuke vile vile Captain Amos yuko pia Team SC41 na wanamtegemea sana katika kupata package hiyo.Anaonekana ni mtu mwenye tamaa sana ya fedha kwani anachukua fedha toka Team SC41,anachukiua fedha kwa Rose na bado anategemea mgawo mkubwa wa fedha toka kwa Dr Joshua .Huyu ni mtu hatari sana na tunatakiwa kumpata haraka sana."
“ Hiyo package ina kitu gani ndani kiasi cha watu wengi namna hii kuitaka? Halafu kwa nini wanunuzi wake wengi wanatokea katika nchi za kiarabu? Akauliza Anitha
“ Nadhani Rose anaweza kutupa majibu ya nini kilichomo katika hiyo package lakini kwa sasa tunatakiwa kumpata Captain Amos.Endapo Amos akipotea ghafla basi Team SC41 na hata huyu Rose hawataweza kupata taarifa zozote kuhusiana na package kwa hiyo sisi tutapata nafasi nzuri ya kuweza kuichukua.” Akasema Mathew
“ Ni Peniela pekee anayeweza kutuelekeza mahala pa kumpata Amos.Nashangaa mpaka mida hii hajanipigia simu wakati nilimuachia maagizo Josh kwamba mara tu atakapozinduka anitafute .” akasema Mathew huku akiitoa sumu yake mfukoni na mara kengele ya getini ikalia.
“ Ngoja nikaangalie yawezekana Eva amerudi.” Akasema Mathew huku akitoka kwenda getini
“ Baada ya kazi hii kukamilika itanilazimu niwarudishe wale walinzi wa getini walikuwa wananisaidia sana
“ akawaza wakati akielekea getini.Alifungua geti na kukutana na Peniela
“ Peniela !! akasema Mathew kwa mshangao kidogo
“ Hello Mathew.Mbona umestuka?
“ Tulikuwa tunakuongelea sasa hivi hapo ndani kumbe uko getini.Mbona silioni gari lako? Umekuja kwa miguu? Akauliza Mathew
“ Nimekuja na taksi.Sikutaka watu wafahamu mahala ninakoenda.” Akasema peniela na mathew akamkaribisha ndani
“ Pole sana Peniela.Unajisikiaje sasa hivi? Nilishindwa kuonana nawe tena baada ya watu ambao nahisi ni Team SC41 kuwasili pale hospitali” akasema Mathew.
“ Kifo cha John kimenipa simanzi kubwa lakini baada ya kuzinduka nikakumbuka kuna jambo zito linalotukabili na ndiyo maana nimekuja hapa ili tujue kinachoendelea.”
“ Pole sana Peniela.Una hakika una nguvu za kutosha kuweza kuendelea na mapambano? akauliza Mathew
“ John amekwenda na maisha lazima yaendelee.Jambo kubwa lililoko akilini mwangu kwa sasa ni kuhakikisha package inapatikana kwa gharama zozote na kisha kuifunga kabisa Team SC41.Kukujibu swali lako ni kweli nina nguvu za kutosha kuendelea kupambana hadi mwisho.” Akasema Peniela
“ Good.Nafurahi kusikia hivyo.” Akasema Mathew
“ Elibariki yuko wapi? Akauliza Peniela
“ Peniela kuna jambo sikuwa nimekufahamisha .Nikiwa pale hospitali nilipigiwa simu na Anitha akanifahamisha kwamba Dr Joshua amempigia simu Dr Kigomba na kumfahamisha kwamba Flaviana amefariki dunia.”
“ What ?!!! Peniela akastuka sana
“ Flaviana amefariki dunia.” Akasema Mathew
“ Oh my God ! Yuko wapi Elibariki? Akauliza Peniela
“ Elibariki yuko chumbani anapumzika kwa mstuko alioupata” akajibu Mathew na bila kupoteza muda Peniela akainuka na kuelekea chumbani kwa jaji Elibariki akaufungua mlango na kuingia ndani.Elibariki alikuwa amekaa kitandani amejiinamia akiwaza na mara tu alipomuona Peniela akajikuta akipata nguvu na kusimama.Wakakumbatana kwa nguvu.
“ Pole sana Elibariki.Pole sana my love”akasema peniela huku akimpiga piga mgongoni.
“ ahsante sana Peniela.Ahsante sana kwa kuja kunifariji.Pole nawe pia.Mathew ameniambia kwamba John amefariki dunia. “ akasema Elibariki
“ Ndiyo amefariki dunia.”
“ Pole sana Peniela.Kifo hakizoeleki hasa kwa mtu wako wa karibu lakini lazima maisha yaendelee.”
“ Ni kweli Elibariki na ndiyo maana nimekuja hapa ili kuweza kuendelea na mikakati yetu “ akasema Peniela. Mara Mathew akasimama mlangoni na kusema
“ Peniela kama hutajali nakuomba ofisini mara moja”akasema Mathew na Peniela na jaji Elibariki wote kwa pamoja wakaelekea ofisini kwa Mathew
“ Peniela kuna jambo limetokea asubuhi ya leo ambalo huna budi kulifahamu.Ni kwamba tumefanikiwa kumpata Rosemary Mkozumi mke wa rais wa zamani wa Tanzania.”
“ Roemary Mkozumi? Akauliza Peniela kwa mshangao
“ Ndiyo Peniela.Katika uchunguzi wetu tumegundua kwamba huyu mama amekuwa na mawasiliano ya karibu na Habib soud ambaye anatajwa kutaka kuzinunua karatasi zile ambazo Edson aliziiba ikulu.Tunaamini kwamba huyu mama ndiye aliyekuwa nyuma ya mpango ule na Edson alitumiwa tu katika kuziiba karatasi hizo.Tumekwenda mbali zaidi katika kumfanyia uchunguzi Rosemary na tumegundua kwamba amekuwa na mawasiliano na mtu mmoja anaitwa Samir asaad na katika mawasiliano hayo Rosemary anamuhakikishia Samir kwamba mzigo utapatikana muda wowote kwani tayari ana mawasiliano na mtu aliyeko karibu sana na rais.Tumeendelea kuchunguza na kugundua kwamba Rosemary amekuwa na mawasiliano na Captain amos.”
“ Captain Amos?!! Peniela akashangaa
“ Ndiyo peniela.”
“ This is weird. Captain Amos yuko team Sc41,kumbe anatumiwa tena na huyu mama? The whole game is full of betrayals” akasema peniela
“ We need to get him as soon as possible” akasema Mathew
“ Tukitaka kufanikiwa katika kuipata hiyo package lazima tumpate Captain Amos ili hao wanaomtumia wakose taarifa sahihi za kuhusiana na kinachoendelea katika biashara hiyo.Katika hili utatusaidia sana tuweze kumpata kwani wewe unaweza kuwasiliana naye muda wowote” akasema Mathew.Peniela akatoa simu yake na kuzitafuta namba za Amos akapiga
“ Hallow Peniela,pole sana na matatizo.Nimepata taarifa za kifo cha John.Zimenistua sana” akasema Amos
“ Amos uko wapi? I need to see you.” Akasema peniela
“ Kuna tatizo gani Peniela?
“ Kuna jambo la muhimu sana la kuongea nawe”
“ Cant we talk on phone?
“ No .I have to meet you face to face” akasema Peniela.Ukapita ukimya wa sekunde kadhaa kisha Amos akajibu
“ Tukutane pale Mlimba restaurant,upande wa nyuma kuna vyumba,nenda hadi chumba namba kumi na nne huwa ninakitumia kwa dharura.Sitaki watu wajue nina mawasiliano nawe” akasema Amos na kukata simu
TUKUTANE SEHEMU IJAYO……
PENIELA SEASON 3
SEHEMU YA 13
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Tukitaka kufanikiwa katika kuipata hiyo package lazima tumpate Captain Amos ili hao wanaomtumia wakose taarifa sahihi za kuhusiana na kinachoendelea katika biashara hiyo.Katika hili utatusaidia sana tuweze kumpata kwani wewe unaweza kuwasiliana naye muda wowote” akasema Mathew.Peniela akatoa simu yake na kuzitafuta namba za Amos akapiga
“ Hallow Peniela,pole sana na matatizo.Nimepata taarifa za kifo cha John.Zimenistua sana” akasema Amos
“ Amos uko wapi? I need to see you.” Akasema peniela
“ Kuna tatizo gani Peniela?
“ Kuna jambo la muhimu sana la kuongea nawe”
“ Cant we talk on phone?
“ No .I have to meet you face to face” akasema Peniela.Ukapita ukimya wa sekunde kadhaa kisha Amos akajibu
“ Tukutane pale Mlimba restaurant,upande wa nyuma kuna vyumba,nenda hadi chumba namba kumi na nne huwa ninakitumia kwa dharura.Sitaki watu wajue nina mawasiliano nawe” akasema Amos na kukata simu
ENDELEA……………………………..
“ Anitha nitaongozana na Peniela kwenda Mlimba Lodge kumchukua Captain Amos.Wewe utabaki hapa kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri na kufuatilia mawasiliano yoyote kati ya Dr Joshua na Dr Kigomba.Vile vile endelea kufuatilia hali ya Rosemary Mkozumi .Eva ameenda kuvifuatilia baadhi ya vifaa na atarejea hapa muda si mrefu.Hakikisha unakuwa karibu na wale madaktari na kuhakikisha Rose anapata nafuu haraka kwa ajili ya kumfanyia mahojian😵ne more thing,usimruhusu Eva afahamu jambo lolote lile tunalolifuatilia na wala usimruhusu akaingia humu ofisini na wala asifahamu chochote kuhusu uwepo wa Elibariki hapa ndani” akasema Mathew
“ Who is this Eva? Akauliza jaji Elibariki
“ Ni rafiki yangu anafanya kazi usalama wa taifa” akajibu Mathew
“ Are you sure you want to go there alone? Akauliza tena jaji Elibariki
“ I’m not alone.Peniela will be there with me” akajibu Mathew.
“ Sawa Mathew,jitahidi kuwasiliana nasi mara kwa mara kutujulisha kila kinakachojiri ili kama kutahitajika msaada wa haraka basi tujue namna ya kujipanga” akasema Anitha
Jaji Elibariki na Peniela wakakumbatiana
“ Please take care Peniela” akasema jaji Elibariki
“ I will” akajibu Peniela halafu Mathew akatoka na kwenda katika chumba alimolazwa Rosemary Mkozumi ambaye kwa sasa hali yake ilianza kuleta matumaini.Mathew akatoka na kuingia chumbani kwake akachukua baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kumsaidia katika shughuli ile kisha akatoka na kuongozana na Anitha wakaingia garini kuelekea Mlimba Lodge.
“ Nilimuamini sana Captain Amos na kumuona kama mwenzangu ninayeweza kumtegemea kumbe ni mtu mbaya sana.Sikuwahi kufikiria kwamba anaweza akatumiwa pia na Rosemary Mkozumi . Kinachoniuma zaidi ni kwamba anatumiwa na Rosemary kupata taarifa za operesheni kubwa kama hii tunayoendelea nayo ya kuipata package toka kwa Dr Joshua.Amos ametuzunguka na kutoa taarifa kwa Rosemary ambaye naye pia anaonekana kuitafuta package hiyo.Jambo hili limeniumiza sana sana.Mathew nashukuru kwa kuligundua jambo hili mapema.Sisi tungeendelea na mipango yetu bila kujua kama mtu tunayedhani ni mwenzetu tayari ametuzunguka na anashirikiana na watu wengine ambao nao wanajipanga kwa ajili ya kuipata package hiyo na tungeweza hata kuuawa kwa kutolijua hili…Damn you Amos kwa nini ukatufanyia hivi? Akasema Peniela kwa hasira
“ Imekuwa vizuri sana tumewahi kulifahamu jambo hili mapema.Tusingeligundua hili mapema tungeweza kupata upinzani mkubwa sana toka kwa watu tusiowafahamu na hili lingetupa ugumu katika kuichukua hiyo package.Kwa sasa kwa kuwa tayari tunaye Rosemary Mkozumi ambaye naye anaitaka package hiyo basi tunatakiwa kwa kila namna tuweze kumpata pia Amos ambaye ndiye mtoa taarifa wake ili tuwe na uhakika kwamba kuna kundi moja tu ambalo tunapambana nao katika kuipata package hiyo nalo ni Team Sc41.Baada ya kumpata Amos kazi kubwa utakayobakiwa nayo peniela ni kuhakikisha unafahamu mikakati yote ya Team SC41 waliyoiweka katika kuhakikisha kwamba wanaipata hiyo package ili tuone namna ya kupambana nao na kuwawahi kabla hawajafanikiwa .” Akasema Mathew
“ Usihofu kuhusu hilo Mathew.Nitafalinyia kazi.Tutakuwa na kikao cha Team SC41 wote ili kujadili kuhusu suala hili nanitawafahamisheni kila kitu” akasema Peniela
“ Kuna chochote kilichopangwa kuhusiana na mazishi ya John Mwaulaya?
“ Mpaka sasa hakuna chochote kilichopangwa.Kutakuwa na kikao cha pamoja nadhani jioni ya leo kufahamishana kuhusu suala hili na hapo ndipo tutakapojua nini kinaendelea na namna tutakavyomzika John Mwaulaya” akasema Anitha
“ Ok Good ! akasema Mathew na kukawa kimya kidogo
“ Nilisikia ukimpa maelekezo Anitha kuhusiana na Eva.Who is she? Akauliza Peniela
“ Eva anafanya kazi katika idara ya usalama wa taifa na ndiye aliyenisaidia nikampata Rosemary Mkozumi.” Akasema Mathew
“ Don’t you trust her? Akauliza Peniela
“ Eva amekuwa ni msaada mkubwa sana kwangu na mara kwa mara amekuwa akinisaidia kufanikisha baadhi ya mambo lakini kusema ukweli bado sijafikia hatua ya kuweza kumuamini.” Akasema Mathew
“ Sawa Mathew,Kuna taarifa zozote kuhusiana na kinachoendelea katika msiba wa Flaviana?
“ Mpaka sasa hivi bado hatujapata taarifa za kinachoendelea ila nina hakika mpaka jioni tutajua nini kinachoendelea.” Akasema Mathew
“ Mathew now that John has gone,kuna mambo ambayo natakiwa niyakamilishe.Yeye mwenyewe alinipa maelekezo kwamba niyakamilisha pindi atakapokuwa amefariki.amenisisitiza sana nisiache kuyakamilisha” Akasema Peniela
“ Tutayakamilisha yote Peniela lakini kwa sasa kitu kikubwa ni kuelekeza nguvu katika suala hili lililoko mbele yetu .Tunatakiwa kwa kila tuwezavyo kuhakikisha kwamba package inatua mikononi mwetu ” akasema Mathew
Walikarbia sana kufika Mlimba Lodge,Mathew akasimamisha gari katika kituo cha basi na kusema
“ Peniela tumekaribia sana kufika.Kutokea hapa itakulazmu uchuke taksi hadi Mlimba lodge.Mimi nitakuwa ninakufuatilia kwa nyuma.Utakapoingia ndani kukutana na Amos tafadhali usionyeshe kwamba unafahamu mambo anayoyafanya.Tafuta namna ya kuongea naye ili kuvuta muda wakati nikijiandaa kuvamia ndaniya chumba ” Akasema Mathew na kufungua droo ya gari akatoa kijimtambo Fulani akakiwasha halafu akachomoa vidude viwili vidogo na kumpatia kimoja peniela akamwambia akiweke sikioni.
“ Hiki ni kifaa cha mawasilino .Nitasikia kila utakachoongea na Amos ” akasema Mathew halaf akampatia Peniela bastora iliyofungwa kiwambo cha sauti. Peniela akashuka garini na kuchukua taksi kuelekea Mlimba Lodge Mathew akafuata kwa nyuma.
Taksi alilopanda Peniela likafika katika megesho ya Mlimba Lodge akashuka na kupiga hatua za haraka haraka kuelekea katika chumba alichoelekezwa na Amos.
“ Ninaelekea chumbani kwa Amos” Peniela akamtaarifu Mathew
“Ninakutazama.Peniela be carefull,this man is very dangerous” akasema Mathew
“ I will” akajibu Peniela
Peniala akafika chumba namba kumi na nne akasima mlangoni kwa sekune kadhaa halafu taratibu akakinyonga kitasa cha mlango na kuingia ndani.Ndani ya chumba kile Captain Amos alikuwa amekaa katika sofa akiwa na chupa ya bia pembeni pamoja na bakuli la supu.
“ Peniela,karibu sana” akasema Amos huku akitabasamu.Peniela akageuka kwa dhumuila kuufunga mlango na ghafla akachomoa bastora na kumuelekezea Amos
“ I trusted you son of a bitch…why you did that ? Why you betrayed us Amos ? Akauliza Peniela huku uso wake ukiwa umejikunja kwa hasira.Captain Amos akabaki anashangaa.hakuwa ametegemea kitendo kile cha Peniela
“ Peniela !!..what happened? Please calm down ! Akasema Amos huku akijaribu kutaka kuinuka
“ Sit down Amos !! akasema kwa hasira Peniela na Amos akagundua kwamba peniela hakuwa akitania akaketi.
“ peniela !!.akataka kusema kitru amos lakini peniela akamzuia.
“ Shut up….!! Akafoka Peniela huku akimuangalia Amos kwa hasira kali.
“ why Amos ? Why you betrayed us? Akauliza Peniela
“ Peniela I dont understand what you are talking about”
“ You don’t know ?? akauliza Peniela kwa ukali
“ Peniela tafadhali weka silaha yako chini…tafadhali weka silaha tuongee..Sielewi unazungumzia kitu gani..”
“ Toka lini umekuwa ukishirikiana na Rosemary Mkozumi na kumpa habari zetu? Akauliza Peniela
Captan amos akastuka sana .
“ How do you know that? Akauliza Amos
“ Ulidhani hatutajua? Kwa nini Amos ukafanya vile? Kwa nini ukaingiwa na tamaa ya pesa kiasi hicho? You sold us all.Sote tungeuawa kwa sababu yako.Huna thamani tena kwangu Amos.!! I hate you !
“ Forgive me Peniela..I did that on purpose.!!
“ On Purpose? Hustahili msamaha kabisa mwanaharamu wewe.”akasema Peniela huku akiuma meno kwa harsira
“ Peniela ! Peniala! …..akaita Mathew kupitia kile kifaa kidogo Peniela alichokiweka sikioni.
“ Today you’ll tell me everything .Ukikataa kunieleza ninachokitaka I swear in heaven and earth I’m going to kill you with my own hand.!! akasema peniela.Captain Amos alogopa,hakuwahi kumuona Peniela akiwa amekasirika namna ile. Macho yake yalionyesha wazi kwamba alidhamiria kukifanya kile alichokuwa anakisema
“ peniela !! ..Peniela !!..akaita Mathew
“ Peniela don’t do that please! Don’t kill him , I’m on the way coming there.Dont shoot him.We need him alive”akasema Mathew .
“ Peniela don’t shoot me..If you do that,you’ll be doing a very big mistake..Me and you we’re all in the same team and everything I’m doing is for you peniela !” akasema Amos .
“ For me ?!! Kutoa siri za mipango yetu ndiyo kufanya jambo kwa ajili yangu? Akafoka peniela
“Peniela kuna mambo mengi ambayo bado huyafahamu but we want to make you and Elibariki very powerfull.. “ akasema Amos na kuzidi kumchanganya peniela.
“ You use the word We ? wewe na nani? Rosemary Mkozumi? Akauliza
“ Peniela najua sio wakati wake kukweleza kuhusu jambo hili lakini sina ujanja lazima nikueleze kila kitu kuhusiana na mipango iliyopo juu yako na Elibariki” akasema Amos lakini ghafla mlango ukapigwa teke na kufunguka,akatokea mwanamke mmoja aliyevaa mavazi meusi na miwani mikubwa myeusi kufunika macho yake ,aliyekuw ana bastora mbili mkononi zilizofungwa kiwambo cha kuzuia sauti .Kama chura Peniela akaruka na kujificha nyuma ya kabati na mwanamke yule akaanza kummiminia risasi Captain Amos.Peniela akaachia risasi mbili toka katika bastora yake kuelekea mlangoni lakini tayari mwanamke Yule alikwisha toweka na Captain Amos alikuwa amelala sakafuni damu nyingi ikimtoka.
“ Ouh My God !!..akasema Peniela kisha akamfuata Amos
“ Amos ! Amos !.akaita Peniela lakini tayari Amos alikwisha fariki kitambo na mara akaingia Mathew.
“ Peniela what happened? Akauliza Mathew huku naye akishangaa
“ Are you ok ? akauliza Mathew
“ I’m ok Mathew.” Akajibu peniela
“ He’s gone Mathew !..Amos is dead” akasema Peniela.
“What happened? Akauliza Mathew
“ Mlango ulipigwa teke ukafunguka ghafla na mwanamke mmoja aliyekuwa na bastora mbili akammiminia Amos risasi.Mathew I’m so scared” akasema Peniela.Mathew akamtazama Amos na kuhakikisha ni kweli amefariki akamsachi na kuchukua simu yake .Akaangaza angaza kwa haraka kuona kama kuna chochote wanachoweza kuondoka nacho hakukuwa na kingine zaidi ya mkoba wa kompyuta,Mathew akauweka begani .
“ Lets get out of here” akasema Mathew wakaufunga mlango na kutoka kwa kasi hadi katika gari wakaondoka
“ I’m sorry Mathew ,Amos ni mtu niliyemuamini kupita kiasi na siri zangu nyingi nilimweleza.Kitendo alichokifanya cha kutusaliti kimeniumza sana na ndiyo maana mara tu nilipomtia machoni nilipandwa na hasira kali na nikashindwa kuwa mstahimilivu nikamtolea bastora.I’m so sorry I failed you.” Akasema Peniela
“ Its ok peniela.Mambo kama haya hutokea.We wanted him alive na ndiyo maana baada ya kusikia maongezi yenu mle chumbani nikagundua ulipandwa na hasira na ukashindwa kujizuia naukiwa na hasira kitu chochote kingeweza kutokea ndiyo maana nikakuita ili kujaribu kukuzuia usifanye chochote.Kuna mambo mengi ambayo tulihitaji kuyafahamu kutoka kwake.” Akajibu Mathew
“ I’m so sorry Mathew.” Akasema Peniela
“ Usijilaumu sana Peniela.Imekwisha tokea na tuangalie yajayo.lakini bado najiuliza mwanamke Yule ni nani? Kwa nini kamuua Amos? Akasema Mathew
“ Inavyoonekana Yule mwanamke alikuwa karibu akifuatilia maongezi yetu mimi na Amos lakini nashindwa kuelewa ni kwa nini amuue Amos hasa pale ambapo alikuwa trayari kunieleza jambola muhimu?
“ Jibu hapa ni rahisi tu.hakutaka Amos akueleze kile alichotaka kukweleza na ndiyo maana suluhisho pekee lilikuwa ni kumuua.But this woman ,who is she? Anaonekana ni mwanamke hatari na mwenye ujuzi wa hali ya juu wa kutumia silaha.kwa namna alivyomuua Amos anaonekana ni muuaji mzoefu sana.We need to find out who is she? Katumwa na nani amuue captain Amos? Na kuna siri gani ambayohakutaka Amos akueleze? Akasema Mathew.
“ Ninaskitikika sana kwa amos kufa namna ile lakini ukweliutabaki wazi kwamba Amos hakuwa vile tulivyomdhania.Alikuwa na mtandao wake wa siri .Wait ! I remember something…..” Peniela akanyamaza ghafla kwamba kuna kitu alikikumbuka
“ Umekumbuka kitu gani? Akauliza Mathew
“ Nimekumbuka usiku ule Elibariki aliposhambuliwa nilipigiwa simu na mwanamke mmoja nisiyemfahamu na akanifahamisha kwamba nikutane naye ili nimchukue elibariki.Ulikuwa ni usiku na kichwani alivaa kofia lakini nilifanikiwa kuiona sura yake.Nimeikumbuka vyema ..Nihuyu mwanamke aliyemuua Amos...Yes it was her. Yule mwanamke aliyemuoka Elibariki ndiye huyu aliyemuua Amos” akasema Peniela
“ are you sure Peniela? Akauliza Mathew
“ I’m sure Mathew.Sura ile nimeikumbuka kabisa na hasa sehemuya mashavu...Its her” akasema Peniela.Mathew akafikiri kidogo na kusema
“ who exactly is this woman? Akauliza Mathew.
“ I don’t know her.Lakini nina hakika kabisa ndiye Yule ambaye alikuwa na Elibariki usiku ule aliposhambuliwa.”
“ Tunatakiwa tumfahamu mwanamke Yule na ndipo tutaweza kumfahamu yeye ni Nani.Anahusikaje katika shambulio lile la Elibariki na kwa nini amemuua Amos? Akasema Mathew
“ How are we going to find her” akauliza Peniela
“ I don’t know how but we must find her.Huu unaonekana ni mtandao hatari.Kama mwanamke Yule alikuwepo usiku ule Elibariki aliposhambuliwa basi yeye na mtandao wake wanafahamu mambo mengi na kuna sababu kubwa ya Amos kuuawa.Amos alikwamba kwamba wana mpango wa kuwafanya wewe na elibariki kuwa na nguvu kubwa.Ni mpango gani huo? Ni akina nani hawa wenye kupanga mipango hiyo ?
“ Mathew hili suala si la kupuuzia hata kidogo.Nina uhakika mkubwa kwamba ni kweli lazima kuna kuna jambo linaloendelea chini kwa chini kuhusiana na mimi na Elibariki.Ni jambo gani hilo na ni akina nani ambao wanapanga mipango hiyo ? Tunahitaji kulifahamu suala hili.Tukifanikiwa kumpata Yule mwanamke tutafahamu kila kitu”akasema Peniela.
Sura ya mwanamke Yule aliyepishana na Mathew huku akikimbia ikaendelea kuzunguka kichwani kwa Mathew.
“ who is this woman? Akajiuliza bila kupata jibu
“ anaonekana ni mwanamke mwenye kufahamu mambo mengi .Nakumbuka Elibariki aliniambia kwamba usiku ule lilipofanyika lile shambulio aliokolewa na mwanamke ambaye alimkabidhi kwa Peniela.kwa mujibu wa peniela ameikumbuka sura ya mwanamke Yule kwamba ni huyu aliyemuua Amos leo.Ninahakika mtandao aliomo utakuwa unafahamu mambo mengi sana kuhusiana na Elibariki na ninahisi kuna mambo mengi wanayafahamu pia kuhusiana na package ile toka kwa Dr Joshua.Lazima tumtafute mwanamke Yule kwa kila njia.Suala hili linazidi kuwa kubwa kila uchao” akawaza Mathew wakiwa garini
“ Unawaza nini Mathew? Akauliza Peniela.
“ Ninawaza mambo mengi sana na kubwa ni namna mambo mapya yanavyozidi kuibuka kila uchao..Hili la kuuawa amos limeniwashia taa nyekundu kuashiria kwamba mapambano haya kwa sasa yamefikia sehemu ya hatari zaidi” akasema Mathew
“ nakubaliana nawe Mathew.hata mimi sikutegemea kabisa kama suala hili lingeweza kufika hapa lilipofika.hata hivyo nawapongeza kwa hatua kubwa iliyofikiwa hadi hivi sasa.Mmegundua mambo mengi makubwa na mazito.Kinachotakiwa kwa sasa nikushirikiana kuhakikisha kwamba mambo haya yanafika mwisho na tunaizika kabisa mitandano hii ya hatari hapa nchini na hasa team SC41”
“Uko sawa Peniela lakini bado tuna kazi kubwa ya kufanya mbeleni.watu tunaopambana nao niwatu hatari na wenye nguvu lakinininwahakikishia kwamba tutapambana hadi tone la mwisho la damu na nitaongoza mapambano kuishinda vita hii” akasema Mathew safari ikaendelea hadi walipowasili nyumbani kwa Mathew.Anitha akawafungulia geti.
“ What happened? Kuna tatizo Mathew ?akauliza Anitha baada ya Mathew na Peniela kushuka garini
“ yes there is a problem.Eva amekwisha rejea?
“Ndiyo amerejea yuko na madaktari chumbani.”akasema Anitha.
“ Naomi yuko wapi? Akauliza Mathew
“ Yuko nyuma bustanini anapumzika.who is she? Akauliza Anitha
“ Nitakufahamisha baadae.kwa sasa muandalie chumba cha kulala ataishi nasi hapa.Vile vile mpeleke peniela chumba cha mapumziko akapumzike kwa muda.”akasema Mathew kisha akaongoza hadi katika chumba alimolazwa Rosemary Mkozumi.hali yake ilikuwa nzuri na alikuwa amekaa kitandani akionge ana madaktari wale wawili pamoja na Eva.Mara tu Rosemary alipomuona Mathew akamkumbuka
“Its you..Its you who shot henry..its you…!!..akapiga ukulele na kutaka kuinuka pale kitandani madaktari wakamzuia kwanialikuwa na pingu mguuni..
“ Anaendeleaje? Mathew akawauliza madkatari
‘Kwa sasa hali yake imetulia na anaendelea vizuri”
“kwa hiyo ninaweza kumfanyia mahojiano? Akauliza Mathew
“ Nadhani ungesubiri kidogo kabla ya kumfanyia mahojiano ili hadi hapo hali yake itakapokuwa nzuri kabisa. “akashauri mmoja wa wale madaktari
“ Thank you doctor ..we’ll take it from here” akasema Mathew
“ what ?! akauliza Eva
“Your job here is done you can go now.! Akasema Mathew
“ You are kidding Mathew.Huyu mama bado anahitaji usimamizi wa madaktari na hawezi kuhojiwa kwa sasa” akasema Eva
“ Thank you so much for your help but you job is done here too,so you can go now.Naomi atabaki hapa kwetu na kama kutakuwa na tatizo lolote nitakutaarifu” akasema Mathew.Eva akaonekana kukerwa sana na kauli ile ya Mathew akamtazama kwa hasira na kusema
“ Mathew can we talk for a minute?
Mathew na Eva wakatoka nje ya kile chumba
“What are you doing Mathew? Akauliza Eva
“ I’m doing my job Eva” akajibu Mathew
“ Mathew mbona unajiweka katika hatari kubwa . Huyu mama bado anaumwa na anatakiwa uangalizi wa madaktari kwa nini unakuwa mbishi Mathew?
“ Eva this is my job and I’m going to do it the way Iwant.Huyu mama ana taaifa za muhimu sana ambazo ni lazima tuzipate.we don’t have that time to wait so if you don’t mind can you please go and let me do my job? Akasema Mathew
“ Ok I’m going but don’t you ever find me again for any help” akasema Eva huku akiingia ndani ya kile chumba kwa hasira na kuwaomba wale madaktari waondoke zao.
Baada ya Eva na madaktarikuondoka Mathew akarejea ndani ya chumba alimokuwamo Rosemary mkozumi akamtazama kwa sekunde kadhaa
“ Now its just me and you..Today I’m your angel of death..” akawaza Mathew na kuufunga mlango akatoka
TUKUTANE SEHEMU IJAYO…